November 2016
no image
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

Na Lorietha Laurence-Mwanza.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella  amiomba Bodi ya Filamu Nchini, kutazama namna yakuwasaidia wasanii wa filamu nchini  kwa kuwajengea uwezo wa namna ya kuwapa mbinu za uendeshaji, ujasiliamali na biashara  wadau hao ili waweze kupenya katika soko la filamu.
 
Akifunga mafunzo ya siku tatu yaliyo washirikisha wasanii wa Filamu nchini, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.Mary Tesha ambaye ni mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, aliyasema alianza kwa kuipongeza Bodi ya Filamu Nchini kwa,
 
“Kwanza naipongeza Bodi ya Filamu Nchini kwa kuandaa warsha hii nzuri ambayo wadau wangetakiwa kuilipia lakini wameipata bure hii ni kwa jinsi gani Serikali inawajali watu wake  hivyo naomba wakati mwingine mtakapotoa warsha mada kuhusu biashara na ujasiliamali ziwepo” alisema Mhe.Tesha

Vilevile Mhe.Mary amempa siku saba Afisa Utamaduni  mkoani hapo Bw. James Willium, kuhakikisha kuwa anayafanyia kazi maadhimio yaliyoafikiwa na wasanii wa filamu mkoa wa Mwanza.

Mkuu wa Wilaya huyo amesema Afisa Utamaduni huyo, kwa kushirikiana na Maafisa Utamaduni wa Halmashauri zote za mkoa wa Mwanza wanapaswa kuhakikisha wanatoa mikakati ya utekelezaji wa maadhimio yaliyotolewa kwenye warsha hiyo ili utekelezaji huo uanze mara moja.

Naye  Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fesso, amesema  lengo la warsha hiyo ni pamoja na  kuwajengea weledi wadau wa filamu waweze  kutengeneza kazi zenye ubora ili kukuza soko la filamu na hivyo kunufaika na kazi zao.

Warsha hiyo ya siku tatu ilihitimishwa kwa mgeni rasmi kutoa vyeti vya ushiriki kwa wadau wa filamu zaidi ya  300 ambapo waliweza kujifunza mada mbalimbali zilizowasilishwa  na wawezeshaji kutoka katika vyuo Vikuu vya Dodoma na Dar es Salaam,Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania pamoja na Bodi ya Filamu nchini .

Mwisho.

 

 

 

 

 
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

MWAKILISHI WA KATIBU TAWALA MKOA WA MWANZA, MWALIMU HAMISI MAULIDI AKIFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO, WAANDAAJI WA FILAMU NCHINI.
PICHANI NI BIBI JOYCE FISOO, KATIBU MTENDAJI WA BODI YA FILAMU NCHINI, AKIWASILISHA MADA WAKATI WA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZOWANATSNIA YA FILAMU MKOANI MWANZA.


RAIS WA SHIRIKISHO LA FILAMU TANZANIA BW. SAIMON MWAKIFWAMBA(KULIA), AKIFAFANUA JAMBO KWA MAAFISA WA  WA HIFADHI YA JAMII WA PPF KANDA YA ZIWA.
Na Lorietha Laurence-Mwanza

Mkoa wa Mwanza waweka mkakati  wa kukuza na kuendeleza sekta ya filamu kwa kuhakikisha inazalisha bidhaa bora zenye kufuata taaluma na weledi wa tasnia hiyo ili kufikia soko la kimataifa.