Articles by "MIchezo Kimataifa"
Showing posts with label MIchezo Kimataifa. Show all posts
no image
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Rock City Marathon kutimua vumbi kesho (JUMAPILI)

Maandalizi ya Rock City Marathon zinazotarajiwa kufanyika kesho Septemba 25  kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza yamekamilika huku ushiriki wa wa wakuu wa mikoa ya Mwanza na Simiyu kwenye mbio hizo ukitajwa kuwa ni miongoni mwa vivutio vikubwa vinavyotarajiwa kupamba mbio hizo.

Mbio hizo zinazofanyika kwa mara  ya nane mfululizo tangu zianze mwaka 2009 zinaratibwa na kampuni ya Capital Plus International kwa kushirikiana na mkoa wa Mwanza zikiwa na baraka zote kutoka Chama cha Riadha Tanzania (RT), pamoja na Chama cha Riadha Mkoa wa Mwanza (MRAA) , zikilenga kilenga kutambua na kuinua vipaji vya wanariadha nchini, kutangaza utalii na vivutio vilivyoko kanda Ziwa pamoja na kupambana na ujangili.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Mwanza leo, Msemaji wa mbio hizo Bw Mathew Kasonta alisema kamati ya maandalizi ya mbio hizo imejiandaa vilivyo na maandalizi yote yamekamilika, ikiwemo kupokea wakimbiaji kutoka nje ya nchi na washiriki wengine.


Alisema wanatarajiwa kuwa na washiriki zaidi ya 1200 wakiwemo wakimbiaji wa kimataifa, wakimbiaji kutoka mashirika mbalimbali, walemavu wa ngozi yaani Albino pamoja na wanafunzi.
“Rock City Marathon inahusisha mbio za kilometa 21 kwa wanaume na wanawake,  mbio za Kilometa tano zitakazohusisha wafanyakazi kutoka makampuni mbalimbali (Corporate) pamoja na watu wenye ulemavu wa ngozi yaani Albino, mbio za Kilometa tatu ambazo zipo mahususi kwa ajili ya wazee, mbio za kilometa 2 zitakazohusisha watoto wenye umri kati ya miaka 7 hadi 10 pamoja na mbio fupi  za mita 100, 400, 800 na 1500 ambazo ni mahususi kwa wanafunzi,’’
“Kubwa zaidi pia ni kuwashukuru sana wadhamini wa mbio hizi kwa kuendelea kutuunga mkono kwenye maandalizi haya yaani kampuni za Freidkin Conservation Fund na African Wildlife Trust, Benki ya NMB,  New Mwanza Hotel, Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Real PR Solutions, kampuni ya Fabec, Tiper, Puma Energies, Clouds Fm, Jembe Fm, Barmedas Tv na EF Out Door,’’ alitaja.
Kuhusu barabara zitakazohusisha mbio hizo zitakazoanza saa 12:00 asubuhi Bw Kasonta alisema; “Kwa washiriki wa mbio za km 21 wataanzia Uwanja CCM Kirumba, kwa wale wa Km 5 wataanzia barabara ya Nyerere eneo la Polisi Mabatini, kwa wale wa Km 3 ambazo ni mbio za wazee wataanzia Barabara ya Nyerere eneo la Makaburi ya Wahindi na kwa mbio za watoto yaani Km 2 wao wataanzia eneo la Mwaloni kuelekea CCM Kirumba,’’

Kwa upande wa zawadi kwenye mbio hizo Bw Kasonta  alisema washindi wa kwanza wa mbio za kilometa 21 kwa wanaume na wanawake watajinyakulia sh.  mil 1.5/- kila mmoja, sh. 900,000/-  kwa washindi wa pili na sh. 700,000/- kwa washindi wa tatu.
“Kwa mbio za Kilometa tano ambazo zitaongowa na wakuu wa mikoa ya Mwanza na Simiyu ambazo pia zitahusisha wafanyakazi kutoka makampuni mbalimbali (Corporate) pamoja na watu wenye ulemavu wa ngozi yaani Albino,  washindi watapatiwa zawadi za heshima kwa makampuni huku pesa zilielekwa washiriki wenye ulemavu wa ngozi.,’’
Akizungumzia usalama katika tukio hilo ambalo litahusisha maelfu ya watu, Mwenyekiti Msaidizi wa kamati yam bio hizo Bw Zenno Ngowi  alisema kamati yake imekuwa ikifanya kazi kwa ukaribu zaidi na jeshi la polisi na jeshi la hilo limeshajipanga vilivyo kwa ajili ya tukio hilo ili kuhakikisha kila kitu kinaisha kwa usalama wakiwemo watazamaji na washiriki mbio hizo
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
HAPA TIMU ZIKIKAGULIWA NA MGENI RASMI, TIMU HIZO ZILITOKA SARE YA GOLI 1-1












Mashindano ya UMISETA, kwa Mkoa wa Mwanza yamefunguliwa rasmi hapo jana na Kaimu katibu Tawala mkoa wa Mwanza Ndaro Kulwijira huku akiwaasa vijana hao wa Sekondari kucheza kwa kuzingatia nidahamu ya hali ya juu.

Zaidi soma katika Hotuba yake aliyoitoa wakati wa Ufunguzi wa michezo hiyo.
 

HOTUBA YA KAIMU KATIBU TAWALA WA MKOA WA MWAZA     WAKATI WA KUFUNGUA MASHINDANO YA NGAZI YA MKOA YA MICHEZO YA SHULE ZA SEKONDARI TANZANIA (UMISSETA) NSUMBA SEKONDARI TAREHE 22 MEI, 2014

Katibu Tawala Msaidizi  wa Mkoa Elimu  - Mwalimu Hamis Maulid

MaafisaElimu wa Halmashauri

Mameneja

Viongozi wa Vyama vya Michezo Mkoa

Wanamichezo

Ndugu Wananchi; na

Wapenda Michezo Wote.

 

Napenda kuchukua fursa hii kukushukuru Katibu Tawala Msaidizi ambaye ni AfisaElimu wa Mkoa, na Viongozi wenzako katika Seksheni ya Elimu kwa kunialika kufungua Mashindano haya ya Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA).

 

Nimeupokea mwaliko huu kwa furaha kwa vile umenipa fursa ya pekee kuwaona na kuzungumza na hadhara hii ya Wanafunzi Wanamichezo na Walimu wao. Aidha, nitumie fursa hii kuupongeza Uongozi wa Nsumba na jumuia yote kwa maandalizi mazuri ya mazingira kwa ajili ya mashindano haya. Ahsanteni sana!

 

Ndugu Viongozi na Vijana Wanamichezo,

Leo tumebahatika kujumuika hapa kupitia Utamaduni wa Michezo. Kwa utaratibu huu, ni dhahiri kwamba tunapata nafasi ya kujenga Umoja wa Kitaifa wa Wanamichezo kupitia Michezo hii ya UMISSETA kuanzia ngazi ya Vijana wetu wa Shule za Sekondari. Ni kweli kwamba Michezo ni Burudani, lakini kwa sasa kutokana na mabadiliko ya Mazingira ya Kisiasa, Kiuchumi na Kijamii, Michezo ni Kipaumbele katika kutoa pia Ajira kwa Vijana wetu, kukuza Biashara na kujenga jamii bora yenye maelewano. Kwa mfano, Nchi za wenzetu za Ulaya na Marekani, Nigeria, Togo, Ivory Coast, Cameroon zinatumia kikamilifu nafasi hii ya Michezo kujitangaza Kisiasa na Kiuchumi.

 

 

Ndugu Wanamichezo,

Natambua kwamba ninyi ni Wanafunzi ambao mnahitaji kukuza Taaluma na Vipaji vyenu. Moja ya nafasi hizo ni Michezo. Ili Michezo iendelee kukua Nchini, ni lazima Ukuzaji wa Vipaji vya Michezo uanzie Mashuleni. Ndiyo maana Michezo ni sehemu ya Mtaala wa Masomo yenu. Kama ambavyo tunawataka mfanye bidii sana katika masomo yenu, fanyeni bidii pia na kukuza Vipaji vyenu katika Michezo mbalimbali.

Ndugu Wanamichezo,

Michezo inatufundisha Ushindani wa Kistaarabu, Ushindani unaozingatia Sheria na Kanuni, Ushindani unaojenga urafiki badala ya uhasama; Ushindani unaoleta Upendo badala ya Chuki na Ushindani unaoleta Amani badala ya Shari. Kwa sababu hiyo Mwanamichezo wa leo anayo nafasi ya kupata mafundisho muafaka na hazina ya uzoefu mkubwa wa Ushindani wa Kistaarabu kutoka kwenye Michezo, vitu ambavyo vinaweza kumfanya kuwa Mtanzania bora wa kesho. Mwanamichezo anakubali ama Kushindwa au Kushinda. Waswahili husema“Asiyekubali Kushindwa Si Mshindani”.

Wanamichezo bora ni Watu Wasikivu, wenye nidhamu na Watiifu. Ninyi Vijana ambao ndio Viongozi wa kesho wa Taifa letu mnahitaji sana kujijengea nidhamu na maadili ya hali ya juu ili muweze kuendana na hali ya maisha ya ushindani yatakayokuwa yanawakabili. Nidhamu, inamuwezesha Mtu kufanya kazi zake kwa mpangilio mzuri unaofuata Taratibu zote za kazi kwa wakati. Hii ndiyo njia ya uhakika ya kufikia malengo yoyote yale na kupata mafanikio.

Aidha, kwa njia ya Michezo, nidhamu Shuleni itaongezeka na matarajio yetu ni kuwa nidhamu hiyo itajitafsiri pia katika matokeo mazuri kwenye Taaluma. Matarajio ni kuwa, Wanafunzi watakuwa na mahusiano mazuri zaidi kati yao na Walimu wao na wale wote wanaopata Burudani ya Michezo. Ama tunatarajia kuwa wataendelea kuwa Watu wenye Nidhamu katika Utu Uzima wao, ili hatimaye tuwe na Taifa la Watu wenye nidhamu ya kutolewa mfano.

Ndugu Wanamichezo,

Tangu zama za kale Michezo ilikuwa ni sehemu ya Maisha ya Jamii. Jamii moja ilijipambanua na Jamii nyingine kutokana na ushupavu na ushujaa wake katika Michezo. Dhana hiyo ya kale bado inaendelezwa kupitia Sera ya Michezo kwa njia ya kisasa zaidi. Sera ya Maendeleo ya Michezo inayaainisha madhumuni ya Michezo wakati huu kuwa ni:  Kujenga na kuimarisha Afya Bora kwa wote;  Kujenga Tabia ya Ushirikiano, Upendo, Undugu na Uzalendo;  Kujenga Uhusiano, Uelewano na Mshikamano Kitaifa; Kujenga Moyo wa Kishujaa na Kujihami na Kukuza Ukakamavu, Ujasiri na Kujiamini; Kuburudisha;  Kulitambulisha na kulitangaza Taifa letu nje ya Mipaka yake; na

 Kumjenga Mwanamichezo kuwa mtu imara Kiakili na Kiroho (kuanzia Utotoni hadi Utu Uzima). Kwa mtiririko huu, napenda kusisitiza kuwa Shule zote, kuanzia za Awali, Msingi, na Sekondari, viwe na Viwanja vya Michezo mbalimbali. Hii ni njia ya kuwatambua na kuwaendeleza Vijana wenye Vipaji Maalum ili hatimaye Washiriki kwenye Mashindano ya Kitaifa na Kimataifa. Aidha, Halmashauri zetu za Miji, Manispaa, Vijiji zihakikishe kuwa maeneo yaliyotengwa kwa Shughuli za Michezo yanatumika kwa shughuli hiyo. Aidha, Viwanja vilivyopo viimarishwe na vitunzwe ipasavyo.  Ndugu Wanamichezo,

Nitumie fursa hii pia kuwakumbusha kwamba mnapofurahia kushiriki katika Michezo hii, ni lazima mkumbuke pia kuwa furaha yenu itaweza kudumu kama mtatambua kuwa kuna mpinzani mkubwa kati yenu aitwaye Virusi vya UKIMWI na UKIMWI. Kila mmoja wenu anaelewa vya kutosha juu ya Adui huyu. Ni wajibu wangu kama Kiongozi na Mlezi wenu kuwakumbusha juu ya hatari inayowakabili msipochukua tahadhari ya kutosha. Kumbukeni UKIMWI bado unaenea kwa kasi kubwa sana hasa miongoni mwa Vijana wa Rika lenu kuliko Rika lolote jingine. Niwakumbushe kwamba kataeni kumalizwa na Ugonjwa huu. Msikubali kukatishwa masomo na msikubali kutenganishwa mapema na Familia zenu. Kwenu ninyi, njia bora pekee ni kusubiri hadi wakati muafaka wa kuwa na ndoa zenu. Wekeni bidii katika masomo, kwani muda ukifika yote yatajipanga vizuri.

 

Nitumie fursa hii kuwakumbusha kuepukana na matumizi ya dawa za kulevya  kama vile bangi, mirungi na cocaine kwa imani ya kuwa dawa za kulevya huwapatia nguvu  na mzuka wa kushindana, huko ni kujidanganya.  Vijana wengi hasa wanamichezo waliojaribu kutumia dawa za kulevya michezoni wameathirika na wamekuwa mataahira. Shirikisho la vyama vya michezo duniani limekataza kabisa matumizi ya dawa hizo na ukigundulika ni kufungiwa maisha na ushindi kunyanganywa. Nawaomba walimu na wanafunzi kuwabaini wale wote watakaojihusisha na utumiaji wa dawa za kulevya na kuwachukulia hatua kali za kiidhamu na kisheria

 

Ndugu Wanamichezo,

Nimeelezwa kuwa baada ya Michezo hii yapo Mashindano ya Kanda ya Ziwa ambapo Mikoa ya Mwanza, Mara na Simiyu hukutana ili kuimarisha mahusiano ya Vijana wa Shule za Sekondari na kuunda timu moja ya Kanda. Ni muhimu Timu zetu zijipange kushiriki vizuri na kutuletea undindi a kishindo. Ni Vizuri sasa Timu hizo ziandaliwe vizuri ili zikashiriki kama Washindani na si Wasindikizaji.Kushiriki kwetu kunatujengea umahiri katika kujenga upeo wa akili za Vijana wetu na kujenga mahusiano mazuri ya kikanda .Natoa rai kwa Mashirika, Vyama vya Michezo na watu wengine  kushiriki kwa  kuchangia kufanikisha ushindi wa timu zetu za Mkoa.

 

Ndugu Wanamichezo,

Mwisho napenda kukumbusha kuwa umahiri katika jambo lolote lile hufikiwa kwa kujifunza na kufanya mazoezi mengi, kwa bidii. Napenda kuwapongeza Walimu na Waamuzi na wote walioziandaa Timu hizi ambazo leo zinashindana hapa. Nawapongeza sana Wanamichezo wa Timu zilizoteuliwa kushindana hapa. Natumaini mliteuliwa kwa kustahili na katika Michezo hii mtapata nafasi ya kuonyesha kuwa kuteuliwa kwenu hakukuwa kwa Bahati. Onyesheni Umoja, Onyesheni Upendo, na Onyesheni“Fair Play” katika mashindano haya. Kumbukeni kwamba Michezo ni Afya, Michezo ni Furaha na Michezo ni Ajira.

 

Ndugu Wanamichezo, Wageni Waalikwa,

Baada ya kusema hayo, napenda sasa nitamke kuwa,Mashindano ya Umoja wa  Michezo Shule za Sekondari UMISSETA  kwa mwaka 2014 yamefunguliwa rasmi.

Ahsanteni kwa Kunisikiliza

 

 

 

 
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
WACHAZAJI WA MADRID HAPA WAKIPONGEZANA BAADA YA ROLNARDO KUTUPIA GOLI.

Ni katika Kombe la Ulaya.
Ronaldo na Bale washerekea ushindi dhidi ya Schalke 04
Mchezaji bora duniani mwaka huu Cristiano Ronaldo Gareth Bale na Karim Benzima walifunga mabao mawili kila mmoja na kuisaidia Real Madrid ya uhispania kufuzu kwenye robo fainali ya kombe la mabingwa barani ulaya baada ya kuinyeshea Schalke 04 ya Ujerumani mabao 6-1 katika mkondo wa kwanza uliosakatwa huko Ujerumani.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Hawa Ndio Munich ambao hata hivyo bado wana kiwewe na Arsenal.

Kocha wa Bayern Munich Pep Guardiola amekiri ni vigumu sana kudhibiti dakika tisini za mechi ya aina yeyote dhidi ya Arsenal ya Uingereza .
Guardiola
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

MBWANA SAMATTA AKIWA ANAONESHA VITU VYAKE UWANJANI.
Shirikisho la kandanda barani Afrika CAF limetangaza majina ya wachezaji wa kiafrika watakaowania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka 2013 na Mchezaji bora wa Afrika anayechezea vilabu vya ndani ya Afrika mwaka 2013.

Katika majina hayo yapo majina mawili ya wachezaji wanaotoka Afrika Mashariki ambao ni Victor Wanyama raia wa Kenya anachezea Southampton FC ya England ambaye ni miongoni mwa wachezaji 25 watakaowania tuzo ya Mchezaji bora wa Afrika, huku Mbwana Samatta raia wa Tanzania anayechezea klabu ya TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo yeye ameteuliwa kuwania tuzo ya Mchezaji bora wa Afrika anayechezea timu za Afrika.

Wachezaji 25 watawania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika na 21 Mchezaji bora wa Afrika anachezea timu za ndani ya Afrika.

Washindi wa tuzo hizo wanatarajiwa kutangazwa Januari 9, mwaka 2014 mjini Lagos nchini Nigeria.

Orodha kamili ya wachezaji waliotangazwa na CAF na timu wanazotoka hii hapa chini.

Mchezaji wa bora wa CAF Afrika

1. Ahmed Musa - Nigeria - CSKA Moscow

2. Asamoah Gyan - Ghana - Al Ain

3.Dame N'Doye - Senegal - Locomotiv Moscow

4. Didier Drogba - Cote d'Ivoire - Galatasaray

5. Emmanuel Emenike - Nigeria - Fenerbahce

6. Islam Slimani - Algeria - Sporting Lisbon

7. John Mikel Obi - Nigeria - Chelsea

8. Jonathan Pitroipa - Burkina Faso - Stade Rennais

9. Kévin Constant - Guinea - AC Milan

10. Kwadwo Asamoah - Ghana - Juventus

11. Luís Carlos Almada Soares (platini) - Cape Verde - AC Omonia

12. Mehdi Benattia - Morocco - AS Roma

13. Mohamed Aboutrika - Egypt - Al Ahly

14. Mohamed Salah - Egypt - Basel FC

15. Nicolas Nkoulou - Cameroon - Marseille

16. Pierre-Emerick Aubameyang - Gabon - Borussia Dortmund

17. Ryan Isaac Mendes da Graça - Cape Verde - Lille

18. Saladin Said - Ethiopia - Wadi Degla FC

Victor Wanyama

19. Seydou Keita - Mali - Dalian Aerbin F.C

20. Sofiane Feghouli - Algeria - Valencia

21. Sunday Mba - Nigeria - Warri Wolves

22. Victor Wanyama - Kenya - Southampton FC

23. Vincent Enyeama - Nigeria - Lille

24. Yao Kouassi Gervais 'Gervinho' - Cote d'Ivoire - AS Roma

25. Yaya Toure - Cote d'Ivoire - Manchester City

Mchezaji bora Afrika anacheza vilabu ndani ya Afrika

1. Adane Girma - Ethiopia - St George

2.Ahmed Fathi - Egypt - Al Ahly

3. Alexis Yougouda Kada - Cameroon - Coton Sport

4. Ali Machani - Tunisia - CAB

5. Bapidi Fils Jean Jules - Cameroon - Coton Sport

6. Daine Marcelle-Klate - South Africa - Orlando Pirates

7. Fakhreddine Ben Youssef - Tunisia - CSS

8. Getaneh Kebede - Ethiopia - Bidvest Wits

9. Idrissa Kouyate - Cote d'Ivoire - CS Sfaxien

10. Iheb Msakni - Tunisia - Esperance

11. Luyanda Lennox Bacela - South Africa - Orlando Pirates

12. Mbwana Samatta - Tanzania - TP Mazembe

 

Mbwana Samatta

13. Moez Ben Cherifia - Tunisia – EST

14. Mohamed Aboutrika - Egypt - Ahly

15. Rainford Kalaba - Zambia - TP Mazembe

16. Senzo Meyiwa - South Africa - Orlando Pirates

17. Soumbeila Diakite - Mali - Stade Malien

18. Sunday Mba - Nigeria - Warri Wolves

19. Tresor Mputu - DR Congo - TP Mazembe

20. Waleed Soliman - Egypt - Al Ahly

21. Yannick N'djeng - Cameroon - EST.
 
 
Kwa hisani Idhaa ya Kiswahili ya BBC.

 
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Arsenal, Chelsea, Barcelona, Porto, Basel na Borussia Dortmond zatakata kwenye ligi ya mabingwa wa Ulaya:

 
Mzunguko wa pili wa ligi ya mabingwa wa Ulaya ulinza jana usiku na kuendelea tena leo jumanne katika viwanja vinanwe barani Ulaya. Siku ya Jumanne usiku, timu zilizopangwa kwenye makundi ya E, F, G na H zilijitupa uwanjani, ili kuwania pointi tatu muhimu.
Mechi zilizochezwa katika kundi E, Basel ya Uswisi iliweza kuitandika Schalke ya Ujerumani bao 1-0. Nchini Romania, klabu ya Steaua Bucharest ya Romania imebugia mabao 4-0  kutoka kwa wageni wao Chelsea ya Uingereza.
Kundi F, Arsenal ya Uingereza  imeonyesha kuwa ni moto wa kuotea mbali msimu huu, baada ya kuibanjua Napoli inayoongoza ligi ya serie A nchini Italia kwa kuitundika mabao 2-0. Kwenye mechi nyingine ya kundi hilo, Borussia Dortmund ya Ujerumani iliigaragaza Olimpique Marseille ya Ufaransa kwa mabao 3-0.
Kundi G, Porto ya Ureno  iliigaragaza Atletico Madrid ya Uhispania kwa mabao 2-1. Kwenye mechi nyingine ya kundi hilo, Zenit St Petersburg ya Russia ilitoka sare ya tasa na Austria Vienna ya Austria katika dimba la Petrovskiy.
Kundi H, AFC Ajax Amsterdam ya Uholanzi yasimamishwa, baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na AC Milan ya Italia, huku Celtic ya Scotland ikisalimu amri ya kufungwa bao 1-0 na Barcelona ya Uhispania.
Leo Jumatano kutashuhudiwa mechi nyingine 8 za makundi A,B,C na D na miongoni mwa pambano linalosubiriwa kwa hamu na washabiki wa soka ni mechi kati ya Manchester City ya Uingereza na Bayern Munich ya Ujerumani.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Theo Walcott aliibuka kinara kwa kupachika mabao 3 kati ya 7 ya Arsenal walioifunga NewCastle United uwanja wa Emirates 29-Desemba-2012
Arsenal imeiangushia kipigo kikali New Castle kwa kuicharaza magoli 7-3 katika mchezo wa ligi kuu ya England uliofanyika Jumamosi kwenye uwanja wa Emirates.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Robin Van Persie mfungaji wa bao la pili la Man U dhidi ya West Brom
Manchester United leo imeilaza West Brom magoli 2-0 na kujihakikishia nafasi ya kwanza kwenye msururu wa ligi kuu ya Premier ya England, mwanzo wa mwaka ujao wa 2013.
Gareth McAuley alijifunga mwenye na kuipa Manchester United, bao lao la kwanza kabla ya Robin Van Persie kufunga bao la pili.
no image
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Kocha wa Manchester Sir Alex Ferguson amemshutumu kocha wa Newcastle Allan Pardew na kumtaja kuwa mfarisayo na mnafiki.
Pardew alimshutumu Ferguson kwa utovu wa nidhamu baada ya mechi yao siku ya jumatano.
Pardew amesema shirikisho la mchezo wa soka nchini England, FA lingemuadhibu Ferguson kwa kukabiliana na maafisa waliokuwa wakisimamia mechi hiyo ambayo Manchester United ilishinda kwa magoli 4-3, katika uwanja wa Old Trafford.
'' Allan Pardew ndiye kocha ambaye mara nyingi huwazomema marefa kwa takriban karibu mechi zote'' alisema Ferguson.
Pardew alipigwa marufuku ya kutohudhuria mecho mbili baada ya kupatikana na hatia ya kumsukuma mmoja wa wasimamizi wa mechi yao mwezi Agosti.
Ferguson alimzomea refa wa mechi hiyo Mike Dean, naibu wake Jake Collin na Neil Swarbrick, mwanzo wa kipindi cha pili ya mechi yao ya ligi kuu ya Premier kupinga goli la pili la Newcastle.
Dean aliidhinisha kuwa Papiss Cisse, hakuwa ameotea wakati Jonny Evans alipojifunga kunako dakika 28.
Pardew hakufurahiswa na uamuzi wa FA wa kutomuadhibu kocha huyo wa Manchester United mwenye umri wa miaka sabini.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Kocha wa Manchester Sir Alex Ferguson amemshutumu kocha wa Newcastle Allan Pardew na kumtaja kuwa mfarisayo na mnafiki
 

Pardew alimshutumu Ferguson kwa utovu wa nidhamu baada ya mechi yao siku ya jumatano.
Pardew amesema shirikisho la mchezo wa soka nchini England, FA lingemuadhibu Ferguson kwa kukabiliana na maafisa waliokuwa wakisimamia mechi hiyo ambayo Manchester United ilishinda kwa magoli 4-3, katika uwanja wa Old Trafford.