HALMASHAURI ya Manispaa ya Ilemela, jijini Mwanza inakabiliwa na changamoto ya uzoaji taka ngumu kutokana na kuharibika kwa magari ya kuzolea taka hizo.
Hayo yalilezwa mwishoni mwa wiki na Mkuu wa wilaya ya Ilemela, Amina Masenza wakati akitoa taarifa ya Januari hadi Machi, mwaka huu ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM.
Alisema katika kipindi hicho uzoaji na utupaji wa taka ngumu ulikuwa wa matatizo kutokana na kuharibika kwa magari ya kuzoa taka ya halmashauri.
Alisema katika kukabiliana na tatizo hilo halmashauri ilikodisha magari kutoka makampuni binafsi ambapo jumla ya tani 1,500 za taka ngumu zilizotolewa katika vituo vya Furahisha na Buzuruga.
Alisema kutokana na uharibifu wa mazingira unaoendelea katika maeneo mbalimbali ndani ya halmashauri kwa ajili ya maendeleo ya kijamii, halmashauri imeandaa mabango kwa ajili ya kusimika yenye ujumbe wa kuzia uharibifu wa mazingira.
Masenza alisema katika bajeti ya mwaka 2013/14 halmashauri ilitenga Sh. Mil. 320 kwa ajili ya kununua magari mawili mapya ya kuzolea taka huku halmashauri ikiwa imeweka makubaliano na mradi wa uboreshaji wa mazingira ya ziwa Victoria.
Aidha kwa upande wa ardhi Masenza alisema katika kipindi hicho jumla ya migogoro ya 67 ya ardhi imetatuliwa  kwa kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa wilaya.
Pia alisema viwanja katika maeneo ya Buhilya, Nyasaka, Bujingwa, Nyamhongholo na Bwiru zimekaguliwa na mipaka yake kutambuliwa  na kwamba katika kudhibiti ujenzi ujenzi holela kwa kushirikiana na ofisi ya Mhandisi wa Manispaa nyumba 14 zilibomolewa.
Na Grace  Chilongola, Mwanza
Axact

Post A Comment: