March 2014
no image
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Katika ushabiki wa mchezo wa soka mara nyingi wanasoka wakipata umaarufu mkubwa hasa kutokana na kusakata kabumbu ambao ndio utamu wa soka lenyewe.
Hata hivyo nchini Tanzania yupo shabiki Bwana Steven Samuel aliyejipatia umaarufu mkubwa kutokana na mapenzi yake kwa timu ya Tanzania hasa inapofungwa.
Ushabiki huu umemletea mafanikio si haba , kama alivyobaini Mwandishi wetu wa Dar es salaaam
kwa hisani ya    BBC
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

Mshambuliaji wa TP Mazembe, Mbwana Samata.

Dar es Salaam. Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samata alifunga bao pekee na kuiongoza TP Mazembe ya DR Congo kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, huku mabingwa watetezi Al Ahly wakiaga mashindano kwa kuchapwa 3-2 nyumbani na Al Ahly Benghazi ya Libya.

Samata aliingia akitokea benchi na kufunga bao hilo dakika ya 68 na kuipa ushindi wa 1-0 dhidi ya Sewe Sport ya Ivory Coast na kusonga mbele kwa sheria ya bao la ugenini baada ya matokeo ya jumla kuwa 2-2 baada ya awali Mazembe kutunguliwa mabao 2-1 jijini Abidjan.

Samata ndiye aliyefunga bao la kufutia machozi Abidjan wiki moja iliyopita pamoja na bao pekee la Jumamosi jijini Lumbumbashi. Sasa Mazembe itasubiri kujua wapinzani wake katika droo itakayopangwa Aprili 29 mjini Cairo.

Nao mabingwa watetezi Al Ahly ya Misri wameaga mashindano hayo baada ya kuchapwa mabao 3-2 nyumbani na Al Ahly Benghazi katika pambano la marudiano lililopigwa mwishoni mwa wiki jijini Alexandria.

Kipigo hicho kinaifanya Al Ahly iondolewe mashindano hayo kwa jumla ya mabao 4-2, baada ya mechi ya kwanza iliyopigwa jijini Tunis, Tunisia ambako Benghazi wanatumia kama uwanja wa nyumbani kutokana na machafuko kushinda 1-0.

Kutoka: Mwananchi.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Baadhi ya wajumbe wa Bunge la Katiba wakishangilia wakati mjumbe mwenzao, Joshua Nassari alipounga mkono kimakosa hoja ya kura ya wazi wakati anatoka upande unaoipinga. Picha na Salhim Shao
HAWA NDIO WABUNGE VITUKO.
Hali ya hewa jana ilichafuka kwenye Bunge la Katiba baada ya mjumbe Ezekiel Wenje kuwatuhumu Waziri Mkuu Mizengo Pinda na baadhi ya mawaziri kuwa waliwahonga baadhi ya wajumbe wa kundi la 201.
Katika tuhuma hizo, Wenje alimtaja Waziri Profesa Jumanne Maghembe, Dk. Shukuru Kawambwa na Gaudensia Kabaka akisema kuwa walitoa rushwa ya vyakula, maji na vinywaji kwa wajumbe hao ili waunge mkono msimamo wa serikali mbili.
Kauli hiyo, iliyotolewa katika mjadala wa mabadiliko ya kanuni, ilisababisha mawaziri hao kunyanyuka kujibu tuhuma hizo, huku Wenje akisisitiza kuwa aliyoyasema ni kweli tupu.
Vilevile baadhi ya wajumbe wanaotoka katika kundi hilo walicharuka na kujaribu kujitetea huku mmojawapo akitishia kuwa iwapo Wenje asingeomba radhi, asingetoka ndani ya Bunge hilo.
Hoja ilipoanzia
Wenje, ambaye pia ni mbunge wa Nyamagana (Chadema), alianza kwa kueleza kwamba wapinzani "walilia" sana kuwa Bunge la Katiba lisingekuwa na usawa kutokana na Chama cha Mapinduzi kuwa na wajumbe wengi, ndipo ikaonekana wapatikane wajumbe wengine 201, lakini jambo la ajabu ni kwamba walioteuliwa katika kundi hilo asilimia 80 ni makada wa CCM akiwamo mzee maarufu ambaye ameingizwa kama mganga wa jadi.
Ingawa hakumtaja jina, Wenje alikuwa anamaanisha kada mkongwe wa CCM, Kingunge Ngombale-Mwiru aliyeteuliwa kupitia kundi la waganga wa jadi.
Kuhusu rushwa, Wenje alisema:"...Sasa kuna wajumbe wa kundi la 201 walipelekwa kwa Profesa Maghembe na Dk. Kawambwa wamepeana rushwa, vikao vingi vilifanyika usiku. Hii haikubaliki."
Baada ya kauli hiyo ya Wenje, Profesa Maghembe alisimama ghafla huku akionekana kutaharuki, ambapo Makamu Mwenyekiti Samia Suluhu Hassan alimpa nafasi ya kujieleza.
Profesa Maghembe alikiri kuwakaribisha baadhi ya wajumbe wa kundi hilo, akieleza kwamba ilikuwa ni katika hali ya ukarimu uliozoeleka miongoni mwa jamii ya Kitanzania.
"Kuna kundi lipo hapa ambalo linafanya kazi ya kudhalilisha wenzao. Ni kweli niliwaalika kwa chakula wajumbe hao kwa taratibu za kawaida, lakini hakuna mbunge hapa anayeshindwa kujinunulia chakula, hakuna anayeweza kupewa rushwa.
"Kwa sababu hiyo ninaomba kiti chako kimtake mjumbe aliyewasilisha hoja hiyo aniombe radhi. Wenje aniombe radhi," alisema Profesa Maghembe akiwa katika hali ya hasira, huku kukiwa na sauti za kuzomea na kushangilia kutoka kwa wajumbe.
Makamu mwenyekiti pia alifanya jitihada za kuwataka wajumbe kuwa wavumilivu, huku akitoa nafasi kwa Dk. Kawambwa kujieleza akisisitiza kwamba ni tuhuma nzito.
Kawambwa alisema: "Ni kweli nilikutana nao; ni wajumbe ambao wanatoka kwenye taasisi zinazojihusisha na masuala ya elimu, lakini mbona wameshafanya mikutano yao mingine mingi ambayo mimi hawakuniita. Kama mtu akiwa hana hoja bora akae chini."
Makamu Mwenyekiti alimtaka Wenje aombe radhi kutokana na kauli yake, lakini katika hali ya kushangaza mjumbe huyo alisisitiza kwamba Profesa Maghembe na Dk. Kawambwa wamekiri.
"Maghembe amekiri aliwaita wafugaji na wavuvi ndiyo waliokula chakula cha rushwa, pia wapo wengine walienda kwa Waziri Gaudensia Kabaka, kuna ushahidi mama mmoja siwezi kumtaja jina hapa alikwenda huko akafukuzwa, nitakupa jina lake mwenyekiti baadaye. Aliambiwa kwamba anatoa siri... hoja iliyojadiliwa huko ilikuwa ni kwamba msimamo ni wa serikali mbili... rushwa ya chakula, maji na bahasha walipewa," alisema Wenje na kusababisha kulipuka kwa kelele zaidi.
Wenje aliongeza kuwa kuna wajumbe wengine walikwenda hadi kwa waziri mkuu ambako walikula, walikunywa hadi saa 7:00 usiku.
Alisema wengine walikwenda kwa Gaudensia Kabaka (Waziri wa Kazi na Ajira) na walikula na kunywa na kupewa bahasha.
Baada ya Wenje kukaa, baadhi ya wajumbe wa kundi la 201 walichachamaa wakitaka kutetea hadhi yao, akiwamo mjumbe kutoka kundi la wafugaji, Esther Juma aliyesema hawatendewi haki kama kundi kusema kwamba walihongwa.
Alisema yeye ana ng'ombe 3,000 na asingeweza kwenda kupokea rushwa ya chakula na kumtaka mbunge huyo kuwaomba radhi la sivyo asingetoka mlangoni.
Wakati mjadala huo ukiendelea, mwenyekiti wa Bunge, Samuel Sitta aliyekuwa ametoka kwa udhuru, alirejea kimya kimya, na kumtaka Wenje kueleza iwapo anadhani kauli yake haikuwaudhi baadhi ya wajumbe.
Wenje alikiri kuwa ni kweli baadhi ya wajumbe wameudhika kutokana na ukweli aliosema dhidi yao na kuwaomba radhi kwa ukweli huo.
Kauli hiyo ilimfanya Sitta kutangaza kuwa anapeleka suala hilo kwenye Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge na uamuzi utakaotolewa atautangaza bungeni.
CHANZO MWANANCHI
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
 
MHE. BERNAD MEMBE WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA TANZANIA.
Serikali ya Tanzania itafanya mazungumzo na Rwanda ili "kutatua tofauti za kisiasa kuhusu mgogoro katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), gazeti la Daily News la Tanzania liliripoti Alhamisi (tarehe 27 Machi).
 
Mazungumzo rasmi yanakusudiwa kuondoa kile Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania Bernard Membe alichokiita "vita ya kimaandishi" kilichosukumwa na propaganda ya vyombo vya habari.
 
"Mazungumzo hayo rasmi yatakuwa ndiyo mwanzo," alisema Membe, akiongeza kwamba watarejesha imani kati ya nchi hizo mbili.Membe alikariri kwamba kwa wajibu wa Tanzania katika mgogoro huo uliopo nchini  DRC ni kwa ajili ya jitihada za kuleta amani tu chini ya umoja wa mataifa.  wajibu wa Tanzania katika mgogoro uliopo nchini DRC ni kwa ajili tu ya jitihada za kuleta amani tu chini ya Umoja wa Mataifa.
 
"Kwa mujibu wa ujumbe wetu ulioko huko Goma [mashariki mwa DRC], amani hatimaye inarejea katika eneo hilo na vijana wetu wataendelea kuwa kule kwa mwaka mmoja hadi amani itakaporejea kikamilifu," alisema Membe.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.


KITANZI TAYARI KWA KUNYONGA.
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ya Tanzania imesema hadi kufikia Februari mwaka huu watanzania 177 wamefungwa katika magereza nchini China, huku miongoni mwao 15 wakiwa wamehukumiwa kunyongwa kutokana na makosa ya dawa za kulevya.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Wizara ya hiyo, John Haule alisema watanzania hao bado hawajanyongwa kutokana na serikali ya China kuthamini ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na China na huenda wakabadilishiwa kifungo na kufungwa kifungo cha maisha jela badala ya Kunyongwa.

Haule amesema serikali ya Tanzania itahakikisha inadumisha ushirikiano na China kwa lengo la kupatikana kwa fursa za kiuchumi na kwamba tayari serikali ya China imetoa vifaa kwa Tanzania kwa ajili ya kugundua watu wanaosafirisha dawa za kulevya katika viwanja vya ndege.

Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
MKUU WA MKOA WA MARA.
HUYU NDIYE JOHN TUPA
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
TAARIFA AMBAZO ZIMENIFIKIA KUTOKA KWA WADAU WA HABARI MKOANI MARA ZIMNASEMA KWAMBA MKUU WA MKOA HUO, AMEFARIKI DUNIA. TAARIFA HIYO IMESEMA KWAMBA MKUU H...UYO WA MKOA ALIKUWA WILAYANI TARIME KWA AJILI YA ZIARA YA KIKAZI. NA KABLA YA ZIARA YAKE ALIKUWA OFISINI KWA MKUU WA WILAYA HIYO, JOHN HENJEWELE AKIPOKEA TAARIFA YA WILAYA. NDIPO ALIPOA ANZA KUTOKWA POVU JINGI MDOMONI, NA KISHA KUKIMBIZWA KATIKA HOSPTALI YA WILAYA, IYOPO KARIBU KABLA YA KUPOTEZA MAISHA. POLENI WANA MARA.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

Huku hali ya taharuki ikiendelea kutanda mjini Mombasa pwani ya Kenya ambapo magaidi walivamia kanisa siku ya Jumapili na kuwapiga risasi waumini, mmoja wa waathiriwa wa shambulizi hilo amefikishwa Nairobi mwa matibabu maalum.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

 
Idadi ya waliofariki kufuatia shambulio la Likoni imeongezeka na kufikia 6 huku 9 waliokua wakipokea matibabu wameruhusiwa kurudi nyumbani na 6 hao walifariki kufuatia majeraha ya risasi,Polisi nchini Kenya imesema bado hawajafutilia mbali uwezekano wa kuwa lilikua shambulio la kigaidi.

Mwandishi wa habari kutoka Dw nchini  Kenya anaelezea kwa sasa kinachoendelea Mombasa>>’Hali ilivyo mjini Mombasa ni hali ya kutatanisha kukosekana kwa usalama kwa sababu kama unavyojua tukio hili  limezua hofu sana hasa kwa wakazi wa mji huu wa Mombasa’

‘Nakumbuka tukio la watu 5 waliuwawa kwenye kanisa moja hapa Likonyi ni kitendo kilichotokea siku 2 baada ya Waziri wa usalama kutoa taarifa kwa wakazi wa hapa kuwa usalama utadumishwa’

‘Hali ni tete hapa Mjini Mombasa baada ya tukio hilo ambalo watu hao waliuwawa msako wa polisi uliendelea kuimarishwa kuanzia saa 8 na msako huo uliendelea usiku kucha na taarifa tulizopokea kwa sasa ni kwamba watu 59 wametiwa nguvuni’

‘Wasiwasi upo kwa sababu hiki ni kitendo kilichotengenezwa ndani ya kanisa na unajua si mara ya kwanza kitendo hiko kutokea hapa Mombasa nakumbuka fujo zilizozuka baada ya kitendo cha ugaidi kutokea hapa Mombasa kuliokua na taharuki miongoni mwa wakazi wake hasa baina ya wakristo na waislam’

‘Hiki ni kitendo ambacho watu wanahofia kimetekelezwa kuzua hofu hasa miongoni mwa waumini wa dini hizo mbili lakini viongozi wa kidini wamekuja pamoja na kusema kwamba hiki ni kitendo kilichofanywa na magaidi tu ili kuzua mtafaruku miongoni mwa waumini baina ya wakristo na waislam hilo ni tukio linaloendelea kuchunguzwa’

‘Hadi kufikia sasa hakujawa na taarifa za kuthibitisha kitendo hiki kilitekelezwa kwa malengo gani na wakina nani hasa,hali ya wasiwasi mjini Mombasa bado ipo na kama unakumbuka kuwa tukio hili limetokea siku chache baada ya watu wawili kukamatwa wakiwa na mabomu Mabomu ambayo yaliharibiwa hivi juzi tu kwa hivyo ni tukio linalozidi kutia hofu kwa wakazi wa Mombasa’.