January 2014
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

·       Leo kujadili Taarifaya halmashauri ya Jiji kwa mara ya pili.

·       Jengo la Uwekezaji latengewa siku yake.
Na Atley Kuni- Mwanza.


Hapa Mheshimiwa Kigwangala Mwenyekiti wa Kamati akiwa amepanda yeye na Wabunge
wenzake, katika Tanki la Maji katika Kijiji cha kayenze.
Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na serikali za Mikoa(TAMISEMI), hapo jana ili endelea na ziara katika halmashauri ya jiji, huku ikianzaidi kwenye  miradi inayosimamiwa na halmashauri ya Jiji la Mwanza na baadae leo itakutana na kwa mara ya pili na watendaji wa Halmashauri hiyo wakingozwa na Mkurugenzi wao Halipha Hida na Wenyeviti kwa ajili ya kufanya marejeo ya taarifa mara baada yakutoa maelekezo ya kufanyia kazi.

Kwa mujibu wa habari ambazo mtandao huu imezipata, hapo jana Timu hiyo inayo ongozwa na Mhe. Kigwangala(MB) ilitembelea miradi ya Usambazaji wa maji katika Kijiji cha Kayenze, Ujenzi  wa kituo cha kukusanyia, kupozea na kuuza maziwa katika Kata ya Mkolani, kikundi ambacho kinamilikiwa na UWAMKO, miradi mingine iliyotembelewa hapo jana ni mradi wa kuongeza thamani ya mazao ya nafaka kwenye kata ya Buhongwa.

Ukaguzi wa bara bara.
 
Mtoa taarifa wetu ametueleza kwamba, miradi  mingine iliyotembelewa na wabunge hao ni matengenezo ya bara bara ya mawe Capripoint Nyakurunduma, barabara ya majengo mapya, Kiwanda cha bia Pasiansi

Tunaendelea na Ujenza

Lumala  kijiji cha kiloleli, vile vile  kama haitoshi na hali ya mshangao mkubwa , wabunge hao, waliomba kubadishiwa uelekeo baada ya kumaliza kukagua miradi waliyo pangiwa na wakaomba kwenda Shule ya Sekondari Mahina, ambapo kuna mradi wa ujenzi wa madarasa 3 yanayo tekelezwa na TASAF sambamba na kituo cha Afya makongoro ambacho kilijengwa baada ya kubomolewa kile kilicho kuwapo katika bara bara ya Airport.

Kwa mujibu wa ratiba yao wabunge hao hivi leo wanaendelea na Ziara yao hiyo, lakini hivi leo wakijikita zaidi katika kupokea Taarifa ambayo hapo juzi waliikataa na wakaomba ikafanyiwe marekebisho.

Katika hatua nyingine kamati hiyo itakutana siku ya kesho kujadili na kutathmini mgawanyo wa mali za Jiji na Ilemela, ambazo zimekuwa na kizungumkuti tangu kutenganishwa kwa Halmashauri hizo mbili.
Mkoa wa Mwanza wenye Halmshauri saba za Wilaya zinategemea kufikiwa na kamati hiyo, ambayo inashughulika zaidi na Mamlaka za mikoa pamoja na Halmashauri.
Zaidi ona katika picha ziara ilivyokuwa.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

Na Julius Kithuure, Nairobi.

MAMBO YA UGATUZI KENYA.
Kadri serikali za kaunti za Kenya zinapokaribia adhimisho ya mwaka mmoja, raia wasema wamekutana na ucheleweshaji zaidi wa huduma kuliko faida kutokana na ugatuzi wa madaraka na mfumo mpya umeshindwa kufikia matarajio.

Francis Mokaya, ambaye anamiliki duka dogo katika kaunti ya Kisii na majengo matatu ya ghorofa ya makaazi katika mji wa Kisii, alisema alitarajia huduma mara tu gavana alipoapishwa kuingia katika kazi mwezi Machi uliopita.

"Nilitumaini kwamba hadi sasa majosho mengi yaliyoharibika yangekuwa yamekarabatiwa lakini kwa bahati mbaya, hakuna kilichotokea na inaonekana nitasubiri kwa muda mrefu," alisema Mokaya, ambaye pia anamiliki mifugo, kama zilivyo familia nyingi za vijijini." Sina jinsi nyingine zaidi ya kunyunyuzia dawa mifugo yangu nyumbani ambayo ni ghali na inatakiwa jitihada."

Majosho ya ng'ombe, ambayo ni ya kawaida katika maeneo ya vijijini, ni mashimo marefu ambapo mifugo wanatumbukia katika maji ambayo yana kemikali za kuua kupe na vimelea vingine.

Mokaya alisema serikali ya kaunti pia inazuia mapato yake ya kodi kwani haijawahi kutoa viwango vya kodi kwa huduma na umiliki wa mali, ambayo matokeo yake inazifanya zishindwe kutoza vizuri wapangaji wake.

Sijui ni kiasi gani ninapaswa kutoza kwani sijui tozo gani ambazo serikali ya kaunti [itanitoza] mimi," Mokaya alisema.

Kero ya Mokaya inawakabili wakaazi wengi nchini kote Kenya. Kaunti nyingi hazijajadili na kupitisha viwango vya mwisho vya kodi kama ilivyoelezwa katika miswada yao ya fedha ya 2013, ambayo imewapa mamlaka kusimamia kodi, tozo na adhabu kwa wasiolipa.

"Inachanganya, lakini nina matumaini kwamba wajumbe wa baraza la Kaunti watatoa kipaumbele katika kupitisha miswada hii ambayo imecheleweshwa baada ya [wajumbe wa baraza la kaunti] kugoma mwezi Novemba kudai kuongezewa mishahara ," alisema Charity Ngina, mwenye umri wa miaka 37, mfugaji wa kuku huko Nyandarua.

Ngina alisema ana matumaini ya kuongeza bei yake mara tu serikali ya Kaunti ya Nyandarua itakapoamua kiasi cha tozo anachopaswa kulipa kwa ugugaji wa ndege.

Kukosekana kwa mipango, uwekaji vipaumbele

Stephen Manoti, mbunge wa jimbo la Bobasi katika Kaunti ya Kisii, alisema maendeleo ya polepole katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika nchi nyingi hutokana na kukosekana kwa mipango mizuri na uwekaji wa vipaumbele.

"Magavana wengi na wajumbe wa mabaraza ya nchi hawana nyaraka za kutunga sheria au nakala kwa ajili ya matamko yao. Malengo yao yalikuwa kwanza kupata mamlaka, kisha mambo mengine yatafuata -- na hii ndiyo sababu wanapambana kuweka miradi yoyote ya maendeleo yenye mafanikio, lakini wanahitaji kulenga upya na kuweka mikakati," aliiambia Sabahi.

Damaris Wanja, mama wa watoto watatu mwenye umri wa maiaka 51 na mmiliki wa mgahawa huko Machakos, alisema hakuwa na furaha kutokana na kushindikana kwa maendeleo katika nchi yake.

"Gavana wangu, Dkt. Alfred Mutua, ameanzisha miradi ya mabilioni ya shilingi kujenga mji mpya wa Machakos kuanzia chini. Ninamkosoa kwa hili," alisema. "Je, tunahitaji jiji la kisasa wakati nchi haina maji ya kutosha [na] vituo vya afya vipo katika hali mbaya vikiwa na dawa muhimu chache? Hapana. Tunahitaji miradi ya umwagiliaji kusaidia upatikanaji wa kudumu wa vyakula na umeme vijijini kuwezesha vijana kuanzisha biashara ndogondogo."

Katika Kaunti ambazo kuna sera ya kodi, wananchi kama wajumbe wa baraza hawaachi kushauriana na jamii na kulumbana hadharani kuhusu sera kabla ya kutoa mamlaka ya kodi mpya.

Serikali ya Kaunti ya Kiambu imependekeza kuwatoza wakulima kodi ya shilingi 2,000 kwa kila eka ya ardhi wanayolima, kuleta upinzani kutoka kwa wakulima wadogo kama David Kariuki mwenye umri wa miaka 43.

"Kodi hizi na adhabu zinaanzisha vikwazo visivyo vya lazima kwa wafanyabiashara. Wanaadhibu na kuumiza uwekezaji," aliiambia Sabahi. "Je, wanasema kuwa ninapaswa kuacha na kutoilima ardhi yangu? Hii si kukatisha tamaa kufanya kazi kwa bidii na kualika njaa nchini?"

Kariuki alisema alitarajia serikali kuanza jitihada kama vile za kuwapa wakulima miche inayotoa mazao mengi, mbolea za msaada na upatikanaji wa kilimo cha kutumia zana rahisi za kilimo, badala ya kuanzisha "ushuru wa kuturejesha nyuma kwa ajili tu ya kukusanya fedha zaidi, ambazo hazimfaidishi mtu wa kawaida".

Kariuki aliliomba bunge la taifa na seneti kubana bajeti na kudhibiti matumizi katika kaunti 47 na kuanzisha kamati ya usimamizi kufuatilia matumizi ya kaunti ili "fursa za mabadiliko yaliyokusudiwa kwa ajili ya watu wa kawaida yasidharauliwe wala kupotea".

Serikali za mitaa zinapaswa kuanzia chini

Hata hivyo, magavana wa kaunti ambao walizungumza na Sabahi walipinga malalamiko hayo, wakisema kuanza taratibu ilikuwa ni kwa sababu ya urefu wa muda iliotumia kupokea rasilimali kutoka katika serikali ya taifa na kupanga miundo ya serikali za kaunti kwa mara ya kwanza.

Sasa ofisi hizo na wafanyakazi wake tayari wapo, magavana walisema wapo tayari kusongesha mbele huduma na utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambayo wananchi wamekuwa na wakiitarajia kwa shauku, kama vile ujenzi wa barabara, kukarabati shule, masoko na taasisi nyingine za serikali, uanzishaji wa mikopo isiyo na riba na misaada, maendeleo ya kilimo na programu za kuanzisha ajira.

Gavana wa Kaunti ya Meru Peter Munya aliiambia Sabahi anasikitika kwamba maendeleo yaliyotarajiwa bado hayajakamilika, lakini alizitetea serikali za mitaa, akisema zilipaswa kuimarisha utawala wake kuanzia chini.

"Ni kweli bado hatujatekeleza sera yoyote kuhusu kilimo, usafirishaji, leseni za biashara, usafi wa mazingira, elimu ya shule za awali na vituo vya afya, ambavyo ni mamlaka muhimu zinazoangukia katika serikali za kaunti," alisema.

Lakini sasa, kwa kuwa na mabaraza ya kaunti yanayofanya kazi, kupitisha bajeti za mwaka, wafanyakazi na fedha, watu wataanza kuona tofauti na mabadiliko waliyokuwa wakiyatarajia, alisema Munya.

"Kwa Hazina ya Taifa kutoa shilingi bilioni 20 (Dola milioni 233) katika serikali ya kaunti Alhamisi tarehe 16 [Januari], tupo tayari kuanza kutekeleza miradi kama ukarabati wa masoko, zahanati na barabara," alisema

 
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.


·      Kamati ya Bunge yagomea Taarifa.
·        Wapewa saa 15, kuwasilisha mbadala wa Taarifa.

Wataalam wa Sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza na mmoja kutoka TAMISEMI wakiwa wanafatilia kwa karibu mambo yanavyojiri wakati Kamati hiyo ilipokuwa inafafanua sehemu ambazo haikuridhika nazo.


Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza akinukuu baadhi ya mambo.
Na: Atley Kuni- Mwanza.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida hapo jana kamati ya Bunge ya kudumu inayohusika na Wizara ya Tawala za Mikoa na  Serikali za Mitaa (TAMISEMI), iligomea kuipokea taarifa ya fedha na Miradi ya halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa madai kwamba fedha ambazo zilipaswa kupelekwa kwenye miradi ya wananchi
Hapa Kaimu katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Bw. Ndaro Kwilijira (kulia) akiwa ananukuu mambo yanayo jitokeza, kutoka kushoto ni Naibu Meya wa Jiji la Mwanza Mhe. Minja na katikati ni Diwani wa  Igoma Mhe. Chagulani. wakati wa kikao hicho.
zilitumika ndivyo sivyo.
Akisoma kwa niaba ya kamati Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Hamis Kigwangala alisema fedha ambazo zilipaswa kupelekwa kwenye miradi ya maendeleo ya wananchi zimetumika kwa ajili ya shughuli za kiutawala na sio  miradi iliyokusudiwa, huku akihoji kutokuwepo na mchanganua wa fedha hizo na jinsi zilivyo ingia na kwenda kwenye matumizi. “ kwa hiyo hata fedha ndogo iliyokuja kwa ajili ya kutekeleza mradi wa shule ya msingi Lwamnyima, ambao ulikuwa unahitaji shilingi milioni 31 kwa ajili ya nyumba za walimu hazikupelekwa na badala yake zikawekwa kwenye shughuli za Administration” anasema na kuongeza “hivyo wajumbe wa kamati wanahoji uchungu wa nyie watumishi wa jiji katika kuwaletea wananchi maendeleo”.
Kipengele kingine kilicho zua utata ni cha kuandaa mpango mkakati wa jiji la Mwanza, ambapo wajumbe walisema fedha iliyokuwa imepangwa kwa ajili ya shughuli hiyo ilipokelewa na ikatumika lakini cha ajabu matumizi ya  fedha hiyo nayo ilielekezwa  kufanya shughuli za kiutala.
Mabali ya matuymizi hayo kamati hiyo pia ilihoji juu ya fedha za mgao katika ngazi za Kata kuwa, kwa mujibu wa taratibu za fedha ugawaji wa fedha kwenye kata hufanyika kwa kuzingatia vigezo ambavyo halmashauri husika imejiwekea, na suala la  idadi ya watu ikitajwa kama kigezo muhimu katika ugawaji wa fedha, kinyume na jiji la Mwanza ambao wao wamekuwa wakigawa fedha kwa uwiano ulio sawia bila kuzingatia idadi ya watu, hivyo kamati hiyo ikaomba ufafanuzi wa vigezo vilivyo tumika kugawa, milioni tano tano kwa kila wilaya bila kujali ukubwa wa kata na Idadi ya watu waliopo kwenye kata husika.
Kama hiyo haitoshi kamati hiyo ya Bunge ilienda mabali zaidi na  kuhoji juu ya makadirio madogo ya makusanyo ya ndani na jinsi fedha hizo zinavyo ishia mikononi mwa watu wachache bila kuwapelekea wananchi maendeleo, huku akitolea mfano mwaka uliopita kwamba, Halmashauri ya Jiji la Mwanza ilipanga katika bajeti yake kukusanya Bil. 2.6 katika mwaka wa 2012/ 2023 lakini katika jambo la kushangaza ikakusanya kiasi cha Mil. 494 tu ambayo alisema ni asilimia ndogo sana kama 20% tu. “hakuna walakini,? Alihoji Kigwangala… “Tunafahamu watumishi wa halmashauri mnakula sana fedha za (Own source), na mnafanyaje nikwa ku fluctuate makusanyo ya ndani” alisema kwa msisitizo.

Mwishoni Mwenyekiti huyo wa kamati, alimuomba Mhe.Wilaya ya Ilemela, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana pamoja na Mhe. Mkuu wa Mkoa Mwanza kukutana na kamati hiyo ili kujua mgongano wa kiutawala uliopo baina ya Halmashauri Jiji na Ilemela, kwakuwa suala la mgawanyo wa mali baina ya Halmashauri ya Jiji na Ilemela havikuwa sawa na kwamba kuna hoja zilizo ibuka kutoka Ilemela juu ya uwiano usio sahihi, “ile instrument wakati mnagawana mali ilikuwa ina eleza wazi juu ya zitakazo kuwa mali za Ilemela na zile zitakazokuwa za Jiji, lakini kwa malalamiko tunayo yapata kutoka Ilemela kwamba baadhi ya miradi iliyopaswa kuwa Ilemela bado ipo Jiji”, anasema Kingwangala na kuongeza “hata kama ikiwezekana tubadilishe
 
structure ya kiutawala”

Akihitimisha mwenyekiti huyo alisema, kwa maana hiyo wao kama wajumbe wa kamati wamepitia na hawajaridhishwa na kwa mantiki hiyo wakatoa muda usiozidi saa 15 ili wapatiwe majibu ndipo waweze kuendelea na shughuli zao katika Wilaya zingine.
 
Kamati hiyo ipo Mkoani mwanza kwa ajili ya kupitia shughuli mbali mbali za maendeleo na kuona jinsi wananchi wanavyo hudumiwa katika kutekeleza suala la utawala bora wa watu.
Awali Nyakati za asubuhi siku ya jana Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi  Evarist Ndikilo, aliwapokea na kuwapa taarifa fupi kuhusu hali ya Mkoa na shughuli zinazofanyika mkoani hapa ikiwa ni pamoja na jitihada zilizopo katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Mkoa wa Mwanza.


 
no image
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Kamati za Bunge zinazo shughulikia masuala ya Nishati pamoja na Serikali za Mitaa, zinategemewa kukutana na uongozi wa mkoa wa Mwanza hivi leo.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo kuninewsblog imezipata, imesema lengo kuu la kukutana na uongozi wa Mkoa wa Mwanza ni pamoja na kukagua shughuli mbali mbali za maendeleo zinazo tekelezwa mkoani hapa.

Habari zimesema kwamba, kamati hizo zitafika nyakati za asubuhi na kuonana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza pamoja na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza na baadhi ya watendaji katika sekretarieti ya mkoa wa mwanza na badae watakwenda halmashauri ya Jiji kabla ya kwenda kukagua Miradi ya Maendeleo.

Miradi inayotazamiwa kutembelewa ni pamoja na Ujenzi wa bara bara za mradi wa TSCP ambao ni watekelezaji wa ujenzi wa bara bara za lami katika jiji la Mwanza na majiji mengine matano ya Tanzania.

Endelea kufatilia kuninews kwa habari hizi na zingine...
no image
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

 

Na: Bosire Boniface, Garissa

Maofisa wa Kenya wamepuuza Ripoti ya Dunia ya hivi karibuni kabisa ya kila mwaka ya shirika la haki za kibinadamu la Human Rights Watch (HRW), ambayo ilitoa tathmini ya ukosoaji uliyo mkali kabisa kuhusu maendeleo na kinga ya haki za binadamu nchini Kenya kwa mwaka uliopita,

Hatua ya taratibu ya mabadiliko ya polisi nchini Kenya, utamaduni wa kutoadhibiwa kwa unyanyasaji unaofanywa na vikosi vya usalama na serikali kushindwa kuwawajibisha wakosoaji wa vurugu za baada ya uchaguzi wa 2007-2008 kumebakia kuwa kero kubwa, kwa mujibu wa ripoti hiyo.

Miongoni mwa mambo mengine, ripoti hiyo ilihoji kiwango cha ushirikiano wa serikali na Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Uhalifu wa Kivita (ICC) katika uhalifu dhidi ya ubinadamu wa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na Makamu wa Rais William Ruto.

"Serikali ya Rais Uhuru Kenyatta na makamu wake, William Ruto, imekuwa ikitumia ushindi wake mdogo wa kura asilimia 50.7 ikikwepa duru ya pili ya uchaguzi kusambaza rasilimali zote za nchi katika kusimamisha mashtaka yao kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Uhalifu wa Kivita kwa majukumu yao ya uongozi yanayodaiwa katika vurugu za baada ya uchaguzi wa 2007-08," ripoti hiyo inasema.

"Kenya iliapa kuendeleza ushirikiano na ICC, lakini kutoka uchaguzi, serikali mpya imepiga kampeni kubwa katika Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kufutwa kwa mashtaka yao, kuahirishwa au kupelekwa katika njia za sheria za ndani," inasema.

Katika kujibu, Waziri wa Mambo ya Nje Amina Mohamed aliitaja ripoti ya HRW kuwa "ya kukasirisha na isiyoeleweka".

"Kwamba nchi haishirikiani na ICC siyo kweli kabisa," aliiambia Sabahi. "Mahudhurio ya Makamu wa Rais Ruto katika mahakama wakati anapohitajika ni ushahidi kwamba kuna ushirikiano. Rais Kenyatta hajasema kwamba hatahudhuria kesi yake wakati itakapofikia kusikilizwa mwezi Februari."

Bado mashtaka ya Kenyatta, ambayo yamepangiwa kuanza tarehe 5, Februari, yameairishwa bila kuja siku ya kuendelea baada ya Mwendesha mashtaka mkuu Fatou Bensouda kutaka muda zaidi kukusanya ushahidi na utetezi kuomba kusimamisha mashtaka.

"Kesi za ICC nchini Kenya zimekuwa zikizuiwa na kujitoa kwa mashahidi wa mashtaka, ikituhumiwa kwa sababu ya rushwa na vitisho; walalamikiwa pia wametuhumu kuharibiwa kwa ushahidi au vitisho kwa mashahidi," ripoti hiyo ilisema, ikiongeza kwamba mwendesha mashtaka wa ICC alikiita kiwango cha kuwachezea mashahidi katika kesi kuwa "hakijawahi kutokea".

Kwa kampeni ya Kenya kujitoa katika ICC  na kuziomba nchi nyingine za Umoja wa Afrika kufanya hivyo, Mohamed alisema kulifanyika ndani ya muundo wa sheria za ndani na za kimataifa.

Kenya inafuata taratibu zote zinazofaa katika hatua hiyo "kwa uwazi na sio kwa siri," Mohamed alisema. "Waandishi wa ripoti hiyo wana ajenda ya siri lakini tutaendelea na uhusiano unaojenga na ICC."

Polisi wa Kenya watuhumiwa

Polisi pia ilipuuza matokeo ya ripoti ambayo ilituhumu vikosi vya usalama kwa mauwaji ya bila kushtakiwa, mateso na ukiukaji mwingine wa haki za binadamu.

"Utafiti uliofanywa na Tume ya Haki za Binadamu ya Kenya uligundua kwamba polisi waliwaua kinyume cha sheria watu 120 kati ya Mei na Agosti 2013 katika hali ambayo ingeweza kuzuilika, na kwamba polisi haikuripoti mauaji hayo kwa mamlaka ya kiraia inayoisimamia, Mamlaka Huru ya Usimamizi ya Polisi, kwa ajili ya uchunguzi kama inavyotakiwa chini ya sheria," ripoti ilisema.

Ripoti hiyo pia iliitaja polisi kwa "mateso, upoteaji, na mauaji kinyume cha sheria ya wanaotuhumiwa kwa ugaidi na watu wa asili ya Kisomali".

Inspekta Jenerali wa Polisi wa Kenya David Kimaiyo aliiambia Sabahi madai katika ripoti ya Tume ya Haki za Binadamu ilizingatia mwenendo wa vikosi vya usalama miaka mingi iliyopita, ikiongeza kwamba katika miaka ya hivi karibuni, maofisa wa usalama wamekuwa waathirika wa magenge ya wahalifu na makundi ya magaidi ambayo ripoti imekwepa makusudi kutaja.

"Nchi inakabiliwa na vitisho vya vurugu kutoka pande zote," alisema. "Katika matukio kadhaa maofisa usalama imebidi wachukue hatua kwa kujizuia na pale ilipolazimu kutumia nguvu. Baadhi ya wahalifu hawawezi kutendewa kwa upole."

Katika kujibu tuhuma za ripoti ambazo wanaharakati wa chama cha kiraia wako katika shinikizo la kuacha kutetea haki kwa waathirika wa vurugu za baada ya uchaguzi, Kimaiyo alisema kwamba polisi ingeweza kutoa ulinzi kwa Wakenya wote, ikiwa ni pamoja na wanaharakati wa vyama vya kiraia na familia zao.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Idara ya Polisi Johnstone Kavuludi alikiri kwamba mchakato wa marekebisho ya idara ya polisi ulikuwa unachelewa, lakini alisema tahadhari ilikuwa lazima.

"Ni kweli kwamba marekebisho yako nyuma kiasi, lakini sasa tunajipanga na kufanya kazi ya kuharakisha marekebisho," aliiambia Sabahi. "Mchakato unaweza kwenda taratibu, lakini pia tunataka kuendesha uchunguzi wa haki kwa wale wote ambao uadilifu wao na rekodi ya haki za binadam vimetiliwa mashaka”

Uhuru wa vyombo vya habari wahojiwa

Kwa upande wake, Waziri wa Habari Habari, Mawasiliano na Teknolojia Fred Matiang'i alikanusha tuhuma za ripoti hiyo kwamba serikali ilikuwa ikizuia uhuru wa vyombo vya habari kwa kuanzisha  “ zuio kali kuhusu vyombo vya habari na mashirika yasiyo na ingiza  faida Alisema kusudi la serikali lilikuwa sio kuvizuia vyombo vya habari. "Sheria ambazo serikali imeanzisha zinamaanisha kuimarisha utoaji wa ripoti sahihi na kuzuia uovu," aliiambia Sabahi.

"Baadhi ya mashirika ya habari yanapotosha kile ambacho sheria mpya zinaeleza kuulaghai umma, na ninashangazwa na mashirika yenye [hadhi] ya Human Rights Watch yameleta uongo kwamba serikali inajikita katika kuzuia vyombo vya habari," alisema.

Hata hivyo, wawakilishi kutoka katika vyombo vya habari na makundi ya jumuiya za kiraia wameiunga mkono ripoti hiyo ya HRW, wakisema inaonyesha ukweli wa hali nchini Kenya.

Makamu Mwenyekiti wa Editors Guild ya Kenya David Ohito aliiambia Sabahi kwamba idhini ya Kenyatta ya sheria mpya kwa vyombo vya habari inatishia kikamilifu uhuru na uhai wa vyombo vya habari nchini.

"Ripoti ya Human Rights Watch iliandaliwa [kabla] sheria hizi hazijatungwa, lakini serikali imetimiza tishio lake na kusaini sheria na kudhibiti vyombo vya habari kabisa," alisema Ohito, ambaye ni mhariri wa gazeti la The Standard.

Alisema wadau wa vyombo vya habari wamekwenda mahakamani kupinga sheria  Marekebisho ya Habari na mawasiliano ya Kenya ya mwaka 2013 na Sheria ya Baraza la Vyombo vya Habari Kenya. Kama sheria hizi hazitapitiwa tena, vyombo vya habari vitakabiliwa na ukaguzi na adhabu kali kutoka serikalini, alisema.

Mwandishi wa habari za picha na mwanaharakati Boniface Mwangi alisema rekodi ya Kenya kuhusu haki za binadamu, nidhamu ya utawala wa sheria na kupambana na rushwa ni mbaya.

"Kutoadhibiwa kumekuwa ni kawaida. Msukumo wa serikali ya Kenya kuondolewa kwa mashtaka ya uhalifu dhidi ya rais na makamu wake ni picha mbaya kwa wengine, hususan kwa vikosi vya usalama," aliiambia Sabahi.

Rais ana nafasi ya kujisafisha yeye mwenyewe katika mahakama ya sheria na anapaswa kuwadhibiti viongozi wa serikali wanaotoa msukumo dhidi ya kesi ya ICC, alisema Mwangi.

"Kenya iko katika hatari ya kujiunga na nchi ambazo hazina uvumilivu katika uhakiki na uwiano," alisema. "Ndiyo sababu sheria mpya zimeharakishwa kutungwa kuzuia uhuru."

 
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

.Wananchi wasema Ahadi ya kupiga picha tarehe 25/12/2013. haikuwa kwa Vitendo.
Mhe Waziri wa Ujenzi John Pombe Magufuli, alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Mwanza siku ya tarehe 14.11.2013, Jijini Mwanza alipofika kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi katika daraja la Mabatini. Hapa ndipo alipo ahidi daraja kukamilika na kuanza kutumika kabla ya Sikukuu ya Chrismas na Mwaka Mpya wa 2014."Nataka tarehe 25.12.2013, ndugu zangu Wasukuma waliokuwa wanapiga picha kwenye samaki waje wapiga hapa mabatini" 

 
Hapa tuna Sikiliza Ahadi ya tarehe 25.12.2013.
Wanachi katika Mkoa wa Mwanza na hususan wale wanaoishi katika katika ya mji wa Mwanza wamesema, Ahadi aliyoitoa Mhe. Magufuli wakati wa kuweka jiwe la msingi katika daraja la Waenda kwa Miguu la Mabatini lililoko Mkoani hapa haikuwa ya kweli kwani mda umepita hata ule ambao waliahidiwa kuwa daraja lingekuwa tayari.
Tulipiga na Picha ya Pamoja.
 
"Fikiria bwana Kuninews, sisi tuliahidiwa na Mhe. magufuli kwamba tarehe 25.12.Mwaka jana tungepiga picha kwenye daraja hili lakini haijawa hivyo, tafsiri ni kwamba Mheshimiwa waziri kapuuzwa" aliniambia bwana Mashauri Kitambo mkaazi wa Miembe giza Mabatini jiji hapa.
 
Kikundi cha Mchele Mchele kikitumbuiza.
Naye Mariam Mayengela anasema" kama utakumbuka ndugu mwandishi sisi hapa mabatini imekuwa kero ya mda mrefu, matumaini yetu ni daraja likamilike na hili tuta linalo sababisha msongamano liweze kuondoshwa." anasema na kuongeza Nyakati za jioni wewe mwenyewe huwa unaona wananchi tunavyo pata shida, na ... na...!!  tulivyosikia kauli ya Mhe. waziri sikuile tulidhani sasa ukombozi umetimia ndio maana nasema wanasuasua sana.
 
Daraja la waenda kwa miguu katika jiji la Mwanza na hususan katika Eneo la mabatini ni mpango ulio ibuliwa na watendaji wa serikali katika Vikao vya ushauri vya Mkoa (RCC), ilikukomesha adha ya Msongamano wa magari katika mji wa Mwanza.
 
Daraja hilo linajengwa na kampuni ya, NODIC Constraction, aidha kukamilika kwa daraja hilo itakuwa ni mwarobaini wa msongamano wa magari kwa magari yapitayo katika njia hiyo ya Nyerere na kuwezesha wananchi wa mji wa Mwanza kuwahi kazini Nyakati za asubuhi na Nyakati za jioni.
 
 
 
 
Mkoa wa Mwanza ambao hivi sasa Unajumla ya watu Mil. 2.7na zaidi kwa mujibu wa sense ya watu na Makaazi ya mwaka 2012, ni moja ya miji ambayo inanyemelewa na msongamano wa magari kutokana na kuwa na bara bara tatu tu zinazo ingia na kutoka jijini humo, ambazo ni Nyerere, itokayo Musoma na Nchi jirani ya Kenya, Kenyata yenye kutokea Shinyanga na Mikoa ya Geita na Simiyu ambayo ndio njia kuu yakupitisha magari yatokayo Dar- Es Salaam na ile ya Uwanja wa Ndege.
 
Mwanza ni mji unaokuwa kwa kasi kusini miongoni mwa miji iliyopo kusini mwa  Jangwa la Sahara na unatajwa nji wa pili kwa kuwa na idadi kubwa ya watu ukitanguliwa na DSM.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akioneshwa kufurahishwa jambo na Wajumbe wa TFDA.
 
Wajumbe wa Bodi ya TFDA walipotembelea Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
Mkuu wa Mkoa amewomba TFDA kuona umhimu wa kujenga kiwanda cha dawa katika Mkoa wa mwanza kutokana na ukuwaji wa Mkoa huo, na ambao unachangia kwa kiasi kikubwa katika kukuza uchumi wa nchi.
Ndikilo aliyasema alipo tembelewa na wajumbe wa Bodi ya mamlaka ya chakula na dawa nchini wakati walipofika kwa ajili ya uona mchango wa Mkoa wa Mwanza katika jitihada za pamoja za masuala ya TFDA.
"kujengwa kwa kituo cha Biashara cha Jiji la mwanza ambapo milango ya biashara nyingi itakuwa wazi hususan bidhaa zinazodhibitiwa na TFDA".
"kwakuwa mamlaka ya chakula na dawa ndiyo yenye dhamana ya kuangalia afya ya mlaji, hivyo ni vema wakawashawishi  wafanya biashara wakubwa kuona umuhimu wa kujenga viwanda vya dawa katika mkoa huo".
Bodi ya  Ushauri ya Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kupitia kwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii (MAB) ilikutana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Injinia Evalist Ndikilo kwa lengo la kutambua mchango wa mkoa na ushirikiano unaotolewa kwa TFDA katika masuala ya Udhibiti wa Bidhaa za Chakula, Dawa, Vipodozi  na Vifaa tiba.

Akizungumza katika ziara hiyo Mwenyekiti wa MAB, Balozi Dkt. Ben Moses, amepongeza ushirikiano uliopo baina ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na TFDA kanda ya Ziwa na kutoa wito wa kudumisha ushirikiano uliopo kwa  kuwa lengo la udhibiti litafanikiwa ikiwa ushirikiano uliopo utadumishwa.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa amesifu kazi kubwa inayofanywa na TFDA katika kulinda afya ya wananchi kwani afya za wananchi zikiimarika basi uchumi wa unchi nao utaimarika. Vilevile,  katika kueleza changamoto ambazo mkoa unakabiliana nazo katika masuala ya udhibiti wa chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba,  Injinia Ndikilo alieleza kuwa  usafi katika machinjio ni changamoto kubwa na kwamba anatarajia kulipatia ufumbuzi hivi karibuni baada ya kuitisha kikao cha wadau wa Machinjio ya Mkoa huo wa Mwanza.

Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
.Ni katika Zahanati ya Nyanguge Iliyoko Mkoani Mwanza.
.Wilaya yajipanga kukamilisha Jengo la X- Ray ili Ahadi yao itimie kama alivyo ahidi Rais ya kupatiwa Mashine ya X Ray.
Hii ilikuwa siku ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete alipofika na kuzindua
Kisha kutoa ahadi ya X RAY pamija na Gari la Wagonjwa katika Wilaya ya Magu, kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Magu Dkt Athumani Pembe, Mkurugenzi wa Halmashauri Bibi Naomi Nnko, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tz. Dkt. Jakaya Kikwete, Mwenyekiti wa Halmashauri na Diwani wa Kitongosima Mhe Desdetery Kiswaga, pamoja Mbunge wa Jimbo la Magu Dkt. Festus Limbu  ( Picha zote na Afisa Habari Mkoa wa Mwanza).



Natazama kama Limekua Likiwa kamili na Gesi yake.
.
Hapa Mkuu wa Mkoa akiwasha Gari mara baada ya Uzinduzi wa gari la Wagonjwa.


Mganga Mkuu wa Wilaya ya Magu hapa akisoma Taarifa wakati wa kukabidhi Gari la Zahanati hiyo.
ya Lugeye, lililo tolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano.
Kibao kilichowekwa wakati wa Uzinduzi wa Zahanati hiyo.


Hapa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akikagua Vifaa vya Ambulence.
Hili ndilo Gari lililotolewa kama Ahadi ya Mheshimiwa Rais aliyo itoa Mwishoni mwa Mwaka jana.
.


Na: Atley Kuni - Afisa Habari Mkoa wa Mwanza.

Nderemo shangwe hoi hoi na Vifijo vilitawala katika Zahanati ya Nyanguge wakati Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evaristi Ndikilo alipokuwa akikabidhi gari la Wagojwa aina ya Land Cruser iliyo ahidiwa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania wakati alipofanya ziara katika Mkoa wa Mwanza Mwishoni mwa mwaka jana tarehe 07. Septemba 2013 na kufungua Zahanati ya Nyanguge na kasha kuwa ahidi mashine ya X ray pamoja na Gari la wagonjwa.
 
 
Alipokuwa akifungua zahanati hiyo rais alisema " Nimefurahishwa sana na kazi mnayo ifanya hapa Lugeye, kwa hiyo na Mimi  Rais wenu, nitashiriki nayi kwa kuwa changia kile kidogo nilicho ncho" alisema rais, na kuongeza "kwa kuanzia nita waletea gari la wagojwa lakini kama hiyo haitoshi, mkiweza kukamilisha jingo la X Ray basi mimi mchango wangu utaongezeka na kuwaletea Mashine ya X- Ray hapa Lugeye".
 
Kwamujibu wa taarifa ambazo kuni newsblog imezipata tayari Gari la wagonjwa limepatikana na tarehe 24.1.2014 Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo alifika katika Kata ya Kitongosima Wilayani Magu kwa ajili ya kuikabidhi gari hilo  lenye namba za usajili STL 938  akiwa katika Ziara ya kukagua shughuli mbali mbali za Maendeleo Mkaoni humo.
 
Aidha katika hatua nyingine wananchi hao hivi sas wanaendelea na Ujenzi wa jingo la X ray, ambapo hadi siku kuninews ilipo tembelea katika mradi huo tayari, msingi ulikuwa umeanza kujengwa, Matofali zaidi ya Elfu nne yalikuwa yamesha Fyatuliwa, huku wananchi wakiwa wamesomba Tripu 10 za Mchanga zenye thamani ya Tsh. 900,000, nayo halmashauri ya Wilaya ya Magu tayari imechangia kiasi cha Mil. 10,000,000, huku ikiwa imetenga kiasi cha sh. Mil. 60,000,000 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo ili waweze kupatiwa X ray waliyo ahidiwa na Mheshimiwa Rais.
 
Kwa upande wao wananchi katika Eneo hilo hawa kuficha furaha yao kwa kusema "kama ni hivi hakika ndio maana huyu ni mtu wa watu, ameahidi Samaki kweli kaleta samaki"
 
Naye Mganga mkuu wa Wilaya ya Magu, akisoma taarifa mbele ya Mkuu wa Mkoa alisema, kupatikana kwa gari hilo kutasaidia kupunguza vifo vya mama na mototo kwani itasaidia kuwafikia wananchi kwa haraka na kisha kuwapeleka katika Zahanati kwa ajili yakupata huduma iliyo bora".
 
Akikabidhi gari hilo kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, amewatasa wananchi hao kulitunza gari hilo, ili liweze kuwa msaada kwa watu wote bila kujali Itikadi zao za Kisiasa, " Kwa hiyo ndigu zangu mimi rai yangu kwenu ni kwamba, Gari hili sasa liwe linapatika kituoni muda wote na isitokee sasa mtu akaanza kulifanyia shughuli zake Binafsi, alisema na kuongeza, lakini pia hakikisheni linafanyiwa matengenezo kwa wakati. sio gari limesha fikisha kilometa za Service ninyi mnaendele kulitumia hapana" samba mba na hilo akawashi kuwa wanaliwekea mafuta mara kwa mara ili pindi linapo hitajika liwe tayari.
 
Mwisho aliuagiza uongozi wa Wilaya ya Magu kuhakikisha bara bara ziendazo Vijijini zina imarishwa ili kufanya gari hili liweze kudumu kwa muda mrefu, " Nimuombe ndugu yangu mkurugenzi aone sasa umuhimu wa kuzifanyia ukarabati bara bara mara kwa mara.
 
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya magu, ameithibitishia kuninews.blogspot.com kwamba kutokana na ahadi ya Rais wanategemea kukamilisha Jengo la X ray ifikapo mwishini mwa Februari 2014.
Wilaya ya magu yenye wakaazi 299,759 inavituo vya kutolea huduma za Afya 46 ambavyo ni Hospitali moja Zahanati za Serikali 30, vya watu binafsi 11 na vituo vya afya 4.
 
 Mkuu wa Mkoa wa mwanza alikuwa katika ziara ya kikazi Wilayani humo ikiwa ni sehemu ya kukagua shughuli za maendeleo, kuzungumza na wana nchi pamoja na kusikiliza kero zao.
 

Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Na Rajab Ramah, Nairobi.

Utengaji wa baadhi ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) katika utekelezaji wa mipango ya muungano kunaweza kusababisha kuvunjika kwa jitihada za muungano kamili wa kanda, wachambuzi wasema.

 

Kutoka kushoto kwenda kulia, Rais wa Rwanda Paul Kagame, Rais wa Burundi Pierre Nkurunzinza na Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete wakitembea pamoja wakati walipowasili kwenye mkutano wa kawaida wa 14 wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki huko Nairobi tarehe 30, 2012. [Tony Karumba/AFP]

Wakuu wa usalama kutoka Uganda, Kenya na Rwanda walikutana mjini Kigali, Rwanda mapema mwezi huu ambapo walitia saini mkataba wa usalama na ulinzi kurahisisha harakati za raia na watalii za kutoka sehemu moja kwenda nyingine katika kanda unaolenga kuongeza biashara kati ya mpaka wa nchi moja na nyingine.

Mkutano huo wa tarehe 9 Januari wa maofisa wa jeshi, polisi, upelelezi na uhamiaji umefuatia uanzishwaji wa visa ya pamoja ya utalii na nchi hizo tatu ambayo ilianza rasmi tarehe 1 Januari.

Hii ilikuwa ni mara ya nne viongozi hao wa Uganda, Kenya na Rwanda kufanya makubaliano kuhusu masuala ya muungano pasipo ushiriki wa Tanzania na Burundi, ambazo pia ni mwanachama wa muungano huo wa nchi tano.

Tanzania na Burundi hazikuhudhuria mkutano uliofanyika Uganda na Kenya mwezi Agosti mwaka uliopita, au mkutano uliofanyika huko Kigali mwezi Oktoba 2013.

Tanzania ililalamika kutengwa katika mazungumzo, na rais Jakaya Kikwete alisema, "Wameunda umoja wa hiari. Nani ambaye hana hiari?"

Kuvunjika Jumuiya ya Afrika Mashariki siku zijazo?

Katika Mkutano wake wa Kawaida wa 15 wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa Wakuu wa Nchi huko Kampala mwezi Novemba mwaka jana, viongozi walisema watajitolea kufanya kazi pamoja, lakini wachambuzi wa mambo wanasema kuwa hakuna uwezekano wa kutokea hilo.

"Nina wasiwasi kama wakuu wa nchi tatu -- Museveni, Kenyatta na Kagame -- walikuwa makini wakati wa mkutano kuhusu ahadi yao ya kusaidia wanachama wote wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika shughuli zao kwa sababu kinyume na azimio lao walikuwa Rwanda peke yao," alisema Rais wa Chama cha Sheria Afrika Mashariki (EALS) James Aggrey Mwamu. "Huo ni uthibitisho wa kutosha kwamba wanajitoa kufanya kazi bila ya Tanzania na Burundi."

Makubaliano ya pande tatu ni tishio kwa mtangamano wa kanda kwa kuwa yanazitenga kwa makusudi Tanzania na Burundi, alisema.

"Kile tunachokiona kinachoitwa hatua ya 'muungano wa hiari' ni ujengaji wa wingu la wasiwasi na jambo baya miongoni mwa nchi wanachama ambavyo vinaweza kuchochea mgawanyiko na kupanda mbegu ya kutoelewana ikisababisha kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, kama ilivyofanya mwaka 1977," Mwamu aliiambia Sabahi. "Kwetu sisi, 'muungano huo wa hiari' haukubaliki kwa kuwa ni kinyume na mkataba ambao uliiunganisha Jumuiya ya Afrika Mashariki."

Kushindwa kwa nchi zote wanachama kuungana katika mipango ya pamoja kisiasa na kimaendeleo ni sawa na kuiacha kanda isambaratike, alisema.

"Kwa sasa kanda inakabiliwa na changamoto nyingi zikianzia katika kukosa utulivu wa kisiasa, uharamia na ugaidi, kwa hiyo, [hatutarajii] kuwatenga wengine na kuhisi kwamba tutafanikiwa," Mwamu alisema, akiwaomba viongozi wa kanda kushauriana mara kwa mara ili wasiendelee kufanya makosa.

Mgawanyiko wadhoofisha mshikamano wa kanda

Ingawa kujumuika pamoja kunachukuliwa kuwa bora na viongozi wa kanda walio wengi, Tanzania imepata sifa ya kutoharakisha masuala ya mtangamano na Burundi inachukuliwa kama nchi isiyo na chochote cha kutoa, alisema George Omondi, mwandishi wa habari wa gazeti la The East African anayeandika kuhusu masuala ya kanda.

"Tanzania imekuwa ikiibua masuala ya umiliki wa ardhi, shirikisho la kisiasa na uraia ambavyo inataka mwongozo ulio wazi, lakini washirika wengine wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, badala ya kukaa chini kutatua hili, wanaliona kama dalili ya kuleta mvutano," Omondi aliiambia kuninews"Wamechagua njia iliyo rahisi zaidi, ambayo ni kujitenga, [na] ambayo sio sahihi."

"Burundi inaonekana kama mshirika masikini ambaye hana thamani katika mtangamano hivyo wanachagua kuipuuza wakisahau kwamba nchi ina watu zaidi ya milioni 9 ambayo inaweza kwa urahisi kuwa soko kwa bidhaa za Kenya, Uganda au hata Rwanda," alisema.

Manu Chandaria, mfanyabiashara wa Kenya na mwenyekiti wa Kundi la Comcraft ambalo linazalisha bidhaa za chuma, plastiki na aluminiamu katika Afrika Mashariki, alisema mgawanyiko wa hivi karibuni utadhoofisha ufanikishaji wa malengo ya mtangamano wa kanda yaliyowekwa.

"Sisi katika sekta ya biashara tunahisi kuwa kuvunjika tena au kujitenga kutaanzisha vikwazo vipya katika biashara," Chandaria aliiambia kuninews. "Kila nchi inaanzisha na kutumia mifumo yake tofauti ya biashara … itakuwa ni pigo kwa biashara huria ambazo tumekuwa tukikabiliana nazo muda wote huu."

Ili kufurahia kikamilifu faida inayotokana na umoja wa forodha na itifaki ya soko la pamoja, na kukamilisha uanzishaji wa fedha ya pamoja na shirikisho la kisiasa, alisema viongozi wa kanda hiyo wanapaswa kuvumiliana na kuwa tayari kushughulikia masuala ya msingi.

Kuiacha nchi moja nyuma kutazuia mchakato mzima, alisema.

"Tunachokiona ni kutokuwa na uvumilivu kwa baadhi ya viongozi. Hatuwezi kudhani kwamba tutaendelea kwa kuwaacha wale walioibua maswali kuhusu mchakato," alisema Chandaria. "Wangepaswa kukaa na kujaribu kutatua matatizo yaliyoibuliwa na Tanzania badala ya kuamua kuendelea."

EAC imeungana na ni yenye malengo, asema Kandie

Kwa upande wake, Katibu wa Wizara ya Masuala ya Afrika Mashariki Kenya Phyllis Kandie alipinga hisia za kujitenga, akisema muungani wa EAC utafanyika kama ilivyopangwa.

"Sitapenda kuingizwa katika mjadala huo 'muungano wa hiyari', lakini ninachoweza kukueleza ni kwamba sisi ni muungano kama tulivyokuwa awali na kwamba tuna malengo ya kufanikisha misingi ya EAC," Kandie aliiambia Sabahi.

Katika kujibu swali la iwapo mikutano ya nchi hizo tatu zinapingana na mkataba wa EAC, alisema, "Uganda, Kenya na Rwanda wanatumia utengano wa nchi kadhaa ambayo imeelezwa katika mkataba."

Utengano huo ni msingi katika Kifungu cha 7 cha Mkataba wa EAC, ambacho kinaruhusu maendeleo katika umoja miongoni mwa kundi dogo la wajumbe katika muungano mkubwa katika maeneo tofauti na katika kasi tofauti.

Hata hivyo, chini ya kifungu hicho, nchi wanachama ambazo zinataka kuendeleza kwa haraka bado zinatakiwa kuwafahamisha wajumbe wengine, ambalo halijafanyika katika suala hili, kwa mujibu wa Mwamu.

Jaribio la kumpata Katibu Mkuu wa EAC Richard Sezibera kwa ajili ya maoni halikufaulu