May 2014
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

BISMARK ROCK MWANZA.
Ndugu Wananchi napenda kuwataarifu kupitia vyombo vya habari juu Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani mwaka 2014 ambayo Mkoa wa Mwanza umechaguliwa kuandaa maadhimisho hayo kitaifa.

 

Ndugu Wananchi, Maadhimisho ya Siku ya mazingira Duniani hufanyika kuanzia tarehe 01 hadi 05 ya mwezi Juni kila Mwaka. Maadhimisho haya huwa na Kauli mbiu iliyoandaliwa mahsusi kwa ajili kuhimizana juu ya umuhimu wa uhifadhi wa Mazingira yetu.

 

Kwa mwaka huu 2014, shirika la Umoja wa mataifa linalo shughulikia mazingira limetangaza Kaulimbiu ya maadhimisho hayo kuwa ni “RAISE YOUR VOICE BUT NOT THE SEA LEVEL” kwa tafsiri ni “CHUKUA HATUA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA  TABIANCHI. Kitaifa, kauli mbiu yetu ni ”TUNZA MAZINGIRA ILI KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIANCHI.

 

Ndugu wananchi

Kama nilivyotanguliwa kusema, Mkoa wa Mwanza umeteuliwa kuwa mwenyeji wa kitaifa, wa maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani mwaka huu. Katika juma hilo shughuli mbalimbali zitafanyika ikiwa ni pamoja na kufanya usafi katika maeneo yote, kuhamasisha wananchi kuhusu utunzaji wa Mazingira  kwa njia ya Makongamano, kupanda miti, kuzoa takataka, maonesho ya utunzaji na mazingira, kuondoa magugu katika Ziwa Victoria na ufugaji wa nyuki pamoja na kufanya ziara kwenye maeneo tofauti yanayo jishughulisha na utunzaji wa mazingira ikiwemo viwanda.

 

Ndugu wananchi,

Ufunguzi wa maadhimisho haya kitaifa utafanyika tarehe 02 Juni, 2014 kuanzia saa 1.00 asubuhi katika Viwanja vya Furahisha, Ufunguzi huo utafanywa na Waziri nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mheshimiwa Dkt, Binilith Mahenge  na siku ya kilele itakuwa tarehe 05 Juni, 2014 ambapo Mgeni rasmi atakuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal.

 

Ndugu wananchi,

Shughuli zitakazo fanyika siku ya tarehe 05 Juni 2014 (Siku ya kilele)  ni pamoja na:- kukabidhi vyeti kwa wadau mbali mbali wa mazingira, zawadi na tuzo ya Rais ya utunzaji na uhifadhi wa mazingira pamoja na zawadi nyinginezo kwa washindi wa kuhifadhi mazingira.

 

Ndugu waandishi wa habari,

 

Natambua kwamba ninyi ni wadau wakubwa sana wa mazingira hasa katika jukumu lenu la kuuelimisha umma, juu ya umuhimu wa kutunza mazingira, kwa nafasi ya pekee niwaombe muweze kuipeleka taarifa hii kwa wananchi wa Mkoa wa Mwanza na maeneo ya jirani ili waweze kujitokeza kwa wingi katika Viwanja vya Furahisha kwa muda wote ambao elimu kuhusu utuzaji wa mazingira itakuwa ikitolewa na wadau mbali mbali.

 

Aidha  Mkoa unategemea kupokea Wageni wa Kitaifa na  Kimataifa, ambao watatembelea  viwanda na kuona utunzaji wa Mazingira na jinsi ya kutenga taka ngumu na zisizo ngumu.

 

Nichukue fursa hii kutoa rai kwa wananchi wa Mwanza kujitokeza kwa wingi na kushirikiana na wageni wetu kama ilivyo ada ya Wana Mwanza. Nawaomba wananchi mjitokeze kwa wingi na kuwalaki wageni wote watakao tufikia katika juma zima kuanzia tarehe 01 hadi 05 Juni 2014. Kama ilivyo desturi yetu wana Mwanza tuonyeshe ukarimu wetu kwa wageni wetu na pindi watakapo ondoka waikumbuke Mwanza.

 

Nimalizie kwa kusema nawashukuru sana kwa kuitika wito wangu.

 

“TUNZA MAZINGIRA, KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIANCHI”

 

MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI TANZANIA

 

ASANTENI KWA KUNISIKILIZA.

 

IMETOLEWA NA MKUU WA MKOA WA MWANZA.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Waziri Sitta akiwasilisha Bajeti ya Wizara yake katika Bunge la Bajeti jana linaloendelea Jijini Dodoma.


Waziri Sitta pamoja na Naibu wake Mhe. Abdulla Juma Abdulla wakifuatilia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Ushirikiano jana Bungeni Dodoma.


Baadhi ya Wabunge wa EALA wakifuatilia mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Ushirikiano jana Bungeni Dodoma


Naibu Waziri Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Abdulla Juma Abdulla akijibu hoja za wabunge kuhusu Wizara yake wakati wa uwasilishaji bajeti jana Bungeni Dodoma


Uongozi wa Wizara ya Ushirikiano katika picha ya pamoja mara baaada ya kupitishwa kwa Bajeti yao.
(Picha zote na Maelezo na: Ofisa habari wa Wizara hiyo Antony Ishengoma)

Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Uga wa Mkufunzi:Somo: Uongozi kutoka kwenye Mambo ya Kipuuzi; sehemu ya pili

Uadilifu/Unyoofu ama kwa lugha ya Kiingereza intergrity ni sifa ya ndani ya msingi ya kiongozi. Intergrity ni neno lenye asili ya Kilatini na hutokana na neno “interger” ambalo humaanisha “One=Moja” au “Wholeness=Ukamilifu” (Kwa tafsiri isiyo rasmi)… 

Mwandishi James Kalekwa

Kwahiyo basi twaweza kugundua kwamba uadilifu ni ile tabia ya kuwa thabiti na msimamo mmoja juu ya jambo fulani. Ni tabia ambayo imejijenga juu ya maneno haya “Ndiyo yenu na iwe ndiyo…”.

Kutobadilika badilika ama kwa maneno mepesi ni kutokuwa na kigeugeu!

Mtu asemaye ndiyo kwa maneno na hapana kwa matendo yake juu ya jambo hilohilo huyo si kiongozi! Lakini pia kuna watu husema ndiyo kwa maneno na matendo katika nyakati fulani au wakiwa na watu fulani na kisha husema hapana kwa maneno na matendo juu ya jambo hilihilo katika nyakati na wakiwa na watu tofauti na wale awali. 
Hawa nao so viongozi! Kwa kifupi uadilifu ni kukiishi kwa maneno na matendo kwa kutokubadilika kile unachokiamini. Hilo ni jambo la kwanza!

Nakumbuka Mfalme Suleimani mwenye hekima husema “Aendaye kwa unyofu (uadilifu) huenda salama….”.

Walimwengu mlioko Tanzania mtakuwa mnakumbuka vyema juu ya Azimio la Arusha la 1967 ambalo lilihimiza na kusimamia uadilifu kwa viongozi wa chama na serikali na nyote ni mashahidi kwamba wasiokuwa na moyo wa uongozi walijikuta nje ya mstari. Kisha likafuatia Azimio la Zanzibar ambalo lilikuwa ni kaburi la Azimio lililotangulia!

Ni mara ngapi umeshuhudia “viongozi” wakivunja miiko na maadili ya uongozi kwa kusema uongo hadharani bila woga wala aibu- tena uongo unaosindikizwa na tafiti na taarifa za kitakwimu ili kujipatia faida fulani?

Walimwengu, mnakumbuka hadithi ya Samsoni na Delilah? Samsoni alichimba kaburi ambalo lingemzika yeye mwenyewe baada ya kuanza “kuona asiyopaswa kuyaona, kwenda ambako hakupaswa kwenda na kutenda ambavyo hakupaswa kutenda” – yaani alivunja miiko mahsusi kwaajili yake na aina ya ungozi wake…
 Alianza taratibu kuingia katika mahusiano ya kimapenzi (ufuska) na hatimaye alijikuta mikononi mwa Delilah na ndipo ndoto zake zikazima (Alitobolewa macho kama ishara ya kifo cha maono/malengo/ndoto yake) na hadithi ikaishia hapo! “Viongozi” wengi hujikuta wameanza kuasi maadili na miiko taratibu (huanza kwa kula rushwa kidogo, kusaliti kidogo, kudanganya kidogo) na hatimaye hukubuhu!

Pili, uadilifu ni kujisikia deni ama kuwiwa kuwajibika au kuwa mkweli juu ya maneno yako. Kuna usemi usemao “Ahadi ni deni” …

 Je, ni mara ngapi umeshuhudia “viongozi” wakitoa ahadi lukuki ambazo hawazitimizi? Ama huja na kukurubuni ukubaliane nao kwamba wamezitimiza (kwa namna waonavyo wao)?-
 Kumbe ki uhalisia hawajatimiza! Walimwengu, Je, mtu anayeahidi kutenda jambo fulani na asitende au kuyakana maneno aliyoyasema awali akiwa mahali fulani mwaweza kumtegemea na/au kuyaamini ayasemayo? La hasha!

Kuna mamia kwa maelfu ya viongozi waliokufa na kwenda kaburini na madeni (ahadi ambazo hawakuzitimiza) kibao! Wapi na ni lini wataenda kulipa baada ya kifo?

Jambo la tatu na la msingi juu ya uadilifu ni ukweli/uaminifu. Wengi huutazama ukweli/uaminifu kama “hali ya kutoshiriki kusema uongo au udanganyifu”.

Lakini ningependa kwenda hatua kubwa zaidi ya hapo kwasababu katika jamii yetu kwa sasa “viongozi” huelezea mambo na kuyatia chumvi katika kuelezea uzuri au ubaya wa jambo husika. Ukweli/Uaminifu ni ni hali ya kuuwasilisha uhalisia kwa kadri inavyowezekana kwa dhamiri safi na kuepuka uwasilishaji ambao hitimisho lake ni udanganyifu. The Joseph Institute of Ethics inaueleza ukweli/uaminifu

“Ni kuepuka uwasilishaji usio sahihi wa uhalisia. Inawezekana kabisa kuwasilisha mambo mengi ya ukweli ambayo humshawishi msikilizaji kuamini vitu visivyo sahihi. 
Hivyo mtu anaweza kuzungumza ukweli pasipo yeye kuwa mkweli. Kwasababu amekuwa na dhamira ya kumfanya mtu afikie hitimisho ambalo si la kweli…. Ni dhamira, nia ama kusudi la mtu…”

Walimwengu wenzangu, mimi nimeshuhudia watu wakisema umri tofauti na umri wao halisi hasa katika michezo na mahusiano kwa nia ya kupata wanayoyahitaji. 
Nimeshuhudia wasomi na wataalamu wakiunda “cook” tafiti, miradi na taarifa mbalimbali vyumbani mwao ili wapate hitaji lao. Nimeona wengi wakigushi risiti na karatasi za kufanyia malipo ili mkono uende kinywani.

Wapendwa walimwengu, hasa mlioko Tanzania, mmewahi kusikia juu ya TAKRIMA? bila shaka mmejionea na/au kusikia wengi wakipewa bahasha za kaki, wengine wakitoa vitu kama mavazi (t-shirt, khanga, kofia, vitambaa n.k) na chakula si kwa upendo bali kwa nia ya kulaghai. 
Mmeshuhudia watu wakizunguka huku na kule wakitoa/wakigawa fedha kwa nia ya kushawishi? Hoja ninayojenga hapa ni kwamba mtu anaweza kutenda mambo yanayoonekana ni mema kwa nia mbaya! Hawa si viongozi hata chembe! Kila asomaye na afahamu.

Nikiwa katika mwaka wangu wa mwisho katika elimu yangu ya sekondari nilikutana na msemo usemao “Asiyejua aendako, ataenda kokote.”…

Miaka kadhaa baada ya kuutafakari niliutengenezea swali ambalo huwa napenda kuwauliza vijana, vikundi na jumuiya, watu walio katika mahusiano n.k. Hebu jaribu kufikiri umemsindikiza ndugu yako kituo kikuu cha mabasi (stendi) na baada ya kuagana naye anatokea mtu mmoja akiwa na mizigo na kwa kumtazama unagundua kuwa ni msafiri na anahitaji masaada.

Huyu msafiri anakufuata na kukuomba umuonyeshe basi (gari la abiria) ili aweze kusafiri. Kwa akili za kawaida, kabla ya kumuonyesha basi ungependa kujua anaelekea wapi (mwisho wa safari yake) ili ujue basi la kumwelekeza. Lakini cha ajabu msafiri huyo anakujibu ya kuwa “Sijui ninataka kwenda wapi…”; 
Je, utamwonyesha basi gani/la kwenda wapi?.... Asiyejua aendako ataenda kokote! Huwezi na ni uendawazimu kuanza safari wakati hujui unaenda wapi. Lazima uujue mwisho wa safari ndipo uianze safari.

Walimwengu wenzangu, jamii yoyote inahitaji kujua inakwenda wapi. Ni jukumu la lazima la kiongozi kujua, kuona na kuielekeza jamii yake kwenda mahali inapopaswa kwenda- HATMA! Je, twaukumbuka mfano ule wa kipofu kumwongoza kipofu mwenzake? Wote huishia shimoni. 
Hivyo ni jukumu la mwongozaji kuwa ni mtu anayeona kule jamii inapaswa kwenda. Uwezo wa kuwa na Maono (Vision), Malengo (Goals) ama Hatma (Destiny) ni lazima kwa kiongozi.

Nikirejea hekima za Mfalme Suleimani asemapo “Pasipo maono/malengo watu huangamia/ hukosa kuwa na adabu…”

(Mkolezo unaonyesha tafsiri zingine) nawiwa kusema kwamba kiongozi ni mtu mwenye uwezo wa kuona mwisho kabla ya mwanzo, kuwaeleza wanajamii juu ya mwisho huo na kuwashawishi kwenda pamoja naye katika mwisho huo huku akiongoza njia! Wapendwa wangu walimwengu,

Je, mkitazama katika jamii zenu mnaona watu wenye uwezo huo? Nazungumza katika Nyanja zote. Niwakumbushe tu kwamba ni muhimu tukitambua kwamba malengo/hatma/maono hayaigwi wala kunakiliwa kwani kuna maono mahsusi kwa kila jamii husika.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
MWANDISHI NGULI NA MWENYE KUFANYA VIPINDI VYA UCHUNGUZI NA  KISIASA NCHINI TANZANIA , KATIKA UKURASA WAKE WA FACE BOOK LEO, NIMEKUTANA NA HABARI HII,  SWALI AMBALO HATA MIMI MWENYEWE NIMEKUWA NAJIULIZA SIKU ZOTE SIPATI JIBU HEBU TUSAIDIANE MAJIBU WAUNGWANA MTAKAOPATA FURSA YAKUISOMA STORI HII KATIKA   www.kuninews.blogspot.com




HAWA NDIO BOKO HARAM WANAODAIWA KUWA NA VIFAA VYA KISASA VYA KIVITA.
 
 
HUYU NI RAIS BARAK OBAMA, RAIS WA NCHI KUBWA KIUCHUMI DUNIANI:  AMERIKA.

 
Na Dotto Bulendu.
 
Binafsi napata utata sana na haya makundi yanayotekeleza mauaji katika nchi mbalimbali hususani barani Afrika,kumekuwa na makundi ya waasi na haya tumepata kuyashuhudia katika nchi za Uganda, DRC Congo, Afrika ya kati, Mali, Misri, Kenya pia makundi yanayotajwa kuwa ni ya kigaidi kama AlQaeda,AlShabaab na Boko Haram Ntarahamwe nk.!..Makundi haya yamekuwa yanafanya mashambulizi ya kushtukiza na kusababisha mauaji ya watu wasio na hatia Duniani ,na hata dunia sasa inahangaika na kundi la Boko Haram,ambalo wakati dunia ikih...angaika kuwanasua mabinti waliotekwa, jana kundi hili limetajwa kutekeleza mauaji kwa kulipua bomu tena huko kaskazini mwa Nigeria na kusababisha vifo vya watu takribani zaidi ya 120, vikundi vya waasi na kigaidi barani Afrika vimekuwa vinatumia silaha za kisasa kupambana na majeshi ya serikali barani Afrika pamoja na kufanya mashambulizi....utata wangu upo katika maeneo haya.
1.Makundi haya ya silaha nzito,nani anawauzia?silaha hizo zinawafikiaje? tunajua silaha zote nzito zinatengenezwa na nchi zilizoendelea na siyo barani Afrika, je makundi haya yanazinunuaje hizi silaha? tunajua biashara za silaha ni biashara yenye faida sana, nahisi nchi za ulaya,marekani na asia zinazotegeneza silaha zinajua fika undani wa makundi haya.
2.Makundi haya yanaajiri vijana wengi, yanakaa mafichoni, yanapata wapi pesa za kununua silaha na malipo pamoja na posho kwa wapiganaji wake? yamehifadhi wapi fedha zao? nani anakwenda benki kuweka na kutoa pesa za makundi haya? naamini zipo taasisi za fedha ambazo zinaujua kwa undani uasili wa makundi haya!!tunajua pesa chafu zinaendesha baadhi ya mataifa.
3.Nani anafadhiri makundi haya? kwa nini makundi haya yanachomoza kwenye nchi zenye utajiri wa mafuta? na wakati makundi haya yakiendelea na uharibifu huu utajiri uliopo katika nchi hizo unaendea kuporwa na wanaopora hawaguswi wala kushambuliwa na makundi haya!
Nani yupo nyuma ya makundi haya? natafakari na karibuni wanajamvi tufanye tafakuri tunduizi(critical thinking),juu ya makundi ya uasi na ugaidi barani Afrika,nani anayafadhiri?ufadhiri wao unapitia wapi? wanatuza wapi fedha zao? wanapitishia wapi silaha zao?..natafakari sana!.
 
Toa maoni yako hata bila kutaja jina nasi tutayachapisha
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
HAPA TIMU ZIKIKAGULIWA NA MGENI RASMI, TIMU HIZO ZILITOKA SARE YA GOLI 1-1












Mashindano ya UMISETA, kwa Mkoa wa Mwanza yamefunguliwa rasmi hapo jana na Kaimu katibu Tawala mkoa wa Mwanza Ndaro Kulwijira huku akiwaasa vijana hao wa Sekondari kucheza kwa kuzingatia nidahamu ya hali ya juu.

Zaidi soma katika Hotuba yake aliyoitoa wakati wa Ufunguzi wa michezo hiyo.
 

HOTUBA YA KAIMU KATIBU TAWALA WA MKOA WA MWAZA     WAKATI WA KUFUNGUA MASHINDANO YA NGAZI YA MKOA YA MICHEZO YA SHULE ZA SEKONDARI TANZANIA (UMISSETA) NSUMBA SEKONDARI TAREHE 22 MEI, 2014

Katibu Tawala Msaidizi  wa Mkoa Elimu  - Mwalimu Hamis Maulid

MaafisaElimu wa Halmashauri

Mameneja

Viongozi wa Vyama vya Michezo Mkoa

Wanamichezo

Ndugu Wananchi; na

Wapenda Michezo Wote.

 

Napenda kuchukua fursa hii kukushukuru Katibu Tawala Msaidizi ambaye ni AfisaElimu wa Mkoa, na Viongozi wenzako katika Seksheni ya Elimu kwa kunialika kufungua Mashindano haya ya Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA).

 

Nimeupokea mwaliko huu kwa furaha kwa vile umenipa fursa ya pekee kuwaona na kuzungumza na hadhara hii ya Wanafunzi Wanamichezo na Walimu wao. Aidha, nitumie fursa hii kuupongeza Uongozi wa Nsumba na jumuia yote kwa maandalizi mazuri ya mazingira kwa ajili ya mashindano haya. Ahsanteni sana!

 

Ndugu Viongozi na Vijana Wanamichezo,

Leo tumebahatika kujumuika hapa kupitia Utamaduni wa Michezo. Kwa utaratibu huu, ni dhahiri kwamba tunapata nafasi ya kujenga Umoja wa Kitaifa wa Wanamichezo kupitia Michezo hii ya UMISSETA kuanzia ngazi ya Vijana wetu wa Shule za Sekondari. Ni kweli kwamba Michezo ni Burudani, lakini kwa sasa kutokana na mabadiliko ya Mazingira ya Kisiasa, Kiuchumi na Kijamii, Michezo ni Kipaumbele katika kutoa pia Ajira kwa Vijana wetu, kukuza Biashara na kujenga jamii bora yenye maelewano. Kwa mfano, Nchi za wenzetu za Ulaya na Marekani, Nigeria, Togo, Ivory Coast, Cameroon zinatumia kikamilifu nafasi hii ya Michezo kujitangaza Kisiasa na Kiuchumi.

 

 

Ndugu Wanamichezo,

Natambua kwamba ninyi ni Wanafunzi ambao mnahitaji kukuza Taaluma na Vipaji vyenu. Moja ya nafasi hizo ni Michezo. Ili Michezo iendelee kukua Nchini, ni lazima Ukuzaji wa Vipaji vya Michezo uanzie Mashuleni. Ndiyo maana Michezo ni sehemu ya Mtaala wa Masomo yenu. Kama ambavyo tunawataka mfanye bidii sana katika masomo yenu, fanyeni bidii pia na kukuza Vipaji vyenu katika Michezo mbalimbali.

Ndugu Wanamichezo,

Michezo inatufundisha Ushindani wa Kistaarabu, Ushindani unaozingatia Sheria na Kanuni, Ushindani unaojenga urafiki badala ya uhasama; Ushindani unaoleta Upendo badala ya Chuki na Ushindani unaoleta Amani badala ya Shari. Kwa sababu hiyo Mwanamichezo wa leo anayo nafasi ya kupata mafundisho muafaka na hazina ya uzoefu mkubwa wa Ushindani wa Kistaarabu kutoka kwenye Michezo, vitu ambavyo vinaweza kumfanya kuwa Mtanzania bora wa kesho. Mwanamichezo anakubali ama Kushindwa au Kushinda. Waswahili husema“Asiyekubali Kushindwa Si Mshindani”.

Wanamichezo bora ni Watu Wasikivu, wenye nidhamu na Watiifu. Ninyi Vijana ambao ndio Viongozi wa kesho wa Taifa letu mnahitaji sana kujijengea nidhamu na maadili ya hali ya juu ili muweze kuendana na hali ya maisha ya ushindani yatakayokuwa yanawakabili. Nidhamu, inamuwezesha Mtu kufanya kazi zake kwa mpangilio mzuri unaofuata Taratibu zote za kazi kwa wakati. Hii ndiyo njia ya uhakika ya kufikia malengo yoyote yale na kupata mafanikio.

Aidha, kwa njia ya Michezo, nidhamu Shuleni itaongezeka na matarajio yetu ni kuwa nidhamu hiyo itajitafsiri pia katika matokeo mazuri kwenye Taaluma. Matarajio ni kuwa, Wanafunzi watakuwa na mahusiano mazuri zaidi kati yao na Walimu wao na wale wote wanaopata Burudani ya Michezo. Ama tunatarajia kuwa wataendelea kuwa Watu wenye Nidhamu katika Utu Uzima wao, ili hatimaye tuwe na Taifa la Watu wenye nidhamu ya kutolewa mfano.

Ndugu Wanamichezo,

Tangu zama za kale Michezo ilikuwa ni sehemu ya Maisha ya Jamii. Jamii moja ilijipambanua na Jamii nyingine kutokana na ushupavu na ushujaa wake katika Michezo. Dhana hiyo ya kale bado inaendelezwa kupitia Sera ya Michezo kwa njia ya kisasa zaidi. Sera ya Maendeleo ya Michezo inayaainisha madhumuni ya Michezo wakati huu kuwa ni:  Kujenga na kuimarisha Afya Bora kwa wote;  Kujenga Tabia ya Ushirikiano, Upendo, Undugu na Uzalendo;  Kujenga Uhusiano, Uelewano na Mshikamano Kitaifa; Kujenga Moyo wa Kishujaa na Kujihami na Kukuza Ukakamavu, Ujasiri na Kujiamini; Kuburudisha;  Kulitambulisha na kulitangaza Taifa letu nje ya Mipaka yake; na

 Kumjenga Mwanamichezo kuwa mtu imara Kiakili na Kiroho (kuanzia Utotoni hadi Utu Uzima). Kwa mtiririko huu, napenda kusisitiza kuwa Shule zote, kuanzia za Awali, Msingi, na Sekondari, viwe na Viwanja vya Michezo mbalimbali. Hii ni njia ya kuwatambua na kuwaendeleza Vijana wenye Vipaji Maalum ili hatimaye Washiriki kwenye Mashindano ya Kitaifa na Kimataifa. Aidha, Halmashauri zetu za Miji, Manispaa, Vijiji zihakikishe kuwa maeneo yaliyotengwa kwa Shughuli za Michezo yanatumika kwa shughuli hiyo. Aidha, Viwanja vilivyopo viimarishwe na vitunzwe ipasavyo.  Ndugu Wanamichezo,

Nitumie fursa hii pia kuwakumbusha kwamba mnapofurahia kushiriki katika Michezo hii, ni lazima mkumbuke pia kuwa furaha yenu itaweza kudumu kama mtatambua kuwa kuna mpinzani mkubwa kati yenu aitwaye Virusi vya UKIMWI na UKIMWI. Kila mmoja wenu anaelewa vya kutosha juu ya Adui huyu. Ni wajibu wangu kama Kiongozi na Mlezi wenu kuwakumbusha juu ya hatari inayowakabili msipochukua tahadhari ya kutosha. Kumbukeni UKIMWI bado unaenea kwa kasi kubwa sana hasa miongoni mwa Vijana wa Rika lenu kuliko Rika lolote jingine. Niwakumbushe kwamba kataeni kumalizwa na Ugonjwa huu. Msikubali kukatishwa masomo na msikubali kutenganishwa mapema na Familia zenu. Kwenu ninyi, njia bora pekee ni kusubiri hadi wakati muafaka wa kuwa na ndoa zenu. Wekeni bidii katika masomo, kwani muda ukifika yote yatajipanga vizuri.

 

Nitumie fursa hii kuwakumbusha kuepukana na matumizi ya dawa za kulevya  kama vile bangi, mirungi na cocaine kwa imani ya kuwa dawa za kulevya huwapatia nguvu  na mzuka wa kushindana, huko ni kujidanganya.  Vijana wengi hasa wanamichezo waliojaribu kutumia dawa za kulevya michezoni wameathirika na wamekuwa mataahira. Shirikisho la vyama vya michezo duniani limekataza kabisa matumizi ya dawa hizo na ukigundulika ni kufungiwa maisha na ushindi kunyanganywa. Nawaomba walimu na wanafunzi kuwabaini wale wote watakaojihusisha na utumiaji wa dawa za kulevya na kuwachukulia hatua kali za kiidhamu na kisheria

 

Ndugu Wanamichezo,

Nimeelezwa kuwa baada ya Michezo hii yapo Mashindano ya Kanda ya Ziwa ambapo Mikoa ya Mwanza, Mara na Simiyu hukutana ili kuimarisha mahusiano ya Vijana wa Shule za Sekondari na kuunda timu moja ya Kanda. Ni muhimu Timu zetu zijipange kushiriki vizuri na kutuletea undindi a kishindo. Ni Vizuri sasa Timu hizo ziandaliwe vizuri ili zikashiriki kama Washindani na si Wasindikizaji.Kushiriki kwetu kunatujengea umahiri katika kujenga upeo wa akili za Vijana wetu na kujenga mahusiano mazuri ya kikanda .Natoa rai kwa Mashirika, Vyama vya Michezo na watu wengine  kushiriki kwa  kuchangia kufanikisha ushindi wa timu zetu za Mkoa.

 

Ndugu Wanamichezo,

Mwisho napenda kukumbusha kuwa umahiri katika jambo lolote lile hufikiwa kwa kujifunza na kufanya mazoezi mengi, kwa bidii. Napenda kuwapongeza Walimu na Waamuzi na wote walioziandaa Timu hizi ambazo leo zinashindana hapa. Nawapongeza sana Wanamichezo wa Timu zilizoteuliwa kushindana hapa. Natumaini mliteuliwa kwa kustahili na katika Michezo hii mtapata nafasi ya kuonyesha kuwa kuteuliwa kwenu hakukuwa kwa Bahati. Onyesheni Umoja, Onyesheni Upendo, na Onyesheni“Fair Play” katika mashindano haya. Kumbukeni kwamba Michezo ni Afya, Michezo ni Furaha na Michezo ni Ajira.

 

Ndugu Wanamichezo, Wageni Waalikwa,

Baada ya kusema hayo, napenda sasa nitamke kuwa,Mashindano ya Umoja wa  Michezo Shule za Sekondari UMISSETA  kwa mwaka 2014 yamefunguliwa rasmi.

Ahsanteni kwa Kunisikiliza

 

 

 

 
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
.Mgonjwa mmoja agundulika
.Serikali ya Mkoa, yatoa tahadhari kwa wananchi.


DALILI ZA DENGUE ZINAVYO JITOKEZA.


 
Mtu mmoja Mkaazi wa Jijini Mwanza katika maeneo ya  kilimahewa mwenye umri wa miaka (62), amelazwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa Sekouture akisumbuliwa na ugonjwa wa Dengue mara baada ya Vipimo kuonesha.
 
Kwa miujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Baraka Konisaga katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, mgonjwa huyo alifikishwa hospitalini hapo siku moja tatu zilizopita kwa ajili ya kuchunguza afya yake, lakini mara baada ya vipimo vya kawaida hakugundulika kuwa na ugonjwa wowote ndipo ilipo mlazimu mtaalam wa maabara kumshauri mgonjwa huyo kupima vipimo vya ugonjwa wa dengue na kupatikana akiwa ameambukizwa  virusi hivyo vinavyo ambukiza ugojwa wa dengue.
 
SOMA TAARIFA NZIMA HAPA CHINI.
 
 
 
 KUWEPO KWA UGONJWA WA DENGUE   KATIKA MKOA WA MWANZA
 
TAARIFA  KWA  UMMA
 
Ndugu, Waandishi wa habari, wawakilishi wa vyombo vya habari na wananchi wote. Napenda kutoa taarifa ya kuwepo kwa ugonjwa wa Dengue katika Mkoa wa Mwanza. Hadi sasa kuna mgonjwa mmoja katika Hospittali ya Rufaa ya Sekou-toure ambaye amethibitika kuwa na ugonjwa huo.  Kufuatia taarifa hii  napenda wananchi wafahamu machache kuhusu ugonjwa wa Dengue. Ugonjwa wa Dengue husababishwa na VIRUS vinavyoitwa “Dengue Virus”  na vinaenezwa na mbu aina ya Aedes.
 
Mbu hawa hupendelea kuzaliana kwenye maji yaliyotuama karibu na makazi ya watu au kwenye vyombo vya kuhitadhia maji majumbani.
 
JINSI UGONJWA WA HOMA YA DENGUE UNAVYOENEZWA
 
Binadamu hupata ugonjwa huu baada ya kuumwa na mbu wa aina ya Aedes aliye na Virusi vya ugonjwa huu.  Mbu  hawa hupendelea kuuma wakati wa mchana.
 
Ugonjwa huu huwapata wetu wa rika zote aidha watoto wenye umri chini ya miaka mitano na mama wajawazito huathirika zaidi.
 
Ndugu wananchi
 
Dalili za Ugonjwa wa Homa ya Dengue
 
Asilimia 90 ya wagonjwa walioambukizwa ugonjwa huu uonyesha dalili awali kuanzia siku ya 3 hadi 14 baada ya kuumwa na mbu mwenye virusi vya ugonjwa huu dalili hizi ni kama zifuatazo:
·         Homa kali ya ghafla
·         Kuumwa kichwa hususani sehemu za machoni
·         Maumivu makali ya misuli pamoja na viungo vya mwili
·         Kichefuchefu au kutapika
·         Kuvimba tezi
·         Kupatwa na harara
Asilimia 10 ya wagonjwa hupatwa na dalili kali kama kutokwa na damu kwenye sehemu za uwazi za mwili mfano mdomoni, masikioni pamoja na sehemu za kutolea haja ndogo na kubwa.
 
Ndugu wananchi,
Njia za kujikinga na Homa ya Dengue
Ugonjwa wa dengue unazuiliwa kwa njia zifuatazo:-
·         Kuangamiza mazalio ya mbu
·         Kufukia madimbwi ya maji au nyunyizia dawa ya kuua viluwiluwi vya mbu kwenye madimbwi hayo
·         Kuondoa  vitu vyote vinavyoweza kuwa mazalia ya mbu kama vile vifuu vya nazi, makopo, chupa na magurudumu ya gari ambavyo vinaweza kufanya maji kutuama karibu na makazi.
·         Kufyeka nyasi na vichaka vilivyo karibu na makazi.
·         Kuhakikisha maua yanayopandwa kwenye makopo au ndoo hayaruhusu maji kutuama
·         Kufunika mashimo ya maji taka kwa mfuniko
·         Kusafisha mitaro na  gata za paa la nyumba ili kutoruhusu maji kutuama.
 
Kuzuia kuumwa na mbu kwa:-
·         Kutumia dawa za kufukuza mbu  (Repellents)
·         Kuvaa nguo ndefu
·         Kuweka wavu wa kuzuia mbu kwenye madirisha na milango
Kwa kufanya hayo, tunaamini tunaweza kuzuia maambukizi ya ugonjwa huu yasiendelee kutokea.  Naomba kila mmoja atimize wajibu wake.
 
Asanteni kwa kunisikiliza,
 
 
 
Baraka M. Konisaga
KAIMU MKUU WA MKOA
MWANZA
 

Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.


 
MKURUGENZI MTENDAJI WA UMATI , LULU NG'WANAKILALA PICHANI AKIFAFANUA JAMBO
KWA WAANDISHI WA HABARI JIJINI MWANZA.
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Chama cha uzazi na malezi bora nchini UMATI, Tanzania kimeazimia kwenda Bungeni Mjini Dodoma kwa ajili yakuwakilisha mambo mbali mbali yanayo kikabili chama hicho, ikiwapo kuongea na mlezi wao ambaye ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akiongea na vyombo vya habari Jijini Mwanza mkurugenzi mtendaji wa UMATI Tanzania, Lulu Ng’wanakilala, alisema kama UMATI wanadhamiria kwenda Bungeni wakati Wizara zinazohusika na masuala ya uzazi na Malezi zitakapokuwa zikiwasilisha bajeti zao za mwaka 2014/2015 ili kuweza kuwashawishi wabunge waweze kuziongezea Wizara hizo bajeti yakutosha kwa ajili yakufikia malengo ya Milenia katika masuala ya uzazi wa mpango, ambapo lengo ni kufikia asilimia 60% ifikapo 2015. “Tunadhamiria kwenda Bungeni na kuonana na wawakilishi wa wananchi, tukiwa na lengo la kuimba Serikali kuziwezesha Wizara ambazo zinahusika na masuala ya Uzazi kwa ujumla ili ziweze kutengewa fedha za kutosha katika bajeti ijayo ili tuweze kufikia malengo ya Milenia” alisema na kuongeza “ kwa hivi sasa kiwango cha matumizi ya uzazi wa mpango ni asilimia 27% na lengo letu nikufikia aslimia 60% jambo ambalo unaona tunakazi ya ziada sana kufikia hatua hiyo” aliwaambia waandishi wa habari waliokuwa wanazungumza nao katika Hoteli ya Ryan's  Bay ya Jijini Mwanza.

Katika hatua nyingine, Ng’wanakilala, alisema katika mataifa Mengine suala la uzazi wa mpango limekuwa linauwakilishi rasmi jambo ambalo linasaidia kurahisisha shughuli hizo kwenda vizuri na sekta husika kutengewa mafungu yakutosha.

UMATI ambayo imekuwa ikijishughulisha na masuala ya uzazi wa mpango, inakabiliwa na changamoto nyingi katika vita hivyo, ikiwamo mila potofu zilizopo kwenye jamii kama vile mwanamke kufanywa chombo cha uzazi hivyo muda mwingi kubakia katika suala la kuzaa na kulea na hivyo kukwamisha hata shughuli za uzalishaji mali.

Katika hatua nyingine UMATI, imesema Mikoa ya kanda ya ziwa inayounganisha mikoa ya Mwanza, Mara, Kagera, Geita, Simiyu na Shinyanga ndio yenye Changamoto kubwa zaidi kwani hadi hivi sasa ni asilimia 13% ya jamii ndiyo inayo zingatia masuala ya uzazi wa mpango ikilinganishwa na wastani wa kitaifa wa asilimia 27% huku lengo la kitaifa likiwa ni asilimia 60% ifikapo 2015, hivyo kuifanya UMATI kuelekeza nguvu kubwa katika kanda hiyo kwa kuanzishwa kwa Mradi mpya wa Water LLo foundation, ambao umekusudia kufanya kazi katika Mkoa wa Mara.

UMATI ambayo ilianzishwa mwaka 1959, imekuwa ikijihusisha na masuala ya uzazi wa mpango kwa Jamii ya watanzania ambao kabla ya Uhuru walikuwa Milioni 9, huku idadi ya sasa ikifikia milioni 45 na zaidi na kukifanya chama hicho kuongeza juhudi katika kuhakikisha Tanzania inakuwa na uzazi salama ili kuweza kumfanya mama naye aweze kuingia katika shughuli za uzalishaji mali.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

THIS  TOWER IS BUILDED IN SENGEREMA MWANZA TO DISAGREE KILLING OF ALBINISM.
Tanzanian police have arrested two alleged witch doctors after an albino woman was hacked to death for body parts, AFP reported Wednesday (May 14th).

Munghu Lugata, 40, was killed after attackers cut off her left leg above the knee and three of her fingers on Monday, said Under the Same Sun, an advocacy group that campaigns for the rights of people with albinism.

"Her grossly mutilated body was discovered outside of her home by her own niece," the group said, adding that more than 70 albinos have been killed since 2000, with a similar number suffering violent attacks.

Charles Mkumbo, police chief of the Simiyu region in north-western Tanzania, said that a man and a woman, Gudawa Yalema and Shiwa Masalu, had been arrested.

In Tanzania, albinos are killed and  dismember  due to a widespread belief that charms made from their body parts bring good fortune and prosperity.

"Witch doctors tell their clients that the skin, hair, blood and organs of persons with albinism when combined with their secret magic potions guarantee success, wealth and election victory," the group said in a statement.

Albinism is a genetic condition characterised by a deficiency of melanin pigmentation in the skin, hair and eyes.

With local polls scheduled for October, people with albinism "fear for their lives", the group said, adding that "the black market demand for the body parts of people with albinism escalates during these times".

 
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

UMATI WA WATU KATIKA BARA BARA YA KENYATTA HAPA WAKISHUHUDIA FOLENI YA MAGARI
NI BAADA YA KARANDINGA KUSABABISHA AJALI.
Fatilia kwa karibu picha hizo ambazo tumezipata kwa hisani ya Blogu ya G. Sengo.

Jana jioni wakazi wa jiji la Mwanza wamepata usumbufu mkubwa mara baada ya barabara muhimu ya Kenyata kufungwa kwa muda katika muda mbaya wa kurejea kutoka makazini mara baada ya karandinga la jeshi la polisi lenye namba za usajili STG 9263 lililokuwa likitokea mahakamani kuelekea gereza la Butimba, likiwa na mahabusu kusababisha ajali mara baada ya kupoteza uelekeo .

Chanzo cha ajali hiyo kinatajwa kuwa  karandinga hilo lilipoteza uelekeo mara baada ya kukata dif ile hali likiwa katika mwendo kasi hivyo likaibamiza kwa nyuma gari lililokuwa mbele yake aina ya Toyota Dutsun yenye namba za usajili T387 AAH, gari ambalo lilipoteza uelekeo na kuvagaa moja kati ya maduka kwenye barabara hiyo linalotazamana na kituo cha mafuta. 

Ajali hiyo imesababisha moja kati mahabusu waliokuwa kwenye karandinga hilo aliyekuwa na majeraha ya kuvunjika kwenye moja ya matukio ya kesi inayomkabili kuteguka zaidi huku wengine wakisalimika kwa muweza kujimudu kukamata sehemu za vishikio vya karandinga hilo wakati ajali ikitokea.

Uhaba wa kutokuwa na gari la ziada kubebea mahabusu limeligharimu jeshi la polisi mkoa wa Mwanza leo kwa jeshi hilo kutumia magari yake ya doria ya kawaida (Defender) kufaulisha wafungwa kwa makundi hali ambayo ilibidi zoezi hilo kutumia muda  mrefu kukamilika.

Pic up aina ya Toyota Dutsun  T387 AAH ikiwa imenasa kwenye moja ya maduka mara baada ya kugongwa na karandinga hilo la mahabusu.

Utaratibu wa kufaulisha mahabusu ukiendelea kufanywa na kikosi cha kuzuia vurugu FFU jeshi la polisi Mwanza.


Usalama ulizingatiwa na wananchi walikatazwa kulifikia eneo la tukio umbali wa mita 100.

Kasheshe ya msongamano barabara ya Kenyata jijini Mwanza.

Fundi akijaribu kuweka japo sawa kwa muda ili karandinga hilo lipate kuondoshwa eneo hilo kuondoa usumbufu wa kuziba njia ya barabara hiyo muhimu....

Si suala la kubeza twahitaji kuboresha vitendea kazi jeshi la polisi nchini kwani ipo siku yatazuka makubwa kuliko hili lililotokea hapo jana.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
WAFANYAKAZI WA CHUO CHA USIMAMIZI WA FEDHA PICHANI,  WAKATI WA SHEREHE ZA MEI MOSI.          (Picha kwa hisani ya Mtandao wa IFM).
Chuo cha usimamizi wa  fedha (IFM) Tanzania kwa kushirikiana na tawi la chuo hicho la Mkoani Mwanza wameandaa maonesho ya kitaaluma yatakayofanyika katika katika Viwanja Nyamagana mkoani hapa.

Kwa mujibu wa Taarifa ambazo mtandao huu imezipata kutoka vyanzo rasmi vya uongozi wa chuo hicho, maonesho hayo ya kitaaluma yanalengo la kutanua shughuli za chuo hicho katika kanda hii ya ziwa na hususan mkoani Mwanza Mkoa ambao umekuwa mstari wa mbele kwa maendeleo ya nchi katika kanda hii.

akizungumza hivi leo Ofisini kwake Dkt. Paul Katto amesema, maonesho hayo ambayo yatafanyika siku ya tarehe 19, 05. 2014 hadi tarehe 02.06.2014, yatafunguliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza mhandisi Evarist Ndikilo. " Tunatazamia kuwa na maonesho ya kitaaluma kwa Mkoa wa Mwanza na tayari shughuli mbali mbali zimekwisha kamilika kwa hivi sasa ikiwapo barua za mialiko kwenda kwa watu mbali mbali ambao tunataraji kuwa siku hiyo watahudhuria." alisema na kuongeza kuwa mbali ya kuwa na maandalizi hayo lakini pia kwa hivi sasa tunaandaa kikao na waandishi wa habari amba kwa namna moja au nyingine wao ni kiungo muhimu sana katika kuwafikishia umma taarifa hizi.

Amesema kwa mujibu wa ratiba yao watakuwa na kikao na waandishi wa vyombo mbali mbali vya habari kutoka magazeti Luninga na Radio ambao kimsingi wao ni wadau wakubwa na kama mambo yatakwenda vizuri tunatazamia kufanya mkutano na waandishi tarehe 17.5.2014 katika ukumbi wa tawi la chuo chetu hapa Mwanza, alisema Dkt. Katto.

Kwa zaidi ya miaka 40 chuo hicho kimekuwa kinara cha kutoa wanataaluma wa usimamizi wa fedha hapa nchini katika ngazi mbali mbali lakini pia usimamizi na uendelezaji wa mifumo mbali mbali ya kitekinolojia..