December 2014
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

. Yazipiku Nyamagana, Ilemela.

. Yafaulisha kwa asilimia 78.9

. Magu yaing'ang'ania nafasi ya tatu.

KATIBU TAWALA MKOA WA MWANZA, DK. FAISAL ISSA ALIPOKUWA AKIFUNGUA KIKAO HICHO CHA KUTANGAZA MATOKEO.
Wilaya ya Ukerewe imeibuka kidedea katika matokeo ya darasa la saba kwa mwaka 2014 na kuzipiku wilaya za Nyamagana na Ilemela ambazo mwaka 2013 zilishika namba moja na mbili ambazo zilifikia ufaulu wa asilimia 74.6 kwa Nyamagana na Ilemela iliyo faulisha kwa asilimia 71.3, hali imekuwa tofauti kwa mwaka huu wa 2014 ambapo wilaya ya Ukerewe iliyongoza, imefikia asilimia 78.9  na kuzidi ufaulu wa mwaka 2013 wa  Nyamagana iliyopata asilimia 77.2 na Ilemela asilimia 72.2 na kufanikiwa kuwa namba moja.
 
Wakati huo huo Ilemela imezidiwa na Wilaya ya Magu iliyoshika nafasi ya tatu kwa mwaka huu na kuisukuma Ilemela hadi nafasi ya nne na kuizidi kwa kupata asilimia 75.5 hali inayo chagiza  kuwa huenda kama kasi hiyo itaendelea basi zipo dalili za wazi kuwa Wilaya za pembezoni mwa mji kuongoza katika miaka ijayo na Wilaya za mjini kushushwa katika suala la ufaulu.
Akitangaza matokeo hayo ya darasa la saba kwenye sekondari ya Mwanza hivi karibuni, Afisa Elimu wa Mkoa wa Mwanza, Mwalimu Hamis Maulid, alisema "Tarehe 10/9/2014 na  11/9/2014 mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi ulifanyika hapa nchini.  Mkoa wa Mwanza ulishiriki katika zoezi hilo,  na jumla ya wanafunzi 54384 walitarajiwa kufanya mtihani huo, kati yao wavulana walikuwa 25889 na wasichana ni 28495 anasema Wanafunzi wote hawa ni kutoka katika jumla ya shule za msingi 891 zilizoshiriki mtihani huo" anasema Maulid na kuongeza kuwa, mbali ya Wilaya ya Ukerewe kuwa na ufaulu mzuri lakini pia imesaidia kuinua ufaulu wa mkoa  mzima wa Mwanza ambao uko chini ya mpango wa Tekeleza sasa kwa matokeo makubwa (BRN) na kuifikia wastan wa asilimia 69.07 kutoka asilimia 57.9 za mwaka 2013 ongezeko la zaidi ya asilimia 10 ambalo sasa linakaribia tarajio la BRN la mwaka 2014 la ufaulu wa asilimia 72. hata hivyo mkoa unabakia katika kibarua kigumu cha kufikisha ufaulu wa asilimia 82 kwa mwaka ujao wa 2015
 
Mbali ya ufaulu huo mkoa pia umeweza kushika nafasi ya 3 kitaifa katika mikoa 25 na umefanikiwa kuingiza shule  19 bora kati ya  shule bora 100, huku shule ya Mugini iliyopo Wilayani magu ya  ikishika nafasi ya pili kitaifa na  ya kwanza kimkoa.
 
AFISA ELIMU MKOA AKIJADILIANA JAMBO NA
KATIBU TAWALA MKOA WAKATI WAKUTANGAZA MATOKEO HAYO.
Maulid pia anasema "Waliofanya mtihani huo kwa mwaka 2014 ni wanafunzi 53597 wakiwemo wavulana 25484 na wasichana 28113  sawa na asilimia  98.5  ya Wanafunzi   waliofanya mtihani huo amabao walianza darasa la kwanza mwaka 2008  wakiwa jumla  ya wanafunzi 72054    kati yao wavulana 35262  na wasichana  36792  Kwa hiyo waliofanya mtihani huu ni sawa na asilimia 74.4 ya wanafunzi wote walioandikishwa darasa la kwanza mwaka 2008". anasema Maulid.
 
Aidha Maulid, alibainisha kwamba ,wanafunzi ambao hawakuweza kufanya mtihani kwa mwaka huo wa 2014 ni kama ifuatanvyo, alisema  "Kati ya wanafunzi 54384  waliotarajiwa kufanya mtihani huo, wanafunzi 787  hawakufanya mtihani huo kwa sababu mbalimbali zikiwemo za utoro, kifo, ugonjwa, kuhama, na mimba kwa wasichana. Idadi hiyo ni sawa na asilimia 1.46".
 
 
BAADHI YA WATENDAJI KUTOKA WILAYA ZOTE ZA MKOA WA MWANZA  WAKIFATILIA UTANGAZAJI MATOKEO KATIKA SHULE YA SEKONDARI MWANZA.
 
AFISA ELIMU  MSINGI WILAYA YA UKERWE FIDES MUNYOGWA AKIELEZA SIRI YAKUFANIKIWA HADI KUSHIKA NAFASI YA KWANZA KIMKOA.
Kwa upande wake Afisa Elimu msingi wa Wilaya ya Ukerewe, bibi Fides Munyogwa ,amesema siri kubwa yakupata ufaulu ulio iwezesha wilaya kushika nafasi ya kwanza kimkoa ni pamoja na ushirikiano baina ya walimu, wazazi pamoja na uongozi mzuri wa wilaya, lakini pia kutatuliwa kwa changamoto ya madai ya walimu waliokuwa wakiidai wilaya hiyo.
Aidha mazoezi ya mara kwa mara pia yamechagiza katika kupata ufaulu huo " Mwenyekiti sisi Wilaya ya Ukerewe tumefanikiwa kulipa madeni ya walimu kwa kutumia fedha za ndani na kuawafanya walimu waliokuwa wanadai waweze kuifanya kazi yao kwa moyo" anabainisha bibi Munyogwa.
   Imeandaliwa na Afisa Habari. Mwanza RS. 

Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Watumishi mkoa wa Mwanza kuwezesha kituo cha damu salama kanda ziwa kuwa na damu yakutosha ili kuweza kukidhi mahitaji halisi yanayo fikia chupa za ujazo 78,000 kwa mwaka.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
 
 
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza amekutana na viongozi wa dini pamoja watendaji wa Sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza kwa ajili yakuzungumzia suala la maendeleo ya Mkoa huo na wa kwanza kukutana nao walikuwa watendaji wa Sekretarieti Mkoa na badaye jioni viongozi wa dini.
 
·        Awapa rungu watendaji, awaambia wasifanye kazi kwa mazoea.

·        Viongozi wa Dini wakerwa na Uchawi, Ukame, na hali duni katika zao la Pamba.

·        “Vijana wengi wana ndoto za kuhamia  Mwanza kuwa Machinga”- Askofu AIC asema.
 

 

SHEKHE HASSAN FEREJI WA MKOA WA MWANZA AKICHANGIA JAMBO KATIKA KIKAO KILICHO WAKUTANISHA VIONGOZI WA DINI NA MKUU WA MKOA WA MWANZA MAGESA MULONGO.
MKUU WA MKOA WA MWANZA MAGESA MULONGO AKIFUNGUA KIKAO NA VIONGOZI WA DINI MKOANI HAPA.

VIONGOZI WA DINI WAKIFURAHIA JAMBO, ANAYE PIGA MAKOFI NI KIONGOZI WA KANISA LA SDA, AITWAE BULENGELA. KUTOKA DAYOSISI YA NYANZA


ASKOFU ANDREW GULLE WA KKKT DAYOSISI YA MASHARIKI YA ZIWA VIKTORIA AKICHANGIA MADA KATIKA KIKAO HICHO.

KATIBU TAWALA MKOA WA MWANZA ALIYE SIMAMA FAISAL ISSA AKIWA ANATOA MUONGOZO JUU YAKUCHANGIA KATIKA KIKAO HICHO.

Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Kuongeza kiwango cha wajawazito kujifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma za afya  kutoka 68%-80% ifikapo desemba 2015, kuongeza  kiwango cha huduma baada ya kujifungua ndani ya siku 7 kutoka 21% mpaka 62% ifikapo  Decemba  2015, kuongeza kiwango cha watoto wanaozaliwa na kina mama wenye maambukizi ya VVU kutumia  ARV (prophylaxis) kutoka 45% to 65% ifikapo Decemba 2015 kuongeza namba ya vituo vinavyotoaa huduma ya IMCI kutoka 69%-80% ifikapo Desemba 2015, mbali ya mikakati hiyo vilevile mkoa umedhamiria Kuboresha utoaji wa taarifa kwa wakati kutoka 66%-100% ifikapo Decemba 2015.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Aagiza Shughuli za usafi zifanywe na Vikundi vidogo vidogo.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo amekerwa na hali ya uchafu iliyopo katika mitaa ya Jiji la Mwanza na kuwaagiza  watendaji wa halmashauri hiyo  kuacha  kukaa ofisini na badala yake watoke na kwenda kuwasikiliza watu katika maeneo yao ya kibiashara. 
Mulongo ametoa kauli hiyo jijini Mwanza, mara baada yakufanya ziara yakutembelea maeneo yaliyotengwa  maalumu kwa ajili ya wafanyabiashara ndogondogo Jijini humo na kukuta hali ya mazingira kiafya ikiwa hairidhishi.
 
Mkuu huyo wa mkoa akiwa ameambatana na kamati ya Ulinzi na usalama ya Mkoa alitembelea maeneo ya Makoroboi, Soko kuu, Sahara na Standi ya Nyegezi.
MKUU WA MKOA WA MWANZA MAGESA MULONGO AKISHANGAA UCHAFU ENEO LA SOKO KUU.
AKIWA KATIKA ENEO LA MAKOROBOI, HAPA VIJANA WA SHULE WAKICHAGUA NGUO ZA MTUMBA
"HAIKUBALIKI KATIKATI YA JIJI PAWE NA HALI YA UCHAFU KIASI HIKI"- MULONGO
UKARABATI WA VIBANDA KATIKA ENEO AMBALO LIMEZUIWA KUFANYA BIASHARA NDOGO NDOGO

ZAWADI NAZO HAZIKUKOSEKANA (PICHA ZOTE NA OFISI YA MKUU WA MKOA)

MKUU WA WILAYA YA NYAMAGANA BARAKA KONISAGA AKITOA MAELEZO MBELE YA MKUU WA MKOA WAKATI WA ZIARA HIYO


ENEO LILILOKUWA NYUMBA YA NHC AMBAPO MKUU HUYO WA MKOA AMETOA SIKU HADI KUFIKIA TAREHE 30 DESEMBA LIWE LIMEENDELEZWA.


KWA MBALI MKUU WA MKOA AKITAZAMA JENGO LA MSIKITI WA JAMII YA WAHINDU AMBAPO WAFANYABIASHARA WAMEKUWA AKIFANYA BAISHARA BILA YA IDHINI YA SERIKALI.


HUU NDIO UCHAFU UNAO NYOOSHEWA KIDOLE NA MKUU WA MKOA WA MWANZA KATIKA ENEO LA STANDI YA TAX JIJINI HUMO.

KAZI NI UHAI KWA KILA BINADAMU, ASIYEFANYA KAZI NA ASILE(PICHA NA OFISI YA RC MWANZA.)

TUPO KAZINI WAJASIRIAMALI KATIKA ENEO LA MTAA WA SOKONI WAKIUZA SAMAKI AINA YA NEMBE.

MKUU WA MKOA ALIYE NYANYUA MWAMVULI KUMSIKILIZA BIBI ASIA RASHIDI ENEO LA SOKO KUU WAKATI WA ZIARA HIYO.(PICHA NA OFISI YA RC MWANZA)

MKUU WA MKOA AKISHUHUDIA WAKINA MAMA WAUZA SAMAKI KATIKA MTAA WA SOKONI.

 Aidha katika hatua nyingine ameuagiza uongozi wa jiji hilo kuhakikisha wana viainisha vikundi vidogo vidogo vinavyo undwa na vijana pamoja na kina mama ili viweze kukabidhiwa jukumu la kutunza mazingira badala ya kazi hiyo kuachiwa mawakala wa usafi ambao kwa namna moja au nyingine wameonekana kulemewa na jukumu hilo .