Articles by "Press Release"
Showing posts with label Press Release. Show all posts
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.




WAKALA WA VIPIMO (WMA) 
SIKU YA VIPIMO DUNIANI
VIPIMO VINAVYOTUMIKA KATIKA SEKTA YA USAFIRISHAJI

(MEASUREMENT FOR TRANSPORT)

Mei, 20 kila mwaka nchi nyingi duniani husherehekea siku ya  vipimo duniani. Mwaka huu kauli  mbiu ( theme) ya maadhimisho ni vipimo katika sekta ya usafirishaji (measurement for transport).
no image
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

 

Serikali Mkoani Mwanza imeamuru shule 11 za msingi  na moja ya Sekondari, zilizokuwa zimefungwa Wilayani Ukerewe kutokana na ukosefu wa vyoo zifunguliwe na wanafunzi warejee kwenye masomo wakati wa  hatua za dharura zinachukuliwa.

 
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
ASKARI JESHI KWENYE SIKU YA MASHUJAA JIJI MWANZA, HAPA WAKILIPUA RISASI HEWANI KUWAKUMBUKA MASHUJAA WALIOJITOLEA KWA NCHI YAO KATIKA VITA YA PILI YA DUNIA 1939-1945.
Serikali Mkoani Mwanza Imekeme tabia ya watu wanaohubiri mambo ya ukabila katika karne ya sasa wakati mkoa huo ukiwa kwenye maadhimisho ya siku ya mashujaa yaliyofanyika kwenye mviringo wa makutano ya barabara ya Nyerere, Kenyatta na makongoro jijini Mwanza.
Akihutubia Mamia ya wananchi hao, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magessa Mulongo, amesema ameshangazwa na tabia ya baadhi ya wanasiasa kuhubiri habari ya ukabila kwenye karne ya sasa hasa kipindi hiki tunacho elekea kwenye uchaguzi mkuu.
MKUU WA MKOA WA MWANZA MAGESA MULONGO
AKITOA HOTUBA FUPI.
”Nimeshangazwa na ndugu zetu wa Chadema, juzi wamekuja hapa eti wamekuja kuwaambia wanamwanza, kuwa Magufuli sio msukuma” alisema Muolongo na kuhoji yaani kweli hiyo ndio meseji mtu aliyo kuja nayo? Amakweli duniani hapa kuna watu wana akili isiyo nzuri alisisitiza Mulongo, na kuuliza hiyo kwa watu wa Mwanza inamaana gani? “ Unapokuja na gari la udini unataka kuwaambia nini, na kusema, Ezekiel Wenje, alichaguliwa na wanamwanza lakini sio msukuma yeye ni Mshashi wa Mara lakini pia Highness alichaguliwa na kuongoza Ilemela lakini yeye ni Mchaga wa Kilimanjaro. Nilazima wakati mwingine na nyie wananchi muwe mnapima watu kwa hoja zao, sio mtu anakuja hapa mkutano mzima yeye ni kutukana tuu na kusema mambo ya hovyo mwanzo hadi mwisho.
BASE KAMANDA CANAL KIVAMBA AKIPOKEA SIME
TAYARI KWA KUWEKA KWENYA MNARA WA MASHUJAA.
Katika hatua nyingine, amekemea tabia ya baadhi ya vijana wanaopita mitaani  mara baada yakumaliza mikutano ya siasa na kuanza kubugudhi watu wenye biashara zao, ”Umemaliza kusikiliza mkutano wa siasa nenda nyumbani kwako  kimya kimya” tabia yakupita mitaani na kuanza kuwakera watu wengine wenye biashara zao sio kitendo kinacho vumilika hata kidogo na niwaombe tu vijana wenzagu, kwamba kwa atakaye thubutu kufanya hivyo tena sinto mvumilia” kwa mara ya kwanza niliwazuia askari kuwachukulia hatua lakini niseme, kwa atakaye kiuka utaratibu huo sinto muonea haya wala aibu eti kwakuwa tu kuchukua hatua utalalamikiwa, haiwezekani mtu yeye avunje sheria halafu aangaliwe na hakuna mtu aliye juu ya sheria aliongeza Mulongo.
Hata hivyo ameviagiza vyombo vya ulizi na usalama kuhakikisha vinasimamia kikamilifu ulinzi na usalama na kuhakikisha kila mchakato unapita salama katika kipindi hiki na maisha mengine yanaendelea kama kawaida.
Awali kabla ya kutoa maonyo hayo, Mkuu huyo wa Mkoa alisisitiza juu ya uzalendo wa mtu mmoja mmoja na umuhimu wa kutunza amani” Ndugu zangu yamkini kama tungempa nafasi mzee wetu Sadalla aeleze kile walichokutana nacho miaka hiyo hangetamani kirudie tena, lakini hata wenyewe mmeshuhudia hiki walichokuwa wakifanya askari wetu hapa na hii ilikuwa ni maonesho tu ,sitaki kusema mengi tuitunze amani kwakuwa hakuna mbadala wa amani, badala ya Amani ni Vita.
MZEE IBRAHIMU SADALA ASKARI MSTAAFU WA KAR
AKIFANYA MAHOJIANO NA AFISA HABARI WA MWANZA.
Naye kwa upande wake Mzee Ibrahimu Saddala aliyepigana vita vya pili vya Dunia(KAR) mwenye umri wa miaka 90 kwa hivi sasa, alisema kila anapokumbuka hali ilivyokuwa hatamani kusikia habari ya vita huku akiwataka watanzania kuilinda amani kama mboni ya jicho. ”Mimi niliingia jeshi wakati ule nikiwa na miaka kumi na tisa na ndio kwanza nilikuwa nimemaliza shule, tukaja tukachukuliwa  na kwenda kujiunga jeshi tukaenda hadi Bama wakati huo tukiongozwa na wazungu” anasema Mzee Saddala na kuongeza kuwa “pamoja na kwamba vita ile iliniwezesha kupata pesa yakununua nyumba kwa shilingi miasaba (700) hapa Mwanza lakini kitu ambacho sitaki kukumbuka ni hali ilivyo kuwa pamoja na umri wangu huu”.
Mzee Saddala mwenye umri wa miaka tisini kwa sasa, ni miongoni mwa  watu  wachache waliosalia kati ya walipigana vita kuu ya pili ya Dunia kati ya Mwaka 1939-1945 na kwa sasa anaishi jijini Mwanza lakini pia ni mwenye nguvu na kuweza kutembea yeye mwenyewe kwa kutumia fimbo ndogo aina ya mkongojo inayo msaidia.
Imeandaliwa na Afisa habari Mwanza zaidi na picha isome kupitia


ASKARI JESHI WAKITOA HESHMA ZAO WAKATI WA MAADHIMISHO HAYO YALIYOFANYIKA LEO.

HAPA ASKARI WA GWARIDE WAKIPOKEA MAELEKEZO KUTOKA KWA MMOJA YA VIONGOZI WAO NAMNA YAKUKABIDHI ZANA HIZO KWA VIONGOZI WATAKAO WEKA KUMBU KUMBU.

HAPA VIONGOZI WA DINI WAKIA WANASIKILIZA KWA MAKINI MAZOEZI YA GWARIDE LA MASHUJAA.


MPIGANAJI WA KAR KITENGO CHA SIGNO, IBRAHIMU SADALLA, AKIWA AMEMALIZA KUWEKA SHOKA KATIKA MNARA WA KUWAENZI MASHUJAA WA VITA YA PILI YA DUNIA.

Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO






(TAARIFA KWA UMMA)

WITO WA KUWASILISHA MUHTASARI WA MADA (ABSTRACT) KWA AJILI YA KONGAMANO LA KITAIFA LA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI LITAKALOFANYIKA MOROGORO 6/03/2015
Tarehe 8 Machi, 2015 Tanzania itaadhimisha Siku ya Wanawake Duniani ambayo itaadhimishwa kitaifa mkoa wa Morogoro. Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake mwaka 2015 ni “Usawa kwa Wanawake ni Maendeleo ya Haraka kwa Wote”.
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, itaadhimisha siku hiyo kwa kuandaa kongamano la kitaifa litakalofanyika tarehe 6/03/2015 mkoani Morogoro sanjari na wiki ya maonesho ya wadau mbalimbali yatakayozinduliwa tarehe 03/03/2015 na kufikia kilele  chake tarehe 8/03/2015. Lengo kuu la kongamano ni kujenga jukwaa la majadiliano ya kina kuhusu masuala ya maendeleo ya wanawake na usawa wa kijinsia.

 Mada kuu nne zimependekezwa kuwasilishwa katika maeneo yafuatayo:
1.     Ukatili wa kijinsia (intimate partner violence- Ukatili katika mahusiano)
2.     Haki za wanawake/binadamu na mchango wa wanaume katika utetetezi wa haki za wanawake (Kwa mfano, ubakaji, ukatili kwa watoto/ wasichana)
3.     Hali ya Mtoto wa Kike (mf. Ndoa za utotoni)
4.     Ajira salama na haki katika ajira,
5.     Tathimini ya sheria na sera (dawati la jisia na polisi) na
6.     Majadiliano ( panel discussion) kuhusu uwezeshaji wa wanawake kiuchumi.

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto inakaribisha mwanajamii yeyote aliyetayari kuandaa mada katika maeneo yaliyotajwa hapo juu, awasilishe muhtasari wa mada yake (ikisiri, abstract) yenye maneno kati ya 300 na 500 kwa ajili ya maandalizi ya kongamano hili muhimu. Siku ya mwisho ya kuwasilisha maelezo hayo (abstract) ni tarehe 20/01/2015.

Waandishi ambao muhtasari wa mada zao utakubaliwa watafahamishwa tarehe 20/01/2015 na watashirikishwa katika maandalizi ya mada kamili tarehe 31/01/2015.

Maelezo ya mada (abstract) yatumwe kwa:

(i)  Elizabeth Makawa: e_palelamakawa@yahoo.com – Simu No. 0655 975478

(ii) Dinah Enock: edinnah@yahoo.com – Simu No. 0766 070376

(iii) Judy Kizenga: kizengajudy@yahoo.com  - Simu No. 0754 564414


Tangazo hili limetolewa na
Anna T. Maembe
Katibu Mkuu
05/01/2015
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Kiongozi wa Albino asema hukumu ikishindikana Duniani, itatolewa Mbinguni.
Watu 15 Wanashikiliwa na Polisi, nayo pikipiki iliyotekeleza mpango yabambwa na polisi, uchunguzi unaendelea.

WANANCHI WA NDAMI TARAFA YA MWAMASHIMBA WAKIMSIKILIZA MKUU WA MKOA WA MWANZA.
WAANDISHI WA HABARI SHEILA SEZI NA GRACE CHILONGOLA WAKIWA NA MAMA PENDO EMMANUEL, AMBAYE HIVI SASA ANA MAJONZI BAADA YA MTOTO WAKE KUTWALIWA NA WATU HAO.
Serikali mkoani Mwanza imesema hakuna kulala hadi mtoto Pendo Emmanuel  miaka 4(Albino) apatikane, kufatia tukio la kutekwa na watu wasio julikana toka tarehe 27, Desemba, 2014 katika kijiji cha Ndami, Tarafa ya Mwamashimba Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza na kisha kutoweka naye kwenda kusiko julikana hadi sasa.  
ALFREDY KAPOLE MWENYEKITI WA ALBINO MKOA WA MWANZA AKIONGEA KATIKA KIKAO HICHO



SUNGU SUNGU KWENYE KIKAO.
  
MWENYEKITI WA CHAWATA MKOA WA MWANZA NA MWENYEKITI WA ALBINO MKOA WA MWANZA WALIPOKUWA WAKIONGEA NA MAMA YAKE NA PENDO EMMENUEL.

 MKUU WA MKOA.

MKUU WA MKOA WA MWANZA MAGESA MULONGO.
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo, alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji hicho katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo na kuwahusisha wananchi wakijiji hicho pamoja na uongozi wa Wilaya na Mkoa huku akitaka kujua hatua iliyofikiwa na wana nchi hao katika kuwabaini walifanya unyama huo.
Mtoto Pendo alitekwa na watu wasiojulikana mnamo usiku wa tarehe 27.12.2014 majira ya saa nne usiku akiwa amelala na wazazi wake huko Nyumbani kwao na kisha watekaji kutoweka naye na kwenda kusiko julikana hadi sasa, huku taarifa za Polisi zikionesha jumla ya watu kumi na watano (15), wakiendelea kushikiliwa na jeshi la Polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi.
Akihutubia wananchi wa kijiji hicho Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, alisema ni tukio la kusikitisha kwani toka mwaka 2007 hakuna tukio la namna hiyo lililo wahi kutokea katika Wilaya hiyo na tukio la mwisho lililotokea lilimkumba mwananchi wa Wilaya hiyo aliyekuwa amesafiri kwenda Mkoani Shinyanga kwa shughuli zake.
Amesema kiburi walicho nacho watekaji hakiwezi kuwa nje ya mipaka ya kijiji hicho cha Ndami bali mpango mzima unajulikana kwa wenyeji na ndio maana ilikuwa rahisi kufanya unyama huo “Kiburi cha watekaji kimo humu humu haiwezekani mtu kutoka mbali aje atekeleze tukio hapa kijijini bila yakuwa na wenyeji lazima kuna mtu au watu walioshirikiana na wahalifu hao”, alisema Mulongo na kuongeza “ kwa mazingira ya Nyumba ya kina Pendo ilipo kule hakuna sehemu yakutokea na kama mliona pikipiki inaranda randa mchana,.. iweje mshindwe kuitilia shaka? Hapana,  hii haikubaliki! mimi nimekuja kuwaambia nataka Pendo apatikane na sio vinginevyo, nawapa siku tano ijumaa nitarudi hapa mniambie Pendo yuko wapi! Alisema mkuu huyo wa Mkoa akionesha kusononeshwa na tukio hilo.
“Mbona mifugo inapo ibwa inapatikana”? Aliwahoji viongozi wa sungu sungu na kusema haiingii akilini kusema wakati wa tukio la utekaji sungu sungu wote walikuwa wamekwenda kula chakula na ndipo kadhia hiyo ilipotokea, mkuu wa mkoa, alihoji kufatia kauli iliyotolewa na kiongozi wa sungu sungu kuwa wakati wa tukio askari wote wa sungu sungu walikuwa wamekwenda kula majira ya saa tatu na tukio kutokea saa nne.
MWENYEKITI WA ALBINO MWANZA.
Awali akielezea kusikitishwa kwake na tukio hilo, Mwenyekiti wa chama cha watu wenye ulemavu wa Ngozi mkoani hapa Alfred Kapole, alisema inasikitisha kuona wanadamu wakiwauwa binadamu wenzao kama vile wanyama bila hata woga na vyombo vya maamuzi vikishindwa kutoa hukumu kwa wakati huku akielekeza lawama zake kwa mahakama na Mkemia Mkuu. “Mh. Mkuu wa mkoa inasikitisha kuona miongoni mwa kesi 72 zilizokuwa mahakamani, ni kesi 3 tu ndizo zilizokwisha kutolewa hukumu” alisema Kapole, na kuongeza ingekuwa ni kesi ya Wabunge wameshindana kwenye masuala ya uchaguzi ingekuwa imekwisha hukumiwa lakini kwakuwa ni mlemavu wa ngozi,   basi kupuuzia kumekuwa kwingi mno. Alisema kapole.
Akinukuu maneno kutoka katika kitabu cha Biblia, Kapole alisema hata kama hukumu zitashindwa kutolewa na wanadamu hapa Duniani, naamini Mungu wa Mbinguni kuna siku haki itatendeka kwa kuwa “Kitabu cha Mika 3.3-7 kinaeleza juu ya hukumu watakayo ipata watu walao nyama za watu bila woga. Kesi zinaendeshwa Polisi wanajitaihidi sana lakini mkemia watendaji wa ofisi ya mkemia mkuu wanatuhujumu kwa kuita nywele zetu albino ni za Midoli, aling’aka Kapole wakati akielezea kusikitishwa na ofisi ya Mkemia mkuu wa serikali pindi inapo pelekewa Nywele.
Mwenyekiti Kapole pia aliomba kwa yeyote aliye na Mtoto huyo kumrejesha na kama wamemdhuru basi warejeshe hata mwili wake ili matanga yaweze kufanyika, akatumia fursa hiyo kumomba Rais wale wote waliohukumiwa kunyongwa wanyongwe ili kuepusha kuendelea kula chakula cha serikali bure.
RC ITIKADI KATIKA KAZI.
Katika kikao hicho Mkuu wa Mkoa aliwataka wanachi kuweka mbali itikadi zao za namna yoyote na kufanya kila linalowezekana  ili kufanikisha zoezi zima la kuwasaka walio husika na utekaji wa mtoto Pendo Emmanuel, ambao unasimuliwa kuleta siamanzi kubwa ndani ya jamii ya wana Kwimba na watanzania  lakini pia kuchafua taswira ya nchi mbele ya mataifa mengine ya Dunia . Huku akiwaonya watu wa haki za binadamu kuacha kupaza sauti za kuwatetea wahalifu. Tanzania inatajwa kuwa kinara cha ukatili huo tangu mauwaji hayo yalipo zuka mwanzoni mwa miaka ya 2006/2007.
TAKWIMU ZA KIMATAIFA.
Kwa Mujibu wa takwimu za kimataifa zinaonesha ni asilimia 2% tu ya watu ambao huzaliwa na ulemavu wa ngozi ndio hufikia na kusherekea miaka 40 ya kuzaliwa kwao, huku pia takwimu zikionesha katika nchi za Afrika mtu mmoja (1) kati ya elfu mbili (2000) huzaliwa wakiwa na ulemavu wa ngozi wakati katika marekani ni mtu mmoja kati ya elfu kumi na saba ndio huishi na ulemavu wa ngozi.
Mauaji ya Albino katika Tanzania yanaonekana kushamiri katika Mikoa ya kanda ya ziwa, ambapo imani za kishirikina zikitajwa kuwa chanzo kikubwa cha mauwaji ya hayo lakini pia yale yalio wahusu vikongwe yanayo husishwa na  masuala ya kujipatia utajiri wa haraka suala ambalo sio la kweli, ambapo takwimu zinaonesha kuwa mauwaji yalianza  siku nyingi japo kuripotiwa katika mamlaka za serikali na vyombo vya habari ilianza  mwaka 2006/2007.
Hivi sasa zipo asasi za kiraia zinazo jihusisha na harakati za kupinga mauwaji hayo ikiwapo asasi ya Under The Same Sun ya Nchini Canada na kwa Tanzania imeshakuwa na tawi toka mwaka 2008.
KAMANDA WA POLISI.
Awali akitoa taarifa ya uchunguzi wa tukio hilo kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Valentino Mulowola alisema tayari watu 15 wanashikiliwa na jeshi la Polisi Mkoani humo kwa mahojiano zaidi akiwapo baba mzazi wa Pendo, lakini pia jeshi hilo limefanikiwa kuipata piki piki iliyotumika kufanya unyama huo. “Hivi sasa tunawashikilia watu wapatao kumi na watano na wanaendelea kuhojiwa na Polisi” alisema Mlowola na kuongeza kuwa huo sio mwisho kwa kuwa jinai haina mwisho hata miaka ishirini tukio hili litaendelea kuchunguzwa”, na kusema hata kama yeye atahamishwa au kustaafu kijana atakayekuja ataendelea na kesi hiyo, hivyo wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa kile wanacho kifahamu, alisema Mlowola na kusema tayari Jeshi hilo mkoani hapa limetangaza kuto Milioni tatu 3 kwa atakayefanikisha kupatikana kwa mtoto  Pendo.
Mtoto Pendo alikuwa ni miongoni mwa alibino 74 waliopo katika wilaya ya Kwimba na alikuwa namba 9 katika suala la kupatiwa ulizi.
Imeandaliwa na Afisa habari Mwanza- Atley Kuni.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
 Taasisi ya Benjamin W. Mkapa HIV/AIDS (BMAF) iliyoanzishwa mwaka 2006 na Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Benjamin W. Mkapa, imekuwa mstari wa mbele kuchangia juhudi za Serikali kupitia miradi mbalimbali inayolenga kuimarisha huduma za afya, hususan katika maeneo ya vijijini na yenye mazingira magumu. Mradi mmojawapo unaotekelezwa na Taasisi ni wa “Mkapa Fellows” wa miaka mitano (2013- 2017) ambao unafikia Halmashauri 15 zilizopo katika mikoa ya Shinyanga, Kagera, Simiyu, Rukwa na Zanzibar.

Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
BALOZI MPYA WA MAREKANI AJITAMBULISHA KWA MHESHIMIWA MAKAMU WA RAIS
Ikulu, Dar es Salaam: 2014-06-09
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal leo amekutana na Balozi mpya wa Marekani, Mheshimiwa Balozi Mark Childress ambaye amefika ofisini kwa mheshimiwa Makamu wa Rais kwa ajili ya kujitambulisha.
Balozi Childress alimueleza Mheshimiwa Mkamu wa Rais kuwa, Tanzania ni nchi yenye uhusiano maridhawa na Marekani na kwamba katika kipindi chake kama Balozi atahakikisha uhusiano huu mzuri uliojengwa unadumishwa na kwamba, nchi hizi mbili zinazidi kuwa na maeneo ya kushirikiana hasa yanayolenga kuboresha maisha ya watu na kuwapatia maendeleo.
Balozi Childress pia alisema kuwa Tanzania imekuwa ikitumia kama mfano kufuatia kuonesha mabadiliko ya haraka katika miradi mbalimbali inayoendeshwa hapa nchini kwa ushirikiano na watu wa Marekani na akafafanua kuwa, kazi iliyoko mbele ni kuhakikisha kuwa Tanzania inapiga hatua zaidi na sio kurudi nyuma.
 
“Mheshimiwa Makamu wa Rais, kila nikipata fursa ya kukutana na wenzangu tumekuwa tukizungumzia suala la Tanzania kupiga hatua kwa haraka. Mna mambo mengi yaliyofanyika na kazi iliyopo ni kuendelea kupiga hatua pasipo kurudi nyuma,” alisema.
Kwa upande wake Mheshimiwa Makamu wa Rais alimueleza Balozi Childress kuwa, Tanzania ipo katika kipindi ambacho kinaonesha mabadiliko makubwa ya kiuchumi na kwamba kazi ya serikali ya Tanzania ni kuhakikisha kuwa uchumi unakuwa na unasaidia vizazi vya sasa na vijavyo.
“Mtazamo wetu katika serikali ni kuwa Tanzania itapiga hatua kubwa katika miaka michache ijayo. Lengo letu ni kutazama kuwa ukuaji wa uchumi hauwi wa muda mfupi, tunatazama pia maendeleo kwa vizazi vijavyo.
Kuhusu suala la utunzaji mazingira, Balozi Childress alisifu hatua za Mheshimiwa Makamu wa Rais hasa katika kazi ya uhamasishaji upandaji miti na akasema, utunzaji wa mazingira ni jambo la muhimu ili kuifanya nchi yetu iweze kuendelea na isikabiliane na matatizo yanayotokana na mazingira kuharibiwa.
“Nakupongeza Mheshimiwa Makamu kwa kazi yako ya uhamasishaji utunzaji wa Mazingira. Usichoke kufanya hivyo maana unasaidia dunia,” Balozi Childress alisema.
 
Imetolewa na : Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es Salaam.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib, akimkaribisha Balozi mpya wa Marekani nchini Tanzani, Mark Childres, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni 9, 2014 kwa mazungumzo na utambulisho wa balozi huyo. Picha na OMR


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Balozi mpya wa Marekani nchini Tanzania, Mark Childres, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni 9, 2014 kwa mazungumzo na utambulisho wa balozi huyo. Picha na OMR
 

 
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

BISMARK ROCK MWANZA.
Ndugu Wananchi napenda kuwataarifu kupitia vyombo vya habari juu Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani mwaka 2014 ambayo Mkoa wa Mwanza umechaguliwa kuandaa maadhimisho hayo kitaifa.

 

Ndugu Wananchi, Maadhimisho ya Siku ya mazingira Duniani hufanyika kuanzia tarehe 01 hadi 05 ya mwezi Juni kila Mwaka. Maadhimisho haya huwa na Kauli mbiu iliyoandaliwa mahsusi kwa ajili kuhimizana juu ya umuhimu wa uhifadhi wa Mazingira yetu.

 

Kwa mwaka huu 2014, shirika la Umoja wa mataifa linalo shughulikia mazingira limetangaza Kaulimbiu ya maadhimisho hayo kuwa ni “RAISE YOUR VOICE BUT NOT THE SEA LEVEL” kwa tafsiri ni “CHUKUA HATUA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA  TABIANCHI. Kitaifa, kauli mbiu yetu ni ”TUNZA MAZINGIRA ILI KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIANCHI.

 

Ndugu wananchi

Kama nilivyotanguliwa kusema, Mkoa wa Mwanza umeteuliwa kuwa mwenyeji wa kitaifa, wa maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani mwaka huu. Katika juma hilo shughuli mbalimbali zitafanyika ikiwa ni pamoja na kufanya usafi katika maeneo yote, kuhamasisha wananchi kuhusu utunzaji wa Mazingira  kwa njia ya Makongamano, kupanda miti, kuzoa takataka, maonesho ya utunzaji na mazingira, kuondoa magugu katika Ziwa Victoria na ufugaji wa nyuki pamoja na kufanya ziara kwenye maeneo tofauti yanayo jishughulisha na utunzaji wa mazingira ikiwemo viwanda.

 

Ndugu wananchi,

Ufunguzi wa maadhimisho haya kitaifa utafanyika tarehe 02 Juni, 2014 kuanzia saa 1.00 asubuhi katika Viwanja vya Furahisha, Ufunguzi huo utafanywa na Waziri nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mheshimiwa Dkt, Binilith Mahenge  na siku ya kilele itakuwa tarehe 05 Juni, 2014 ambapo Mgeni rasmi atakuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal.

 

Ndugu wananchi,

Shughuli zitakazo fanyika siku ya tarehe 05 Juni 2014 (Siku ya kilele)  ni pamoja na:- kukabidhi vyeti kwa wadau mbali mbali wa mazingira, zawadi na tuzo ya Rais ya utunzaji na uhifadhi wa mazingira pamoja na zawadi nyinginezo kwa washindi wa kuhifadhi mazingira.

 

Ndugu waandishi wa habari,

 

Natambua kwamba ninyi ni wadau wakubwa sana wa mazingira hasa katika jukumu lenu la kuuelimisha umma, juu ya umuhimu wa kutunza mazingira, kwa nafasi ya pekee niwaombe muweze kuipeleka taarifa hii kwa wananchi wa Mkoa wa Mwanza na maeneo ya jirani ili waweze kujitokeza kwa wingi katika Viwanja vya Furahisha kwa muda wote ambao elimu kuhusu utuzaji wa mazingira itakuwa ikitolewa na wadau mbali mbali.

 

Aidha  Mkoa unategemea kupokea Wageni wa Kitaifa na  Kimataifa, ambao watatembelea  viwanda na kuona utunzaji wa Mazingira na jinsi ya kutenga taka ngumu na zisizo ngumu.

 

Nichukue fursa hii kutoa rai kwa wananchi wa Mwanza kujitokeza kwa wingi na kushirikiana na wageni wetu kama ilivyo ada ya Wana Mwanza. Nawaomba wananchi mjitokeze kwa wingi na kuwalaki wageni wote watakao tufikia katika juma zima kuanzia tarehe 01 hadi 05 Juni 2014. Kama ilivyo desturi yetu wana Mwanza tuonyeshe ukarimu wetu kwa wageni wetu na pindi watakapo ondoka waikumbuke Mwanza.

 

Nimalizie kwa kusema nawashukuru sana kwa kuitika wito wangu.

 

“TUNZA MAZINGIRA, KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIANCHI”

 

MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI TANZANIA

 

ASANTENI KWA KUNISIKILIZA.

 

IMETOLEWA NA MKUU WA MKOA WA MWANZA.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
HAPA TIMU ZIKIKAGULIWA NA MGENI RASMI, TIMU HIZO ZILITOKA SARE YA GOLI 1-1












Mashindano ya UMISETA, kwa Mkoa wa Mwanza yamefunguliwa rasmi hapo jana na Kaimu katibu Tawala mkoa wa Mwanza Ndaro Kulwijira huku akiwaasa vijana hao wa Sekondari kucheza kwa kuzingatia nidahamu ya hali ya juu.

Zaidi soma katika Hotuba yake aliyoitoa wakati wa Ufunguzi wa michezo hiyo.
 

HOTUBA YA KAIMU KATIBU TAWALA WA MKOA WA MWAZA     WAKATI WA KUFUNGUA MASHINDANO YA NGAZI YA MKOA YA MICHEZO YA SHULE ZA SEKONDARI TANZANIA (UMISSETA) NSUMBA SEKONDARI TAREHE 22 MEI, 2014

Katibu Tawala Msaidizi  wa Mkoa Elimu  - Mwalimu Hamis Maulid

MaafisaElimu wa Halmashauri

Mameneja

Viongozi wa Vyama vya Michezo Mkoa

Wanamichezo

Ndugu Wananchi; na

Wapenda Michezo Wote.

 

Napenda kuchukua fursa hii kukushukuru Katibu Tawala Msaidizi ambaye ni AfisaElimu wa Mkoa, na Viongozi wenzako katika Seksheni ya Elimu kwa kunialika kufungua Mashindano haya ya Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA).

 

Nimeupokea mwaliko huu kwa furaha kwa vile umenipa fursa ya pekee kuwaona na kuzungumza na hadhara hii ya Wanafunzi Wanamichezo na Walimu wao. Aidha, nitumie fursa hii kuupongeza Uongozi wa Nsumba na jumuia yote kwa maandalizi mazuri ya mazingira kwa ajili ya mashindano haya. Ahsanteni sana!

 

Ndugu Viongozi na Vijana Wanamichezo,

Leo tumebahatika kujumuika hapa kupitia Utamaduni wa Michezo. Kwa utaratibu huu, ni dhahiri kwamba tunapata nafasi ya kujenga Umoja wa Kitaifa wa Wanamichezo kupitia Michezo hii ya UMISSETA kuanzia ngazi ya Vijana wetu wa Shule za Sekondari. Ni kweli kwamba Michezo ni Burudani, lakini kwa sasa kutokana na mabadiliko ya Mazingira ya Kisiasa, Kiuchumi na Kijamii, Michezo ni Kipaumbele katika kutoa pia Ajira kwa Vijana wetu, kukuza Biashara na kujenga jamii bora yenye maelewano. Kwa mfano, Nchi za wenzetu za Ulaya na Marekani, Nigeria, Togo, Ivory Coast, Cameroon zinatumia kikamilifu nafasi hii ya Michezo kujitangaza Kisiasa na Kiuchumi.

 

 

Ndugu Wanamichezo,

Natambua kwamba ninyi ni Wanafunzi ambao mnahitaji kukuza Taaluma na Vipaji vyenu. Moja ya nafasi hizo ni Michezo. Ili Michezo iendelee kukua Nchini, ni lazima Ukuzaji wa Vipaji vya Michezo uanzie Mashuleni. Ndiyo maana Michezo ni sehemu ya Mtaala wa Masomo yenu. Kama ambavyo tunawataka mfanye bidii sana katika masomo yenu, fanyeni bidii pia na kukuza Vipaji vyenu katika Michezo mbalimbali.

Ndugu Wanamichezo,

Michezo inatufundisha Ushindani wa Kistaarabu, Ushindani unaozingatia Sheria na Kanuni, Ushindani unaojenga urafiki badala ya uhasama; Ushindani unaoleta Upendo badala ya Chuki na Ushindani unaoleta Amani badala ya Shari. Kwa sababu hiyo Mwanamichezo wa leo anayo nafasi ya kupata mafundisho muafaka na hazina ya uzoefu mkubwa wa Ushindani wa Kistaarabu kutoka kwenye Michezo, vitu ambavyo vinaweza kumfanya kuwa Mtanzania bora wa kesho. Mwanamichezo anakubali ama Kushindwa au Kushinda. Waswahili husema“Asiyekubali Kushindwa Si Mshindani”.

Wanamichezo bora ni Watu Wasikivu, wenye nidhamu na Watiifu. Ninyi Vijana ambao ndio Viongozi wa kesho wa Taifa letu mnahitaji sana kujijengea nidhamu na maadili ya hali ya juu ili muweze kuendana na hali ya maisha ya ushindani yatakayokuwa yanawakabili. Nidhamu, inamuwezesha Mtu kufanya kazi zake kwa mpangilio mzuri unaofuata Taratibu zote za kazi kwa wakati. Hii ndiyo njia ya uhakika ya kufikia malengo yoyote yale na kupata mafanikio.

Aidha, kwa njia ya Michezo, nidhamu Shuleni itaongezeka na matarajio yetu ni kuwa nidhamu hiyo itajitafsiri pia katika matokeo mazuri kwenye Taaluma. Matarajio ni kuwa, Wanafunzi watakuwa na mahusiano mazuri zaidi kati yao na Walimu wao na wale wote wanaopata Burudani ya Michezo. Ama tunatarajia kuwa wataendelea kuwa Watu wenye Nidhamu katika Utu Uzima wao, ili hatimaye tuwe na Taifa la Watu wenye nidhamu ya kutolewa mfano.

Ndugu Wanamichezo,

Tangu zama za kale Michezo ilikuwa ni sehemu ya Maisha ya Jamii. Jamii moja ilijipambanua na Jamii nyingine kutokana na ushupavu na ushujaa wake katika Michezo. Dhana hiyo ya kale bado inaendelezwa kupitia Sera ya Michezo kwa njia ya kisasa zaidi. Sera ya Maendeleo ya Michezo inayaainisha madhumuni ya Michezo wakati huu kuwa ni:  Kujenga na kuimarisha Afya Bora kwa wote;  Kujenga Tabia ya Ushirikiano, Upendo, Undugu na Uzalendo;  Kujenga Uhusiano, Uelewano na Mshikamano Kitaifa; Kujenga Moyo wa Kishujaa na Kujihami na Kukuza Ukakamavu, Ujasiri na Kujiamini; Kuburudisha;  Kulitambulisha na kulitangaza Taifa letu nje ya Mipaka yake; na

 Kumjenga Mwanamichezo kuwa mtu imara Kiakili na Kiroho (kuanzia Utotoni hadi Utu Uzima). Kwa mtiririko huu, napenda kusisitiza kuwa Shule zote, kuanzia za Awali, Msingi, na Sekondari, viwe na Viwanja vya Michezo mbalimbali. Hii ni njia ya kuwatambua na kuwaendeleza Vijana wenye Vipaji Maalum ili hatimaye Washiriki kwenye Mashindano ya Kitaifa na Kimataifa. Aidha, Halmashauri zetu za Miji, Manispaa, Vijiji zihakikishe kuwa maeneo yaliyotengwa kwa Shughuli za Michezo yanatumika kwa shughuli hiyo. Aidha, Viwanja vilivyopo viimarishwe na vitunzwe ipasavyo.  Ndugu Wanamichezo,

Nitumie fursa hii pia kuwakumbusha kwamba mnapofurahia kushiriki katika Michezo hii, ni lazima mkumbuke pia kuwa furaha yenu itaweza kudumu kama mtatambua kuwa kuna mpinzani mkubwa kati yenu aitwaye Virusi vya UKIMWI na UKIMWI. Kila mmoja wenu anaelewa vya kutosha juu ya Adui huyu. Ni wajibu wangu kama Kiongozi na Mlezi wenu kuwakumbusha juu ya hatari inayowakabili msipochukua tahadhari ya kutosha. Kumbukeni UKIMWI bado unaenea kwa kasi kubwa sana hasa miongoni mwa Vijana wa Rika lenu kuliko Rika lolote jingine. Niwakumbushe kwamba kataeni kumalizwa na Ugonjwa huu. Msikubali kukatishwa masomo na msikubali kutenganishwa mapema na Familia zenu. Kwenu ninyi, njia bora pekee ni kusubiri hadi wakati muafaka wa kuwa na ndoa zenu. Wekeni bidii katika masomo, kwani muda ukifika yote yatajipanga vizuri.

 

Nitumie fursa hii kuwakumbusha kuepukana na matumizi ya dawa za kulevya  kama vile bangi, mirungi na cocaine kwa imani ya kuwa dawa za kulevya huwapatia nguvu  na mzuka wa kushindana, huko ni kujidanganya.  Vijana wengi hasa wanamichezo waliojaribu kutumia dawa za kulevya michezoni wameathirika na wamekuwa mataahira. Shirikisho la vyama vya michezo duniani limekataza kabisa matumizi ya dawa hizo na ukigundulika ni kufungiwa maisha na ushindi kunyanganywa. Nawaomba walimu na wanafunzi kuwabaini wale wote watakaojihusisha na utumiaji wa dawa za kulevya na kuwachukulia hatua kali za kiidhamu na kisheria

 

Ndugu Wanamichezo,

Nimeelezwa kuwa baada ya Michezo hii yapo Mashindano ya Kanda ya Ziwa ambapo Mikoa ya Mwanza, Mara na Simiyu hukutana ili kuimarisha mahusiano ya Vijana wa Shule za Sekondari na kuunda timu moja ya Kanda. Ni muhimu Timu zetu zijipange kushiriki vizuri na kutuletea undindi a kishindo. Ni Vizuri sasa Timu hizo ziandaliwe vizuri ili zikashiriki kama Washindani na si Wasindikizaji.Kushiriki kwetu kunatujengea umahiri katika kujenga upeo wa akili za Vijana wetu na kujenga mahusiano mazuri ya kikanda .Natoa rai kwa Mashirika, Vyama vya Michezo na watu wengine  kushiriki kwa  kuchangia kufanikisha ushindi wa timu zetu za Mkoa.

 

Ndugu Wanamichezo,

Mwisho napenda kukumbusha kuwa umahiri katika jambo lolote lile hufikiwa kwa kujifunza na kufanya mazoezi mengi, kwa bidii. Napenda kuwapongeza Walimu na Waamuzi na wote walioziandaa Timu hizi ambazo leo zinashindana hapa. Nawapongeza sana Wanamichezo wa Timu zilizoteuliwa kushindana hapa. Natumaini mliteuliwa kwa kustahili na katika Michezo hii mtapata nafasi ya kuonyesha kuwa kuteuliwa kwenu hakukuwa kwa Bahati. Onyesheni Umoja, Onyesheni Upendo, na Onyesheni“Fair Play” katika mashindano haya. Kumbukeni kwamba Michezo ni Afya, Michezo ni Furaha na Michezo ni Ajira.

 

Ndugu Wanamichezo, Wageni Waalikwa,

Baada ya kusema hayo, napenda sasa nitamke kuwa,Mashindano ya Umoja wa  Michezo Shule za Sekondari UMISSETA  kwa mwaka 2014 yamefunguliwa rasmi.

Ahsanteni kwa Kunisikiliza