WAZIRI DKT. JOHN POMBE MAGUFULI KWENYE UWEKAJI JIWE LA MSINGI.
        MALORI YALIO PIGWA STOP NA MAGUFULI.






 
MKUU WA MKOA WA MWANZA, MHANDISI EVARIST NDIKILO KWENYE UWEKAJI JIWE LA MSINGI.
 
Na: Atley Kuni- Afisa habari Mwanza.

Waziri wa Ujenzi Dr. John Pombe Magufuli, ameonya wenye malori kupita katikati ya jiji la Mwanza mara baada ya kukamilika kwa Mradi wa ujenzi wa barabara ya km. 17 kutoka Kisesa hadi Usagara ili kuweza kuzifanya barabara hizo ziweze kudumu.

Magufuli aliyasema hayo, wakati alipokuwa akiweka jiwe la Msingi kwenye maradi wa ujenzi wa daraja la Mabatini linalojengwa kwa ajili ya kuepusha ajali za mara kwa mara zilizo kuwa zinatokea katika eneo hilo, alisema “ilikuzifanya barabara za katikati ya Jiji ziweze kudumu ni lazima tuzitunze na kuzitunza ni kwa wenye malori kuhakikisha wanapita kwenye bara bara tunazo zifungua pembezoni mwa mji, alisema na kuongeza kuwa katika hilo hakuna mjadala” kwa kuwa yeye aliaminiwa na Mhe. Rais hivyo anazo nguvu zote za kuweza kudhibiti, pindi barabara zitakapokamilika wenye malori wasivumiliwe tena kupita katikati ya Jiji.

Katika hatua nyingine Magufuli ameahidi kuwekewa kwa uzio kwenye darajahilo la mabatini ili waenda kwa miguu wasiweze kukatisha kwa urahisi,” Ni kweli Mstahiki Meya amenikumbusha jambo la maana, ilituweze kuepusha ajali za mara kwa mara tutahakikisha tunaweka uzio mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa daraja hili na kabla ya kuanza kutumika” alisema Magufuli.

Awali kabla kuhutubia umati wa watu waliofika kumshuhudia uwekaji wa jiwe la Msingi, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza aliwasilisha ombi la kupanuliwa kwa barabara ya Airport, ambayo inategemewa na idadi kubwa ya watu, “Mhe. Waziri wahenga walinena unapokutana na Jumbe, umsalimie hapo hapo,na mimi Mhe waziri sisi wana Mwanza Jiji letu linakuwa kwa kasi sana na msongamano wa watu unazidi kuongezeka, alisema na kuongeza “kukamilika kwa Soko la kimataifa la Ghana, ambalo litakuwa na uwezo wa kuchukua magari 2000 kwa wakati mmoja na pikipiki 200 ni dhahiri kwamba…! hata msongamano utakuwa mkubwa…..! lakini sio hilo tu Mhe Waziri kukamilika kwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwanza ni ishara kwamba, tuna kila sababu ya kuongeza barabara hiyo na kuwa njia nne alisema Ndikilo huku akishangiliwa na umati wa watu waliokuwa wamefurika eneo hilo la mabatini.

Akijibu, Magufuli alisema ameyasikia maombi hayo na tayari mchakato umekwisha anza ikiwa ni pamoja na kuona awezekano wa kuwa na usafiri wa majini ambao utarahisisha usafiri na kuondoa msongamano wa watu mjini  lakini pia Boti zitakazo kuwa zinatumika ni haraka (Speedboats), na itawawezesha watumia Boti kufanya utalii wa Majini alisema waziri.

Katika hatua nyingine Waziri Magufuli, alisema ameyapokea maombi yaliyotolewa na Diwani wa kata ya Mbugani bwana Hashimu Kijuu kwa niaba ya wananchi wa mabatini juu ya ujenzi wa barabara ya Nyerere “A” ambayo inahudumia zaida ya watu 5000 kwa siku,” Huyu Diwani ni mtu mzuri kwa sababu amesema juu ya maendeleo na sio ushabiki wa vyama ombi lake nimelielewa na nipende kumuahidi kuwa katika mwaka ujao wa fedha halmashauri ya jiji imuandikie barua ili aweze kulishughulikia, Diwani huyo aliwasilisha maombi ya ujenzi wa barabara moja miongoni mwa tatu alizo zitaja.

DARAJA AMBALO SASA LINATAJWA KWAMBA LITAPUNGUZA AJALI ZA BARABARANI NA KICHOCHEO CHA UCHUMI.
 
Daraja la Mabatini linajengwa kwa fedha za serikali kiasi cha Tanzania Milioni 888.5, na litakapokamilika litakuwa na uwezo wa kuchukua watu 60 kwa wakati mmoja.

Kwa upande wao wananchi waliongea na mtandao huu wamesema kukamilika kwa mradi huo itakuwa ni ukombozi kwa wananchi wa jiji la Mwanza kwani itasidia kupunguza ajali za barabarani ambazo zinatajwa kutokea ajali 48 kati ya kipindi cha 2010/2013 ambapo ajali 22 zilisababisha watu kupoteza maisha na watu 26 kupata vilema vya maisha” Ni ukweli kwamba kipato cha wachuuzi wa picha madhari ya Jiji kunakishka ni vitu ambavyo tutegemee” aliniambia Mwandishi mwandamizi wa ITV na Radio One, bw. Mabere Makubi.
Axact

Post A Comment: