Articles by "habari"
Showing posts with label habari. Show all posts
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mh. Seleman Jafo, akizungumza wakati wa kikao na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa kuhusu ukarabati wa vituo 172 vya Afya nchini kote.
 
Serikali imepanga kukarabati vituo vya afya 172 kutokana na fedha kutoka Benki ya Dunia na Ubalozi wa Canada ambapo wametoa jumla ya Dolla za Kimarekani Mil 88 sambamba na Bil.12 fedha za kitanzania zilizovuka katika mwaka wa fedha wa 2016/2017.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.


Nteghenjwa Hosseah, Tamisemi – Dodoma.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Selemani Jafo akizungumza  katika hafla ya kufungua mafunzo ya Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi  katika Ukumbi wa Hazina Mjini Dodoma Leo
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala  za Mikoa  na Serikali za Mitaa  Mhe. Selemani Jafo amewataka Wakuu wa Wilaya  na Wakurugenzi wote nchini kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi  ili kutimiza matarajio  ya watanzania  ambao wanaitegemea Wizara hii kama chachu ya  mabadiliko  katika utendaji kazi wa Serikali ya awamu ya Tano.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey W. Zambi akitoa maagizo  kwa Wakala wa Vipimo kusimamia matumizi ya vipimo sahihi katika msimu wa ununuzi wa mazao



Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godyfrey W. Zambi akisaini Kitabu cha wageni katika Maonesho ya Nanenane.

 



Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godyfrey Zambi akipewa Maelezo na Afisa Vipimo namna ya kutambua mawe sahihi ya Mizani yaliyo hakikiwa na Wakala wa Vipimo


 Mkuu wa mkoa wa Lindi Godfrey Zambi amepiga marufuku kutumia kipimo kinacho tumiwa na baadhi ya wanunuzi wa mazao katika mkoa huo maarufu kama Kangomba ambacho kimeonsha kutokuwa rafiki wa mkulima.
Zambi ametoa kauli hiyo  alipotembelea banda la wakala wa vipimo nchini (WMA), katika maonesho ya nane nane ambayo kitaifa yanafanyika katika mkoa wa Lindi kwenye viwanja vya Ngongo. 

Akizungumza katika banda hilo, amewataka Wakala wa Vipimo kuongeza nguvu zaidi katika kusimamia matumizi sahihi ya vipimo katika maeneo mbalimbali,  ili wakulima na Wananchi kwa ujumla waweze kunufaika na mazao wanayolima pindi waendapo kuyauza wakati wa msimu.

Ameongeza kuwa,  maafisa wa vipimo ni muhimu kwa  kushirikiana na maafisa waliopo katika ofisi za wakuu wa mikoa katika kuhakikisha wakulima hawapunjwi pindi waendapo kuuza mazao yao kwakuwa baadhi ya wafanyabiashara  wasio waaminifu, huchezea mizani yao kwa lengo la kuwapunja wakulima kwa lengo la kupata faida zaidi.

Awali wakitoa maelezo kuhusu kangomba maafisa wa wakala wa vipimo walimuelezea mkuuhuyo wa mkoa namna kangomba inavyowapunja wakulima, kwa kuwa siyo kipimo sahihi kinachopaswa kutumika kununulia mazao. 

Kufuatia maelezo kutoka kwa wakala wa vipimo ndipo ikamalazimu mkuu huyo wa kutoa tamko kali dhidi ya wale wote wenye kutumia kangomba katika kuuza au kununua mazao ya wakulima.

“Lazima tuelewe falasafa ya Rais wetu, anataka mapinduzi ya viwanda lakini mwenye kuzalisha malighafi ni mkulima hivyo lazima, katika mazao yake aone faida, vinginevyo atauchukia ukulima na kukatishwa tamaa”, alinukuliwa mkuu wa mkoa.

Wakala nchini imekuwa na jukumu la kuwapa wakulima elimu ya matumizi sahihi ya mizani iliyo hakikiwa na kutambua alama zinazowekwa kwenye vipimo vilivyohakikiwa na Wakala ambazo ni   stika maalum, pamoja na kugongwa nembo ya Taifa na tarakimu mbili za mwisho za mwaka husika. Mfano kwa mwaka huu 2017, itasomeka namba 17.

Kwa upande wake Afisa Vipimo wa mkoa wa  Lindi bw. Nyagabona Mkanjabi alisema, wamejipanga vizuri katika kusimamia matumizi ya vipimo sahihi na kuhakikisha mizani zote zinazotumika katika vyama vya ushirika vya msingi zinakaguliwa kabla ya misimu ya kuuza mazao kuanza huku  aki wahakikishia kaguzi mbalimbali za kustukiza zinafanyika kipindi cha msimu wa kuuza mazao unapofika.

Pia, amewakaribisha viongozi wa vyama vya ushirika vya msingi pamoja na wananchi wote kutembelea banda la wakala wa vipimo katika maonesho ya nanenane mkoa wa Lindi na kujionea Mizani mbalimbali zinazopaswa kutumika katika ununuzi wa bidhaa mbali mbali na mazao ukiwemo mzani wa digital wa tani 2 ambao unapima bidhaa/mazao na kutoa  risiti hapo hapo

Akizungumza pembeni mwa mkutano huo, kaimu Afisa Vipimo mkoani hapo, Andrew Mbwambo ametoa wito kwa Wakulima, wafanyabiashara na Wananchi wote kutojihusisha na vitendo vya kuchezea vipimo kwani kwa sasa adhabu ni kubwa baada ya Sheria ya Vipimo Sura namba 340 na Mapitio yake ya mwaka 2002 kufanyiwa marekebisho mwaka 2016.

Kila mwaka wakala wa vipimo imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha inashiriki maonesho mbalimabali ikiwapo ya Nanenane huku wakiwa na jukumu la kutoa elimu ya mara kwa mara kwa wakulima na wanunuzi wa mazao na umuhimu wa kutumia vipimo sahihi.

Maonesho ya Nane nane kitaifa yamefanyika  mkoani Lindi kwa mara ya tatu mfululizo huku yakiongozwa na kaulimbiu “Zalisha kwa tija mazao na biadhaa za Kilimo, Mifugo na Uvuvi ili kufikia Uchumi wa kati”.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Bw. Johanes Bukwali, Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na uzalisha Sekretarieti ya mkoa wa Mwanza, akisoma Hotuba ya Katibu Tawala wa Mkoa huu wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo ya Siku nane kuhusiana na PlanRep kwa watendaji wa a Mikoa ya Kanda ziwa  
 
Serikali mkoani hapa imesema, Mfumo mpya wa kuandaa Mipango na Bajeti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa, ulioboreshwa utakuwa msaada kwa Mwananchi kwani utaweza kumshirikisha moja kwa moja wakati wakuibua vipaumbele vya maendeleo katika maeneo yao.
 
Isome Habari hii kwa Undani kupitia. www.mwanza.go.tz
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
> Nibaada yakushindwa Marshrti.
Moja ya Mashine katika kiwanda hicho ambayo baadhi ya vifaa vyake vimenyofolewa.

Mtambo huu unatajwa ndio kwanza Tekinolojia yake inaingia Afrika lakini hapa kwetu ulifungwa miaka mingi iliyopita.


Mkuu wa mkoa wa Mwanza akiwa ameambatana na baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama hapa wakifanya ukaguzi wa ndani ya Kiwanda hicho.

 
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, ameamuru kufungwa kwa kiwanda cha Ngozi cha Mwanza ambacho kilibinafsishwa wakati wa zoezi la ubinafsishaji mwanzoni mwa miaka ya tisini  kufuatia utata uliogubika  umiliki halali  wa kiwanda hicho.
Hatua ya mkuu wa Mkoa inafuatia ziara yake aliyoifanya kiwandani hapo tarehe 10 Julai, 2017 na kuwaamuru wahusika kuwa na mpango kazi ambao ungeonesha kwa namna gani wataanza kazi ifikapo Januari, 2018, huku akiwataka wahusika wote ambao wanamaslahi na kiwanda hicho kuwepo kiwandani hapo ifikapo 20 Julai, 2017.
Kinyume na matarajio ya Mkuu wa Mkoa, alipowasili kiwandani akiwa ameambatana na kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo, majira ya saa 5.43 za asubuhi siku ya tarehe 20 Julai, 2017, alikuta hakuna maendeleo yoyote juu ya hatma ya kiwanda hicho na hata mpango kazi aliokuwa ameagiza hakuuona.
Kwaundani isome kupitia    www.mwanza.go.tz
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo kwa Wakulima nchini akiteta jambo na Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella mapema kabla ya makabidhiano hayo kwenye eneo la tukio(Picha zote na Ofisi ya Mkuu wa mkoa)
Wakulima wa mkoa wa kanda ya ziwa kwa ujumla wameshukiwa na neema ya pekee kufuatia jitihada za serikali ya awamu  tano kuwaanzishia Benki yao katika kanda hii, ambayo itakuwa na makao yake makuu katika Mkoa wa Mwanza.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Pichani Eng. Mussa Iyombe Katibu Mkuu OR- TAMISEMI  (kutoka Maktaba).
 
Serikali imeonya na kusema, walimu 381 na mafundi sanifu wa maabara 137 ambao mara baada ya maombi yao kupitishwa na kupangiwa kazi wanapaswa kuripoti katika vituo hivyo vya kazi walivyo pangiwa na  watakaochukua fedha na kisha kutoweka kwenye vituo vya kazi watachukuliwa hatua kali za kishesheria ikiwapo kufikishwa mahakamani.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh. John Mongella, akikagua moja mashine katika Kiwanda cha ngua MWATEX
 
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, ameuagiza uongozi wa kiwanda cha kusindika ngozi ghafi cha African tanneries kuhakikisha kinafanya kazi ndani ya miezi sita ijayo ili kutekeleza azma ya Serikali ya awamu ya tano ya  kuwa nchi ya Uchumi wa kati na yenye viwanda vitakavyotoa ajira kwa watanzania.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

Serikali mkoani hapa, imewapa jukumu kubwa viongozi wa dini kutoka baadhi ya  mikoa ya kanda ya ziwa kuhakikisha wanakuwa bega kwa bega katika kulitunza ziwa Viktoria na Maliasili zake ili liweze kuwa tegemeo kwa kizazi cha sasa na kijacho. 


Sheik Hassan Kabeke,  Mwenyekiti mwenza wa Kamati ya Amani ya mkoa wa Mwanza, akifafanua umuhimu wa mazingira kwa Waandishi wa habari 
Dkt. Charles Mlingwa Mkuu wa mkoa wa Mara akifungua warsha hiyo ya Viongozi wa Dini, Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa mikoa ya kanda ya Ziwa.
 


Akifungua Semina ya siku moja mkoani hapa Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, na risala yake kusomwa na Mkuu wa Mkoa wa Mara Dkt. Charles Mlingwa, Mongella amesema, viongozi wa dini wanalo jukumu kubwa kwani wao husimamia imani za watu. “Ninyi Viongozi wa dini dhima mliyonayo ndani ya jamii ni kubwa sana na chochote mtakacho waelekeza waumini wenu lazima waweze kukitekeleza, hivyo niwaombe sana viongozi wangu tulilinde ziwa viktoria kwa jitihada zetu zote’’ alisema Mongella.

Aidha Mongella amesema kuwa, kuwepo kwa Ziwa Victoria ni fursa ya uendelezaji ya kauli mbiu ya “Tanzania ya Viwanda” ambayo Serikali ya awamu ya Tano inasisitiza,  Ziwa hili linasaidia upatikanaji wa rasilimali zinazotumika kwa matumizi ya nyumbani na viwandani, usafiri na usafirishaji na uzalishaji wa nishati ya umeme Hivyo basi hatuna budi kuhifadhi mazingira ya Ziwa na Bonde lake” amesisitiza Mkuu huyo wa mkoa.

Kwa upande wao, viongozi wa dini wakiongea wamesema, wao wanatambua na hata vitabu vya dini vinaelekeza juu ya mwanadamu anachopaswa kufanya katika kulinda mazingira ikiwepo ziwa Viktoria.

Mwenyekiti mwenza wa Kamati ya amani ya madhehebu ya dini katika Mkoa wa Mwanza, Sheik Hassan Kabeke, amesema katika Uislam  na hususan ni katika mafundisho ya Mtume Muhama S.A.W,  inafafanua juu ya mito miwili yaani mto Nile na Furabu ambayo mtume aliipitia huku akisema kwamba, Mto Nile ambao unafungamanishwa na Ziwa Viktoria Mtume amesisitiza kuyatunza mazingira, “Katika kupanda miti kwenye uislamu mtu hupata thawabu, tunaimani kabisa kwamba kila mmoja wetu akitunza mazingira ni sehemu ya Ibada, amesema Kabeke.

Naye Baba Askofu Michael Msonganzila wa Jimbo Katoliki la Musoma, kwa upande wake amesema kwa habari ya mazingira, tunaona ni jukumu la jamii nzima bila kujali itikadi zetu “ Kukutana kwetu hapa tunataka kuangalia nikwa namna gani tutaziangazia sababu za kiuchumi na kijamii, alisema Msonganzila na kuongeza kwamba kwa sasa wao katika Mkoa wa Mara wanayo kampeni kwenye eneo la Serengeti ambayo wanaendelea kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa Utunzaji wa mazingira na mabadiliko ya hali ya nchi.

Mradi wa Hifadhi ya Mazingira wa Ziwa Victoria (LVEMP II) utakamilika mwezi Disemba, 2017, aidha warsha hiyo ni kati ya warsha nne zilizoandaliwa na Mradi kwa madhumuni ya kukusanya maoni ya wadau ambayo yatawezesha kuandaa awamu ijayo ya Mradi inayotarajiwa kuanza kutekelezwa kuanzia mwaka 2018.
Kikao hicho kimewakutanisha Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa pamoja na Viongozi wa dini kutoka mikoa ya Mwanza, Geita, Kagera, Simiyu na Mara
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.


Hatma ya mgogoro wa watumishi ambao walikuwa na vyeti feki itajulikana mwishoni mwa mwezi wa sita mara baada ya zoezi la kusikilizwa kwa rufaa kukamilika.

Akizungumza Mkoani Mwanza juzi na watumishi wa Mkoa wakati wa juma la Utumishi wa Umma, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Laurian Ndumbaro    alisema, hadi kufikia Juni 30, 2017 hatma ya wale wote waliokuwa na vyeti vya bandia itajulikana mara baada ya kupitia rufaa zote ambazo ziliwasikishwa ofisini kwake.

“Baada ya uchambuzi kutokana na malalamiko yaliyowasilishwa na wahusika, mnamo kesho Juni 30 tutatoa majibu,” alisema.

Ndumbaro alifafanua kwamba wapo watakaorejeshwa lakini wapo pia ambao uwezekano wa kurejeshwa hautakuwepo kutokana na ushahidi uliopatikana.

“Lazima tuelewane katika hili, wapo ambao wao walikuwa na vyeti vya daraja sifuri, wakaenda wakatengeneza vyeti vyenye dara la pili au la kwanza au latatu, hawa tulipojaribu kuitisha vyeti vingine kama vya ndoa nk. Ilionekana kutofautina hawa itabidi watupishe” alisema Ndumbaro.

 Aidha aliongeza kamba, “wapo baadhi ambao wao walipoteza vyeti lakini kwa uvivu hawakutaka kufuatilia Polisi au barazani kwa ajili yakutapatiwa nakala zingine badala yake wakaenda kutengeneza kwa matokeo yale yale ya vyeti vyao halisi hawa tutawafikiria kwani dhamira yao ilikuwa sio kughushi bali walikwepa usumbufu,”

Ndumbaro amesema mara baada yakukamilika kutolewa kwa taarifa ndipo vibali vya ajira vitatolewa ili kuweza kuziba nafasi zitakazo kuwa zimebaki wazi, lakini pia kuongezwa kwa baadhi ya watumishi kulingana na mahitaji kwenye maeneo tofauti tofauti.

”Ni kwamba mara baada ya zoezi hilo tutakuwa tunahitimisha utumishi hao walikata rufaa na wale watakaoshindwa wataungana na wale 8000, ili watupishe tufanya taratibu zingine” alisema Ndumbaro.

Ndumbaro pia aliwaagiza watumishi wote kuwasilisha taarifa zao sahihi kwa maafisa Utumishi ili waweze kuzinakilisha kisha kuziweka kwenye mfumo wa kieletroniki.

 “Kuna watu Place of Domicile, hazieleweki ni vema sasa kila mmoja aweke mambo yake sawa nakupeleka taarifa kwa maafisa utumishi,” alisema.

Sambamba na Maagizo hayo, Katibu Mkuu huyo amesema kwasasa serikali ipo katika mchakato wa kuanzisha mfumo wa (Service Delivery point), ambayo itasaidia kutambua mtumishi mahali alipo, lakini pia kuyajua majukumu anayoyatekeleza mtumishi husika. Zoezi hili litaanza na sekta za afya na elimu.

 

Awali akisoma taarifa  ya Utumishi wa umma katika  mkoa wa Mwanza kwa niaba ya katibu Tawala wa Mkoa huo Clodwig Mtweve, Katibu Tawala Msaidizi wa uapnde wa Utawala na rasilimali watu, katika Sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza, Projestus Rubanzibwa, alisema mkoa huo umeendelea nashughuli za  uboreshaji wa shughuli za umma katika Nyanja mbali mbali ikiwapo Afya na Elimu, ambapo, katika afya Mpango wa malipo kwa ufanisi (Result Basing Financing), mpango huu ulio anza  Mkoani Mwanza Mwezi, Aprili, 2016 ulio  na lengo la kuboresha huduma za afya ya msingi, ambapo kwa upande wa watumishi mazingira ya kazi yameboreshwa kwa kuwapatia  vitendea kazi, ukarabati wa miundo mbinu ya kutolea huduma na kulipa motisha kwa watumishi wa sekta husika kwa kuzingatia matokeo ya utendaji kwa vigezo vilivyoanishwa.

 

 

Rubanzibwa amesema “Baada ya tathmini kufanyika  kupitia mpango huu  imeonekana kuwa kumekuwa na ongezeko la ubora wa takwimu kutoka asilimia 43.4 hadi asilimia 70.7 kwa kipindi cha kuanzia Aprili, 2016 hadi Aprili, 2017”. Aidha amesema “Kuongezeka kwa morale ya utendaji kazi kwa watumishi kutokana malipo yanaolipwa kupitia utendaji na ufanisi Ukarabati wa miundo mbinu ya vituo vya kutolea huduma ambapo ofisi na majengo ya vituo yamekarabatiwa” aliongeza Rubanzibwa.

Katibu Mkuu Menejimenti ya Utumishi wa Umma Laurean Ndumbaro, alipokuwa akiongea na baadhi ya watumishi wa Umma katika mkoa wa Mwanza wakati wa juma la Utumishi wa Umma.



Akizungumzia maboresho katika sekta ya elimu, Rubanzibwa amesema Mpango wa Ulipaji kwa Matokeo umeendelea kutekelezwa kama ulivyokusudiwa, kati ya mwezi Februari na Aprili, 2017 Wakuu wa Idara za  Elimu Msingi na Sekondari wa  Halmashauri walipatiwa mafunzo juu ya utekelezaji wa mpango huo. Alisema mpango huo unalenga kuinua utendaji kazi wa walimu wanaofundisha darasani pamoja na wanafunzi ili kuwezesha kusawazisha ikama (Pupil Teacher’s Ratio) kwa kulipa gharama za uhamisho kwa walimu wanaohamishwa kwenda kujaza ikama katika shule zenye upungufu.

Lakini pia kuboresha miundo mbinu kwa kufanya ukarabati wa madarasa na ujenzi wa matundu ya vyoo kutoa motisha kwa wanafunzi na walimu wanaofanya vizuri katika matokeo ya mitihani mbalimbali ya kitaifa.

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa pamoja na Halmashauri zake nane (8) kwa taarifa za Mwezi Aprili, 2017 zina jumla ya watumishi 25,734 Kati ya hao watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa ni 632 na watumishi wa Halmashauri ni 24,742.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

Mh. Seleman Jafo Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, alipokuwa akifunua mkutano wa RBF ulioshirikisha Mikoa minane inayotekeleza mradi wa RBF nchini.
Serikali imesema haita wavumilia watendaji watakaoshindwa kusimamia ipasavyo mradi wa  Malipo kwa Ufanisi katika kuboresha utoaji wa huduma za Afya “Results Based  Finance” (RBF) ambao hivi sasa unatekelezwa katika mikoa minane hapa nchini.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

Hii ndio Keki Maalum iliyo andaliwa na AGPAHI mara baada yakumalizika kwa Kambi ya siku tano ya Malezi ya Vijana
Mkoani Mwanza.
Vijana wapatao 50 kutoka Mikoa ya Geita, Mwanza na Shinyanga, ambao walikuwa katika kambi ya malezi kwa vijana waishio na VVU/UKIMWI kwa muda wa siku tano katika Jiji la Mwanza  wamelipongeza Shirika AGPAHI kwa jinsi linavyoweza kutumia ipasavyo fedha wazipatazo kutoka kwa wadau wa Maendeleo.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

Bibi Leah Mwainyekule, akitoa ufafanuzi kuhusu Semina hiyo juu ya utunzaji fedha katika Vituo vya Afya na Shule Jiji Mwanza
Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Wakili Msomi Kiomoni Kiburwa Kibamba, amewagiza wataalam kutoka ngazi ya Kata za Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela kuzitumia ipasavyo tovuti za Halmashauri na mikoa katika kuweka mapato na matumizi ili kuongeza uwazi kwa wananchi.
Kaimu Mkurugenzi wa jiji la Mwanza, Omary Kamatta akifungua Semina hiyo ya siku mbili inayo washirikisha, Waratibu Elimu kata wa Jiji na Manispaa ya Ilemela katika ukumbi wa mkuu wa Mkoa wa Mwanza.


Akisoma hotuba kwa niaba ya Mkurugezi wa Jiji la Mwanza, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji hilo, Omary Kamatta, amesema ili wananchi wawe na imani na serikali yao, suala la uwazi lazima litiliwe maanani “nielekeze matumizi ya tovuti za Mikoa na Halmashauri katika kuweka taarifa zote za mapato na matumizi ya fedha za umma” alisema Kamatta na kuongeza kuwa   suala hilo ni maelekezo ya Serikali, na kila mmoja analijua na anapaswa kutekeleza.
Bwanakher Mmmoja ya Wakufunzi wakati wa Semina hiyo kwa Waratibu Elimu Kata na wasimamizi wa Vituo vya Afya.

Kamatta amesema, Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma ujulikanao kwa Kiingereza kama Public Sector Systems Strengthening, (PS3), uliowezesha mafunzo hayo ya Mfumo wa Uhasibu na Utoaji Taarifa za Fedha kwa ngazi ya Kituo cha Kutolea Huduma [Facility Financial Accounting and Reporting System (FFARS)], una lengo la kuongeza ufanisi, hususan katika masuala mazima ya mapato, na ndio utakuwa mtatuzi wa malalamiko ya wananchi.

Ameongeza kuwa, lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo watoa huduma katika vituo vya kutolea huduma, na kusaidia upatikanaji wa taarifa sahihi katika mahesabu ya mapato na matumizi katika halmashauri kote nchini.Mafunzo haya yanafanyika sambamba katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu, ili kuhakikisha kwamba nyote mnakuwa katika nafasi ya kwenda kuwafundisha watoa huduma mbalimbali katika Vituo vyote vya kutolea Huduma Tanzania Bara, yaani (Service providers or Facilities), ambavyo vinajumuisha Zahanati, Vituo vya Afya, Hospitali, Shule za Sekondari na za Msingi” alisema Kamatta.
Mkurugenzi wa Manispaa ya ilemea John Wanga, akisema maneno yakuwaasa washiriki wa Semina hiyo juu yakuzingatia yote watakayo fundishwa.

Akitoa maelezo ya awali, msimamizi mafunzo hayo katika Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela, Mkuu wa Mawasiliano wa PS3, Bibi Leah Mwainyekule, amesema kuanzia mwaka ujao wa fedha, yaani Julai 1, 2017, Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania itaanza kupeleka rasilimali fedha moja kwa moja kwenye vituo vya afya kwa ngazi za vituo vya kutolea huduma ambavyo vitapokea fedha hizo vinavyojumuisha Zahanati, Vituo vya Afya, na Hospitali za Wilaya.  Aidha zoezi hilo litakwenda sambamba na inavyotekelezwa kwenye sekta za elimu, Serikali za Vijiji na Ofisi za Kata.

Bibi Mwainyekule amesema, Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), wametoa mafunzo ya kina kwa wakufunzi  490 katika ngazi ya taifa na halmashauri nchini kote.  Mafunzo hayo yalifanyika katika mikoa ya Dodoma, Mbeya, Mtwara, na Shinyanga, ambao nao sasa wanajukumu kuwawezesha watumishi katika vituo vya Sekta ya Afya na Elimu kupata ujuzi wa namna ya kutumia mfumo mpya wa FFARS.

 

Mwainyekule  amesema, wakufunzi hao kwa sasa ndio wanaotoa elimu hiyo kwa watumiaji wa mwisho wa mfumo wa FFARS kwa ngazi ya Vituo vya Afya 550, Zahanati 6800, Hospitali za Wilaya 135, na takribani Shule za Msingi na Sekondari 20,000 katika mikoa yote 26 ya Tanzania Bara, vikiwemo vituo vya kutolea huduma kutoka Mikoa 13 na Halmashauri 93 zinazotekeleza Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3).

Mafunzo hayo yatahakikisha kuwa watoa huduma katika vituo wana ujuzi unaohitajika katika usimamizi wa fedha na kutoa huduma bora kwa wananchi wote Tanzania na kwa jamii zenye uhitaji.

Mfumo wa FFARS unatekelezwa kwa ushirikiano baina ya Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI); Wizara ya Fedha na Mipango; Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi; na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, pamoja na USAID
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Jumla ya mizani 3,070 Iliyo Hakikiwa katika mikoa ya kanda ya ziwa kwa ajili ya matayarisho ya ununuzi wa pamba kwa msimu wa 2017/2018 imekutwa salama mara baada ya kuhakikiwa na wakala wa Vipimo nchini.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella, amesema kukwama kwa mpango wa Milenia yaani Millennium Development Goals (MDGs), nikutokana na mpango huo kutoshirikisha serikali za Mitaa kikamilifu.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Meneja wa wakala wa Vipimo mkoa wa Mwanza,  Hemed Kipengela, wakati wa Utoaji wa Elimu juu ya Matumizi sahihi ya Mizani mkoani humo.
 
Wakala wa Vipimo (WMA) Tanzania imeendelea na zoezi la utoaji wa elimu  pamoja na uhakiki wa mizani kwenye  makampuni mbalimbali  ya wafanyabiashara Mkoani Mwanza   katika  Wilaya za  Kwimba, Magu, Misungwi  na Sengerema ikiwa ni maandalizi ya msimu wa Pamba.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

Kamishna mkuu wa TRA nchini Charles Kichere, akizungumza katika kikao hicho na waandishi wa habari hawapo pichani.

Mamlaka ya mapato nchini imetoa muda hadi kufikia  Juni 30, mwaka huu wananchi wote wanaodaiwa kodi ya majengo kuhakikisha wanailipa kodi hiyo ilikuepuka kufikishwa mahakamani na kutozwa faini.

Kauli hiyo imetolewa na kamishina mkuu wa TRA nchini ndugu Charles Kichere, alipokuwa akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Jijini Mwanza hii leo.

 

Mwisho wa kulipa kodi ya majengo bila adhabu ni tarehe 30 Juni, 2017. Hivyo wenye majengo yaliyopo katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza (Nyamagana), na Manispaa ya Ilemela wafike ofisi za TRA zilizopo karibu nao kuchukua ankara zao endapo hawajazipokea kutoka kwa viongozi wa serikali za mitaa yao au kujisajili  na kulipa kupitia benki yoyote ya biashara” alisema Kichere.

Kichere amefafanuakuwa kwa walioko sehemu ambazo nyumba zimethaminishwa watalipa kiwango cha asilimia ya thamani ya jengo kama inavyoonesha kwenye ankara zao na walioko maeneo ambayo hayajapimwa au kuthaminishwa watalipa viwango maalum vilivyopitishwa na mabaraza ya madiwani na kutangazwa na TRA kwenye vyombo vya habari.

Kichere amevitaja viwango hivyo vilivyopitishwa kuwa, ni shilingi za kitanzania (20,000) kwa Jiji la Mwanza na kumi na tano elfu (15,000) kwa Manispaa ya Ilemela.

TRA pia imepongeza ushirikiano mkubwa inaoupata kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na safu yake nzima ya uongozi ikiwemo Serikali za Mitaa husika. “Mhe mkuu wa Mkoa ushirikiano huo umetuwezesha kutoa makadirio sahihi ya tozo, kutumia viwango rafiki, kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji, Kutoa elimu kwa jamii, kushughulikia pingamizi za kodi ya majengo kwa wakati na kuendelea kuimarisha uthamini wa majengo” amesema Kichere.
Mh. John Mongella mkuu wa Mkoa wa Mwanza, akizunguza kabla yakumkaribisha Kamishna Mkuu wa TRA kutoa taarifa kwa vyombo vya habari.

Kwa Upande wake Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella, amesema katika kufikia adhma hiyo ya ukusanyaji mapato, wakurugenzi wote wa Halmashauri za mkoa huo hawataruhusiwa kutoka nje ya vituo vyao vya kazi hadi kuisha kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017. “Ajenda yetu kuu ni kukusanya Mapato, hivyo Ndugu kamishna mimi nikuthibitishie tu kuwa kwa sasa, hatuta ruhusu Mkurugenzi atoke katika kituo chake cha kazi labda kama amepata Msiba” amesema Mongella.