November 2014
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

MKUU WA MKOA WA MWANZA MAGESA MULONGO AKITOA MAELEKEZO KWA WATENDAJI.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mgesa Mulongo, amewaagiza wakurugenzi wote kuhakikisha Ujenzi wa  vyumba vya Maabara unakamilika ifikapo Novemba 30 na kinyume na hapo basi itabidi kila mmoja awajibike.

Mulongo ameyasema hayo katika siku yake ya kwanza kikazi mkoani humo alipo wasili kwa ajili ya  kuripoti tangu alipoteuliwa na Rais kushika wadhifa huo Novemba 5 mwaka huu.

Amesema kwakuwa wenyeviti wa mabaraza ya madiwani wote walisha onesha nia kwa kusukuma na kuhimiza ujenzi huo wa maabara na tayari kamati za fedha zilikwisha idhinisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa maabara lililopo kwa sasa ni kuhakikisha mamlaka zinazo takiwa kupeleka fedha kwa ajili ya ujenzi  zitekeleze majukumu yake huku akiwakazia sauti wakurugenzi wa halmashauri.

Amesema amekuja kuwaomba licha ya kwamba ni mgeni katika mkoa huo, huku akimuagiza Katibu Tawala Mkoa kuhakikisha kuwa kila siku taarifa ya ujenzi wa maabara zinawasilishwa mezani kwake na hatua zilizo fikiwa “Nimekuja kuwaomba na nazidi kuwaomba nazidi kuwaomba tena leo natumia nafasi hii na ugeni wangu huu kamalizeni maabara,  alisema na kuongeza kuwa ataendelea kulifatilia suala hilo kwa kufanya Monitoring yeye mwenyewe.

Aidha amehimiza kuwa wakurugenzi wahakikishe taarifa hizo zinasainiwa na wakurugenzi wenyewe na sio watumishi wengine wanao kaimu ofisi za wakurugenzi.
Ameawaambia wakuu wa Wilaya ikifika tarehe 30 Novemba, kama hakuna maabara hajui ni hatua zipi zitakazo fuata kwakuwa  wakati maelekezo yanatolewa na Rais wakuu hao wawilaya walikuwepo na kila mmoja alisaini moyoni mwake kuhusiana na ujenzi wa maabara hizo.
Mkuu huyo wa Mkoa alikuwa katika siku yake ya kwanza mkoani humo
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Na: Mdau Kutoka Ruvuma.


Bomu lililotengenezwa kienyeji  kama linavoonekana katika picha.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela akipata maelekezo kutoka kwa mtaaram wa mabomu ambaye ni kamanda wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) kabla ya kulitegua bomu hili.


Hili ni eneo la tukio ambalo limezungushiwa mkanda huu wa pilisi uliandikwa hairuhusiwi kupita eneo hili,Lakini chini ya huo mti kama inavoonekana katika picha kukiwa na udongo umetifuliwa ndipo mahara ambapo lilitegwa bomu hili la kutengenezwa kienyeji pia hapo ndipo huwa wanakaa askari wa Usalama barabarani kwa kujikinga na jua ama kupumzika pindi wanapokuwa kazini

Bomu lililotengenezwa kienyeji
Mtaaramu toka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania akiweka vifaa vyake vya kutegulia bomu hilo lililo tengenezwa kienyeji.

Mtaalamu kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania akiwa anaonyesha umahili wake alionao aweze kulitegua bila kuleta madhara yoyote yale katika jamii(Picha na demasho.com)
 

 Jeshi la polisi kwa kushirikiana na Jeshi la Ulinzi la wananchi Tanzania(JWTZ) wamefanikiwakutegua bomu lililotegwa katika eneo la kituo cha kurushia matangazo kilichopo Mshangano cha shirika la utangazaji Tanzania (TBC) Songea Mkoani Ruvuma siku yachache zilizopita.

Bomu hilo linalosadikiwa kutengenezwa kienyeji na watu wasiojulikana lilitegwa hatua  zinazokadiliwa thelathini kutoka katika kituo kilipo katika eneo ambalo askari wa usalama barabarani wanakaa kwa ajili kufanya kazi zao za kila siku.

 Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela amesema, kwamujibu wa wataalamu wa milipuko kutoka jeshi la Ulinmzi la wananchi wa Tanzania bomu hili linaonekakana limetengenezwa kienyeji.
 
Katika hatua nyingine ameitaka jamii kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili liweze kuwabaini watu waliohusika kayika utegaji wa  bomu hilo  lililotengenezwa kienyeji.
Msikhela amesema Jeshi la polisi linafanya jitihada za kuwapata watu walio husika na mtandao huu wa utegaji wa mabomu na ulipuaji,

 Hii ni mara ya pili katika manispaa ya songea kutokea kwa matukio haya ambapo tarehe Oktoba 16 mwaka huu askari watatu wa jeshi la polisi katika wilaya ya Songea mkoani Ruvuma,  walijeruhiwa kwa kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu la kutupwa kwa mkono ambalo lilisadikiwa kutengenezwa kienyeji, katika eneo la matarawe mjini songea mkoani Ruvuma.

Askari hao walikutwa na mkasa huo saa moja na nusu usiku wakati wakiwa katika doria ambao ni WP Felista Abel, PC John Kaduma na PC Ramadhani Ally

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songea Joseph Mkirikiti akizungumza na mtandao huu   kwa njia ya simu amesikitishwa na kitendo hicho cha utegeji wa Mabomu ikiwa nikutaka kuhatarisha amani iliyopo katika mkoa huu wa Ruvuma.
Aidha amesema serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama watahakikisha wanawasaka na kuwakamata wale wote walio husika na vitendo hivi.