MKUU WA MKOA WA MWANZA JOHN MONGELLA, AKIFUNGUA MAONESHO YA MIAKA 50 YA CHUO CHA MALIASILI CHA PASIANSI KILICHOPO MKOANI MWANZA. |
PICHA YA PAMOJA KWAAJILI YA KUMBUKUMBU NI MUHIMU PIA HAWA NI WALIMU NA WATUMISHI WENGINE KATIKA CHUO HICHO. |
MHE. MKUU WA MKOA TAFADHALI POKEA HUU MTI KWAAJILI YAKUTUWEKEA KUMBU KUMBU SAHIHI ZA MIAKA 50 YA CHUO CHETU. |
MKUU WA MKOA IKAMLAZIMU KUPANDA MTI KWAAJILI YA KUMBUKUMBU YA MIAKA 50 YA CHUO HICHO. |
MKUU WA MKOA WA MWANZA JOHN MONGELLA, AKISALIMIANA NA MMOJA WA WAKUFUNZI WA CHUO HICHO MARA BAADA YAKUWASILI CHUONI HAPO KWA AJILI YAKUZINDUA MAONESHO YA MIAKA 50 YA CHUO. |
MKUU WA TAASISI YA WANYAMAPORI CHA PASIANSI, CHA JIJINI MWANZA, BIBI LOWAELI DAMALU, WAKATI WA SHUGHULI ZA UZINDUZI WA MAONESHO YA MIAKA 50 YA CHUO HICHO. |
WAKURUFUNZI WAKIMSIKILIZA KWA MAKINI MKUU WA CHUO WAKATI AKITOA MAELEZO KUHUSU MAENDELEO YA CHUO HICHO |
BURUDANI NI SEHEMU YA SHUGHULI, HII NI BENDI YA CHUO HAPA IKITUMBUIZA KWENYE SHUGHULI HIYO. |
Akizungumza katika uzinduzi wa
maonesho ya sherehe za maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa chuo hicho
nchini Tanzania, Mongella amesema, badala ya wakurufunzi hao kwenda kufanya
mazoezi kwenye maeneo ya nje ya mkoa ambapo huwalazimu kutumia gharama kubwa,
ni vema kuanzia sasa wakaanza kutumia visiwa vyetu,
“Ndani ya ziwa viktoria, hasa huko
visiwani kuna watu wanafanya uvuvi haramu sana, hivyo ni vema wakati wa masomo
kwa vitendo, mkawa mnafanyia kwenye maeneo ambayo yamekithiri kwa uharamia na
uvuvi usio salama wala tija”, alisema Mongella na kuongeza, “lakini sio
kukomesha tuu, uvuvi haramu bali pia itachagiza kwenye suala zima la utunzaji
wa mazingira na maliasili”
Amesema kuwa, endapo taasisi hiyo
ikitumia sehemu ya mafunzo kwa vitendo, kama mkoa utakuwa hauna haja yakufunga
shughuli za uvuvi kwa msimu na badala yake itasaidia kwenye uzazi salama wa
samaki na viumbe wengine wa majini.
Kwa upande wake mkuu wa chuo hicho
bi Lowael Damalu, amemuelezea mkuu wa mkoa kuwa chuo hicho hivi sasa, kinauwezo
wakudahili wakurufunzi 415 kwa msimu mmoja, ambalo ni ongezeko kubwa
ikilinganishwa na wakurufunzi 50, waliokuwa wakidahiliwa na chuo hicho wakati
kinaanza mwaka 1966, amesema mafanikio mengine yaliyopatikana ni pamoja na
kupata ithibati ya kutoka baraza la Elimu ya ufundi, ongezeko la kozi za askari
kuwa (basic technician, Law Enforcement, uboreshaji wa maslahi ya watumishi,
mafanikio mengine ameyataja kuwa ni kuongezeka kwa miundombinu na vifaa vya
kufundishia, lakini pia taasisi kuwa na tovuti yake ya www.pasiansiwildlife.ac.tz
sambamba na taasisi kujipatia ardhi.
Mkuu huyo wa chuo amesema mbali
yakuwa na mafanikio chuo hicho bado kinakabiliwa na matatizo ya uchakavu wa
baadhi ya mabweni, uchache wa nyumba za watumishi, vilevila kutokuwepo kwa
sheria ya uanzishwaji wa taasisi sambamba na uhaba wa ajira kwa wakurufunzi
wanao hitimu katika chuo hicho.
Anaandika Atley Kuni- Ofisa habari wa mkoa wa Mwanza.
Post A Comment: