TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mkuu wa Mkoa wa
Mwanza John Mongella, amewaapisha wakuu wapya wa Wilaya za Mkoa wa Mwanza na kuwapa vitendea
kazi ikiwapo Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ilani ya Chama Tawala
Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Mwaka 2015- 2020, kwaajili ya kwenda kutimiza
wajibu wao wa Kikatiba kwenye wilaya walizo pangiwa.
Akizungumza baada
yakuwaapisha, Mhe. Mongella, amewataka waende wakasimamie shughuli za
maendeleo, kuhimiza suala la ulinzi na usalama kwenye Wilaya zao, huku akitilia
mkazo ukomeshwaji wa mauwaji ya watu
wenye Ulemavu wa Ngozi Albino pamoja na Vikongwe, amesema, ikiwa jamii ya watu
hao itapata madhara basi ni dhahiri Mkuu huyo wa Wilaya husika atakuwa
ameshindwa kusimamia majukumu yake.
Mkuu huyo wa mkoa
pia, amerudia kauli yake nakuwataka viongozi hao wapya watambue wanajukumu zito
lililoko mbele yao, ikiwa ni pamoja na kukomesha Utumiaji wa dawa zakulevya.
Aidha ameonya uchezaji wa
Pool na unywaji wa Pombe wakati
wa saa kazi, huku akimsisitiza mkuu wa
Wilaya ya Nyamagana kuhakikisha ifikapo Agosti mosi, suala la wafanya biashara
wanaofanya biashara kwenye maeneo ambayo hayaruhusiwi liwe limepatiwa ufumbuzi.
Mongella amesema,
katika Mkoa wa Mwanza, Hotel na Klabu, yeyote ile, iwe ya kawaida au ya
Kitalii, ikibainika inafanya biashara ya Shisha, hawata ivumilia na badala yake
wataifutia Leseni ya biashara.
Walio apa mbele ya
Mkuu wa Mkoa, ambao waliteuliwa na Mhe. Rais Tarehe 26, Juni, 2016 ni Emmanuel Enock Kipole, Mkuu wa Wilaya ya
Sengerema, Estomin Francis Chang’a Mkuu
wa Wilaya ya Ukerewe, Hadija Rashid
Nyembo Mkuu wa Wilaya ya Magu, wengine ni Juma Samwel Sweda Mkuu wa Wilaya ya
Misungwi, Dkt. Leonard Moses Masale Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Mary Onesmo
Tesha Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana na Mhandisi Mtemi Msafiri Simioni Mkuu wa
Wilaya ya Kwimba.
Imetolewa
na
Atley
J. Kuni
Afisa
habari na Mahusiano
Ofisi
ya Mkuu wa Mkoa.
MWANZA. 04,
Julai, 2016.
Post A Comment: