Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini |
WATU WAWILI WAFARIKI KATIKA MATUKIO TOFAUTI
WATU WAWILI wamefariki dunia Mkoani
Manyara katika matukio tofauti likiwemo la mmoja kufa maji wakati mwengine
akiokotwa huku akiwa ameharibiwa sehemu zake za siri kutokana na kubakwa na
kulawitiwa.
Akiongea na Waandishi wa Habari ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoani hapa Bw. Akili Mpwapwa alisema tukio moja lilitokea Januari 10 majira ya saa 11.30 jioni katika maeneo ya Mrara Mjini Babati mwanamke mmoja aliokotwa kwenye korongo akiwa amefariki. Alimtaja marehemu kuwa ni Mwanaisha Iddi (25) mkulima na mkazi wa kijiji cha Gichameda, ambaye alikutwa amefariki huku akiwa amechuchumaa na sehemu zake za siri kuharibiwa vibaya kutokana na kuingiliwa kwa nguvu.
Kamanda alieleza kuwa kufuatia uchunguzi wa Jeshi la Polisi Mkoani hapa mtu mmoja amekamatwa kutokana na kuhusishwa na tukio hilo ambapo ilidaiwa kuwa mtuhumiwa na marehemu walikuwa na mahusiano ya kimapenzi.
Aidha alimtaja mtuhumiwa kwa jina la John Mathayo Barani (35) mkulima na mkazi wa kijiji cha Gichameda ambapo alielezwa kuwa wana watoto wawili na siku ya tukio mtuhumiwa alimpigia simu marehemu na walikutana katika eneo hilo. Kamanda Mpwapwa aliendelea kueleza kwamba wakati mtuhumiwa alipokuwa akiendelea kumfanyia marehemu kitendo cha kumlawiti alimkaba koo mpaka akafariki na kuongeza kuwa chanzo cha tukio hilo hakijafahamika.
Wakati huohuo tukio jingine lilitokea Januari 13 majira ya asubuhi katika kijiji cha Qash, Wilayani Babati ambapo mwanafunzi mmoja wa darasa la tatu katika shule ya msingi Qash alifariki dunia wakati akiwa anaogelea katika bwawa lililochimwa kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji.
Na Alex Mchomvu.

Post A Comment: