Articles by "Afya."
Showing posts with label Afya.. Show all posts
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

Mh. Seleman Jafo Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, alipokuwa akifunua mkutano wa RBF ulioshirikisha Mikoa minane inayotekeleza mradi wa RBF nchini.
Serikali imesema haita wavumilia watendaji watakaoshindwa kusimamia ipasavyo mradi wa  Malipo kwa Ufanisi katika kuboresha utoaji wa huduma za Afya “Results Based  Finance” (RBF) ambao hivi sasa unatekelezwa katika mikoa minane hapa nchini.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

Hii ndio Keki Maalum iliyo andaliwa na AGPAHI mara baada yakumalizika kwa Kambi ya siku tano ya Malezi ya Vijana
Mkoani Mwanza.
Vijana wapatao 50 kutoka Mikoa ya Geita, Mwanza na Shinyanga, ambao walikuwa katika kambi ya malezi kwa vijana waishio na VVU/UKIMWI kwa muda wa siku tano katika Jiji la Mwanza  wamelipongeza Shirika AGPAHI kwa jinsi linavyoweza kutumia ipasavyo fedha wazipatazo kutoka kwa wadau wa Maendeleo.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
 
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amezindua Bodi mpya ya ushauri ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekouture inayoundwa na wajumbe wapatao 15, huku akiibebesha jukumu lakuhakikisha hospitali hiyo inachana na mfumo wa ukusanyaji mapato wa kawaida na badala yake watumie mfumo wa kieletroniki
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

Serikali mkoani Mwanza imeitaka jamii kote nchini kuwapeleka watoto wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) shule, badala ya kuwanyanyapaa na baadhi kuwaficha ndani na kisha kufifisha ndoto zao za maisha.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO






(TAARIFA KWA UMMA)

WITO WA KUWASILISHA MUHTASARI WA MADA (ABSTRACT) KWA AJILI YA KONGAMANO LA KITAIFA LA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI LITAKALOFANYIKA MOROGORO 6/03/2015
Tarehe 8 Machi, 2015 Tanzania itaadhimisha Siku ya Wanawake Duniani ambayo itaadhimishwa kitaifa mkoa wa Morogoro. Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake mwaka 2015 ni “Usawa kwa Wanawake ni Maendeleo ya Haraka kwa Wote”.
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, itaadhimisha siku hiyo kwa kuandaa kongamano la kitaifa litakalofanyika tarehe 6/03/2015 mkoani Morogoro sanjari na wiki ya maonesho ya wadau mbalimbali yatakayozinduliwa tarehe 03/03/2015 na kufikia kilele  chake tarehe 8/03/2015. Lengo kuu la kongamano ni kujenga jukwaa la majadiliano ya kina kuhusu masuala ya maendeleo ya wanawake na usawa wa kijinsia.

 Mada kuu nne zimependekezwa kuwasilishwa katika maeneo yafuatayo:
1.     Ukatili wa kijinsia (intimate partner violence- Ukatili katika mahusiano)
2.     Haki za wanawake/binadamu na mchango wa wanaume katika utetetezi wa haki za wanawake (Kwa mfano, ubakaji, ukatili kwa watoto/ wasichana)
3.     Hali ya Mtoto wa Kike (mf. Ndoa za utotoni)
4.     Ajira salama na haki katika ajira,
5.     Tathimini ya sheria na sera (dawati la jisia na polisi) na
6.     Majadiliano ( panel discussion) kuhusu uwezeshaji wa wanawake kiuchumi.

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto inakaribisha mwanajamii yeyote aliyetayari kuandaa mada katika maeneo yaliyotajwa hapo juu, awasilishe muhtasari wa mada yake (ikisiri, abstract) yenye maneno kati ya 300 na 500 kwa ajili ya maandalizi ya kongamano hili muhimu. Siku ya mwisho ya kuwasilisha maelezo hayo (abstract) ni tarehe 20/01/2015.

Waandishi ambao muhtasari wa mada zao utakubaliwa watafahamishwa tarehe 20/01/2015 na watashirikishwa katika maandalizi ya mada kamili tarehe 31/01/2015.

Maelezo ya mada (abstract) yatumwe kwa:

(i)  Elizabeth Makawa: e_palelamakawa@yahoo.com – Simu No. 0655 975478

(ii) Dinah Enock: edinnah@yahoo.com – Simu No. 0766 070376

(iii) Judy Kizenga: kizengajudy@yahoo.com  - Simu No. 0754 564414


Tangazo hili limetolewa na
Anna T. Maembe
Katibu Mkuu
05/01/2015
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Kiongozi wa Albino asema hukumu ikishindikana Duniani, itatolewa Mbinguni.
Watu 15 Wanashikiliwa na Polisi, nayo pikipiki iliyotekeleza mpango yabambwa na polisi, uchunguzi unaendelea.

WANANCHI WA NDAMI TARAFA YA MWAMASHIMBA WAKIMSIKILIZA MKUU WA MKOA WA MWANZA.
WAANDISHI WA HABARI SHEILA SEZI NA GRACE CHILONGOLA WAKIWA NA MAMA PENDO EMMANUEL, AMBAYE HIVI SASA ANA MAJONZI BAADA YA MTOTO WAKE KUTWALIWA NA WATU HAO.
Serikali mkoani Mwanza imesema hakuna kulala hadi mtoto Pendo Emmanuel  miaka 4(Albino) apatikane, kufatia tukio la kutekwa na watu wasio julikana toka tarehe 27, Desemba, 2014 katika kijiji cha Ndami, Tarafa ya Mwamashimba Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza na kisha kutoweka naye kwenda kusiko julikana hadi sasa.  
ALFREDY KAPOLE MWENYEKITI WA ALBINO MKOA WA MWANZA AKIONGEA KATIKA KIKAO HICHO



SUNGU SUNGU KWENYE KIKAO.
  
MWENYEKITI WA CHAWATA MKOA WA MWANZA NA MWENYEKITI WA ALBINO MKOA WA MWANZA WALIPOKUWA WAKIONGEA NA MAMA YAKE NA PENDO EMMENUEL.

 MKUU WA MKOA.

MKUU WA MKOA WA MWANZA MAGESA MULONGO.
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo, alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji hicho katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo na kuwahusisha wananchi wakijiji hicho pamoja na uongozi wa Wilaya na Mkoa huku akitaka kujua hatua iliyofikiwa na wana nchi hao katika kuwabaini walifanya unyama huo.
Mtoto Pendo alitekwa na watu wasiojulikana mnamo usiku wa tarehe 27.12.2014 majira ya saa nne usiku akiwa amelala na wazazi wake huko Nyumbani kwao na kisha watekaji kutoweka naye na kwenda kusiko julikana hadi sasa, huku taarifa za Polisi zikionesha jumla ya watu kumi na watano (15), wakiendelea kushikiliwa na jeshi la Polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi.
Akihutubia wananchi wa kijiji hicho Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, alisema ni tukio la kusikitisha kwani toka mwaka 2007 hakuna tukio la namna hiyo lililo wahi kutokea katika Wilaya hiyo na tukio la mwisho lililotokea lilimkumba mwananchi wa Wilaya hiyo aliyekuwa amesafiri kwenda Mkoani Shinyanga kwa shughuli zake.
Amesema kiburi walicho nacho watekaji hakiwezi kuwa nje ya mipaka ya kijiji hicho cha Ndami bali mpango mzima unajulikana kwa wenyeji na ndio maana ilikuwa rahisi kufanya unyama huo “Kiburi cha watekaji kimo humu humu haiwezekani mtu kutoka mbali aje atekeleze tukio hapa kijijini bila yakuwa na wenyeji lazima kuna mtu au watu walioshirikiana na wahalifu hao”, alisema Mulongo na kuongeza “ kwa mazingira ya Nyumba ya kina Pendo ilipo kule hakuna sehemu yakutokea na kama mliona pikipiki inaranda randa mchana,.. iweje mshindwe kuitilia shaka? Hapana,  hii haikubaliki! mimi nimekuja kuwaambia nataka Pendo apatikane na sio vinginevyo, nawapa siku tano ijumaa nitarudi hapa mniambie Pendo yuko wapi! Alisema mkuu huyo wa Mkoa akionesha kusononeshwa na tukio hilo.
“Mbona mifugo inapo ibwa inapatikana”? Aliwahoji viongozi wa sungu sungu na kusema haiingii akilini kusema wakati wa tukio la utekaji sungu sungu wote walikuwa wamekwenda kula chakula na ndipo kadhia hiyo ilipotokea, mkuu wa mkoa, alihoji kufatia kauli iliyotolewa na kiongozi wa sungu sungu kuwa wakati wa tukio askari wote wa sungu sungu walikuwa wamekwenda kula majira ya saa tatu na tukio kutokea saa nne.
MWENYEKITI WA ALBINO MWANZA.
Awali akielezea kusikitishwa kwake na tukio hilo, Mwenyekiti wa chama cha watu wenye ulemavu wa Ngozi mkoani hapa Alfred Kapole, alisema inasikitisha kuona wanadamu wakiwauwa binadamu wenzao kama vile wanyama bila hata woga na vyombo vya maamuzi vikishindwa kutoa hukumu kwa wakati huku akielekeza lawama zake kwa mahakama na Mkemia Mkuu. “Mh. Mkuu wa mkoa inasikitisha kuona miongoni mwa kesi 72 zilizokuwa mahakamani, ni kesi 3 tu ndizo zilizokwisha kutolewa hukumu” alisema Kapole, na kuongeza ingekuwa ni kesi ya Wabunge wameshindana kwenye masuala ya uchaguzi ingekuwa imekwisha hukumiwa lakini kwakuwa ni mlemavu wa ngozi,   basi kupuuzia kumekuwa kwingi mno. Alisema kapole.
Akinukuu maneno kutoka katika kitabu cha Biblia, Kapole alisema hata kama hukumu zitashindwa kutolewa na wanadamu hapa Duniani, naamini Mungu wa Mbinguni kuna siku haki itatendeka kwa kuwa “Kitabu cha Mika 3.3-7 kinaeleza juu ya hukumu watakayo ipata watu walao nyama za watu bila woga. Kesi zinaendeshwa Polisi wanajitaihidi sana lakini mkemia watendaji wa ofisi ya mkemia mkuu wanatuhujumu kwa kuita nywele zetu albino ni za Midoli, aling’aka Kapole wakati akielezea kusikitishwa na ofisi ya Mkemia mkuu wa serikali pindi inapo pelekewa Nywele.
Mwenyekiti Kapole pia aliomba kwa yeyote aliye na Mtoto huyo kumrejesha na kama wamemdhuru basi warejeshe hata mwili wake ili matanga yaweze kufanyika, akatumia fursa hiyo kumomba Rais wale wote waliohukumiwa kunyongwa wanyongwe ili kuepusha kuendelea kula chakula cha serikali bure.
RC ITIKADI KATIKA KAZI.
Katika kikao hicho Mkuu wa Mkoa aliwataka wanachi kuweka mbali itikadi zao za namna yoyote na kufanya kila linalowezekana  ili kufanikisha zoezi zima la kuwasaka walio husika na utekaji wa mtoto Pendo Emmanuel, ambao unasimuliwa kuleta siamanzi kubwa ndani ya jamii ya wana Kwimba na watanzania  lakini pia kuchafua taswira ya nchi mbele ya mataifa mengine ya Dunia . Huku akiwaonya watu wa haki za binadamu kuacha kupaza sauti za kuwatetea wahalifu. Tanzania inatajwa kuwa kinara cha ukatili huo tangu mauwaji hayo yalipo zuka mwanzoni mwa miaka ya 2006/2007.
TAKWIMU ZA KIMATAIFA.
Kwa Mujibu wa takwimu za kimataifa zinaonesha ni asilimia 2% tu ya watu ambao huzaliwa na ulemavu wa ngozi ndio hufikia na kusherekea miaka 40 ya kuzaliwa kwao, huku pia takwimu zikionesha katika nchi za Afrika mtu mmoja (1) kati ya elfu mbili (2000) huzaliwa wakiwa na ulemavu wa ngozi wakati katika marekani ni mtu mmoja kati ya elfu kumi na saba ndio huishi na ulemavu wa ngozi.
Mauaji ya Albino katika Tanzania yanaonekana kushamiri katika Mikoa ya kanda ya ziwa, ambapo imani za kishirikina zikitajwa kuwa chanzo kikubwa cha mauwaji ya hayo lakini pia yale yalio wahusu vikongwe yanayo husishwa na  masuala ya kujipatia utajiri wa haraka suala ambalo sio la kweli, ambapo takwimu zinaonesha kuwa mauwaji yalianza  siku nyingi japo kuripotiwa katika mamlaka za serikali na vyombo vya habari ilianza  mwaka 2006/2007.
Hivi sasa zipo asasi za kiraia zinazo jihusisha na harakati za kupinga mauwaji hayo ikiwapo asasi ya Under The Same Sun ya Nchini Canada na kwa Tanzania imeshakuwa na tawi toka mwaka 2008.
KAMANDA WA POLISI.
Awali akitoa taarifa ya uchunguzi wa tukio hilo kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Valentino Mulowola alisema tayari watu 15 wanashikiliwa na jeshi la Polisi Mkoani humo kwa mahojiano zaidi akiwapo baba mzazi wa Pendo, lakini pia jeshi hilo limefanikiwa kuipata piki piki iliyotumika kufanya unyama huo. “Hivi sasa tunawashikilia watu wapatao kumi na watano na wanaendelea kuhojiwa na Polisi” alisema Mlowola na kuongeza kuwa huo sio mwisho kwa kuwa jinai haina mwisho hata miaka ishirini tukio hili litaendelea kuchunguzwa”, na kusema hata kama yeye atahamishwa au kustaafu kijana atakayekuja ataendelea na kesi hiyo, hivyo wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa kile wanacho kifahamu, alisema Mlowola na kusema tayari Jeshi hilo mkoani hapa limetangaza kuto Milioni tatu 3 kwa atakayefanikisha kupatikana kwa mtoto  Pendo.
Mtoto Pendo alikuwa ni miongoni mwa alibino 74 waliopo katika wilaya ya Kwimba na alikuwa namba 9 katika suala la kupatiwa ulizi.
Imeandaliwa na Afisa habari Mwanza- Atley Kuni.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
WAZIRI MKUU AKIPOKEA ZAWADI YA PICHA
KUTOKA KWA CEO WA BMAF DR. HELEN SENKORO.


WAALIKWA WAKIWA WANAANGALIA HARAMBEE INAVYOKWENDA.



MC WA SHGHULI HIYO ALEX  NGUSSA
AKICHAGIZA JAMBO KWENYE HARAMBEE HIYO.


NAIBU WAZIRI WA KITWANGA AKIMSIKILIZA
WAZIRI MKUU KWA JAMBO FULANI HAPO.




DR. HELEN AKIMPA WAZIRI MKUU
MPANGO WA HARAMBEE UTAKAVYO KWENDA.











KIONGOZI WA KANGARUU AKIWAKILISHA MCHAO WA TAASISI HIYO.



MKURUGENZI WA JIJI LA MWANZA HALIFA
HIDA MARA BAADA YAKUSILISHA MCHO WA JIJI LA MWANZA.


AFISA UHUSIANO WA JIJI LA MWANZA, BW. JOSEPH MLIZI
AKIPEANA MKONO NA WAZIRI MKUU MARA
BAADA YAKUWASILISHA MCHO WA MWANZA CITY COMMECIA COMPLEX.


KANALI MSTAAFU NA MKUU WA MKOA WA KAGERA
AKISOMA MICHANGO KUTOKA MKOA HUO.


RC WA GEITA KULIA AKIMTAMBULISHA MKUU WA WILAYA YA
 GEITA MANZIE MANGOCHIE MARA
BAADA YA KUWASILISHA MICHANGO YA MKOA HUO.


MKUU WA MKOA WA SHINYANGA AKIKABIDHI MICHAO YA MKOA HUO.



SEKRETARIETI WAKISIKILIZA KWA MAKINI JINSI WACHANGIAJI WALIVYO KUWA WANACHANGIA KATIKA HARAMBEE HIYO.


MFANYABIASHARA WA MWANZA BW. MWITA GACHUMA
 AKITETA JAMBO NA MHE. BENJAMIN MKAPA KATIKA HAFLA HIYO.




MKUU WA WILAYA YA NYAMAGANA KUSHOTO, BARAKA KONISAGA
NA MKUU WA WILAYA YA ILEMELA BIBI AMINA MASENZA
 WALIPOFIKA MBELE KWA AJILI YAKUTOA MICHANGO YAO.








KAMATI YA MAANDALIZI WALIPATA FURSA YAKUPIGA PICHA YA PAMOJA
 NA MGENI RASMI WAZIRI MKUU WA JAMAHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
 
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
.Mgonjwa mmoja agundulika
.Serikali ya Mkoa, yatoa tahadhari kwa wananchi.


DALILI ZA DENGUE ZINAVYO JITOKEZA.


 
Mtu mmoja Mkaazi wa Jijini Mwanza katika maeneo ya  kilimahewa mwenye umri wa miaka (62), amelazwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa Sekouture akisumbuliwa na ugonjwa wa Dengue mara baada ya Vipimo kuonesha.
 
Kwa miujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Baraka Konisaga katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, mgonjwa huyo alifikishwa hospitalini hapo siku moja tatu zilizopita kwa ajili ya kuchunguza afya yake, lakini mara baada ya vipimo vya kawaida hakugundulika kuwa na ugonjwa wowote ndipo ilipo mlazimu mtaalam wa maabara kumshauri mgonjwa huyo kupima vipimo vya ugonjwa wa dengue na kupatikana akiwa ameambukizwa  virusi hivyo vinavyo ambukiza ugojwa wa dengue.
 
SOMA TAARIFA NZIMA HAPA CHINI.
 
 
 
 KUWEPO KWA UGONJWA WA DENGUE   KATIKA MKOA WA MWANZA
 
TAARIFA  KWA  UMMA
 
Ndugu, Waandishi wa habari, wawakilishi wa vyombo vya habari na wananchi wote. Napenda kutoa taarifa ya kuwepo kwa ugonjwa wa Dengue katika Mkoa wa Mwanza. Hadi sasa kuna mgonjwa mmoja katika Hospittali ya Rufaa ya Sekou-toure ambaye amethibitika kuwa na ugonjwa huo.  Kufuatia taarifa hii  napenda wananchi wafahamu machache kuhusu ugonjwa wa Dengue. Ugonjwa wa Dengue husababishwa na VIRUS vinavyoitwa “Dengue Virus”  na vinaenezwa na mbu aina ya Aedes.
 
Mbu hawa hupendelea kuzaliana kwenye maji yaliyotuama karibu na makazi ya watu au kwenye vyombo vya kuhitadhia maji majumbani.
 
JINSI UGONJWA WA HOMA YA DENGUE UNAVYOENEZWA
 
Binadamu hupata ugonjwa huu baada ya kuumwa na mbu wa aina ya Aedes aliye na Virusi vya ugonjwa huu.  Mbu  hawa hupendelea kuuma wakati wa mchana.
 
Ugonjwa huu huwapata wetu wa rika zote aidha watoto wenye umri chini ya miaka mitano na mama wajawazito huathirika zaidi.
 
Ndugu wananchi
 
Dalili za Ugonjwa wa Homa ya Dengue
 
Asilimia 90 ya wagonjwa walioambukizwa ugonjwa huu uonyesha dalili awali kuanzia siku ya 3 hadi 14 baada ya kuumwa na mbu mwenye virusi vya ugonjwa huu dalili hizi ni kama zifuatazo:
·         Homa kali ya ghafla
·         Kuumwa kichwa hususani sehemu za machoni
·         Maumivu makali ya misuli pamoja na viungo vya mwili
·         Kichefuchefu au kutapika
·         Kuvimba tezi
·         Kupatwa na harara
Asilimia 10 ya wagonjwa hupatwa na dalili kali kama kutokwa na damu kwenye sehemu za uwazi za mwili mfano mdomoni, masikioni pamoja na sehemu za kutolea haja ndogo na kubwa.
 
Ndugu wananchi,
Njia za kujikinga na Homa ya Dengue
Ugonjwa wa dengue unazuiliwa kwa njia zifuatazo:-
·         Kuangamiza mazalio ya mbu
·         Kufukia madimbwi ya maji au nyunyizia dawa ya kuua viluwiluwi vya mbu kwenye madimbwi hayo
·         Kuondoa  vitu vyote vinavyoweza kuwa mazalia ya mbu kama vile vifuu vya nazi, makopo, chupa na magurudumu ya gari ambavyo vinaweza kufanya maji kutuama karibu na makazi.
·         Kufyeka nyasi na vichaka vilivyo karibu na makazi.
·         Kuhakikisha maua yanayopandwa kwenye makopo au ndoo hayaruhusu maji kutuama
·         Kufunika mashimo ya maji taka kwa mfuniko
·         Kusafisha mitaro na  gata za paa la nyumba ili kutoruhusu maji kutuama.
 
Kuzuia kuumwa na mbu kwa:-
·         Kutumia dawa za kufukuza mbu  (Repellents)
·         Kuvaa nguo ndefu
·         Kuweka wavu wa kuzuia mbu kwenye madirisha na milango
Kwa kufanya hayo, tunaamini tunaweza kuzuia maambukizi ya ugonjwa huu yasiendelee kutokea.  Naomba kila mmoja atimize wajibu wake.
 
Asanteni kwa kunisikiliza,
 
 
 
Baraka M. Konisaga
KAIMU MKUU WA MKOA
MWANZA