Mzee Nelson Mandela-Rais Mstaaf wa Afrika Kusini
Rais mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, amelezwa hospitali kwa siku ya pili mjini Pretoria ambako alipelekwa Jumamosi.
Maafisa wamesema kwamba amekuwa akifanyiwa uchunguzi, ingawaje haijajulikana kwamba ni uchunguzi wa aina gani.

Rais Jacob Zuma, aliyemtembelea Jumapili, alisema kwamba hali yake ilikuwa nzuri. Bwana Mandela ana miaka 94.
Awali, Mandela alilazwa hospitali mnamo Februari ili kutibiwa matatizo ya tumbo yaliyokuwa yamemsumbua kwa muda mrefu.

Hajaonekana hadharani tangu Afrika Kusini ilipofungua michezo ya Kombe la Dunia mwaka wa 2010.
Axact

Post A Comment: