May 2017
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Meneja wa wakala wa Vipimo mkoa wa Mwanza,  Hemed Kipengela, wakati wa Utoaji wa Elimu juu ya Matumizi sahihi ya Mizani mkoani humo.
 
Wakala wa Vipimo (WMA) Tanzania imeendelea na zoezi la utoaji wa elimu  pamoja na uhakiki wa mizani kwenye  makampuni mbalimbali  ya wafanyabiashara Mkoani Mwanza   katika  Wilaya za  Kwimba, Magu, Misungwi  na Sengerema ikiwa ni maandalizi ya msimu wa Pamba.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

Kamishna mkuu wa TRA nchini Charles Kichere, akizungumza katika kikao hicho na waandishi wa habari hawapo pichani.

Mamlaka ya mapato nchini imetoa muda hadi kufikia  Juni 30, mwaka huu wananchi wote wanaodaiwa kodi ya majengo kuhakikisha wanailipa kodi hiyo ilikuepuka kufikishwa mahakamani na kutozwa faini.

Kauli hiyo imetolewa na kamishina mkuu wa TRA nchini ndugu Charles Kichere, alipokuwa akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Jijini Mwanza hii leo.

 

Mwisho wa kulipa kodi ya majengo bila adhabu ni tarehe 30 Juni, 2017. Hivyo wenye majengo yaliyopo katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza (Nyamagana), na Manispaa ya Ilemela wafike ofisi za TRA zilizopo karibu nao kuchukua ankara zao endapo hawajazipokea kutoka kwa viongozi wa serikali za mitaa yao au kujisajili  na kulipa kupitia benki yoyote ya biashara” alisema Kichere.

Kichere amefafanuakuwa kwa walioko sehemu ambazo nyumba zimethaminishwa watalipa kiwango cha asilimia ya thamani ya jengo kama inavyoonesha kwenye ankara zao na walioko maeneo ambayo hayajapimwa au kuthaminishwa watalipa viwango maalum vilivyopitishwa na mabaraza ya madiwani na kutangazwa na TRA kwenye vyombo vya habari.

Kichere amevitaja viwango hivyo vilivyopitishwa kuwa, ni shilingi za kitanzania (20,000) kwa Jiji la Mwanza na kumi na tano elfu (15,000) kwa Manispaa ya Ilemela.

TRA pia imepongeza ushirikiano mkubwa inaoupata kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na safu yake nzima ya uongozi ikiwemo Serikali za Mitaa husika. “Mhe mkuu wa Mkoa ushirikiano huo umetuwezesha kutoa makadirio sahihi ya tozo, kutumia viwango rafiki, kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji, Kutoa elimu kwa jamii, kushughulikia pingamizi za kodi ya majengo kwa wakati na kuendelea kuimarisha uthamini wa majengo” amesema Kichere.
Mh. John Mongella mkuu wa Mkoa wa Mwanza, akizunguza kabla yakumkaribisha Kamishna Mkuu wa TRA kutoa taarifa kwa vyombo vya habari.

Kwa Upande wake Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella, amesema katika kufikia adhma hiyo ya ukusanyaji mapato, wakurugenzi wote wa Halmashauri za mkoa huo hawataruhusiwa kutoka nje ya vituo vyao vya kazi hadi kuisha kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017. “Ajenda yetu kuu ni kukusanya Mapato, hivyo Ndugu kamishna mimi nikuthibitishie tu kuwa kwa sasa, hatuta ruhusu Mkurugenzi atoke katika kituo chake cha kazi labda kama amepata Msiba” amesema Mongella.

 
 

 

 

 

 

 

 
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Wakala wa Vipimo nchini imezuia matumizi ya mizani 94 kati 150 ya vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS) katika Wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi, isitumike hadi pale itakapo fanyiwa marekebisho na kuonekana inafaa kwa matumizi.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Ikiwa leoni tarehe 21 Mei 2017, wananchi katika mkoa wa Mwanza wakiongozwa na mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, wameendele kuwalilia na kuwakumbuka watu waliozama na Meli Mv. Bukoba, huku simanzi na majonzi vikishindwa kufutika katika fikra na mawazo ya  watanzania.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
WAKALA WA VIPIMO (WMA) 
SIKU YA VIPIMO DUNIANI
VIPIMO VINAVYOTUMIKA KATIKA SEKTA YA USAFIRISHAJI

(MEASUREMENT FOR TRANSPORT)

Mei, 20 kila mwaka nchi nyingi duniani husherehekea siku ya  vipimo duniani. Mwaka huu kauli  mbiu ( theme) ya maadhimisho ni vipimo katika sekta ya usafirishaji (measurement for transport).
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
 
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amezindua Bodi mpya ya ushauri ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekouture inayoundwa na wajumbe wapatao 15, huku akiibebesha jukumu lakuhakikisha hospitali hiyo inachana na mfumo wa ukusanyaji mapato wa kawaida na badala yake watumie mfumo wa kieletroniki
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

Serikali mkoani Mwanza imeitaka jamii kote nchini kuwapeleka watoto wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) shule, badala ya kuwanyanyapaa na baadhi kuwaficha ndani na kisha kufifisha ndoto zao za maisha.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

ZOEZI ZA UKAGUZI WA MIZANI LIKIENDELEA

Wakala wa Vipimo (WMA) wa Vipimo Tanzania imeendelea na zoezi la utoaji wa elimu  pamoja na uhakiki wa mizani kwenye vyama  mbalimbali vya  wakulima ( AMCOS) Wilayani Masasi Mkoani Mtwara ikiwa ni maandalizi ya msimu wa korosho pamoja na mazao mengine kama vile choroko, mbaazi pamoja na ufuta.