Bilawal Bhutto Zardari-Mtoto wa Benazir Bhutto
MWANAWE waziri mkuu wa Pakistan aliyeuawa, Benazir Bhutto, amezindua kuingia
kwake kwenye siasa hii leo ikiwa ni maadhimisho ya mwaka wa tano tangu mamake
kuuawa.
Bilawal Bhutto Zardari anatarajiwa kutangaza malengo yake kwa mara ya kwanza mbele ya maelfu
ya wafuasi nyumbani mwao katika jimbo la Sindh.
Mamia ya maelfu ya wafuasi wa chama cha Pakistan Peoples Party walianza kufurika Larkana kabla
ya siku hiyo kubwa.

Wanaharakati waliobeba picha za Benazir Bhutto, na babake, waziri Mkuu wa zamani Zulfiqar Ali
Bhutto, wamekita kambi kote mjini humo.

Chama hicho tawala kinataka kutumia sherehe hiyo kuonyesha kuwa licha ya shutuma kuhusu
utendakazi wake katika miaka mitano iliyopita, bado kina wafuasi wengi.

Hotuba kuu itatolewa namwanawe Bhutto, Bilawal Bhutto Zardari.

Itakuwa mara ya kwanza kwake kuhutubia mkutano wa maelfu ya wafuasi kuelezea maono ya chama
hicho.

Aliteuliwa mwenyekiti wa chama hicho punde tuu baada ya kuuwawa kwa mamake na wapiganaji
wa taliban mwaka wa 2007, lakini hajajitokeza hadharani kutokana na umri wake mdogo na kukosa
uzoefu wa kisiasa.

Huku uchaguzi wa Bunge ukitarajiwa Pakistan katikati ya mwaka wa 2013, waliochoshwa na siasa za
rais Zardari, wanamuangalia, kijana huyo mwenye umri wa miaka 24 na aliyehitimu kutoka chuo cha
Oxford, kufufua umaarufu wa chama hicho
Axact

Post A Comment: