WAZIRI WA VIWANDA NA UWEKEZAJI CHARLES MWIJAGE WAKATI WA MKUTANO ULIOANDALIWA NA WAKALA WA VIPIMO NCHINI, HAPA ALIKUWA AKIJIBU BAADHI YA HOJA ZA WAJUMBE WA MKUTANO HUO |
MKUU WA WILAYA YA MSOMA, HAMPHREY POLE POLE WAKATI AKICHANGIA JAMBO KWENYE MKUTANO HUO, POLE POLE ALIMWAKILISHA MKUU WA MKOA WA MARA MAGESSA MULONGO. |
PICHA YA PAMOJA NA WAZIRI ALIYE KETI WANNE KUTOKA KUSHOTO WALIOKETI AKIWA NA WAKUU WA MIKOA ILIYO HUSIKA KATIKA MKUTANO HUO. |
Na: Atley Kuni- Mwanza
Waziri
wa Viwanda Biashara na uwekezaji Charles Mwijage, amesema hayupo tayari kurudi
kwenye makongamano, semina wala warsha ambazo hazina tija kwa manufaa kwa
mustakabali wa zao la pamba nchini na badala yake amesema, kuanzia hivi sasa
nguvu itaelekezwa kwenye utendaji zaidi ili kuleta matokea chanya kwa zao hilo
ambalo lilikuwa mkombozi wa mkulima wa Tanzania katika miaka ya nyuma.
Mwijage
ametoa kauli hiyo Jijini Mwanza wakati wa kongamano la wadau wa Sekta ya Pamba
lililokutana Jijini humo kwa lengo la kujadili suala la vipimo sahihi kwa
biashara endelevu ya zao la Pamba, “ Kuanzia sasa nimesema nimesikia kilio cha
wadau, na nimeelewa lugha wanayo itaka sasa na mimi sipo tayari kuona
makongamano na semina ambazo wenzetu wa Bodi ya Pamba wamekuwa wakiziitisha
kila mwaka bila kuwa na matokeo chanya zinaendelea ” amesema Mwijage na
kuongeza “lakini pia niseme kuna baadhi ya mambo ambayo yameongelewa hapa
nadhani kama waziri mwenye dhamana nitayachukua nakwenda kuyafanyia kazi kwa
yale yaliyo katika ngazi inayo nihusu.
Kauli
ya Mwijage ilikuja mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Harrison Mtaka,
kuitupia lawama bodi ya Pamba nchini, kuwa, imekuwa ikiendesha makongamano na
warsha kwa wadau wa Pamba kila mwaka bila mafanikio, Mtaka katika maelezo yake
alianza kwakusema “kama tunataka mabadiliko kwenye sekta ya Pamba lazima yawepo
mabadiliko na kama ni suala la mabadiliko nilazima makongamano ya Bodi ya Pamba
nchini yafutwe, kwani mamlaka hiyo haina Bodi ya wakurugenzi kwa zaidi ya miaka
mitano (5), alisema mtaka na kuongeza “Inashangaza
kila mwaka wadau wanakaa kujadili haya haya ambayo tuna yajadili leo,
Mhe. Waziri hawa watakudanganya hapa kama mawaziri wenzako walivyo wahi
kudanganywa huko nyuma alisema Mtaka”,
huku akitaka bodi ya Pamba iondoshwe na maafisa wa Bodi hiyo wapangiwe majukumu
mengine ambayo wanayaweza, mtaka aliwatupia lawama hizo maafisa hao huku
akisema wamekuwa madalali wakuhafanya ubadhilifu wa kuharibu mizani “ Haiwezekani
mizani ziharibike halafu aliye haribu asijulikane, Mhe. Waziri hawa wachukuliwe
waende maeneo mengine wakasome magazeti ili waje na mawazo mapya”
Mtaka
pia amelaani kitendo cha Maafisa wa Bodi ya Pamba kukaa Dar es Salaam, huku
matatizo lukuki yakiwa yapo maeneo ambapo pamba inalimwa, ameutaka uongozi huo
kuona namna yakuwa karibu na maeneo ambapo Pamba inalimwa kwa wingi badala
yakukaa Dar Es Salaam na kungojea kupanda ndege kuja kusuluhisha matatizo.
Katika
hatua nyingine, Mtaka alishauri, kama serikali inataka kufanikiwa, zile Milioni
50, ambazo Mhe. Rais aliziahidi kwa kila kijiji wakati wa kampeni ni vema fedha
hizo zikaelekezwa kwenye vikundi ili vikundi hivyo viweze kuanzisha viwanda
vidogo vidogo, vinginevyo fedha hizo zinaweza kutafunwa na wajanja wachache
ambao watajinufaisha wao na familia zao kama ilivyokuwa kwenye Mabilioni ya JK.
Kwa
upande wao chama cha wadau wa Sekta ya Pamba nchini, Tanzania Cotton
Association (TCA), wao wameshauri kuondolewa kwa Siasa katika suala la Pamba
kwakuwa mipango mingi inakwama kutoka na wanasiasa kuingilia mipango endelevu
ya zao la pamba, akisoma taarifa ya chama hicho mwakilishi wake bwana Muhamed
Sharifu alisema “ Imefika wakati wanasiasa wakae pembeni na waichie sekta hiyo
wadau wafanyekazi yao lakini pia tunawaomba maafisa uagani waache kukaa
maofisini na badala yake waende mashambani wakatoe ushauri wa kitaalam” alisema
Sharifu.
Hata
hivyo kauli hiyo yakuwashutumu wanasiasa ilipingwa vikali na Mbunge wa Geita
Vijijini Msukuma Kasheku, ambaye katika kuchangia kwake alidai mtu pekee
wakuweza kuyapigania maslahi yamkulima mnyonge ni mwana siasa huku akijinasibu
kwakusema hata iwe vipi hawatakuwa tayari kupitisha sheria yakuwaengua
wanasiasa kwenye zao la Pamba “Sisi ndio wabunge mtaona kama hilo mnalo litaka
litakuwa haiwezekani kila kukicha mnanyonya mkulima halafu leo mnataka eti
wanasiasa waondelewe kwenye kulisemea zao la pamba.
Mkutano
huo wa siku moja uliandaliwa na Wakala wa Vipimo (WMA) na kuwakutanisha wadau
wa sekta ya pamba kutoka mikoa inayo lima Pamba ya Mwanza, Simiyu, Geita, Mara,
Shinyanga, Singida, Kigoma, na Kagera kwa minajili yakuangalia vipimo sahihi
kwa biashara endelevu ya zao la Pamba.
MWISHO.
Post A Comment: