September 2014
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Wakutana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Fatilia matukio katika Picha zote Na, Afisa habari RS Mwanza.
MKUU WA MKOA WA MWANZA AKIPOKEA ZAWADI YA NGAO KUTOKA KWA KIONGOZI WA MSAFARA HUO BREGEDIA GENERAL KAPINGA WAKATI WA ZIARA HIYO.
MAKAMANDA WA CHUO CHA UKAMANDA WAKIWA WANAFATILIA KWA KARIBU MAELEZO YA MKUU WA MKOA WA MWANZA HAYUPO PICHANI  WAKATI WA ZIARA HIYO.

MAKAMANDA KUTOKA NCHI ZA RWANDA NA ZAMBIA WAKIWA MAKINI NA MAELEZO YA MHE. MKUU WA MKOA WA MWANZA.

MAKAMANDA KUTOKA TANZANIA WAKINUKUU BAADHI YA MAELEZO YA MHE. MKUU WA MKOA.


HAPA MAKAMANDA WAKIFATILIA JAMBO.


HIVI NDIVYO UKUMBI ULIVYOKUWA UNAFANANA.

KIONGOZI WA MSAFARA HUO BREGEDIA KAPINGA AKITOA MAELEZO MAFUPI KWA MKUU WA MKOA KABLA YA KUANZA MAONGEZI YAO NA MAKAMANDA HAO.


MOJA YA MAKAMANDA ALIYETAKA KUJUA KUHUSU JITIHADA ZA MKOA KATIKA KUMKOMBOA MKULIMA KWA KUWA KILIMO NI UTI WA MGONGO WA TAIFA LA TANZANIA.HAPA MAKAMANDA WALILAZIMIKA KUPIGA PICHA YA PAMOJA KAMA SEHEMU YA KUMBU KUMBU YA UGENI HUO KUTOKA (CSC- ARUSHA)

NI PICHA YA PAMOJA.
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua rsmi Kivuko cha Tegemeo tayari kuanza kufanya safari zake kati ya Kisiwa cha Maisome- Sengerema, wakati wa hafla ya uzinduzi wa kivuko hicho iliyofanyika Kijiji cha Kahunda Wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza leo, Septemba 26, 2014. Kulia kwake ni Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli na baadhi ya viongozi. Picha na OMR


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akibonyeza Kitufye kuashiria uzinduzi  rasmi wa Kivuko cha Tegemeo tayari kuanza kufanya safari zake kati ya Kisiwa cha Maisome- Sengerema, wakati wa hafla ya uzinduzi wa kivuko hicho iliyofanyika Kijiji cha Kahunda Wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza leo, Septemba 26, 2014. Kuhoto  kwake ni Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli na baadhi ya viongozi. Picha na OMRMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala Ufundi wa Umeme-TEMESA, Eng. Mseline Magesa, wakati alipokuwa akikagua Kivuko cha Tegemeo baada ya kukizindua rasmi leo Septemba 26, 2014 kwa ajili ya kuanza kazi ya kusafirisha abiria na mizigo kati ya Kisiwa cha Maisome- Sengerema, wakati wa hafla ya uzinduzi wa kivuko hicho iliyofanyika Kijiji cha Kahunda Wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala Ufundi wa Umeme-TEMESA, Eng. Mseline Magesa, wakati alipokuwa akikagua Kivuko cha Tegemeo baada ya kukizindua rasmi leo Septemba 26, 2014 kwa ajili ya kuanza kazi ya kusafirisha abiria na mizigo kati ya Kisiwa cha Maisome- Sengerema, wakati wa hafla ya uzinduzi wa kivuko hicho iliyofanyika Kijiji cha Kahunda Wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza. Picha na OMR

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya viongozi wakati akikagua Kivuko hicho. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wananchi wa Kahunda Wilaya ya Sengerema, wakati wa hafla ya uzinduzi wa kivuko hicho iliyofanyika leo, Septemba 26, 2014. Picha na OMR

Mhe. Dkt Mohamed Gharib Bilal Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mara baada ya Uzinduzi huo alipiga picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi waliokuwa wamehudhuria katika hafala hiyo

Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Rais wa Shirika la NEC Corporation la Japan, Dkt. Nobuhiro Endo, wakati alipofika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Septemba 12, 2014 akiwa ameongozana na ujumbe wake kwa ajili ya mazungumzo. Picha na OMR
Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal leo amekutana na Uongozi wa Kampuni ya NEC yenye makao yake makuu jijini Tokyo nchini Japan. Ujumbe wa NEC-Japan umeongozwa na Rais wa Kampuni hiyo inayojishughulisha na masuala ya Mawasiliano na Teknolojia, Dkt. Nobuhiro Endo.

 

Ujio wa Kampuni hii nchini Tanzania unatokana na mwaliko wa Tanzania kwa makampuni ya Japan kufuatia ziara ya kikazi aliyoifanya Mheshimiwa Makamu wa Rais nchini Japan, mwezi wa Mei mwaka huu. Mheshimiwa Makamu wa Rais alitembelea Makao Makuu ya Kampuni hiyo wakati za ziara hiyo.

 

Katika mazungumzo na uongozi wa NEC Mheshimiwa Makamu wa Rais aliwaeleza wageni wake nia ya Tanzania kuona inatanua mawasiliano na teknolojia nchini ili kuinua uchumi na akafafanua kuwa teknolojia yoyote kutoka NEC inakaribishwa hapa nchini ili kusaidia Tanzania kupiga hatua.

Uongozi wa NEC nao ulimueleza Mheshimiwa Makamu wa Rais kuwa, NEC inaushirikiano wa karibu na Shirika la Simu Tanzania (TTCL) na kwamba wanatarajia kukutana na uongozi wa wizara ya Mambo ya Ndani kwa lengo la kutazama fursa za kusaidia teknolojia katika ulinzi.

Imetolewa na:              Ofisi ya Makamu wa Rais

Ikulu Dar es Salaam Septemba 12, 2014
 
 

 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Uongozi wa Shirika la NEC Corporation la Japan, wakiongozwa na Rais wao Dkt. Nobuhiro Endo, wakati walipofika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Septemba 12, 2014 kwa ajili ya mazungumzo. Picha na OMR
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Uongozi wa Shirika la NEC Corporation la Japan, wakiongozwa na Rais wao Dkt. Nobuhiro Endo, wakati walipofika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Septemba 12, 2014 kwa ajili ya mazungumzo. Picha na OMR
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwakatika picha ya pamoja na Rais wa Shirika la NEC Corporation la Japan, Dkt. Nobuhiro Endo (kushoto) na Balozi wa Japan Nchini Tanzania, Masaki Okada, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Septemba 12, 2014. Picha na OMR
 

Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
KATIBU MKUU UTUMISHI GEORGE YAMBESHI AKIZUNGUMZA NA WATUMISHI WA RS MWANZA.
 
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi George Yambeshi, amewataka watumishi wa Umma wa Sekretarieti ya mkoa wa Mwanza kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria, kanuni na miongozo iliyopo ili kuleta tija katika ufanisi wa kazi zao.
 
 
Ameyasema hayo wakati alipokutana na watunishi wa sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mwanza hii leo alipokuwa ziarani mkoani humo kwa shughuli za kijamii na kuamua kutumia fursa hiyo kukutana na watumishi hao.
 
Yambeshi amesema kama watumishi wa umma ni lazima kuzingatia miiko inayo ongoza utumishi wa umma huku akitolea mfano wa mavazi nadhifu kwa watumishi na yasiyo na utata kwa watu " kama watumishi wa ni vema kuzingatia miiko inayo tuongoza" alisema na kuongeza.  kuwa suala la kuvujisha siri za serikali ni suala lisilo kubalika hivyo moja ya sifa ya mtumishi wa umma ni lazima ajue kutunza siri.
 
Katika hatua nyingine Katibu Mkuu huyo ameonya watumishi wa kuacha kuchanganya mambo ya siasa mahali pa kazi" Ndugu zangu haikazwi kuwa mwanachama wa chama cha siasa lakini sio vema mtumishi kufanya masuala ya siasa mahali pa kazi kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na taratibu za utumishi wa umma.
 
Mbali na masuala la siasa na uadilifu katika kazi ,pia katibu Mkuu huyo ametumia fursa hiyo, kusilikiliza kero mbali mbali za watumishi hao ikiwapo suala la kodi kubwa, mikopo kwa watumishi pamoja na kukosekana kwa baadhi ya miundo ya kada mpya za utumishi serikialini.
 
Awali akimkaribusha katibu Mkuu kiongozi kuzungumza na watumishi hao wa Skretarieti ya Mkoa wa Mwanza, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Bwana Ndaro Kulwijila, alimuelezea kuhusu hali halisi ya watumishi katika mkoa wa Mwanza huku akitoa kilio chake kwa Katibu Mkuu huyu juu ya utofauti Mkubwa wa mishahara baina ya watumishi waliopo kwenye wakala wa serikali na wale wa serikali kuu.
 
Hata hivyo katika majibu yake Katibu Mkuu huyo aliahidi kushughulikia changamoto zote zilizo jitokeza katika kikao hicho na kuzipatia ufumbuzi kwa kadri itakavyowezekana.
 
Katibu Mkuu Utumishi ndiye mkuu wa masuala ya Utumishi wa umma katika Serikali ya jamahuri ya Muungano wa Tanzania. 

 

PICHANI ALIYE SIMAMA NI BWANA KIGERE AFISA MANUNUZI WA RS MWANZA

KATIBU MKUU UTUMISHI AKISIKILZA MAONI NA KERO MBALI MBALI KUTOKA KWA WATUMISHI WA RS MWANZA

PICHANI HAPA WATUMISHI WAKIMSIKILIZA KWA MAKINI KATIBU MKUU UTUMISHI, HAYUPO PICHANI KATIKA SEKRETARIETI YA MKOA WA MWANZA.


BWANA DANNY  TEMBA, AMBAYE NI KATIBU WA AFYA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA SEKOUTURE AKINUKUU DONDOO MUHIMU WAKATI WAKIKAO CHA KATIBU MKUU NA WATUMISHI.
 FARIDA MUSHI AFISA UTUMISHI RS MWANZA, AKITOA MOJA YA KERO KUHUSU KUTOKUELEWEKA KWA BAADHI YA MIIUNDO MIPYA YA UTUMISHI KWA BAADHI YA KADA ZA UTUMISHI WA UMMA.

MJIOLOJIA WA RS MWANZA PICHANI XAVERY HUMBO ALIPOKUWA AKITOA DUKU DUKU LAKE LA MALIPO MBALI MBALI YALIYOKUWA NA UTATA DHIDI YAKE.


SAIDI KITINGA PICHANI AKIELEZEA KERO KUHUSU MIKOPO YENYE RIBA KUBWA KWA WATUMISHI.

MCHAMBUZI MKUU WA MIFUMO YA KOMPUTA BIBI FATMA MATOPE, HAKUKOSA CHA KUMSHAURI KATIBU MKUU UTUMISHI JUU YAKUBORESHA MASLAHI YA WATUMISHI.

KATIKA PICHA YA PAMOJA, WALIO KAA NI KUTOKA KUSHOTO NI MKUURUGEZI WA RASILIMALI WATU
OFISI YA RAIS UTUMISHI, KATIBU MKUU UTUMISHI, KAIMU KATIBU TAWALA WA MKOA WA MWANZA, NA KATIBU TAWALA MSAIDIZI RASILIMALI WATU NA UTAWALA  RS MWANZA

KATIKA PICHA YA PAMOJA, WALIO KAA NI KUTOKA KUSHOTO NI MKUURUGEZI WA RASILIMALI WATU
OFISI YA RAIS UTUMISHI, KATIBU MKUU UTUMISHI, KAIMU KATIBU TAWALA WA MKOA WA MWANZA, NA KATIBU TAWALA MSAIDIZI RASILIMALI WATU NA UTAWALA  RS MWANZA KWA NYUMA NI BAADHI YA WATUMISHI WA RS MWANZA WALIO SIMAMA.
 
 
Kuni News Blog. Habari, matukio na uchambuzi wa makala.
Mara baada yakuwa katika sintofahamu kwa muda wa wiki tatu hatimaye  shinano la kumpata mrembo wa Kanda ya Ziwa 2014/2015 (Miss Lake Zone 2014)   liliafanyika katika  uwanja  wa CCM Kirumba usiku wa kuamkia  tarehe 30/Agosti/2014, ambapo bibie Rachel Clavery aliibuka na ushindi kwa kuwapiku walimbwende wengine wa kanda hii wapatao 17, na  hivyo kukirithi kiti cha ulimbwende  kutoka kwa mshindi wa mwaka 2013/2014, Lucy Charles.
Mashindano hayo yamehusisha mikoa miatno  ya kanda ya ziwa ambayo ni; Mara, Kagera, Shinyanga, Geita,  na Mwanza..
Katika mashindano hayo Bibi Nicole Sarakikya aliibuka kuwa Mrembo aliyependeza zaidi katika picha, hivyo kuwa Miss Photogenic 2014/2015 kwa kanda ya ziwa. hata hivyo wadau na wapenzi wa urembo katika shindano hilo walikosoa baadhi ya kasoro ikiwapo ile yakumpa ushindi mtu ambaye alishindwa kujieleza vizuri mbele ya hadhira iliyokuwa imekusanyika katika uwanja huo. Nabadalaya Bibie Nicolle Sarakikya aliyekuwa ameonesha umahiri kwenye kujieleza akaachwa na kupewa mwinge.

Mashindano ya mwaka huu yameandaliwa na Flora Solun wa Jiji Mwanza.
 

Rachel Clavery katikati akiwa pamoja na mshindi wa pili Mary Emanuel - Kulia pamoja na mshindi wa tatu Nikole Sarakikya katika fainali za Miss Lake Zone 2014 CCM Kirumba - Mwanza
Hapa ni jaji mkuu wa shindano hilo, Hashim Lundenga alipokuwa akitangaza tano bora

 
Gari alilopata mshindi wa Miss Lake Zone 2014
  ORODHA YA WASHIRIKI WA SHINDANO HILO NI HII HAPA;

Christina Jilulu(20), Doreen Robert(20) Moshi Shaaban(20),  Jacklin
Kimambo(22), Nyange Waryoba(22) na Fauzia Haruna(18), Winfrida Nashon(20), Martha John(21) na Elinaja Nnko(21)  Mary Emmanuel (20), Rachel Judica(21) Nicole Sarakikya ,Christina John(22), Evelne Charles(23) Cecilia Kibada(22) na Geita ni Farida Ramadhan(20),Rose Msuya(18) , Rachel Clavery(20).