April 2014
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Samuel Sitta akiangalia vitabu katika maktaba ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kabla ya kushuhudia uzinduzi wa kituo cha taarifa katika maktaba hiyo.


Mawaziri kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanaoshoghulikia masuala ya Jumuiya wakiwa wanapitia machapisho mbalimbali katika maktaba ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kabla ya kushuhudia uzinduzi wa kituo cha taarifa katika maktaba hiyo.
 

Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa Tanzania  Mhe. Samwel akiwa ndani ya maktaba iliyo sheheni Machapisho
mbali mbali yanayohusu Jumuiya hiyo tangu jumuiya iliyovunjika ya mwaka 1967, ndani ya maktaba hiyo iliyopo mjini Arusha.


Naibu waziri wa Afrika Mashariki wa Tanzania Mhe. Adam Malima akiwa ndani ya maktaba hiyo akiangalia vitabu mbali mbali pembeni ni Maafisa wa Wizara ya Jumuiya ya Afrika ya mashariki kabla ya kushuhudia uzinduzi wa kituo cha taarifa katika maktaba hiyo..

Waziri wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki wa Tanzania Mhe. Samweli Sitta, akizungumza na Vyombo mbali mbali vya habari ambavyo havionekani pichani.

Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Waziri Sitta akiwa katika kikao cha Nchi cha ushauri na makatibu wakuu wa Wizara hawapo pichani leo asubuhi kujiandaa na Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki baadae leo.


Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Joyce Mapunjo katikati na Naibu Katibu Wizara ya Fedha Profesa Adoft F. Mkenda pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa kwanza  kushoto ndugu Amatius C. Msole wakichangia ushauri leo asubuhi katika kikao cha kujiandaa na Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki baadae leo.


Waziri Sitta pamoja na Naibu Waziri wa Fedha Mhe.Adam Malima akiwa katika kikao cha Nchi cha ushauri na makatibu wakuu wa Wizara hawapo pichani leo asubuhi kujiandaa na Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki baadae leo.Wataalamu Wazara ya Fedha, Wizara ya Ushirikiano Wa Afrika Mashariki na Wizara ya Viwanda na Biashara,wakiwa katika kikao cha Nchi cha ushauri na makatibu wakuu wa Wizara hawapo pichani leo asubuhi kujiandaa na Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki baadae leo.


Wataalamu Wazara ya Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa katika kikao cha Nchi cha ushauri na makatibu wakuu wa Wizara hawapo pichani leo asubuhi kujiandaa na Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki baadae leo.


Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
HAWA NI MORANI WA KIMASAI WAKIWA WANABARIZI
SORONERA CAMP NI SEHEMU YA NAKSHI ZA MBUGA ZETU.

TUKISEMA TUNAO WANYAMA WAKUTOSHA HII NDIO TAFSIRI YAKE.

NDEGE NAO UTAWAONA UKIWA MBUGANI.MITI MIZURI YAKUVUTIA NDANI YA NGORO NGORO


TARATIBU WATU WANAZAMA SHIMONI.

MNYAMA AMBAYE HUAMINIKA MUDA WOTE HUWA AMENONA.

NDOVU WANYAMA WALIOKUWA WANATESWA SANA SIKU ZA HIVI KARIBUNI.

MR. ATLEY KUNI- MWANZA RS Information Officer ndani ya Crater.

BWAWA HILI HUTOKEA ZIWA VIKTORIA KWA MUJIBU WA WATAALAM.
 

SIMBA HAWAOGOPI WATU HUMU CRATER.
TUNATOKA KUVUNA KUNI MBUGANI SISI WAMASAI WA NGORO NGOROKuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
 
HALMASHAURI ya Manispaa ya Ilemela, jijini Mwanza inakabiliwa na changamoto ya uzoaji taka ngumu kutokana na kuharibika kwa magari ya kuzolea taka hizo.
Hayo yalilezwa mwishoni mwa wiki na Mkuu wa wilaya ya Ilemela, Amina Masenza wakati akitoa taarifa ya Januari hadi Machi, mwaka huu ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM.
Alisema katika kipindi hicho uzoaji na utupaji wa taka ngumu ulikuwa wa matatizo kutokana na kuharibika kwa magari ya kuzoa taka ya halmashauri.
Alisema katika kukabiliana na tatizo hilo halmashauri ilikodisha magari kutoka makampuni binafsi ambapo jumla ya tani 1,500 za taka ngumu zilizotolewa katika vituo vya Furahisha na Buzuruga.
Alisema kutokana na uharibifu wa mazingira unaoendelea katika maeneo mbalimbali ndani ya halmashauri kwa ajili ya maendeleo ya kijamii, halmashauri imeandaa mabango kwa ajili ya kusimika yenye ujumbe wa kuzia uharibifu wa mazingira.
Masenza alisema katika bajeti ya mwaka 2013/14 halmashauri ilitenga Sh. Mil. 320 kwa ajili ya kununua magari mawili mapya ya kuzolea taka huku halmashauri ikiwa imeweka makubaliano na mradi wa uboreshaji wa mazingira ya ziwa Victoria.
Aidha kwa upande wa ardhi Masenza alisema katika kipindi hicho jumla ya migogoro ya 67 ya ardhi imetatuliwa  kwa kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa wilaya.
Pia alisema viwanja katika maeneo ya Buhilya, Nyasaka, Bujingwa, Nyamhongholo na Bwiru zimekaguliwa na mipaka yake kutambuliwa  na kwamba katika kudhibiti ujenzi ujenzi holela kwa kushirikiana na ofisi ya Mhandisi wa Manispaa nyumba 14 zilibomolewa.
Na Grace  Chilongola, Mwanza
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.


BAADHI YA PICHA KUTOKA MAKTABA ZIKIMUONESHA RC AKIWA ZIARANI.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo, anaanza ziara ya kukagua shughuli za maendeleo katika Mkoa wa Mwanza ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa ziara hizo ambazo amekuwa akizifanya mara kwa mara.
 
Kwa mujibu taarifa iliyopatikana kutoka katika ofisi hiyo, mkuu huyo wa Mkoa atanza rasmi ziara yake katika Wilaya ya Misungwi katika kijijicha Mwalolabagole ambapo atakagua mwalo wa eneo hilo na kujionea maradi wa Udhibiti wa Magugumaji, uzalishaji vifaranga wa samaki na ufugaji wa samaki.
 
Mara baada yakuhitimisha ziara yake siku ya leo hapo kesho ata tembelea katika Wilaya ya Sengerema kabla yakuendelea na ziara yake katika  Wilaya ya Magu kwa siku inayofuata.
 
Mkoa wa Mwanza ni mmoja ya Mikoa inayotekeleza mpango wa BRN ambapo mambo yaliyopewa kipaumbele katika Mkoa huo ni Maji na suala la Elimu.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Vijana wa CCM wakiwa wanaingia katika Mkoa wa Mwaza wakitokea Mkoa wa Shinyanga.
TUMEKUJA KWA SHANGWE,
UMOJA WETU NDIO USHINDI WETU.MKUU WA MKOA WA MWANZA MHANDISI EVARIST NDIKILO NA MKUU WA WILAYA YA
MISUNGWI KWA PAMOJA NA DC NYAMAGA WAKIWASHANGILIA VIJANA.


BANGO LAKUHAMASISHA UMOJA NA MSHIKA MANO.


IYENA IYENA IKANOGA.

NINYI VIJANA MNAYO DHIMA YAKULINDA MUUNGANO HUU.

 Katika hotuba yake mkuu hyo wa Mkoa amewataka Vija kushikamana na kuutetea Muungano kwa dhati. Kwani Taifa la Tanzania limekuwa mstari wa mbela katika harakati mbali mbali ndani na nje ya Nchi.
 
Amesema Muungano wa nchi hizi haukutokea kwa bahati mbaya bali ni maono ya waasisi wa Taifa hili waliotaka nchi hizi ziungane kutokana na Historia, lakini siku zote Nguvu ya Mnyonge ni Umoja, hivyo wakati wazungu wanawaza kuwa Taifa moja nasi tuwe na malengo yakuwa nchi moja kama maona ya wazee wetu.
 
Mbio hizo zitamalizika tarehe 17.04.2014 Huko Mkoani Kigoma na badae kwenda Taifani siku ya Tarehe 26 Ambapo itakuwa kilele cha Siku ya Muungano katika Uwanja wa Taifa DSM.
Taarifa kamili ni hapo kesho............!!!!!!!!!!