November 2013
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo anatazamiwa kufanya ziara ya kikazi katika Wilaya za Mkoa wa Mwanza kwa lengo la kuhimiza shughuli mbali mbali za maendeleo kwenye wilaya hizo.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza katika moja ya Majukumu hapa alikuwa akitoa cheti.  
  
Kwa mujibu wa ratiba ambayo mtandao huu imeupata inaonesha kuwa, ziara hiyo ya kikazi itaanzia katika wilaya ya Sengerema siku ya tarehe 02.12.2013.

Katika ziara hiyo Mkuu huyo wa Mkoa atapata fursa ya kujionea shughuli mbali mbali za maendeleo zinazotekelezwa kwenye wilaya hizo, kukagua pamoja na kuhutubia wananchi kwenye mikutano ya hadhara.

Mkoa wa Mwanza unaundwa na Wilaya za Sengerema, Ukerewe, Ilemela, Nyamagana, Magu, Misungwi na Kwimba na kwa mujibu wa sensa ya watu ma makaazi ya mwaka 2012 mkoa huo unajumla ya wakaazi  2,772,509 , huku  shughuli kuu za uzalishaji mali ikiwa ni Kilimo, Madini, Mifugo Viwanda pamoja na Biashara.

Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Na:  Atley  Kuni.
Mamlaka ya mawasiliano Tanzania hivi leo imeadhimisha miaka kumi toka kuanzishwa kwake kwa mafanikio makubwa.
Katibu Tawala Msaidizi kwenye Sekretariti ya Mkoa wa Mwanza Bw. Wambura Sabora alipokuwa akifungua
Kongamano la Miaka kumi ya TCRA waliokutana Mkoani Mwanza katika Ukumbi wa Victoria Pales wa Jiji Mwanza.

Hayo yamesemwa na Meneja wa TCRA kanda ya ziwa bw.Lawi Odiero wakatia akitoa maelezo mafupi ya juu ya nini kimtendeka tangu kuanzishwa kwa mamlaka ya mawasiliano nchini miaka kumi iliyopita.

Amesema katika kipindi cha miaka kumi ilyopita shughuli za mawasiliano zimekuwa kwa kasi kubwa sambamba na kukua kwa TEHAMA katika kilimo, miofugo,ufugaji, madini pamoja na biashara mbali mbali.
Amesema katika kipindi hicho cha miaka kumi vile vile kumekuwepo na ongezeko la vyombo vya habari, ambapo ndani ya Miaka kumi ya Mamlaka ya mawsiliano vyombo vya habari na TV vimeongezeka kwa kasi ikiwapo kutoka TV Moja hadi 27 na Redio kutoka 1 hadi 84 hivi sasa.
Amesema lengo la kuanzishwa kwa mamlaka hiyo ilikuwa na kusudio la utekelezaji wa Dhima ya taifa Tanzania Vission 2025, sera ya Taifa ya Teknolojia ya habari na mawasiliano ya mwaka 2003 na Sera ya Taifa ya Posta ya mwaka 2003.
 
Ameongeza kuwa mamalaka ya mawasiliano kwa hivi sasa inatekeleza wajibu wa  kusuluhisha migogoro kadha wa kadha kutoka kwa watumiaji kwa maana ya watumiaji wa huduma za mawasiliano, kutunga sharia za mawasiliani lakini pia kushirikiana na mamlaka nyingine kutoka nchi tofauti tofauti ulimwenguni.
 
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ambaye alikuwa mgeni rasmi na kuwakilishwa na Katibu Tawala Msaidizi wa Seksheni ya miundo mbinu bwana Wambura Sabora, amesema kuwa kila Mdau anatakiwa kuiga mfano wa TCRA ambao kwa namna moja au nyingine wameonesha mafanikio makubwa, alisema kutokana na kukuwa kwa teknlojia ya Mawasiliano nchini kumesaidia kukuza Teknolojia, ushindani wa soko umekuwa,uwekezaji umeongezeka lakini pia umeongeza uhuru wa mlaji kuchagua huduma gani aweze kutumia katika kujipatia huduma ya mwsiliano.
 
Sabora amesema pia kuwa kila Jambo linafaida na hasara lakini kwa hili la TCRA yeye kama mdau wa mawasiliano anasikia fahari kuona masuala ya mawsiliano yamekuwa ukilinganisha na miaka kumi au hata hamsini iliyopita, "hivyo ndugu zangu tusibeze jitihada na juhudi ambazo serikali imekwisha zifanya katika suala Zima la mawasiliano nchini" alisema na kuongeza kuwa kwa mada hizo ambazo zilikuwa zinawasilishwa ni vema wanasemina wakazingatia na kutilia maanani mafunzo hayo.
 
katika hatua nyingine takwimu zinaonesha kuwa kuanzia mwaka 2005 Mamlaka imeongeza idadi ya watoa huduma za leseni za mawasiliano imeongezeka kutoka wanne(4) hadi kufikia wanane(8) sawa na ongezeko la asilimia mia(100)., huku idadi ya watumiaji wa wavuti kwa hivi sasa ikifikia Milioni 7.5 na idadi hiyo inazidi kuongezeka siku hadi siku.
 

Kwa hivi sas mamlaka ya mawasiliano inatoa leseni za Miundombinu ya mawasiliano, Leseni za kutoa huduma za Mawasiliano, Leseni za kutoa huduma( Application Services Licence pamoja na Leseni za Utangazaji.
 
 
Eng. Lawi Odiero Meneja wa kanda ya Ziwa akiongea na vyombo vya habari.
 
 
 
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Na Atley Kuni. Mwanza.

HILI NDILO KOMBE LINALO INGIA MWANZA. 

KIKAO NA WAANDISHI WA HABARI MWANZA.

Kwa mara ya kwanza Kombe la Dunia litapokelewa Mkoani Mwanza na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uwanja wa CCM Kirumba.
  
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo, mbele ya waandishi wa habari na kamati ya maandalizi ya ujio huo katika ukumbi wa Mwanza Hotel hivi leo.
 
Ndikilo amesema hii ni mara ya kwanza kwa kombe hilo kupokelewa katika Mkoa huo na akawataka wanachi kujitokeza kwa wingi ili kuweza kulipokea,amesema na kuongeza kuwa "Mhe shimiwa Rais ambaye yupo ziarani katika Mkoa wa Simiyu amekubali kulilaki kombe hilo katika mkoa wetu wa Mwanza hii ni heshima kubwa kama wananchi wa Mkoa huu na wapenda michezo kwa ujumla.
 
Amesema kombe hilo litawasili katika uwanja wa ndege wa mwanza majira ya saa tatu asubuhi na badae kupelekwa katika uwanja wa CCM Kirumba, ambapo pamoja na mambo mengine baadhi ya wananchi watapata fursa ya kupiga picha na kombe hilo.
 
Kwa upande wake Mwakilishi wa Coca Cola Nchini bw. Eyebolt Gretchen, amesema ujio wa Kombe hilo kwa mara ya tatu katika nchi ya Tanzania nia pamoja na amani ya nchi iliyopo na ukarimu wa watu wake, Miongoni mwa nchi za Afrika ambazo zimekuwa na utulivu hata kufanya kutembelewa na kombe la Dunia ni Tanzania, amesema na kuongeza kwamba, kama Coca cola wamekuwa mstari wa mbele kwenye jitihada za kukuza soka nchini ikiwapo mashindano ya Kopa Coca cola.
 
Kwa upande wake kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Ernest Mangu amewahakikishia wanachi wote wa Mkoa wa Mwanza amani na utulivu, aidha amewaomba wananchi kutokuja wanjani hapo wakiwa na watoto wadogo ili kuepusha adha wanayoweza kupata watoto hao" Labda niombe ndugu zangu kwa wale watoto wadogo ni vema wakaachwa nyumbani kuepuka usumbufu". alisema na kuongeza kuwa watu hawataruhusiwa kusogea karibu na eneo la Pitch ya uwanja huo.
 
Hii ni mara ya tatu kombe hilo linakuja hapa nchini ambapo mara zote limekuwa likipokelewa na kulakiwa na wananchi waishio katika Mkoa wa Dar es Salaam. 
 
Wadadisi wa mambo wanasema kwamba, ujio wa kombe hilo si tu kwamba linakuja kutazamwa na wanachi wa Mwanza bali pia ni frsa nzuri kwa mkoa huo kujitangaza kimataifa lakini pia kutangaza rasilimali zinazo patikana katika Mkoa huo alkini pia iwe chachu kwa vingozi kuona kuna umuhimu wa kuipa kipaumbele michezo yote, anasema Mashaka Baltazari mwandishi mwandamizi wa Jambo Leo na Mwakilishi Mkoani Mwanza.
 
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

.NA  FRANCIS GODWIN -- IRINGA
Tanzania yazibagwa nchi sita barani Afrika katika mashindano ya vyuo  vikuu ya  kuwania tuzo ya heshima   ya sheria  za  vita  yaliyomalizika  hivi karibuni .


Katika  shindano hilo lililofanyika   kati ya Novemba   16-23 mwaka  huu  jijini  Arusha chuo  kikuu  cha Iringa  kiliwakilishwa na  washiriki  watatu  ambao ni Anneny Nahum ,Janeth Nagai   na Joanna Mcintype vijana  hao  waliweza kufanya  vema  kiasi  cha  kuiwezesha nchi ya Tanzania kuibuka mshindi  wa kwanza wa  tuzo hiyo.

Wakizungumza leo chuoni  hapo katika hafla  fupi ya kukabidhi  tuzo hiyo kwa uongozi wa  chuo hicho ,washirikia hao  walisema  kuwa  ushindi  huo  umetokana na ushirikiano  ulioonyeshwa na nidham iliyotukuka miongoni mwao.

Hata  hivyo  walisema  kuwa  tuzo  hiyo  ni  heshima kubwa kwa Tanzania  na ni heshima kwa  chuo  hicho .

mkuu msaidizi wa  kitivo cha  sheria chuo kikuu cha Iringa Jane  Massey alisema  kuwa washiriki hao  wamepata kushinda kutokana na kuonyesha  uwezo wa hali ya  juu katika mashindano hayo na  kuwa  heshima kubwa ambayo  chuo hicho  imepata  ni jambo na kujivunia na kumshukuru Mungu  pia. Alisema  kinachoangaliwa katika mashindano hayo na lengo la tuzo hiyo ni kuenzi amani na kuona hakuna matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu ambayo yanatokea wakati wa vita ,hivyo sheria  hiyo  inapaswa  kuendelea  kutolewa hata kwa Tanzania pia

Kwa  upande wake makamu Mkuu  wa  chuo   kikuu  cha Tumaini Iringa, Prof Nicholaus Bangu alisema  kuwa chuo  hicho  kitaendelea  kufanya  vema si katika mashindano pekee  bali katika mambo mbali mbali yakiwemo ya  kitaalum .

Kwani  alisema  kuwa moja kati  ya mambo  yanayozingatiwa katika  ufundishaji chuoni hapo ni pamoja na kuwafundisha  wanafunzi katika maadili na nidham na ndio mafanikio ya wanafunzi kufanya vema.

Tuzo  hiyo  ambayo  inatolewa kama  njia ya kumuenzi aliyekuwa mwanzilishi wa msalaba mwekundi  ilianzishwa  mwaka 2010 na  kuanza  kushindaniwa  mwaka 2011 ambapo ilichukuliwa na nchi  ya  Ephiopia  ilinyakuwa kwa mara ya kwanza na mwaka 2012 ilichukuliwa na Kenya na  mwaka huu Tanzania i meweza  kuzishinda nchi   hizo sita  ambazo ni South Afrika, Uganda,Kenya, Rwanda, Ethiopia na Zimbabwe

 
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Maafisa wa Israel wameshutumu vikali mkataba  wa nuklia na Iran uliofikiwa mapema Jumapili mjini Geneva. Wanasema mkataba huo kamwe huzuii Iran kuendelea na juhudi zake za kutengeneza silaha za nuklia.


Netanyahu alisema dunia inakabiliwa na hatari zaidi kutokana na kile alichoita utawala hatari zaidi duniani  ambao umepiga  hatua kubwa  katika azma yake ya kupata  silaha hatari duniani.

Bw. Netanyahu aliongeza kuwa Israel ina wajibu wa kujilinda kutokana na vitisho vyovyote vile na akaapa kuwa hatakubalia Iran kutengeneza silaha za nuklia.
Iran pamoja na nchi sita sita zenye nguvu duniani zilitangaza kufikiwa mkataba huo wa muda  Jumapili alfajiri baada ya siku nne za majadiliano mazito.

Mkataba huo unailazimu Iran kukubalia wakaguzi wa kimataifa wa silaha za nuklia kukagua viwanda vyake vya nuklia kwa maelewano kuwa ikiwa itatii masharti yote yaliyowekwa,haitawekewa vikwazo vya kiuchumi kwa miezi sita.

Lakini Israel na baadhi ya serikali za Magharibi zinasema zitafanya maamuzi zenyewe juu ya kutumia majeshi kushambulia viwanda vyovyote vile vya nuklia nchini Iran endapo zitagundua  kuwa vipo.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alishtumu vikali mkataba wa nuklia wa Iran mara tu ulipotangazwa akisema “ huu sio mkataba wa kihistoria, ni kosa la kihistoria.”


Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

Kufuatia  kuzingirwa na wanamgambo wenye silaha wako kwenye hatari ya kupata maradhi yatokanayo na maji machafu ikiwa hawatapata msaada wa haraka wa kibinadamu, lilionya Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya (KRCS) siku ya Jumanne (tarehe 26 Novemba).

Wanajeshi wakijiandaa kwenda kuwaokoa watu walio zingirwa.
"Hali ya kiafya inaweza ikawa mbaya zaidi kutokana na uwezekano mdogo wa kupata maji, huduma ya matibabu na chakula," alisema meneja wa KRCS kwa eneo la North Rift, Patrick Nyongesa, kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation la Kenya. "Wahanga hao, hasa watoto na wazee wasiojiweza, wana hatari ya kupatwa na homa ya mapafu na maradhi yatokanayo na maji kama vile kipindupindu kwa sababu ya uchafu."

Shirika la KRCS limesambaza msaada wa chakula na mengine iliyochangwa na serikali ya Kaunti ya Turkana kwa familia zilizookolewa.

Kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa huko, Lucas Ngasike, hali ya utulivu imerejea kwenye eneo hilo lakini licha ya kuwepo kwa jeshi, kuna wasiwasi sana.

Aliiambia Sabahi kwamba kulikuwa na hofu kwamba watu wa jamii ya Pokot nchini Uganda walikuwa wanapanga kuivamia jamii ya Turkana na kuwatoa kwenye eneo hilo, na matokeo yake jamii ya Turkana wanajihami kwa silaha.

Lakini msemaji wa polisi ya Kenya, Zipporah Gatiria Mboroki, alisema mzingiro wa kijiji hicho ulimalizika pale wazee wa huko walipoingilia kati na kuwashawishi wanamgambo kujiondoa.

"Utulivu umerejea na barabara imefunguliwa na hakuna mtu aliyejeruhiwa," alisema na kuongeza kwamba polisi bado walikuwa wanaondosha miti iliyowekwa njiani kuzuia kijiji hicho kufikika.

Shirika la KRCS limeitolea wito serikali ya Kenya kuunga mkono suluhisho endelevu kwa mzozo huo kati ya jamii hizo mbili, ikiashiria kwamba mgogoro huo si jambo jipya, kiliripoti kituo cha Capital FM cha Kenya.

 
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Rais akipokelewa katika uwanja wa Ndege wa Mwanza.
 
 
Na Atley Kuni.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, ameanza ziara ya siku tano Mkoani Simiyu kwa ajili ya ziara ya Kiserikali.
 
Hivi leo katika siku yake ya kwanza ameweka jiwe la Msingi katika mradi wa barabar wenye km. za mraba 71 kutoka Ramadi hadi Maswa kwa kiwango cha Lami kwa kutumia fedha za ndani.
 
Kwa mujibu wa taarifa iliyopatikana kutoka kwenye mamlaka ya Mawasiliano Ikulu, imesema rais akiwa Mkoani Simiyu atazindua, kuweka mawe ya Msingi na kufungua miradi mbali mbali ya Maendeleo inayo tekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na Wananchi.
 
Mkoa wa Simiyu unaundwa na Wilaya za Maswa na Bariadi zilizomegwa kutoka  Mkoani Shinyanga pamoja na jimbo la Busega lililokuwa Mkoani Mwanza.
 
Aidha kukamilika kwa barabara hiyo itakuwa ni kichocheo kikubwa cha maendeleo katika ukanda huo na Mkoa huo kwa ujumla, Mkoa ambao huzalisha zao la Pamba kwa wingi.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

MWENYEKITI wa Klabu ya Simba, Ismail Aden Rage ameliambia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania lililomtaka aitishe Mkutano Mkuu wa Dharura ndani ya siku 14, ili kutatua mgogoro kati yake na Kamati ya Utendaji.

Rage aliyasema hayo Dar es Salaam jana alipokutana na waandishi wa habari kuzungumzia agizo hilo sanjari na la Kamati ya Utendaji ya Simba iliyomsimamisha siku chache zilizopita.

“Kikao cha Kamati ya Utendaji kilichokaa na kuamua kunisimamisha ni batili kwa kuwa aliyeitisha mkutano huo hana mamlaka ya kufanya hivyo kwa Katiba ya Simba, hivyo ni sawa cha harusi,” amesema.

Amesema alidhani kwa kitendo hicho (kusimamishwa), TFF ingepinga jambo hilo kwa kuwa ni kinyume na taratibu za michezo kuhusu kufanya mapinduzi lakini na wao ndio kwanza wamempa siku 14 kuitisha mkutano.

Amesema kutokana na kukiukwa kwa Katiba ya TFF na Klabu ya Simba, hataitisha mkutano wowote kama alivyotakiwa ili naye asivunje Katiba na kama atalazimishwa kufanya hivyo yuko tayari kujiuzulu.

Rage ame tolea mfano wa msuguano uliotokea katika kipindi cha uchaguzi wa TFF uliofanya Serikali kuingilia kati sanjari na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kimataifa (Fifa), amesema baada adha hiyo kutokea, Fifa iliamuru TFF iitishe uchaguzi na kuwapangia tarehe na agenda.

Anadai kuwa  kitendo cha TFF kumwagiza kuitisha mkutano ndani ya siku 14 pamoja na kumchagulia agenda ni kinyume cha Katiba yake (TFF) , hivyo hatoitisha mkutano kama alivyotakiwa.

Akizungumzia kuhusu tuhuma zinazomakabili zilizochangia kusimamishwa kwake, kuhusu mshambuliaji wao za zamani, Emmanuel Okwi, alisema suala hilo linashughulikiwa na Ofisa wa Fifa anayeitwa Laura Santaniel.

Ameongeza kuwa suala la uchelewashaji wa fedha hizo ilitokana na klabu iliyomsajili ya Etoile du Sahel  (ESS) ya nchini Tunisia kukabiliwa na matatizo ya kiuchumi hali iliyofanya baadhi ya viongozi wa Simba akiwemo Hanspoppe kulifuatilia na sasa linashughulikiwa na Fifa.

Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Boniface Wambura alipotakiwa kueleza ni hatua gani zitachukuliwa ikiwa Rage hataitisha Mkutano Mkuu wa Dharura kama alivyoagizwa, alisema kwa kuwa bado siku 14 hazijaisha watasubiri ili kuchukua hatua nyingine.

“Tunashukuru kuwa amekiri kupokea barua yetu, hivyo tunasubiri hadi siku 14 ziishe ndio atajua TFF nini itafanya dhidi yake, tusubiri muda uishe na leo (jana) ikiwa ni siku ya pili, alisema.

Awali TFF ilitoa agizo la kumtataka Rage aitishe Mkutano Mkuu wa Dharura ili kumaliza mgogoro uliopo, kwa kutumia Ibara 1(6) ya Katiba ya Simba inayosema, “Simba Sports Club ni mwanachama wa TFF, itaheshimu Katiba, kanuni, maagizo na uamuzi wa TFF na Fifa na kuhakikisha kuwa zinaheshimiwa na wanachama wake.”

 

Wakati huohuo, Rage katika mkutano huo, alitangaza kumteua, Richard Wambura kuwa mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji wa klabu ya Simba.

Rage akizungumzia suala la kusaini Mkataba na Azam TV alisema suala hilo halihitaji shule kwa kuwa mhusika mkuu ni TFF, hivyo iwe isiwe ni lazima klabu isani na ndio sababu alifanya hivyo miezi minne iliyopita na klabu kupewa mil 100.

Akiweza wazi Rage alishangazwa kusikia Joseph Itang’ale na Evans Aveva kushiriki katika mazungumzo Zook na kubainisha kuwa yuko tayari kujiuzuru ikiwa Zouk watatoa mil 700.

 
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

1.    1. Utangulizi

Katika kikao chake cha siku mbili kilichofanyika tarehe 20 - 22 Novemba 2013, Kamati Kuu ya CHADEMA, pamoja na mambo mengine, iliazimia kunivua nafasi zangu zote za uongozi ndani ya chama. Kwa mujibu wa taarifa ya chama iliyotolewa katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Ijumaa tarehe 22 Novemba 2013, ilielezwa kwamba sababu za kuvuliwa uongozi mimi na Dk Kitila Mkumbo ni uhaini na hujuma kwa chama kutokana na waraka unaojulikana kama mkakati wa uchaguzi 2013. Ukweli ni kwamba waraka uliotajwa si sababu ya mimi kuvuliwa nafasi zangu za uongozi kama ilivyojadiliwa katika Kikao cha Kamati Kuu.

Sababu za kufukuzwa kwangu kama zilizojadiliwa katika kikao cha Kamati Kuu ni tuhuma lukuki ambazo si mara yangu ya kwanza kuzisikia zikijadiliwa ndani na nje ya vikao vya chama. Hitimisho la tuhuma hizi ni kwamba mimi nimekuwa nikikisaliti chama kwa kutumika na CCM na Usalama wa Taifa. Nitazianisha tuhuma hizi na kuzijibu kama ambavyo nimekuwa nikizijibu katika vikao mbalimbali vyama.

Ninatambua kwamba chama changu kinapita katika wakati mgumu sana sasa hivi. Nataka nitamke mapema sana kwamba mimi Zitto Zuberi Kabwe sitokuwa chanzo cha CHADEMA kuvunjika. Hiki ndicho chama kilichonilea na kunifikisha hivi nilivyo. Ningependa chama hiki mtoto wangu atakapokuwa mtu mzima na atakapoamua kujiunga na siasa aingie CHADEMA. Bado nina imani kubwa na chama changu na ninaamini ndicho kinachostahili kuendesha nchi jana, leo na kesho.

2. Kuhusu tuhuma mbalimbali zinazo elekezwa kwangu

Zipo tuhuma nyingi ambazo zimekuwa zikirudiwarudiwa katika vikao vya chama na nje ya vikao na baadhi ya viongozi wenzangu. Tuhuma hizi zinalenga kuonyesha kwamba mimi ni mbinafsi na kwamba ninapokea rushwa ili kukihujumu chama changu. Nitazianisha tuhuma kwa kifupi na kuzijibu kama ambavyo nimekuwa nikizijibu katika vikao mbalimbali vya chama.

i) Tuhuma kwamba sikushiriki kumpigia kampeni mgombea wetu wa urais katika uchaguzi wa mwaka 2010. Ningependa kueleza yafuatayo kuhusu jambo hili:

Mimi nilikuwa mgombea wa ubunge katika Jimbo la Kaskazini huko Kigoma.
Pamoja na kuwa mgombea wa ubunge, nilifanya kampeni katika majimbo mengine 16 katika mikoa mbalimbali, ikiwemo Dar es Salaam, Mtwara, Pwani, Shinyanga, Mara na Rukwa. Hakuna kiongozi yeyote wa juu aliyefanya kampeni katika majimbo mengi kama mimi, ukiacha mgombea urais.
Kote nilipopita nilimpigia kampeni wagombea wetu wa udiwani, ubunge na Rais.
Katika Mkoa wa Kigoma nilizunguka na mgombea urais katika kata zote za Kigoma Kaskazini na majimbo yote manane ya Mkoa wa Kigoma.


ii) Tuhuma kwamba katika Mkoa wa Kigoma nilishindwa kuwapigia kampeni wagombea wetu kiasi kwamba peke yangu ndiye niliyeshinda katika uchaguzi huo. Ukweli ni kwamba niliwapigia sana kampeni wagombea wetu, na hivyo ndivyo wapiga kura wa Kigoma walivyoamua.

iii) Tuhuma kwamba nilishiriki kuwashawishi wagombea wetu katika baadhi ya majimbo kujitoa katika uchaguzi wa mwaka 2010 ili kuwapisha wagombea wa CCM wapite bila kupingwa kwa njia ya rushwa. Majimbo yanayotajwa ni pamoja na Sumbawanga, Musoma Vijijini na Singida Mjini. Kama nilivyokwisha kueleza katika vikao mbalimbali vya chama jambo hili si la kweli na hakuna popote ambapo watoa tuhuma hizi wamewahi kutoa ushahidi kwamba nilifanya jambo hili. Nipo tayari kwa uchunguzi ndani ya chama na watoa tuhuma waje na ushahidi bayana wa jambo hili. Si afya kwa chama kuendelea kurudiarudia tuhuma hizi kila mara tangu mwaka 2010 bila uchunguzi wowote kufanyika na jambo hili lifikie mwisho.

iv) Tuhuma kwamba nimekuwa sishiriki katika operesheni mbalimbali za chama: Ukweli ni kwamba nimeshiriki sana katika operesheni mbalimbali za chama ndani na nje ya nchi. Kwa mfano, mwaka 2011 tulikuwa na operesheni kubwa katika mikoa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini na nilikwenda katika mikoa yote tuliyotembelea. Mwaka 2012 baada ya hoja ya mkonge bungeni nilifanya ziara Mkoa wa Tanga. Mwaka 2012 kulikuwa na operesheni kubwa moja katika mikoa ya kusini ya Mtwara na Lindi. Operesheni hii sikushiriki kwa sababu nilikuwa nchini Marekani kufungua matawi kwa mwaliko wa Watanzania wanaoishi huko.

v) Tuhuma kwamba nimekidhalilisha chama kwa tamko la PAC kwamba Hesabu za Vyama hazijakaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG): Katika jambo hili ninatuhumiwa kwamba mimi kama Naibu Katibu nilipaswa kuwasiliana kwanza na viongozi wa chama 'kuwatonya' ili wajiandae. Kwamba kutokuwatonya kumekidhalilisha chama na kukiweka kundi moja na CCM na nastahili kuadhibiwa vikali kwa kuwa katika taarifa yangu nilikuwa na nia mbaya na chama chetu. Maelezo yangu niliyoyatoa na ambayo ningependa kuyakariri hapa kuhusu jambo hili ni kama ifuatavyo:

Utawala bora hautaki mimi kutumia nafasi yangu ya uenyekiti wa PAC kulinda chama changu na kuonea vyama vingine. Kufanya hivyo ni kuendeleza tabia zile zile ambazo tunazipinga na ambazo tunapigania kuzibadilisha
Napenda kusisitiza kwamba hakuna chama ambacho kimewahi kukaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG). Natambua kwamba mahesabu ya chama changu yamekuwa yakikaguliwa na wakaguzi wa nje kwa utaratibu tuliojiwekea. Lakini matakwa ya kisheria ni kwamba mahesabu ya vyama vya siasa hayajakaguliwa na CAG, na hili ni kosa la kisheria, bila kujali kosa hili ni la nani.


vi) Tuhuma kwamba mimi ni mnafiki katika kukataa kwangu kuchukua Posho za Vikao
Mtakumbuka kwamba mimi nilikataa kuchukua posho tangu mwaka 2011 kama ishara ya kuonyesha kwa vitendo msimamo wa chama chetu wa kupinga posho za kukaa na matumizi mengine yasiyofaa katika fedha za umma kama ilivyoanishwa kwenye Ilani yetu ya mwaka 2010-2015. Mtakumbuka kwamba hivi karibuni Mheshimiwa Lema amenishutumu kwamba kukataa kwangu kuchukua posho ni unafiki kwa sababu ninapokea posho kubwa zaidi katika mashirika ya umma ambapo mimi ni mwenyekiti wa kamati husika. Ninapenda kueleza yafuatayo kuhusu jambo hili:

Sipokei posho yeyote ya vikao (sitting allowance) ndani na nje ya Bunge tangu mwaka 2011. Hii ni pamoja na vikao vyote katika Kamati za Bunge ninavyohudhuria. Mtu yeyote mwenye ushahidi vinginevyo auweke hadharani.
Swala la kukataa posho (sitting allowance) ni swala la kiilani katika chama chetu, na kwangu ni swala la kimisingi zaidi. Katika Wilaya yangu vifo vya kina mama wajawazito ni 1900 kati ya wanawake 100,000 wenye ujauzito. Vifo hivi vinatokana na ukosefu wa huduma kwa sababu ya bajeti finyu. Ndiyo maana nilifurahi sana kwa chama chetu kuliweka swala la kupunguza matumizi ya Serikali katika Ilani, na kuondoa posho za wabunge, ambao tayari wanapokea mishahara mikubwa, kungesaidia sana kupatikana fedha ambazo zingeokoa vifo vingi vya kina mama.
Jambo hili si suala la ugomvi baina yangu na Mheshimiwa Lema. Ni suala la msingi katika chama chetu.3. Usambazaji wa Ripoti ya Siri kuhusu Zitto Kabwe
Hivi karibuni kulisambazwa waraka unaoitwa ripoti ya siri kuhusu mimi ukibeba lundo la tuhuma kwamba nimehongwa fedha nyingi ili kukihujumu chama changu. Waraka huu ulidaiwa kuwa umechomolewa kutoka makao makuu ya CHADEMA. Jambo hili pia lilijadiliwa katika kikao cha juzi kwa kifupi, na majibu ya viongozi wa chama ilikuwa ni kwamba waraka huu haukuandaliwa wala kusambazwa na makao makuu. Katika mchango wangu nililalamikia mambo matatu yafuatayo:

Kwamba baadhi ya waliokuwa wanasambaza waraka ule walikuwa ni viongozi wa chama chetu. Bahati mbaya hadi leo hakuna hata mmoja ambaye amekwishachukuliwa hatua za kinidhamu. Ninaamini kwamba kuna siku watu hao watachukuliwa hatua kwa mujibu wa taratibu za chama chetu.
Kwa kuwa chama kimekana rasmi kuhusika na waraka huu, nitaendelea na taratibu za kisheria ili kuhakikisha kwamba wote waliohusika kutengeneza hekaya ile wanachukuliwa hatua stahiki za kisheria.4. Hitimisho
Ninatambua kwamba kuna watu walitegemea leo ningejibu mapigo na ningewazodoa watu kwa majina kama ilivyo kawaida katika siasa za Tanzania. Natambua pia kwamba, kama ilivyo kawaida wakati wa migogoro katika vyama vya siasa hapa Tanzania, kuna watu walitegemea leo ningetangaza 'maamuzi magumu'. Natambua kwamba wapo ambao wangependa kupata nafasi ya kuendelea kutumia suala hili katika harakati zao za kudhoofisha mapambano ya demokrasia na uthabiti wa siasa za ushindani nchini mwetu. Napenda wanachama wa CHADEMA na wapenda demokrasia na siasa safi wote nchini watambue kwamba mimi bado ni mwanachama mwaminifu wa chama hiki na nitakuwa wa mwisho kutoka kwenye chama hiki kwa hiari yangu. Nitafuata taratibu zote ndani ya chama katika kuhitimisha jambo hili.

Naomba wanachama waelewe kwamba mimi kama binadamu ninaumia ninapopigwa. Tuhuma ninazorushiwa ni kubwa na zinanikwaza. Tuache siasa za uzushi ili tujenge chama chetu na nchi yetu, ili hatimaye tuwakomboe Watanzania wenye matarajio na imani kubwa kwa chama chetu.

Kama mwanasiasa kijana niliyekaa katika siasa kwa muda sasa yapo mengi mazuri nimeyafanya. Lakini kuna maeneo nilipojikwaa na yapo makosa niliyofanya kisiasa katika maisha yangu ya siasa.

Kinachoendelea ndani ya chama chetu ni mapambano ya kukuza demokrasia. Ni mapambano baina ya wapenda demokrasia dhidi ya wahafidhina, waumini wa uwajibikaji dhidi ya wabadhirifu na wapenda siasa safi dhidi ya watukuzao siasa majitaka. Hii ni changamoto kubwa ndani ya chama chetu inayohitaji uongozi shupavu kuikabili. Nitasimama daima upande wa demokrasia. Kama alivyopata kunena mmoja ya wanasiasa maarufu, 'kiwango cha juu kabisa cha uzalendo katika nchi ni kukubali kutofautiana kimawazo', na ninatamani huu ndio uwe utamaduni wa chama chetu.


Kabwe Zuberi Zitto, Mb
Dar es Salaam.
24 Novemba, 2013

Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

 

Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete alipokutana na Mjumbe wa UN. Ikulu JIji Dar es Salaam

Mary Robinson Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Ukanda wa Maziwa Makuu ya Afrika amewasili nchini Tanzania, akiwa katika safari ya kiduru itakayochukua muda wa wiki moja katika nchi za eneo hilo.

Mara baada ya kuwasili mjini Dar es Salaam, Bi Robinson ameunga mkono juhudi kubwa zinazofanywa kwa ajili ya kurejesha amani  mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Aidha mwakilishi huyo wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, analipa kipaumbele kwenye safari yake hiyo suala la kufikiwa kwenye tija na mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Kinshasa na waasi wa M23 huko Kampala Uganda.

Taarifa zinasema kuwa, jana Bi Robinson alikutana na Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania, ambapo nchi hiyo hivi sasa inaongoza kikosi cha Umoja wa Mataifa kinachopambana na makundi ya waasi mashariki mwa Kongo. Imeelezwa kuwa, mwakilishi huyo wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Maziwa Mkuu ya Afrika leo ataelekea Rwanda na baada ya hapo ataelekea nchini Kongo Brazzaville.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

 

Ujerumaini imeamua kupiga marufuku simu zote za "smart" aina ya iPhone baada ya afisa mmoja wa zamani wa kijasusi wa Marekani Edward Snowden kufichua kuwa, simu aina hiyo zilitumika kufanyia ujasusi mazungumzo ya simu ya viongozi wa nchi 35 duniani.

Kabla ya hapo ilibainika kuwa, Wakala wa Usalama wa Taifa wa Marekani NSA ulikuwa unadoya na kudukua mazungumzo ya simu ya Kansela wa Ujerumaini, Angela Merkel tangu mwaka 2002, ujasusi ambao umeikasirisha mno Bundestag (bunge la Ujerumani).

Huku hayo yakiripotiwa, wabunge wa vyama viwili vikuu katika bunge la Ujerumani wamepasisha sheria inayowapiga marufuku wabunge wa nchi hiyo na viongozi wote wa ngazi za juu serikalini kutumia simu ambazo hazina kinga ya kufanyiwa ujasusi yaani simu zisizo na chujio la kudhibiti mawasiliano na barua.

Imebainika kuwa machujio hayo hayawezi kufanya kazi kwenye simu za "smart" aina iPhone zinazotengenezwa na shirika la Apple la Marekani na hivyo kuwapiga marufuku wabunge na viongozi wa ngazi za juu wa Ujerumaini kutumia simu hizo maarufu.

Wachambuzi wa mambo wanaamini kuwa, kutofanya kazi programu  hizo zinazokusudiwa na wabunge wa Ujerumaini ambazo zinachuja mazungumzo na barua katika simu ya iPhone kumetumiwa kama kisingizio tu bali ukweli wa mambo ni kuwa shirika la Apple lina makubaliano ya siri na Wakala wa Usalama wa Taifa wa Marekani NSA yanayoruhusu mawasiliano yote ya simu za iPhone yapitishwe kwenye chujio linalowasilisha taarifa zake moja kwa moja kwa wakala huo wa kijasusi wa Marekani.

 
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

.

Jumla ya Waendesha Pikipiki 1167 wamepatiwa mafunzo ya kuendesha Pikipiki na kupatiwa Leseni daraja “A” katika kipindi cha Januari – Agosti, 2013.

 

Boda boda hii kama ilivyonaswa ikiwa imekiuka sharia usalama barabarani.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo mtandao huu umezipata ni kwamba mpango huo unatekelezwa baina ya Polisi Mkoa wa Mwanza, VETA na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) unao lengo la kupunguza tatizo la ajira kwa Vijana pamoja na kuepusha ajali za barabarani zinazo weza kusababishwa na makosa ya kizembe kutokana na kutijua sharia.

 

“Ni kweli tuna mpango wa kuwafanya Vijana waweze kujiajiri wenyewe ili kuweza kujiongezea kipato lakini pia mpango huu unasaidia kupunguza ajali za barabarani” aliniambia Sajini Kitia wa jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza kitengo cha usalama barabarani tuliyezungumza naye kwa njia ya simu.

 

Imeelezwa pia katika mpango huo Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza kwa kushirikiana na Chuo cha Ufundi VETA, huwapatia mafunzo na badaye jeshi la polisi kwa ushirikiano na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), huwakatia Leseni za daraja “A” na kuwasajili kwenye maeneo wanayofanyia kazi pamoja na kufatilia mwenendo wao wa kazi za kila siku.

 

Ni kwamba kiwango cha ajali kimepungua kwa asilimia 17.8% ikilinganishwa na kipindi kama hicho cha Januari – Augusti, 2012, ambapo kulitokea ajali 118, ikilinganishwa na ajali 97 kwa kipindi hicho hicho cha Januari hadi Agost 2013.

 

Mpango huo unafuatia agizo lililotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kuwaelekeza  Viongozi wa Polisi Mkoani hapa kubaini mbinu zitakazosaidia kupunguza ajali za barabarani kwa asilimia ikilinganishwa na mwaka uliopita 50%.

Hivi sasa Mkoani humo hali imekuwa tofauti ilinganishwa na siku za nyuma wakati biashara hiyo yakundesha pikipiki ikonekana kama biashara haramu na iliyokuwa ikipoteza nguvu kazi ya taifa kutokana na ajali zilizokuwa zikitokea.

Hata hivyo uchunguzi uliofanywa na Blog hii ya kuninews.blogspot, umeonsha kwa bado kuna baaadhi ya waendesha boda boda wasiotii sheria  kwa kupakiza abiria zaidi ya mmoja huku wakiwa hawana kofia ngumu za kujikinga na ajali.

 
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

MBWANA SAMATTA AKIWA ANAONESHA VITU VYAKE UWANJANI.
Shirikisho la kandanda barani Afrika CAF limetangaza majina ya wachezaji wa kiafrika watakaowania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka 2013 na Mchezaji bora wa Afrika anayechezea vilabu vya ndani ya Afrika mwaka 2013.

Katika majina hayo yapo majina mawili ya wachezaji wanaotoka Afrika Mashariki ambao ni Victor Wanyama raia wa Kenya anachezea Southampton FC ya England ambaye ni miongoni mwa wachezaji 25 watakaowania tuzo ya Mchezaji bora wa Afrika, huku Mbwana Samatta raia wa Tanzania anayechezea klabu ya TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo yeye ameteuliwa kuwania tuzo ya Mchezaji bora wa Afrika anayechezea timu za Afrika.

Wachezaji 25 watawania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika na 21 Mchezaji bora wa Afrika anachezea timu za ndani ya Afrika.

Washindi wa tuzo hizo wanatarajiwa kutangazwa Januari 9, mwaka 2014 mjini Lagos nchini Nigeria.

Orodha kamili ya wachezaji waliotangazwa na CAF na timu wanazotoka hii hapa chini.

Mchezaji wa bora wa CAF Afrika

1. Ahmed Musa - Nigeria - CSKA Moscow

2. Asamoah Gyan - Ghana - Al Ain

3.Dame N'Doye - Senegal - Locomotiv Moscow

4. Didier Drogba - Cote d'Ivoire - Galatasaray

5. Emmanuel Emenike - Nigeria - Fenerbahce

6. Islam Slimani - Algeria - Sporting Lisbon

7. John Mikel Obi - Nigeria - Chelsea

8. Jonathan Pitroipa - Burkina Faso - Stade Rennais

9. Kévin Constant - Guinea - AC Milan

10. Kwadwo Asamoah - Ghana - Juventus

11. Luís Carlos Almada Soares (platini) - Cape Verde - AC Omonia

12. Mehdi Benattia - Morocco - AS Roma

13. Mohamed Aboutrika - Egypt - Al Ahly

14. Mohamed Salah - Egypt - Basel FC

15. Nicolas Nkoulou - Cameroon - Marseille

16. Pierre-Emerick Aubameyang - Gabon - Borussia Dortmund

17. Ryan Isaac Mendes da Graça - Cape Verde - Lille

18. Saladin Said - Ethiopia - Wadi Degla FC

Victor Wanyama

19. Seydou Keita - Mali - Dalian Aerbin F.C

20. Sofiane Feghouli - Algeria - Valencia

21. Sunday Mba - Nigeria - Warri Wolves

22. Victor Wanyama - Kenya - Southampton FC

23. Vincent Enyeama - Nigeria - Lille

24. Yao Kouassi Gervais 'Gervinho' - Cote d'Ivoire - AS Roma

25. Yaya Toure - Cote d'Ivoire - Manchester City

Mchezaji bora Afrika anacheza vilabu ndani ya Afrika

1. Adane Girma - Ethiopia - St George

2.Ahmed Fathi - Egypt - Al Ahly

3. Alexis Yougouda Kada - Cameroon - Coton Sport

4. Ali Machani - Tunisia - CAB

5. Bapidi Fils Jean Jules - Cameroon - Coton Sport

6. Daine Marcelle-Klate - South Africa - Orlando Pirates

7. Fakhreddine Ben Youssef - Tunisia - CSS

8. Getaneh Kebede - Ethiopia - Bidvest Wits

9. Idrissa Kouyate - Cote d'Ivoire - CS Sfaxien

10. Iheb Msakni - Tunisia - Esperance

11. Luyanda Lennox Bacela - South Africa - Orlando Pirates

12. Mbwana Samatta - Tanzania - TP Mazembe

 

Mbwana Samatta

13. Moez Ben Cherifia - Tunisia – EST

14. Mohamed Aboutrika - Egypt - Ahly

15. Rainford Kalaba - Zambia - TP Mazembe

16. Senzo Meyiwa - South Africa - Orlando Pirates

17. Soumbeila Diakite - Mali - Stade Malien

18. Sunday Mba - Nigeria - Warri Wolves

19. Tresor Mputu - DR Congo - TP Mazembe

20. Waleed Soliman - Egypt - Al Ahly

21. Yannick N'djeng - Cameroon - EST.
 
 
Kwa hisani Idhaa ya Kiswahili ya BBC.

 
no image
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya kisiasa Jeffrey Feltman amesema katika kikao cha Baraza la Usalama kwamba ujenzi haramu wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi unaofanywa na Israel katika ardhi za Palestina unazozikalia kwa mabavu umekuwa na taathira hasi kwa mazungumzo kati ya Wapalestina na Israel.

Akielezea hali inavyojiri katika Mashariki ya Kati, Feltman amesema, mazungumzo ya kusaka amani kati ya Palestina na Israel baada ya kupita miezi minne tangu yaanze yamefikia katika hali tete ambapo pande mbili zinajadili maudhui muhimu. Ameongeza kwamba, mwenendo wa mazungumzo hayo unakwamishwa na ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika Ukingo wa Magharibi likiwemo eneo la Quds Mashariki na kwamba Umoja wa Mataifa unafuatilia kadhia hiyo kwa wasiwasi mkubwa. Afisa huyo wa UN ameeleza kwamba, maafisa wa juu wa kimataifa akiwemo Ban Ki-moon Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa mara nyingine wamesisitiza msimamo wao kwamba vitongoji vya walowezi wa Kizayuni si halali na kubainisha kuwa, ujenzi huo unakinzana na sheria za kimataifa na unakwamisha mwenendo wa amani.

Feltman amesema, maafisa wa Umoja wa Mataifa wanataka Israel isimamishe mara moja ujenzi huo na kusisitiza ulazima wa kuundwa nchi huru ya Palestina kama njia pekee ya kustawishwa amani na usalama wa eneo hilo.

Sisitizo la jamii ya kimataifa kuwa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika maeneo ya Palestina ni kinyume cha sheria na kwamba hatua hiyo ya Israel ni pingamizi kwa mwenendo wa amani, kwa mara nyingine limeweka wazi utambulisho usio wa amani wa utawala huo na kukinzana kwake na sheria na kanuni za kimataifa.

Ijapokuwa malalamiko ya kimataifa dhidi ya siasa za kupenda kujitanua za Israel hasa ujenzi wa vitongoji yameongezeka, lakini utawala huo ghasibu bila kujali malalamiko hayo unaendeleza hatua hizo kutokana na uungaji mkono wa madola ya Magharibi hasa Marekani. Matamshi yaliyotolewa na Waziri wa Nyumba wa Israel yanaonesha kuwa, Tel Aviv sio tu haijasimamisha ujenzi wa vitongoji kwenye maeneo ya Palestina bali pia inaendelea kujenga nyumba mpya na kupanua vitongoji vya walowezi wa Kizayuni huku mazungumzo hayo yakiendelea. Auri Ariel amesema kuwa, sehemu kubwa ya ujenzi wa vitongoji vya utawala huo katika maeneo tofauti ya Palestina haikusimamishwa na bado unaendelea hata wakati wakati huu wa mazungumzo. Hii ni katika hali ambayo, Bunge la Israel limetenga bajeti kubwa kwa ajili ya kuendeleza shughuli hizo.

Kung'ang'ania Israel kujenga vitongoji hivyo licha ya Umoja wa Mataifa kutangaza kuwa ni kinyume cha sheria, kunabainisha kwamba utawala huo unaokalia kwa mabavu Quds Tukufu hauheshimu sheria na maazimio ya kimataifa na unaendeleza siasa hizo za kujitanua ili ufikie malengo yake haramu.

Lengo la utawala wa Kizayuni la kujenga vitongoji vya walowezi katika maeneo ya Wapalestina ni kubadilisha muundo wa kijamii na kijiografia wa maeneo hayo na kuyafanya yawe na sura ya Kizayuni ili uendelee kukalia kwa mabavu maeneo tofauti ya Palestina. Vilevile Israel kwa kujenga vitongoji hivyo vya walowezi wa Kizayuni, inakusudia kuyatenganisha maeneo ya Palestina ili izuie kivitendo kuundwa nchi huru ya Palestina.

Itakumbukwa kuwa suala la kuundwa nchi huru ya Palestina linahesabiwa kuwa ni haki ya mwanzo kabisa na isiyokuwa na shaka ya wenyeji wa asili wa ardhi ya Palestina, haki ambayo inasisitizwa pia na viongozi wa Umoja wa Mataifa akiwemo Jeffrey Feltman.