Mkuu wa mkoa wa Mwanza akipokea maelezo kuhusu maendeleo ya utengenezaji wa Madawati kwa mkoa wa Mwanza hususan Jiji la Mwanza. |
Mmmoja wa maafisa wa Jiji la Mwanza aliyekutwa eneo la Utengeneza akisimamia zoezi hilo. |
Twende nikajionee mwenyewe hatua mliyopiga hadi hivi sasa. |
Gari lililokutwa eneo la Buhongwa chuoni likiwa linapakia madawati yaliyo kamilika kwaajili yakupeleka mashuleni. |
Na. Atley Kuni. RS Mwanza.
Mkuu
wa mkoa wa Mwanza John Mongella, amefanya ziara ya kushtukiza katika chuo cha
Ufundi Buhongwa kwa lengo la kujionea utengenezaji wa madawati ambapo
Halmashauri ya Jiji la Mwanza imepiga kambi katika eneo hilo kwa ajili ya
madawati ya Wilaya ya Nyamagana.
Ziara
hiyo imekuja ikiwa zimesalia siku ishirini na mbili kabla ya tarehe ya mwisho
kwa mikoa kukabidhi takwimu za madawati kwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa
Tanzania Mhe. Dr. John Pombe Magufuli, ambaye alitoa muda kwamba hadi kufikia
tarehe 30, Juni, 2016 kila mkoa uwe umejitosheleza kwa madawati.
Akiwa
katika eneo la tukio mkuu wa mkoa amewahimiza watengenezaji hao kuongeza bidii
ili ifikapoa tarehe yakuwasilisha wawe wamekamili shughuli hiyo.
“Nadhani
mnafahamu muda umekwenda, ni vema
mkaongeza spidi yenu ya utengenezaji ili tuweze kumaliza kwa wakati kama mkoa
kisha nasi tuweze kuwasilisha kama jinsi maelezo ya Mhe. Rais yalivyo elekeza.
Kwa
upande wake, mkufunzi katika chuo hicho ameahidi kukamilisha kazi hiyo kwa
wakati na kusema kama hali itakwenda vizuri basi kufikia tarehe 20, Juni
watakuwa wamekamilisha “Tulikuwa na changamoto ya vyuma hapa katikati lakini
hivi sasa tatizo hilo limekwisha na spidi yetu kama mnavyo iona niyakuridhisha”.
Mkoa
wa Mwanza wenye mahitaji ya madawati 277,865 kwa takwimu za mwisho kabla
yakuanza zoezi hilo ulikuwa unakabiliwa na upungufu wa madawati 168,354. Kukamilika
kwa madawati hayo kutauwezesha mkoa kujitosheleza kwa kila shule mtoto kukaa
juu ya daati.
Post A Comment: