June 2017
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

Serikali mkoani hapa, imewapa jukumu kubwa viongozi wa dini kutoka baadhi ya  mikoa ya kanda ya ziwa kuhakikisha wanakuwa bega kwa bega katika kulitunza ziwa Viktoria na Maliasili zake ili liweze kuwa tegemeo kwa kizazi cha sasa na kijacho. 


Sheik Hassan Kabeke,  Mwenyekiti mwenza wa Kamati ya Amani ya mkoa wa Mwanza, akifafanua umuhimu wa mazingira kwa Waandishi wa habari 
Dkt. Charles Mlingwa Mkuu wa mkoa wa Mara akifungua warsha hiyo ya Viongozi wa Dini, Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa mikoa ya kanda ya Ziwa.
 


Akifungua Semina ya siku moja mkoani hapa Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, na risala yake kusomwa na Mkuu wa Mkoa wa Mara Dkt. Charles Mlingwa, Mongella amesema, viongozi wa dini wanalo jukumu kubwa kwani wao husimamia imani za watu. “Ninyi Viongozi wa dini dhima mliyonayo ndani ya jamii ni kubwa sana na chochote mtakacho waelekeza waumini wenu lazima waweze kukitekeleza, hivyo niwaombe sana viongozi wangu tulilinde ziwa viktoria kwa jitihada zetu zote’’ alisema Mongella.

Aidha Mongella amesema kuwa, kuwepo kwa Ziwa Victoria ni fursa ya uendelezaji ya kauli mbiu ya “Tanzania ya Viwanda” ambayo Serikali ya awamu ya Tano inasisitiza,  Ziwa hili linasaidia upatikanaji wa rasilimali zinazotumika kwa matumizi ya nyumbani na viwandani, usafiri na usafirishaji na uzalishaji wa nishati ya umeme Hivyo basi hatuna budi kuhifadhi mazingira ya Ziwa na Bonde lake” amesisitiza Mkuu huyo wa mkoa.

Kwa upande wao, viongozi wa dini wakiongea wamesema, wao wanatambua na hata vitabu vya dini vinaelekeza juu ya mwanadamu anachopaswa kufanya katika kulinda mazingira ikiwepo ziwa Viktoria.

Mwenyekiti mwenza wa Kamati ya amani ya madhehebu ya dini katika Mkoa wa Mwanza, Sheik Hassan Kabeke, amesema katika Uislam  na hususan ni katika mafundisho ya Mtume Muhama S.A.W,  inafafanua juu ya mito miwili yaani mto Nile na Furabu ambayo mtume aliipitia huku akisema kwamba, Mto Nile ambao unafungamanishwa na Ziwa Viktoria Mtume amesisitiza kuyatunza mazingira, “Katika kupanda miti kwenye uislamu mtu hupata thawabu, tunaimani kabisa kwamba kila mmoja wetu akitunza mazingira ni sehemu ya Ibada, amesema Kabeke.

Naye Baba Askofu Michael Msonganzila wa Jimbo Katoliki la Musoma, kwa upande wake amesema kwa habari ya mazingira, tunaona ni jukumu la jamii nzima bila kujali itikadi zetu “ Kukutana kwetu hapa tunataka kuangalia nikwa namna gani tutaziangazia sababu za kiuchumi na kijamii, alisema Msonganzila na kuongeza kwamba kwa sasa wao katika Mkoa wa Mara wanayo kampeni kwenye eneo la Serengeti ambayo wanaendelea kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa Utunzaji wa mazingira na mabadiliko ya hali ya nchi.

Mradi wa Hifadhi ya Mazingira wa Ziwa Victoria (LVEMP II) utakamilika mwezi Disemba, 2017, aidha warsha hiyo ni kati ya warsha nne zilizoandaliwa na Mradi kwa madhumuni ya kukusanya maoni ya wadau ambayo yatawezesha kuandaa awamu ijayo ya Mradi inayotarajiwa kuanza kutekelezwa kuanzia mwaka 2018.
Kikao hicho kimewakutanisha Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa pamoja na Viongozi wa dini kutoka mikoa ya Mwanza, Geita, Kagera, Simiyu na Mara
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, amewataka vijana wanamichezo wa UMITASHUMTA na UMISETA pamoja na walimu wao kujizatiti katika suala zima la taaluma mara baada yakufanya vizuri katika michezo hiyo iliyo malizika mkoani hapa kwa mwaka huu wa 2017 na mkoa huo kuibuka mshinda wa kwanza na wapili.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.


Hatma ya mgogoro wa watumishi ambao walikuwa na vyeti feki itajulikana mwishoni mwa mwezi wa sita mara baada ya zoezi la kusikilizwa kwa rufaa kukamilika.

Akizungumza Mkoani Mwanza juzi na watumishi wa Mkoa wakati wa juma la Utumishi wa Umma, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Laurian Ndumbaro    alisema, hadi kufikia Juni 30, 2017 hatma ya wale wote waliokuwa na vyeti vya bandia itajulikana mara baada ya kupitia rufaa zote ambazo ziliwasikishwa ofisini kwake.

“Baada ya uchambuzi kutokana na malalamiko yaliyowasilishwa na wahusika, mnamo kesho Juni 30 tutatoa majibu,” alisema.

Ndumbaro alifafanua kwamba wapo watakaorejeshwa lakini wapo pia ambao uwezekano wa kurejeshwa hautakuwepo kutokana na ushahidi uliopatikana.

“Lazima tuelewane katika hili, wapo ambao wao walikuwa na vyeti vya daraja sifuri, wakaenda wakatengeneza vyeti vyenye dara la pili au la kwanza au latatu, hawa tulipojaribu kuitisha vyeti vingine kama vya ndoa nk. Ilionekana kutofautina hawa itabidi watupishe” alisema Ndumbaro.

 Aidha aliongeza kamba, “wapo baadhi ambao wao walipoteza vyeti lakini kwa uvivu hawakutaka kufuatilia Polisi au barazani kwa ajili yakutapatiwa nakala zingine badala yake wakaenda kutengeneza kwa matokeo yale yale ya vyeti vyao halisi hawa tutawafikiria kwani dhamira yao ilikuwa sio kughushi bali walikwepa usumbufu,”

Ndumbaro amesema mara baada yakukamilika kutolewa kwa taarifa ndipo vibali vya ajira vitatolewa ili kuweza kuziba nafasi zitakazo kuwa zimebaki wazi, lakini pia kuongezwa kwa baadhi ya watumishi kulingana na mahitaji kwenye maeneo tofauti tofauti.

”Ni kwamba mara baada ya zoezi hilo tutakuwa tunahitimisha utumishi hao walikata rufaa na wale watakaoshindwa wataungana na wale 8000, ili watupishe tufanya taratibu zingine” alisema Ndumbaro.

Ndumbaro pia aliwaagiza watumishi wote kuwasilisha taarifa zao sahihi kwa maafisa Utumishi ili waweze kuzinakilisha kisha kuziweka kwenye mfumo wa kieletroniki.

 “Kuna watu Place of Domicile, hazieleweki ni vema sasa kila mmoja aweke mambo yake sawa nakupeleka taarifa kwa maafisa utumishi,” alisema.

Sambamba na Maagizo hayo, Katibu Mkuu huyo amesema kwasasa serikali ipo katika mchakato wa kuanzisha mfumo wa (Service Delivery point), ambayo itasaidia kutambua mtumishi mahali alipo, lakini pia kuyajua majukumu anayoyatekeleza mtumishi husika. Zoezi hili litaanza na sekta za afya na elimu.

 

Awali akisoma taarifa  ya Utumishi wa umma katika  mkoa wa Mwanza kwa niaba ya katibu Tawala wa Mkoa huo Clodwig Mtweve, Katibu Tawala Msaidizi wa uapnde wa Utawala na rasilimali watu, katika Sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza, Projestus Rubanzibwa, alisema mkoa huo umeendelea nashughuli za  uboreshaji wa shughuli za umma katika Nyanja mbali mbali ikiwapo Afya na Elimu, ambapo, katika afya Mpango wa malipo kwa ufanisi (Result Basing Financing), mpango huu ulio anza  Mkoani Mwanza Mwezi, Aprili, 2016 ulio  na lengo la kuboresha huduma za afya ya msingi, ambapo kwa upande wa watumishi mazingira ya kazi yameboreshwa kwa kuwapatia  vitendea kazi, ukarabati wa miundo mbinu ya kutolea huduma na kulipa motisha kwa watumishi wa sekta husika kwa kuzingatia matokeo ya utendaji kwa vigezo vilivyoanishwa.

 

 

Rubanzibwa amesema “Baada ya tathmini kufanyika  kupitia mpango huu  imeonekana kuwa kumekuwa na ongezeko la ubora wa takwimu kutoka asilimia 43.4 hadi asilimia 70.7 kwa kipindi cha kuanzia Aprili, 2016 hadi Aprili, 2017”. Aidha amesema “Kuongezeka kwa morale ya utendaji kazi kwa watumishi kutokana malipo yanaolipwa kupitia utendaji na ufanisi Ukarabati wa miundo mbinu ya vituo vya kutolea huduma ambapo ofisi na majengo ya vituo yamekarabatiwa” aliongeza Rubanzibwa.

Katibu Mkuu Menejimenti ya Utumishi wa Umma Laurean Ndumbaro, alipokuwa akiongea na baadhi ya watumishi wa Umma katika mkoa wa Mwanza wakati wa juma la Utumishi wa Umma.



Akizungumzia maboresho katika sekta ya elimu, Rubanzibwa amesema Mpango wa Ulipaji kwa Matokeo umeendelea kutekelezwa kama ulivyokusudiwa, kati ya mwezi Februari na Aprili, 2017 Wakuu wa Idara za  Elimu Msingi na Sekondari wa  Halmashauri walipatiwa mafunzo juu ya utekelezaji wa mpango huo. Alisema mpango huo unalenga kuinua utendaji kazi wa walimu wanaofundisha darasani pamoja na wanafunzi ili kuwezesha kusawazisha ikama (Pupil Teacher’s Ratio) kwa kulipa gharama za uhamisho kwa walimu wanaohamishwa kwenda kujaza ikama katika shule zenye upungufu.

Lakini pia kuboresha miundo mbinu kwa kufanya ukarabati wa madarasa na ujenzi wa matundu ya vyoo kutoa motisha kwa wanafunzi na walimu wanaofanya vizuri katika matokeo ya mitihani mbalimbali ya kitaifa.

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa pamoja na Halmashauri zake nane (8) kwa taarifa za Mwezi Aprili, 2017 zina jumla ya watumishi 25,734 Kati ya hao watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa ni 632 na watumishi wa Halmashauri ni 24,742.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

Mh. Seleman Jafo Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, alipokuwa akifunua mkutano wa RBF ulioshirikisha Mikoa minane inayotekeleza mradi wa RBF nchini.
Serikali imesema haita wavumilia watendaji watakaoshindwa kusimamia ipasavyo mradi wa  Malipo kwa Ufanisi katika kuboresha utoaji wa huduma za Afya “Results Based  Finance” (RBF) ambao hivi sasa unatekelezwa katika mikoa minane hapa nchini.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

Hii ndio Keki Maalum iliyo andaliwa na AGPAHI mara baada yakumalizika kwa Kambi ya siku tano ya Malezi ya Vijana
Mkoani Mwanza.
Vijana wapatao 50 kutoka Mikoa ya Geita, Mwanza na Shinyanga, ambao walikuwa katika kambi ya malezi kwa vijana waishio na VVU/UKIMWI kwa muda wa siku tano katika Jiji la Mwanza  wamelipongeza Shirika AGPAHI kwa jinsi linavyoweza kutumia ipasavyo fedha wazipatazo kutoka kwa wadau wa Maendeleo.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
/>
Mkurugenzi wa Miradi kutoka shirika la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative (AGPAHI) Dk. Safila Telatela akizungumza wakati wa kufungua Ariel Camp (Kambi ya Ariel) ya siku tano kuanzia June 19,2017 - June 23,2017 iliyokutanisha watoto na vijana 50 kutoka mikoa ya Shinyanga,Mwanza na Geita jijini Mwanza.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Serikali imesema ni marufuku kwa shule ambayo itakuwa haina viwanja vya michezo kupatiwa kibali cha kufungua shule ikiwa ni utekelezaji wa Sheria ya Elimu namba 25 ya mwaka 1978.






 
Akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mashindano ya kwashule za msingi nchini UMITASHUMTA mkoani Mwanza, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMO) Mh. George Simbachawene, amemuagiza Kamishna wa Elimu nchini, kutozipatia vibali shule zinazo hitaji kufunguliwa endapo zitakuwa hazina viwanja vya michezo.

 

Simbachawene, amesema kutokana na sheria ya Elimu namba 25 ya mwaka 1978, ambayo inataka kila shule inapofunguliwa lazima iwe na viwanja visivyo pungua vitano hivyo nilazima hili lizingatiwe, “nichukue nafasi hii kumuagiza kamishna wa Elimu kuanzia sasa asisajili shule yeyote ile ambayo itakuwa haina Viwanja vya michezo, kwani bila kufanya hivyo azma yetu yakuinua michezo nchini haiwezi kutimia” alisema.

 

Mbali na kutoa maagizo hayo waziri Simbachawene, ameziagiza pia halmashauri na wilaya kote nchini kutenga sehemu ya mapato yao ya  ndani kwaajili ya kitengo cha michezo, huku akizihimiza kuweka katika bajeti ijayo ya serikali fedha kwenye vifungu vinavyo husiana na michezo na kuonya kuwa endapo Halmashauri itashindwa kufanya hivyo basi yeye kama waziri mwenye dhamana hatakubali ipite.

 

Amesema Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015 sehemu ya (61) inatambua suala la Michezo lakini pia Sera ya Elimu ya Mwaka 1995, hivyo kama Serikali lazima waweke kipaumbele katika suala zima la michezo.

 

Ameongeza kuwa, Msingi wa Michezo nchini ni michezo ya UMITASHUMTA NA UMISETA ndio Dira ya timu zetu za Taifa, “Tukiwaandaa vijana wetu vizuri na kutokana kaulimbiu hii ya masula ya viwanda, hatuna wasiwasi kuwa hawa ndio viwanda vyenyewe, mchezaji mmoja aliyefikia viwango vya kimataifa huweza kugharamia hata bajeti ya nchi” alisema Simbachawene.

 

Katika hatua nyingine Simbachawene, amewaagiza makatibu Tawala kote nchini, kusimamia suala la taaluma na michezo, amesema hakuna taaluma bila Michezo na Hakuna michezo bila Taaluma kwa mantiki hiyo lazima nidhamu ya hali ya juu iongezwe miongoni mwa vijana na wanamichezo kwa ujumla.  

 

Naye  Mkurugenzi wa Michezo nchini kutoka Wizara ya Habari, Michezo Sanaa na Wasanii Dkt. Yusuph Singo amesema Tayari Wadau Mbali mbali wa Michezo wakiongozwa na Chama cha Mpira wa Miguu na Riadha wapo Mkoani Mwanza kwaajili ya Kuangalia Vipaji kwa ajili ya Timu mbali mbali za Taifa lakini pia vilabu vyao.

 

Aidha amesema kuwa wizara ipo katika Mazungumzo na Timu Manchester City kupitia wakala wao wa TECHNO kwaajili yakuchukuwa Vijana wapatao kumi kutoka Tanzania kwaajili yakuwaendeleza kimichezo.

 

Awali akimkaribisha Mgeni rasmi, Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, aliishukuru serikali kwakuichagua Mwanza kuwa mwenyeji wa mashindano hayo huku akiomba kwa mwaka ujao mashindano hayo kufanyika tena mkoani humo, kutokana na madhari mazuri lakini pia ubora wa viwanja na hali ya ulinzi na usalama inayotamalaki katika mkoa huo, “Mh. Waziri mimi niombe tu, haya mashindando katika mwaka ujao myalete tena Mwanza sisi tupo tayari, huo ndio mtazamo wangu lakini pia wenzangu wataniunga mkono” alisema Mongella.

 

Mashindano ya shule za msingi (UMITASHUMTA) ya 2017 ni mashindano ya 22 ambapo yanashirikisha wanamichezo wapatao 2522 kutoka mikoa 26 ya Tanzania Bara.

 

 

 

 
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
 Meneja wa Wakala wa Vipimo Mkoa wa Mwanza, akishuhudia mzani unaopima Pamba mara baada ya msimu wa Ununuzi kuanza

Elimu ya Mizani kwa wakulima wa Pamba Mkoani Shinyanga hata baada ya Msimu wa Ununuzi wa pamba kuanza

Marobota ya Pamba yanayo subiri kuuzwa baada ya msimu kufunguliwa mkoani Simiyu



Maafisa wa Wakala wa Vipimo wakiangali Mawe ya Mizani yanayotumika katika Mizani Mbalimbali.
Waliosimama chini ni Maafisa wa Wakala wa Vipimo wakionesha Mizani zilizo hakikiwa tayari kwa msimu huu wa ununuzi wa Pamba



Mkulima akiwa amepima Pamba yake katika Mizani iliyo hakikiwa na Wakala wa Vipimo Mkoani Simiyu


Afisa wa wakala wa Vipimo, Bibi Rehema Michael akipima usahihi wa robota la Pamba kwakutumia mizani iliyohakikiwa na wakala wa Vipimo  mkoani Simiyu mara baada yakufunguliwa kwa Msimu (Picha zote na Wakala wa Vipimo)

Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

Bibi Leah Mwainyekule, akitoa ufafanuzi kuhusu Semina hiyo juu ya utunzaji fedha katika Vituo vya Afya na Shule Jiji Mwanza
Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Wakili Msomi Kiomoni Kiburwa Kibamba, amewagiza wataalam kutoka ngazi ya Kata za Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela kuzitumia ipasavyo tovuti za Halmashauri na mikoa katika kuweka mapato na matumizi ili kuongeza uwazi kwa wananchi.
Kaimu Mkurugenzi wa jiji la Mwanza, Omary Kamatta akifungua Semina hiyo ya siku mbili inayo washirikisha, Waratibu Elimu kata wa Jiji na Manispaa ya Ilemela katika ukumbi wa mkuu wa Mkoa wa Mwanza.


Akisoma hotuba kwa niaba ya Mkurugezi wa Jiji la Mwanza, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji hilo, Omary Kamatta, amesema ili wananchi wawe na imani na serikali yao, suala la uwazi lazima litiliwe maanani “nielekeze matumizi ya tovuti za Mikoa na Halmashauri katika kuweka taarifa zote za mapato na matumizi ya fedha za umma” alisema Kamatta na kuongeza kuwa   suala hilo ni maelekezo ya Serikali, na kila mmoja analijua na anapaswa kutekeleza.
Bwanakher Mmmoja ya Wakufunzi wakati wa Semina hiyo kwa Waratibu Elimu Kata na wasimamizi wa Vituo vya Afya.

Kamatta amesema, Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma ujulikanao kwa Kiingereza kama Public Sector Systems Strengthening, (PS3), uliowezesha mafunzo hayo ya Mfumo wa Uhasibu na Utoaji Taarifa za Fedha kwa ngazi ya Kituo cha Kutolea Huduma [Facility Financial Accounting and Reporting System (FFARS)], una lengo la kuongeza ufanisi, hususan katika masuala mazima ya mapato, na ndio utakuwa mtatuzi wa malalamiko ya wananchi.

Ameongeza kuwa, lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo watoa huduma katika vituo vya kutolea huduma, na kusaidia upatikanaji wa taarifa sahihi katika mahesabu ya mapato na matumizi katika halmashauri kote nchini.Mafunzo haya yanafanyika sambamba katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu, ili kuhakikisha kwamba nyote mnakuwa katika nafasi ya kwenda kuwafundisha watoa huduma mbalimbali katika Vituo vyote vya kutolea Huduma Tanzania Bara, yaani (Service providers or Facilities), ambavyo vinajumuisha Zahanati, Vituo vya Afya, Hospitali, Shule za Sekondari na za Msingi” alisema Kamatta.
Mkurugenzi wa Manispaa ya ilemea John Wanga, akisema maneno yakuwaasa washiriki wa Semina hiyo juu yakuzingatia yote watakayo fundishwa.

Akitoa maelezo ya awali, msimamizi mafunzo hayo katika Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela, Mkuu wa Mawasiliano wa PS3, Bibi Leah Mwainyekule, amesema kuanzia mwaka ujao wa fedha, yaani Julai 1, 2017, Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania itaanza kupeleka rasilimali fedha moja kwa moja kwenye vituo vya afya kwa ngazi za vituo vya kutolea huduma ambavyo vitapokea fedha hizo vinavyojumuisha Zahanati, Vituo vya Afya, na Hospitali za Wilaya.  Aidha zoezi hilo litakwenda sambamba na inavyotekelezwa kwenye sekta za elimu, Serikali za Vijiji na Ofisi za Kata.

Bibi Mwainyekule amesema, Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), wametoa mafunzo ya kina kwa wakufunzi  490 katika ngazi ya taifa na halmashauri nchini kote.  Mafunzo hayo yalifanyika katika mikoa ya Dodoma, Mbeya, Mtwara, na Shinyanga, ambao nao sasa wanajukumu kuwawezesha watumishi katika vituo vya Sekta ya Afya na Elimu kupata ujuzi wa namna ya kutumia mfumo mpya wa FFARS.

 

Mwainyekule  amesema, wakufunzi hao kwa sasa ndio wanaotoa elimu hiyo kwa watumiaji wa mwisho wa mfumo wa FFARS kwa ngazi ya Vituo vya Afya 550, Zahanati 6800, Hospitali za Wilaya 135, na takribani Shule za Msingi na Sekondari 20,000 katika mikoa yote 26 ya Tanzania Bara, vikiwemo vituo vya kutolea huduma kutoka Mikoa 13 na Halmashauri 93 zinazotekeleza Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3).

Mafunzo hayo yatahakikisha kuwa watoa huduma katika vituo wana ujuzi unaohitajika katika usimamizi wa fedha na kutoa huduma bora kwa wananchi wote Tanzania na kwa jamii zenye uhitaji.

Mfumo wa FFARS unatekelezwa kwa ushirikiano baina ya Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI); Wizara ya Fedha na Mipango; Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi; na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, pamoja na USAID
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Jumla ya mizani 3,070 Iliyo Hakikiwa katika mikoa ya kanda ya ziwa kwa ajili ya matayarisho ya ununuzi wa pamba kwa msimu wa 2017/2018 imekutwa salama mara baada ya kuhakikiwa na wakala wa Vipimo nchini.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella, amesema kukwama kwa mpango wa Milenia yaani Millennium Development Goals (MDGs), nikutokana na mpango huo kutoshirikisha serikali za Mitaa kikamilifu.