Articles by "Michezo"
Showing posts with label Michezo. Show all posts
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, amewataka vijana wanamichezo wa UMITASHUMTA na UMISETA pamoja na walimu wao kujizatiti katika suala zima la taaluma mara baada yakufanya vizuri katika michezo hiyo iliyo malizika mkoani hapa kwa mwaka huu wa 2017 na mkoa huo kuibuka mshinda wa kwanza na wapili.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Serikali imesema ni marufuku kwa shule ambayo itakuwa haina viwanja vya michezo kupatiwa kibali cha kufungua shule ikiwa ni utekelezaji wa Sheria ya Elimu namba 25 ya mwaka 1978.






 
Akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mashindano ya kwashule za msingi nchini UMITASHUMTA mkoani Mwanza, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMO) Mh. George Simbachawene, amemuagiza Kamishna wa Elimu nchini, kutozipatia vibali shule zinazo hitaji kufunguliwa endapo zitakuwa hazina viwanja vya michezo.

 

Simbachawene, amesema kutokana na sheria ya Elimu namba 25 ya mwaka 1978, ambayo inataka kila shule inapofunguliwa lazima iwe na viwanja visivyo pungua vitano hivyo nilazima hili lizingatiwe, “nichukue nafasi hii kumuagiza kamishna wa Elimu kuanzia sasa asisajili shule yeyote ile ambayo itakuwa haina Viwanja vya michezo, kwani bila kufanya hivyo azma yetu yakuinua michezo nchini haiwezi kutimia” alisema.

 

Mbali na kutoa maagizo hayo waziri Simbachawene, ameziagiza pia halmashauri na wilaya kote nchini kutenga sehemu ya mapato yao ya  ndani kwaajili ya kitengo cha michezo, huku akizihimiza kuweka katika bajeti ijayo ya serikali fedha kwenye vifungu vinavyo husiana na michezo na kuonya kuwa endapo Halmashauri itashindwa kufanya hivyo basi yeye kama waziri mwenye dhamana hatakubali ipite.

 

Amesema Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015 sehemu ya (61) inatambua suala la Michezo lakini pia Sera ya Elimu ya Mwaka 1995, hivyo kama Serikali lazima waweke kipaumbele katika suala zima la michezo.

 

Ameongeza kuwa, Msingi wa Michezo nchini ni michezo ya UMITASHUMTA NA UMISETA ndio Dira ya timu zetu za Taifa, “Tukiwaandaa vijana wetu vizuri na kutokana kaulimbiu hii ya masula ya viwanda, hatuna wasiwasi kuwa hawa ndio viwanda vyenyewe, mchezaji mmoja aliyefikia viwango vya kimataifa huweza kugharamia hata bajeti ya nchi” alisema Simbachawene.

 

Katika hatua nyingine Simbachawene, amewaagiza makatibu Tawala kote nchini, kusimamia suala la taaluma na michezo, amesema hakuna taaluma bila Michezo na Hakuna michezo bila Taaluma kwa mantiki hiyo lazima nidhamu ya hali ya juu iongezwe miongoni mwa vijana na wanamichezo kwa ujumla.  

 

Naye  Mkurugenzi wa Michezo nchini kutoka Wizara ya Habari, Michezo Sanaa na Wasanii Dkt. Yusuph Singo amesema Tayari Wadau Mbali mbali wa Michezo wakiongozwa na Chama cha Mpira wa Miguu na Riadha wapo Mkoani Mwanza kwaajili ya Kuangalia Vipaji kwa ajili ya Timu mbali mbali za Taifa lakini pia vilabu vyao.

 

Aidha amesema kuwa wizara ipo katika Mazungumzo na Timu Manchester City kupitia wakala wao wa TECHNO kwaajili yakuchukuwa Vijana wapatao kumi kutoka Tanzania kwaajili yakuwaendeleza kimichezo.

 

Awali akimkaribisha Mgeni rasmi, Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, aliishukuru serikali kwakuichagua Mwanza kuwa mwenyeji wa mashindano hayo huku akiomba kwa mwaka ujao mashindano hayo kufanyika tena mkoani humo, kutokana na madhari mazuri lakini pia ubora wa viwanja na hali ya ulinzi na usalama inayotamalaki katika mkoa huo, “Mh. Waziri mimi niombe tu, haya mashindando katika mwaka ujao myalete tena Mwanza sisi tupo tayari, huo ndio mtazamo wangu lakini pia wenzangu wataniunga mkono” alisema Mongella.

 

Mashindano ya shule za msingi (UMITASHUMTA) ya 2017 ni mashindano ya 22 ambapo yanashirikisha wanamichezo wapatao 2522 kutoka mikoa 26 ya Tanzania Bara.

 

 

 

 
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

MWAKILISHI WA KATIBU TAWALA MKOA WA MWANZA, MWALIMU HAMISI MAULIDI AKIFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO, WAANDAAJI WA FILAMU NCHINI.
PICHANI NI BIBI JOYCE FISOO, KATIBU MTENDAJI WA BODI YA FILAMU NCHINI, AKIWASILISHA MADA WAKATI WA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZOWANATSNIA YA FILAMU MKOANI MWANZA.


RAIS WA SHIRIKISHO LA FILAMU TANZANIA BW. SAIMON MWAKIFWAMBA(KULIA), AKIFAFANUA JAMBO KWA MAAFISA WA  WA HIFADHI YA JAMII WA PPF KANDA YA ZIWA.
Na Lorietha Laurence-Mwanza

Mkoa wa Mwanza waweka mkakati  wa kukuza na kuendeleza sekta ya filamu kwa kuhakikisha inazalisha bidhaa bora zenye kufuata taaluma na weledi wa tasnia hiyo ili kufikia soko la kimataifa.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Bw John Mongella (kulia) akipokea cheti cha kutambua jitihada zake katika kufanikisha Rock City Marathon kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mbio hizo Bw Zenno Ngowi. Mbio hizo zilizofanyika Septemba 25 mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba
 
Na Mwandishi wetu,
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Bw John Mongella amesema mkoa wake umejipanga kutumia michezo kama nyenzo muhimu katika kutangaza fursa na vivutio vya utalii vilivyopo mkoani humo.
no image
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Rock City Marathon kutimua vumbi kesho (JUMAPILI)

Maandalizi ya Rock City Marathon zinazotarajiwa kufanyika kesho Septemba 25  kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza yamekamilika huku ushiriki wa wa wakuu wa mikoa ya Mwanza na Simiyu kwenye mbio hizo ukitajwa kuwa ni miongoni mwa vivutio vikubwa vinavyotarajiwa kupamba mbio hizo.

Mbio hizo zinazofanyika kwa mara  ya nane mfululizo tangu zianze mwaka 2009 zinaratibwa na kampuni ya Capital Plus International kwa kushirikiana na mkoa wa Mwanza zikiwa na baraka zote kutoka Chama cha Riadha Tanzania (RT), pamoja na Chama cha Riadha Mkoa wa Mwanza (MRAA) , zikilenga kilenga kutambua na kuinua vipaji vya wanariadha nchini, kutangaza utalii na vivutio vilivyoko kanda Ziwa pamoja na kupambana na ujangili.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Mwanza leo, Msemaji wa mbio hizo Bw Mathew Kasonta alisema kamati ya maandalizi ya mbio hizo imejiandaa vilivyo na maandalizi yote yamekamilika, ikiwemo kupokea wakimbiaji kutoka nje ya nchi na washiriki wengine.


Alisema wanatarajiwa kuwa na washiriki zaidi ya 1200 wakiwemo wakimbiaji wa kimataifa, wakimbiaji kutoka mashirika mbalimbali, walemavu wa ngozi yaani Albino pamoja na wanafunzi.
“Rock City Marathon inahusisha mbio za kilometa 21 kwa wanaume na wanawake,  mbio za Kilometa tano zitakazohusisha wafanyakazi kutoka makampuni mbalimbali (Corporate) pamoja na watu wenye ulemavu wa ngozi yaani Albino, mbio za Kilometa tatu ambazo zipo mahususi kwa ajili ya wazee, mbio za kilometa 2 zitakazohusisha watoto wenye umri kati ya miaka 7 hadi 10 pamoja na mbio fupi  za mita 100, 400, 800 na 1500 ambazo ni mahususi kwa wanafunzi,’’
“Kubwa zaidi pia ni kuwashukuru sana wadhamini wa mbio hizi kwa kuendelea kutuunga mkono kwenye maandalizi haya yaani kampuni za Freidkin Conservation Fund na African Wildlife Trust, Benki ya NMB,  New Mwanza Hotel, Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Real PR Solutions, kampuni ya Fabec, Tiper, Puma Energies, Clouds Fm, Jembe Fm, Barmedas Tv na EF Out Door,’’ alitaja.
Kuhusu barabara zitakazohusisha mbio hizo zitakazoanza saa 12:00 asubuhi Bw Kasonta alisema; “Kwa washiriki wa mbio za km 21 wataanzia Uwanja CCM Kirumba, kwa wale wa Km 5 wataanzia barabara ya Nyerere eneo la Polisi Mabatini, kwa wale wa Km 3 ambazo ni mbio za wazee wataanzia Barabara ya Nyerere eneo la Makaburi ya Wahindi na kwa mbio za watoto yaani Km 2 wao wataanzia eneo la Mwaloni kuelekea CCM Kirumba,’’

Kwa upande wa zawadi kwenye mbio hizo Bw Kasonta  alisema washindi wa kwanza wa mbio za kilometa 21 kwa wanaume na wanawake watajinyakulia sh.  mil 1.5/- kila mmoja, sh. 900,000/-  kwa washindi wa pili na sh. 700,000/- kwa washindi wa tatu.
“Kwa mbio za Kilometa tano ambazo zitaongowa na wakuu wa mikoa ya Mwanza na Simiyu ambazo pia zitahusisha wafanyakazi kutoka makampuni mbalimbali (Corporate) pamoja na watu wenye ulemavu wa ngozi yaani Albino,  washindi watapatiwa zawadi za heshima kwa makampuni huku pesa zilielekwa washiriki wenye ulemavu wa ngozi.,’’
Akizungumzia usalama katika tukio hilo ambalo litahusisha maelfu ya watu, Mwenyekiti Msaidizi wa kamati yam bio hizo Bw Zenno Ngowi  alisema kamati yake imekuwa ikifanya kazi kwa ukaribu zaidi na jeshi la polisi na jeshi la hilo limeshajipanga vilivyo kwa ajili ya tukio hilo ili kuhakikisha kila kitu kinaisha kwa usalama wakiwemo watazamaji na washiriki mbio hizo
no image
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

Awali ya yote napenda kuchukua fursa hii kukushukuru Katibu Tawala Msaidizi ambaye ni Afisaelimu wa Mkoa na Viongozi wenzako katika seksheni ya Elimu kwa kunialika kufungua Mashindano haya ya Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA).

Nimeupokea mwaliko huu kwa furaha kwa vile umenipa fursa ya pekee kuwaona na kuzungumza na hadhara hii ya wanafunzi, Wanamichezo na Walimu wao.  Aidha, nitumie fursa hii kuupongeza uongozi wa Nsumba na Jumuia yote kwa maandalizi mazuri ya Mazingira kwa ajili ya mashindano haya.  Ahsanteni sana.

Ndugu Viongozi na Wanamichezo:

Leo tukumbushane umuhimu wa Michezo kwa Taifa na kwa mwanamichezo, mashindano haya ni nyenzo mojawapo ya kujenga Umoja wa Kitaifa na hivyo kufanya maelewano na mshikamano kwa Watanzania.  Michezo ni Burudani lakini kwa sasa kutokana na mabadiliko ya Mazingira ya Kisiasa, Kiuchumi na Kijamii, Michezo ni Kipaumbele katika kutoa pia Ajira kwa vijana wetu, kukuza Biashara  na kujenga jamii bora yenye maelewano.  Kwa mfano, Nchi za wenzetu za Ulaya na Marekani, lakini nchi zingine za Afrika za Mataifa kama Nigeria, Togo, Ivory Coast, Cameroon zinatumia kikamilifu nafasi hii ya Michezo kujitangaza  kiuchumi na kijamii.

Natambua kwamba ninyi ni Wanafunzi ambao mnahitaji kukuza Taaluma na vipaji vyenu. Moja ya nafasi hizo ni Michezo ili michezo iendelee kukua nchini, ni lazima ukuzaji wa vipaji vya michezo uanzie shuleni, ndiyo maana michezo ni sehemu ya Mtaala wa masomo yenu, kama ambavyo tunawataka mfanye bidii katika masomo yenu, fanye bidii pia na kukuza vipaji vyenu katika michezo kwa kushiriki kikamilifu kuonesha ubunifu.

Ndugu Wanamichezo,

Wanamichezo bora, ni Watu wasikivu, wenye nidhamu na watiifu.  Ninyi vijana ambao ndio viongozi wa kesho wa Taifa letu mnahitaji sana kujijengea nidhamu na maadili ya hali ya juu ili muweze kuendana na hali ya maisha ya ushindani yatakayokuwa  yanawakabili.  Nidhamu, inamuwezesha Mtu kufanya kazi zake kwa mpangilio mzuri unaofuata taratibu zote za kazi kwa wakati.  Hii ndiyo njia ya uhakikika ya kufikia malengo yoyote yale na kupata mafanikio.

Aidha, kwa njia ya Michezo, nidhamu shuleni itaongezeka na matarajio yetu ni kuwa nidhamu hiyo itajitafsiri pia katika matokeo  mazuri kwenye Taaluma.  Matarajio ni kuwa, wanafunzi watakuwa na mahusiano mazuri zaidi kati yao na walimu wao na wale wote wanaopata Burudani ya Michezo.  Ama tunatarajia kuwa wataendelea kuwa watu wenye Nidhamu katika Utu Uzima wao, ili hatimaye tuwe na Taifa la Watu wenye nidhamu ya kutolewa mfano.

Ndugu Wanamichezo,

Nitumie fursa hii pia kuwakumbusha kwamba mnapofurahia kushiriki katika Michezo hii, ni lazima mkumbuke  kuwa furaha yenu itandelea  kudumu kama mtatambua kuwa kuna mpinzani mkubwa kati yetu aitwaye Virusi vya UKIMWI na UKIMWI.  Kila mmoja wenu anaelewa vya kutosha juu ya Adui huyu.  Ni wajibu wangu kama Kiongozi na Mlezi wenu kuwakumbusha juu yahatari inayowakabili msipokuchua tahadhari ya kutosha.  Kumbukeni UKIMWI bado unaenea kwa kasi kubwa sana hasa miongoni mwa Vijana wa Rika lenu kuliko rika lolote jingine.  Niwakumbushe kwamba upingine kwa nguvu zote   Ugonjwa huu.  Msikubali kukatishwa masomo na msikubali kutenganishwa mapema na familia zenu.  Kwenu ninyi, njia bora pekee ni kusubiri hadi wakati muafaka wa ndoa.  Wekeni bidii katika masomo, kwani muda ukifika yote yatajipanga vizuri.

Ndugu Wanamichezo,

Nimeelezwa kuwa baada ya Michezo hii yapo Mashindano ya Kanda ya Ziwa ambapo Mikoa ya Mwanza, Mara na Simiyu hukutana ili kuimarisha mahusiano ya Vijana wa Shule za Sekondari na kuunda timu moja ya Kanda.  Ni muhimu timu zetu zijipange kushiriki vizuri na kutuletea ushindi wa kishindo.  Aidha  timu hizo ziandaliwe vizuri ili zikashiriki kama washidani na si wasindikizaji. Kushiriki kwenu kunatujengea heshima  katika kujenga upeo wa akili za vijana wetu na kujenga mahusiano mazuri ya kikanda.  Natoa rai kwa Mashirika, Vyama vya Michezo na watu wengine kushiriki kwa kuchangia kufanikisha ushindi wa timu zetu za Mkoa.

Ndugu Wana Michezo,

Nimalizie hotuba yangu kwa kuwatakia kila la kheri kwa kipindi chote cha mashindano, aidha msisite kuwasiliana na ofisi yangu pale mtakapoona kuna ulazima wa kufanya hivyo kwa  ushauri na maelekezo kwa ajili ya kuboresha michezo hii.

 

Michezo hoyeeeeee!!!!

 

Asanteni kwa kunisikiliza

 
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
CCM KIRUMBA STADIUM, THE BEST PEACH IN MWANZA.
HAVING ALOTE OF TREES  IS MAKE MWANZA TO VERY ATRACTIVE PLACE.


YOU MAY LOOK THE MWANZA CITY COMMERCIAL COMPLEX. ALONG SIDE  OF CCM KIRUMBA STADIUM.


CCM KIRUMBA IN OTHER ANGLE.

ROAD TO BWIRU VIA KIRUMBA POLICE STATION

Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Kulikuwa na mechi mbili za mkondo wa kwanza wa robo fainali ya ligi kuu ya mabingwa barani Ulaya iliyochezwa Jumanne usiku, Manchester United ya Uingereza ikikabana koo na mabingwa watetezi waligi hiyo Bayern Munich ya Ujerumani.

Nayo Barcelona ya Uhispania ikikabiliana na Athletico Madrid vilevile ya Uhispania.

Licha ya kuwa Bayern Munich ilikuwa imepigiwa upatu kutamba dhidi ya Manchester United vijana wa pep Gardiola walikabiliwa na ukuta mrefu wa Manchester uwanjani Old Traford.

Na walipopata fursa nahodha wa Manchester Nemanja Vidic alifunga bao maridadi la kichwa baada ya kuunganisha vizuri kona kutoka kwa Wayne Rooney kunako dakika ya 58 ya kipindi cha pili.

Gonga gonga ya Wajerumani ilikosa kuzaa matunda lakini bao la Bastian Schweinsteiger kunako dakika ya 66 iliwatunuku mabingwa hao wao watetezi bao muhimu la ugenini kabla ya mkondo wa pili utakaochezwa huko Ujerumani .
MAN. U ILIPOKUWA INAKABILANA NA MUNICH YA UJERUMANI.
Bila shaka mashabiki na watani wa kocha David Moyes watakubaliana naye kuwa United itajutia fursa aliopoteza Danny Welbeck alipokuwa ni yeye pekee dhidi ya kipa wa Bayern Manuel Neuer .

United vilevile itamshukuru kipa David de Gea aliyefanya kazi ya ziada kuzuia mashambulizi haswa kutoka kwa Arjen Robben.

Kutokana na sare hiyo sasa mkufunzi Pep Guardiola ana kibarua kigumu pale Man United itakapozuru uwanja wa Allianz Arena wiki ijayo.
Mechi nyingine 2 zimeratibiwa kuchezwa baadaye Jumatano, Real Madrid ya Uhispania ikivaana na Borussia Dortmund kutoka Ujerumani nayo Paris st Germain ikiikaribisha wawakilishi wengine wa Uingereza Chelsea ya Uingereza Katika uwanja wa Parc des Princes
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
WACHAZAJI WA MADRID HAPA WAKIPONGEZANA BAADA YA ROLNARDO KUTUPIA GOLI.

Ni katika Kombe la Ulaya.
Ronaldo na Bale washerekea ushindi dhidi ya Schalke 04
Mchezaji bora duniani mwaka huu Cristiano Ronaldo Gareth Bale na Karim Benzima walifunga mabao mawili kila mmoja na kuisaidia Real Madrid ya uhispania kufuzu kwenye robo fainali ya kombe la mabingwa barani ulaya baada ya kuinyeshea Schalke 04 ya Ujerumani mabao 6-1 katika mkondo wa kwanza uliosakatwa huko Ujerumani.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Hawa Ndio Munich ambao hata hivyo bado wana kiwewe na Arsenal.

Kocha wa Bayern Munich Pep Guardiola amekiri ni vigumu sana kudhibiti dakika tisini za mechi ya aina yeyote dhidi ya Arsenal ya Uingereza .
Guardiola
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Na Atley Kuni. Mwanza.

HILI NDILO KOMBE LINALO INGIA MWANZA.



 

KIKAO NA WAANDISHI WA HABARI MWANZA.

Kwa mara ya kwanza Kombe la Dunia litapokelewa Mkoani Mwanza na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uwanja wa CCM Kirumba.
 



 
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo, mbele ya waandishi wa habari na kamati ya maandalizi ya ujio huo katika ukumbi wa Mwanza Hotel hivi leo.
 
Ndikilo amesema hii ni mara ya kwanza kwa kombe hilo kupokelewa katika Mkoa huo na akawataka wanachi kujitokeza kwa wingi ili kuweza kulipokea,amesema na kuongeza kuwa "Mhe shimiwa Rais ambaye yupo ziarani katika Mkoa wa Simiyu amekubali kulilaki kombe hilo katika mkoa wetu wa Mwanza hii ni heshima kubwa kama wananchi wa Mkoa huu na wapenda michezo kwa ujumla.
 
Amesema kombe hilo litawasili katika uwanja wa ndege wa mwanza majira ya saa tatu asubuhi na badae kupelekwa katika uwanja wa CCM Kirumba, ambapo pamoja na mambo mengine baadhi ya wananchi watapata fursa ya kupiga picha na kombe hilo.
 
Kwa upande wake Mwakilishi wa Coca Cola Nchini bw. Eyebolt Gretchen, amesema ujio wa Kombe hilo kwa mara ya tatu katika nchi ya Tanzania nia pamoja na amani ya nchi iliyopo na ukarimu wa watu wake, Miongoni mwa nchi za Afrika ambazo zimekuwa na utulivu hata kufanya kutembelewa na kombe la Dunia ni Tanzania, amesema na kuongeza kwamba, kama Coca cola wamekuwa mstari wa mbele kwenye jitihada za kukuza soka nchini ikiwapo mashindano ya Kopa Coca cola.
 
Kwa upande wake kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Ernest Mangu amewahakikishia wanachi wote wa Mkoa wa Mwanza amani na utulivu, aidha amewaomba wananchi kutokuja wanjani hapo wakiwa na watoto wadogo ili kuepusha adha wanayoweza kupata watoto hao" Labda niombe ndugu zangu kwa wale watoto wadogo ni vema wakaachwa nyumbani kuepuka usumbufu". alisema na kuongeza kuwa watu hawataruhusiwa kusogea karibu na eneo la Pitch ya uwanja huo.
 
Hii ni mara ya tatu kombe hilo linakuja hapa nchini ambapo mara zote limekuwa likipokelewa na kulakiwa na wananchi waishio katika Mkoa wa Dar es Salaam. 
 
Wadadisi wa mambo wanasema kwamba, ujio wa kombe hilo si tu kwamba linakuja kutazamwa na wanachi wa Mwanza bali pia ni frsa nzuri kwa mkoa huo kujitangaza kimataifa lakini pia kutangaza rasilimali zinazo patikana katika Mkoa huo alkini pia iwe chachu kwa vingozi kuona kuna umuhimu wa kuipa kipaumbele michezo yote, anasema Mashaka Baltazari mwandishi mwandamizi wa Jambo Leo na Mwakilishi Mkoani Mwanza.
 
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

MWENYEKITI wa Klabu ya Simba, Ismail Aden Rage ameliambia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania lililomtaka aitishe Mkutano Mkuu wa Dharura ndani ya siku 14, ili kutatua mgogoro kati yake na Kamati ya Utendaji.

Rage aliyasema hayo Dar es Salaam jana alipokutana na waandishi wa habari kuzungumzia agizo hilo sanjari na la Kamati ya Utendaji ya Simba iliyomsimamisha siku chache zilizopita.

“Kikao cha Kamati ya Utendaji kilichokaa na kuamua kunisimamisha ni batili kwa kuwa aliyeitisha mkutano huo hana mamlaka ya kufanya hivyo kwa Katiba ya Simba, hivyo ni sawa cha harusi,” amesema.

Amesema alidhani kwa kitendo hicho (kusimamishwa), TFF ingepinga jambo hilo kwa kuwa ni kinyume na taratibu za michezo kuhusu kufanya mapinduzi lakini na wao ndio kwanza wamempa siku 14 kuitisha mkutano.

Amesema kutokana na kukiukwa kwa Katiba ya TFF na Klabu ya Simba, hataitisha mkutano wowote kama alivyotakiwa ili naye asivunje Katiba na kama atalazimishwa kufanya hivyo yuko tayari kujiuzulu.

Rage ame tolea mfano wa msuguano uliotokea katika kipindi cha uchaguzi wa TFF uliofanya Serikali kuingilia kati sanjari na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kimataifa (Fifa), amesema baada adha hiyo kutokea, Fifa iliamuru TFF iitishe uchaguzi na kuwapangia tarehe na agenda.

Anadai kuwa  kitendo cha TFF kumwagiza kuitisha mkutano ndani ya siku 14 pamoja na kumchagulia agenda ni kinyume cha Katiba yake (TFF) , hivyo hatoitisha mkutano kama alivyotakiwa.

Akizungumzia kuhusu tuhuma zinazomakabili zilizochangia kusimamishwa kwake, kuhusu mshambuliaji wao za zamani, Emmanuel Okwi, alisema suala hilo linashughulikiwa na Ofisa wa Fifa anayeitwa Laura Santaniel.

Ameongeza kuwa suala la uchelewashaji wa fedha hizo ilitokana na klabu iliyomsajili ya Etoile du Sahel  (ESS) ya nchini Tunisia kukabiliwa na matatizo ya kiuchumi hali iliyofanya baadhi ya viongozi wa Simba akiwemo Hanspoppe kulifuatilia na sasa linashughulikiwa na Fifa.

Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Boniface Wambura alipotakiwa kueleza ni hatua gani zitachukuliwa ikiwa Rage hataitisha Mkutano Mkuu wa Dharura kama alivyoagizwa, alisema kwa kuwa bado siku 14 hazijaisha watasubiri ili kuchukua hatua nyingine.

“Tunashukuru kuwa amekiri kupokea barua yetu, hivyo tunasubiri hadi siku 14 ziishe ndio atajua TFF nini itafanya dhidi yake, tusubiri muda uishe na leo (jana) ikiwa ni siku ya pili, alisema.

Awali TFF ilitoa agizo la kumtataka Rage aitishe Mkutano Mkuu wa Dharura ili kumaliza mgogoro uliopo, kwa kutumia Ibara 1(6) ya Katiba ya Simba inayosema, “Simba Sports Club ni mwanachama wa TFF, itaheshimu Katiba, kanuni, maagizo na uamuzi wa TFF na Fifa na kuhakikisha kuwa zinaheshimiwa na wanachama wake.”

 

Wakati huohuo, Rage katika mkutano huo, alitangaza kumteua, Richard Wambura kuwa mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji wa klabu ya Simba.

Rage akizungumzia suala la kusaini Mkataba na Azam TV alisema suala hilo halihitaji shule kwa kuwa mhusika mkuu ni TFF, hivyo iwe isiwe ni lazima klabu isani na ndio sababu alifanya hivyo miezi minne iliyopita na klabu kupewa mil 100.

Akiweza wazi Rage alishangazwa kusikia Joseph Itang’ale na Evans Aveva kushiriki katika mazungumzo Zook na kubainisha kuwa yuko tayari kujiuzuru ikiwa Zouk watatoa mil 700.

 
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
 

By Otieno Otieno

Harambee Stars will play Tanzania's Taifa Stars next Tuesday in an international build-up match in Dar es Salaam.
Goal can exclusively reveal that Kenya tactician Adel Amrouche has called a full squad for the fixture which falls under the Fifa calender and already a number of foreign based players have arrived in Nairobi ready for the duel.
AC Ajaccio striker and former captain Dennis Oliech arrived on Sunday and he told Goal, he looks forward to the match. “It is great to come back and represent my country and I look forward to this match which we hope can help the team rise in the Fifa rankings,” said Oliech.
Amrouche confirmed he has also recalled Norway-based goalkeeper Arnold Origi, who is expected in the country on Thursday. “Victor Wanyama (Southampton), David ‘Cheche’ Ochieng (Al Tawuon) and Jamal Mohammed (Oman), have all arrived and are ready for the match,” said Amrouche.
Amrouche further said he will use the opportunity to have a meeting with the senior players and plan for the 2015 Africa Cup of Nations qualifiers.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

PAZIA la michuano ya Kombe la Mapinduzi, linafunguliwa leo kwa michezo miwili kwa Simba kuivaa Jamhuri ya Pemba, huku Tusker ya Kenya wakipepetana na Bandari mechi zote zikichezwa kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

MABINGWA wa soka Bara, Simba jana waliogelea kipigo cha mabao 3-0 kutoka Tusker ya Kenya katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa, huku ujio wa kocha wao, Patrick Liewig kutoka Ufaransa ukizidi kutia shaka.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Theo Walcott aliibuka kinara kwa kupachika mabao 3 kati ya 7 ya Arsenal walioifunga NewCastle United uwanja wa Emirates 29-Desemba-2012
Arsenal imeiangushia kipigo kikali New Castle kwa kuicharaza magoli 7-3 katika mchezo wa ligi kuu ya England uliofanyika Jumamosi kwenye uwanja wa Emirates.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Robin Van Persie mfungaji wa bao la pili la Man U dhidi ya West Brom
Manchester United leo imeilaza West Brom magoli 2-0 na kujihakikishia nafasi ya kwanza kwenye msururu wa ligi kuu ya Premier ya England, mwanzo wa mwaka ujao wa 2013.
Gareth McAuley alijifunga mwenye na kuipa Manchester United, bao lao la kwanza kabla ya Robin Van Persie kufunga bao la pili.
no image
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Kocha wa Manchester Sir Alex Ferguson amemshutumu kocha wa Newcastle Allan Pardew na kumtaja kuwa mfarisayo na mnafiki.
Pardew alimshutumu Ferguson kwa utovu wa nidhamu baada ya mechi yao siku ya jumatano.
Pardew amesema shirikisho la mchezo wa soka nchini England, FA lingemuadhibu Ferguson kwa kukabiliana na maafisa waliokuwa wakisimamia mechi hiyo ambayo Manchester United ilishinda kwa magoli 4-3, katika uwanja wa Old Trafford.
'' Allan Pardew ndiye kocha ambaye mara nyingi huwazomema marefa kwa takriban karibu mechi zote'' alisema Ferguson.
Pardew alipigwa marufuku ya kutohudhuria mecho mbili baada ya kupatikana na hatia ya kumsukuma mmoja wa wasimamizi wa mechi yao mwezi Agosti.
Ferguson alimzomea refa wa mechi hiyo Mike Dean, naibu wake Jake Collin na Neil Swarbrick, mwanzo wa kipindi cha pili ya mechi yao ya ligi kuu ya Premier kupinga goli la pili la Newcastle.
Dean aliidhinisha kuwa Papiss Cisse, hakuwa ameotea wakati Jonny Evans alipojifunga kunako dakika 28.
Pardew hakufurahiswa na uamuzi wa FA wa kutomuadhibu kocha huyo wa Manchester United mwenye umri wa miaka sabini.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Kocha wa Manchester Sir Alex Ferguson amemshutumu kocha wa Newcastle Allan Pardew na kumtaja kuwa mfarisayo na mnafiki
 

Pardew alimshutumu Ferguson kwa utovu wa nidhamu baada ya mechi yao siku ya jumatano.
Pardew amesema shirikisho la mchezo wa soka nchini England, FA lingemuadhibu Ferguson kwa kukabiliana na maafisa waliokuwa wakisimamia mechi hiyo ambayo Manchester United ilishinda kwa magoli 4-3, katika uwanja wa Old Trafford.