Mara baada yakuwa katika sintofahamu kwa muda wa wiki tatu hatimaye  shinano la kumpata mrembo wa Kanda ya Ziwa 2014/2015 (Miss Lake Zone 2014)   liliafanyika katika  uwanja  wa CCM Kirumba usiku wa kuamkia  tarehe 30/Agosti/2014, ambapo bibie Rachel Clavery aliibuka na ushindi kwa kuwapiku walimbwende wengine wa kanda hii wapatao 17, na  hivyo kukirithi kiti cha ulimbwende  kutoka kwa mshindi wa mwaka 2013/2014, Lucy Charles.
Mashindano hayo yamehusisha mikoa miatno  ya kanda ya ziwa ambayo ni; Mara, Kagera, Shinyanga, Geita,  na Mwanza..
Katika mashindano hayo Bibi Nicole Sarakikya aliibuka kuwa Mrembo aliyependeza zaidi katika picha, hivyo kuwa Miss Photogenic 2014/2015 kwa kanda ya ziwa. hata hivyo wadau na wapenzi wa urembo katika shindano hilo walikosoa baadhi ya kasoro ikiwapo ile yakumpa ushindi mtu ambaye alishindwa kujieleza vizuri mbele ya hadhira iliyokuwa imekusanyika katika uwanja huo. Nabadalaya Bibie Nicolle Sarakikya aliyekuwa ameonesha umahiri kwenye kujieleza akaachwa na kupewa mwinge.

Mashindano ya mwaka huu yameandaliwa na Flora Solun wa Jiji Mwanza.
 

Rachel Clavery katikati akiwa pamoja na mshindi wa pili Mary Emanuel - Kulia pamoja na mshindi wa tatu Nikole Sarakikya katika fainali za Miss Lake Zone 2014 CCM Kirumba - Mwanza




Hapa ni jaji mkuu wa shindano hilo, Hashim Lundenga alipokuwa akitangaza tano bora

 
Gari alilopata mshindi wa Miss Lake Zone 2014
 



 ORODHA YA WASHIRIKI WA SHINDANO HILO NI HII HAPA;

Christina Jilulu(20), Doreen Robert(20) Moshi Shaaban(20),  Jacklin
Kimambo(22), Nyange Waryoba(22) na Fauzia Haruna(18), Winfrida Nashon(20), Martha John(21) na Elinaja Nnko(21)  Mary Emmanuel (20), Rachel Judica(21) Nicole Sarakikya ,Christina John(22), Evelne Charles(23) Cecilia Kibada(22) na Geita ni Farida Ramadhan(20),Rose Msuya(18) , Rachel Clavery(20).
Axact

Post A Comment: