October 2014
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

MTAALAM BWA ONUR OZLY KUTOKA WB AKITOA MCHANGO WAKE JUU YA UMUHIMU WA MFUMO GIS.









JEMA NGWALE MWAKILISHI WA DANIDA AKIZIASA HALMASHAURI KUONA UMUHIMU WA KUTENGA FEDHA ZA MAFUNZO KWA KWA AJILI YA MFUMO WA GIS UNAOTUMIKA KATIKA UKUSANYAJI MAPATO. 
Mfumo wa Ukusanyaji mapato ya Serikali katika Ngazi ya Halmashauri na majiji utakuwa wenye tija na wenye manufaa endapo Halmashauri zote nchini zitafanikiwa kuingia katika mfumo mpya wa ukusanyaji mapato kwa njia ya Kieletroniki na kuachana na mfumo wa Analogi ambao tija yake imekuwa ndogo kadri siki zinavyokwenda,
 
Haya yamebainika katika kikao kinachoendelea katika jijini Mwanza, ambapo wataalam  kutoka katika halmashauri za manispaa na Majiji yaliochini ya mpango wa TSCP wanaendelea na kikao chao kwa siku ya tatu mfulululizo.
 
Akiwasilisha mada katika kikao hicho mhasibu kutoka katika Jiji la Arusha Prosper Mlacha  amesema  kabla yakuanza kutumika kwa mfumo  mapato yalikuwa kidogo ukilinganisha na kiwango cha sasa mara baada ya kuanza kutumia mfumo wa Ukusanyaji mapato wa halmashauri kwa kutumia komputa (Local government Revenue Collection Information System) (LGRCIS) amesema, kabla ya kuanza kutumika kwa mfumo katika kipindi cha mwaka 2012/2013 makusanyo yalikuwa bilioni 5.8 na mara baada yakuanza kutumika kwa mfumo mapato yalipanda kutoka bilioni tano hadi kufikia bilioni 8.8 ambapo ni ongezeko la karibia asilimia 44.2.
 
Kwa upande wake Judith Ngulwa kutoka Jiji la Mbeya alisema mapato kwa upande wao yalipungua kutoka mwaka 2012/ 2013 katika robo ya kwanza 844,947940 na kushuka zaidi 7,52,892,452 kabla yakuanza kutumika kwa mfumo wa LGRCIS kwani  mara baada yakuanza kutumika kwa mfumo wa LGRCIS, mapato katika robo ya kwanza yameongezeka kutoka kiasi tajwa hapo juu kwani katika kipindi hicho hicho katika robo ya kwanza ya mwaka 2014 wamepanda  na kufikia   Bil. 1,778,962.
 
Kwa upande wake mtaalamu mshauri kutoka DANIDA Jema Ngwale, amezitaka Halmashauri kutenga fedha kwa ajili yaku karabati mifumo ya ili iweze kuendelea kufanya kazi, "Tusitegemee kwamba hawa wahisani wataendelea kuwepo siku zote ni lazima sasa tujifunze ili hata pale watakapo maliza muda wao basi tuendelee sisi wenyewe" alisema na kuongeza " Lakini pia tuone namna yakutenga fedha kwa ajili ya mafunzo kwa watumishi wapya lakini pia wale wa zamani kwani mifumo katika kipindi hiki cha sayansi na teknolojia inabadilika sana" aidha katika hatua nyingine ameziasa halmashauri hizo kuwa zina badilishana taarifa mbali mbali kuhusiana masuala mazima ya mfumo" Ni vema mkawa mna share Information kwa ajili yakujua wenzenu katika maeneo mengine wanafanyaje. 
 
Hadi hivi sasa halmashauri ambazo zipi chini ya mpango huo ni pamoja na Mtwara Mikindani, Mwanza, Manispaa ya Ilemela, Jiji la Arusha, Dodoma Manispaa, Dodoma CDA, Tanga pamoja na Kigoma ambayo ndio imeanza hivi karibuni.
Katika awamu ya pili jumla ya halmashauri zipatazo kumi na nane zina tarajiwa kufikiwa na mfumo  huo ili kuimairisha ukusanyaji wa mapato. Hata hivyo makao makuu itakuwa Dodoma ambapo saver itafungwa kwa ajili yakuwezesha mfumo.

FATILIA KWA PICHA ZAIDI HABARI HII.

BI JUDITH NGULWA KUTOKA MANISPAA YA MBEYA  AKITOA MADA JUU YA MATUMIZI YA GIS KWENYE HALMASHAURI JIJI LA MBEYA.


WASHIRIKI WAKIWA WANAFATILIA KWA MAKINI MADA ZILIZOKUWA ZIKIWASILISHWA PICHANI NI BI ZAINAB NGONYANI NA NEPHA,

JABRI SHEKIMWERI WA POM-RALG,AKITOA MADA JUU YA MFUMO WA GIS KATIKA HALMASHAURI.


BRUNO MLACHA AKIELEZA JINSI JIJI LA ARUSHA LILIVYO FANIKIWA KUTOKANA NA MFUMO WA GIS.

VITUS KAKOKO AKITOA MADA NA KUELEZE JINSI MANISPAA YA MTWARA ILIVYO ANZA KUNUFAIKA MFUMO MPYA WA UKUSANYAJI MAPATO.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Kwa hisani ya Mdau G. SENGO!

KAMA UNADHANI MIUJIZA ILIKUWA WAKATI ULE HADI HII LEO IPO, MSUKUMA HUYU KACHIMBIA
KICHWA KWENYE MCHANGA KWA DAKIKA KADHAA, MBWEMBWE ZA MCHEZO TU HAPOA

Mbunge wa Jimbo la Kisesa (CCM), Luhaga Mpina akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mwandu Itinje wilayani Meatu mkoani Simiyu, waliofika eneo hilo kushuhudia mpambano ulioandaliwa na mbunge huyo wa ngoma za asili ya watu wa kabila la Wasukuma kati ya Malogi Hamsini na Magise Jilunga.
MBUNGE wa Jimbo la Kisesa(CCM), Luhaga Mpina ameahidi kuendelea kuenzi utamaduni wa ngoma za kabila la wasukuma kwani zimekuwa ni sehemu ya kuimarisha mshikamano miongoni mwa jamii hiyo.
Mpina alitoa kauli hiyo juzi wakati akifunga mpambano wa ngoma za asili katika Kijiji cha Mwandu Itinje wilayani Meatu mkoani Simiyu uliwakutanisha Malogi Hamsini Mgika na Magise Jilunga Mgalu.

Hata hivyo katika mpambano huo ulihudhuriwa na watazamaji zaidi elfu nane kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Simiyu ambapo Magise Jilunga aliibuka mshindi baada ya kumbwaga Malogi.

Akizungumza mara baada ya mpambano huo, Malogi Hamsini alikubali kushindwa na mpinzani wake na kueleza kuridhika na uamuzi uliofanywa na kuomba kukutanishwa tena siku nyingine na mpinzani wake huyo.

Naye Magisa Jilunga alisema pamoja na kumshinda mpinzani wake lakini alikiri pambano hilo lilikuwa gumu kwake na kuamba nae pia kurudiana ombi ambalo lilikubaliwa na Mbunge wa jimbo hilo.

Pambano hilo lililodhaminiwa na Mbunge Mpina lilivuta hisia za mashabiki wengi na kuomba kufanyika mara kwa mara kwa pambano hilo kwani linaleta umoja na mshikamano miongoni mwa jamii.

Mpina aliwazawadia shilingi milioni moja kila mmoja katika mpambano huo na kuahidi kudhamini tena pambano lingine kama hilo baadae mwakani.ZAIDI BOFYA PLAY KUSIKILIZA YALIYOJIRI
Wachezaji wa ngoma toka kundi la Malogi Hamsini ambaye ni Mgika wakifanya yao.
Mbunge wa Jimbo la Kisesa (CCM), Luhaga Mpina akipiga ngoma kuashiria ufunguzi wa mpambano wa ngoma asili kati ya Malogi Hamsini na Magise Jilunga.
Kiongozi wa Wagika, Malogi Hamsini (kulia) akiwa amesimama barabara kuuanza mpambano ambapo alizidiwa nguvu ya uchawi na Mpinzani wake Magise Jilunga ambaye Mgalu.
Wachezaji wa kundi la Malogi Hamsini wakionyesha kazi.
Mara baada ya kuona ameshindwa katika nguvu za kichawi Malogi Hamsini alipandwa na hasira ampazo alizielekeza kweye tunguli zake.
Na hapo ndipo alipo amua kuziteketeza kwa kuzifumua kwa mateke..... PwachAaA!!
Wingi wa watu ndiyo pointi za ushindi watu walihama toka kwa Malogi Hamsini na kuelekea kwa Magise Jilunga ambapo kila mmoja alikuwa akipiga ngoma kwa wakati mmoja (yaani kulia na kushoto wapi pananoga?).
Wananchi wakiwa wameizunguka himaya ya Magise Jilunga.
Kiongozi wa Wagalu, Magise Jilunga wa pili kutoka kushoto akiwa tayari kulianzisha kwenye mpambano kati yake na Malogi Hamsini ulioandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Kisesa Luhaga Mpina.
Hatari kama anaporomoka vile...
Malogi Hamsini alituma nyoka kuja kuharibu ngoma ya Magise Jilunga lakini hakufua dafu.
Mapanga dizaini....
Akinamama wakiingia kwenye lango kuu kushuhudia mpambano.
Michezo ya hatari balaa ni mwendo kugalagala kwenye moto.
Silaha ya ushindi kwa Magise Jilunga ilikuwa ni kubadilika badilika.
Si kubadilika tu bali alikuwa na vionjo kama kuoga moto mchana kweupe na kunywa mafuta ya dizeli...tobA!
Ni balaa mwanawane!!!
Jamaa aliamua kukizika kichwa kwa dakika kadhaa kiasi cha kusisimua mashabiki!!
Kiongozi wa Wagalu, Magise Jilunga akipiga ngoma kuusaka ushindi.
Viongozi wa kada mbalimbali nao wamo.
Mbunge wa Jimbo la Kisesa (CCM), Luhaga Mpina akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mwandu Itinje wilayani Meatu mkoani Simiyu, waliofika eneo hilo kushuhudia mpambano ulioandaliwa na mbunge huyo wa ngoma za asili ya watu wa kabila la Wasukuma kati ya Malogi Hamsini na Magise Jilunga.
Maelfu waliofika eneo hilo kushuhudia mpambano ulioandaliwa na Mhe. Mbunge, ngoma za asili ya watu wa kabila la Wasukuma kati ya Malogi Hamsini na Magise Jilunga.
Ni wakati wa jaji Mkuu kutangaza matokeo rasmi:- Mpambano wa ngoma za asili ya watu wa kabila la Wasukuma kati ya Malogi Hamsini na Magise Jilunga.
"Mshindi ni Magise Jilunga...!!"
 Malogi Hamsini (kushoto) akimpongeza kiroho safi Magise Jilunga mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi....
Full m-banano.
Mbunge wa Jimbo la Kisesa (CCM), Luhaga Mpina akiwaaga wananchi wa Jimbo lake mara baada ya kumalizika mpambano.
Mbunge wa Jimbo la Kisesa (CCM), Luhaga Mpina akiwaamezungukwa na maelfu ya wananchi waliofika eneo la uwanja wa kusanyiko.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
NDG. ZUBERI M. SAMATABA, KAIMU KATIBU MKUU- OWM-TAMISEMI. ALIPOKUWA AKIFUNGUA MKUTANO HUO .
 
Halmashauri za majiji na manispaa zimehimizwa kutunza na kuhifadhi miradi yote ya maendeleo inayo tekelezwa katika maeneo yao na kuhakikisha inadumu kwa manufaa ya kizazi cha leo na kijacho.
 
Kauli hiyo imetolewa mapema hivi leo na Zuberi Samataba, Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) katika hoteli ya Gold Crest Jijini Mwanza wakati wa kikao cha pamoja baina ya TAMISEMI, Benki ya Dunia (World Bank), DANIDA na watendaji kutoka halmashauri zinazo tekeleza miradi ya Tanzania Strategic Cities Project (TSCP).
 
Samataba, amesema, kuna haja kwa kila halmashauri kuhakikisha inatunza miradi yote ambayo inafadhiliwa na wahisani hata baada ya wahisani kumaliza muda wao na kuondoka  kisha  miradi hiyo kukabidhiwa mikononi mwa Halmashauri. "Nivema mkawa  mnatenga fedha kwa ajili yakuhudumia miradi inayo anzishwa na wafadhili kwa ajili ya ukarabati na kuimarisha  ili iendelee kudumu kwa muda mrefu hata baada ya miradi hiyo kuisha muda wake na wafadhili kuicha mikononi mwetu".
 
Katika hatua nyingine  amewaagiza watendaji hao kutoa taarifa kwa wakati ili kujenga imani kwa wafadhili wanao toa fedha zao kwa ajili ya miradi mbali mbali ya maendeleo wanayo ifadhili, "Wenzetu suala la mrejesho ni muhimu sana lakini zaidi sana mrejesho kwa wakati,  kwani  ni kama wanasheria wanavyo amini kuwa HAKI ILIYO CHELEWESHWA NI HAKI ILIYO NYIMWA". kwa mantiki hiyo kutoa taarifa kwa wakati ni suala muhimu sana,  vinginevyo au kinyume chake nikuwafanya wafadhili kupoteza imani kwa wanao wafadhili kwenye miradi amesema na kuongeza kuwa kwakuwa serikali inaondoka kwenye utendaji wa kawaida na kuelekea kwenye utendaji wa upimaji ufanisi kwa matokeo (Performance for Result ) hivyo moja ya kigezo muhimu kitakachotumika katika   kupima matokeo ni uwasilishaji wa taarifa kwa wakati.
 
Kikao hicho cha siku tatu kina wakutanisha Watendaji kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Halmashauri Jiji la Mwanza , Manispaa ya Ilemela, Manispaaya Kigoma Ujiji, Manispaa ya Dodoma, (CDA), Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Halmashauri ya mikindani Mtwara, Jiji la Tanga, Jiji la Arusha pamoja na wawakilishi wa DANIDA sambamba na  World Bank.
 
Hapa fatilia habari picha
BIBI JEMA  NGWALE - MWAKILISHI WA DANIDA ALIPOKUWA AKITOA SALAM KUTOKA DANIDA NA UMUHIMU WAKUTUMIA KWA USAHIHI FEDHA ZA WAFADHILI.



(Eng) Ezekiel Magoti Kunyaranyara.  WA JIJI LA MWANZA , AKIWASILISHA MADA KATIKA MKUANO HUO KUHUSU UTEKELEZAJI WA MIRADI YA TSCP.


MR. ONOUR OZLY- MWAKILISHI WA BENKI YA DUNIA (WB), ALIPOKUWA AKITOA MALEZO MAFUPI KUHUSU LENGO LA MKUTANO HUO.
 
MKURUGENZI WA JIJI LA MWANZA HALIFA HIDA, AKITOA SALAM ZA UKARIBISHO KWA WAJUMBE WA MKUTANO HUO KABLA YA MKUTANO HUO KUANZA.
KUTOKA KUSHOTO NI MHANDISI JOHN BUTINDI(RS-MWANZA), Ezekiel Magoti Kunyaranyara. (Eng,REHEMA AHMED MRATIBU WA TSCP KATIKA JIJI LA MWANZA NA PASCHAL MZINGA   WAKIFATILIA KWA MAKINI KIKAO HICHO.
MHANDISI DAVIS SHAMANGAL AMBAYE NI MRATIBU WA MIRADI YA BENKI YA DUNIA, AKIPIA MOJA YA VITABU VYENYE MKUSANIKO WA MIRADI INAYOTEKELEZWA NCHINI KOTE.

BAADHI YA WASHIRIKI WA MKUTANO HUO WAKISHANGILIA JAMBO WAKATI MADA ZILIPOKUWA ZIKIWASILISHWA.



 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Hakika ilikuwa simanzi pale mwili wa marehemu Dkt. William Shija ulipokuwa ukiagwa katika safari yake ya mwisho. Makamu wa Rais akimuelezea Dkt. Shija alisema alikuwa ni mtu wa vitendo na aliyaamini yale aliyo yasimamia huku akitolea mfano suala la uwanzishaji wa TCU taasisi ambayo inahusika na wanafunzi wanaotaka kujiunga na elimu ya Vyuo vikuu.
 
Naye Spika wa Bunge la Tanzania mama Anne Makinda, alisema marehemu Dkt. Shija, aliamini kuwa siasa sio ugomvi bali siasa inatakiwa itumike kufanya wengine kuwajibika kwa tija na manufaa kwa umma.
 
Akihubiri katika Ibada ya mwisho Paroko wa Parokia hiyo alisema, Dkt. William Shija alitumia nafasi yake kwa jamii yake na sio kujinufaisha kama ilivyo kwa viongozi wa leo, kwani viongozi wengi wa leo imekuwa kinyume kwa kujijali zaidi wao kuliko jamii wanazo zitumikia, huku akitolea mfano wa uwekaji Umeme katika mji wa Nyampande ambapo Mhe Shija alianza kupeleka Umeme kwenye nyumba za Ibada kabla hata ya kuunganisha Nyumbani kwake.
 
.

Hapa chini fuatilia kwa karibu kwa njia ya picha matukio yalivyo kuwa.





MWILI WA MAREHEMU DKT. WILLIAM SHIJA UKIWA UMEHIFADHIWA NA IBADA IKIENDELEA.
 






VIONGOZI WA SERIKALI WAKIWA KATIKA VYUSO ZA HUZUNI WAKATI WA MSIBA WA WILLIAM SHIJA.

MJANE WA  MAREHEMU PAMOJA NA WATOTO WAKIWA KATIKA  SIMANZI NZITO WAKATI WA IBADA YA MWISHO KWA MAREHEMU DKT WILLIAM SHIJA.

HILI NDILO KANISA LA KWANZA KUWEKEWA UMEME KATIKA KIJIJI CHA NYAMPANDE IKIWA NI SEHEMU YA UTUME ALIO UFANYA DKT. WILLIAM SHIJA AKIWA MBUNGE WA SENGEREMA MIAKA YA 90'S.

MAKAMU WA RAIS AKITOA HESHMA ZA MWISHO KWENYE MWILI WA MAREHEMU.

SPIKA WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ANNE MAKINDA AKITOA HESHMA ZA MWISHO.

HAPA NI WAZIRI WA NCHI OFISI RAIS BUNGE SERA NA URATIBU.

MKUU WA MKOA WA MWANZA EVARIST NDIKILO AKITOA HESHMA ZA MWISHO.

DKT. TIZEBA NAIBU WAZIRI UCHUKUZI AKITOA HESHMA ZA MWISHO.

ZITTO KABWE MBUNGE WA KIGOMA KASKAZINI AKITOA HESHMA ZA MWISHO MBELE YA MWILI WA MAREHEMU.


MHE. ZITTO KABWE ALIPOKUWA AKISOMA WASIFU WA MAREHEMU DKT. SHIJA.

WAOMBOLEZAJI WAKIWA WANASIKILIZA MAHUBIRI.


WATOTO WA MAREHEMU WAKITOA YALE AMBAYO WALIHUSIWA NA MAREHEMU BABA YAO DKT. WILLIAM SHIJA, WAKISEMA ALIPENDA DINI NA ELIMU.

BWANA WETENGULA MWAKILISHI KUTOKA NCHINI KENYA NAYE ALIFIKA KWA AJILI YAKUWAKILISHA NCHI YAKE NA BUNGE WALILOKUWA WAKILITUMIKIA NA DKT. SHIJA..

SAFARI YA MWISHO ILIVYO ANZA KWENDA KWENYE NYUMBA YA MILELE.

MHE. DKT. BILALI AKIWEKA SHADA LA MAUWA KWENYE KABURI LA DKT. WILLIAM SHIJA, ALIPO IWAKILISHA SERIKALI KATIKA MSIBA HUO.