Jumla ya wahamiaji haramu 4 wanne kutoka Somalia wamekamatwa Mkoani Morogoro wakiwa
kwenye basi la Elisaidi lililokuwa likielekea Mkoani Mbeya kutokea Dar Es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Afisa uhamiaji Mkoa waMorogoro bw.Max Lugadi,
amesema wahamiaji hao wamekamatwa katika eneo la Msavu, wakati basi hilo lilipo simama
kwaajili yakuchuka abiria wanao elekea Mbeya.



Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wahamiaji hao wamesema watatu walikuwa hawana vibali ilihali
mmoja wao alisema yeye Pasi yake ya kusafiria ilikuwa imepotea, taarifa ambazo Maafisa hao
wa Uhamiaji wamezitilia shaka na kufanya waweke chini ya ulinzi.

Katika hatua nyingine wahamiaji hao wamesema walikuwa wanaelekea Mkoani Mbeya kwa
ndugu yao jambo ambalo pia askari hao wa uhamiaji wali litilia shaka kwani simu hiyo ilivyo
tafutwa ilikuwa haipatikani takriba ni muda wote ilipokuwa inapigwa.

Katika siku za hivi karibuni kumekuwepo na wimbi la wahamiaji haramu katika nchi ya
Tanzania ambapo mwezi June mwaka jana wahamiaji haramu 83 walikamatwa katika viji vya
Chitego na Mkoka Mkoani Dododoma wakiwa wamefariki Dunia.

Hata hivyo Mkuu huyo wa Uhamiaji Mkoa wa Morogoro ameonya juu ya Wahamiaji wote
watakao kamatwa moani humo kuwa sheria itachukua mkondo wake na kuwataka wanachi
wa Mkoa huo kutoa ushirikiano wakutosha kwa vyombo vya usalama ili kuwabaini wahamiaji
wote haramu. Katika siku za hivi karibuni Mkoa huo umukuwa katika harakati za kuhakikisha
wanakomesha Wimbi la wahamiajai haramu.

Na: Atley Kuni
Axact

Post A Comment: