PICHANI MBIO ZA MWENGE ZILIPO WASILI KATIKA WILAYA YA MAGU NA HAPO NI KATIKA ENEO LA NYANGUGE.

MKUU WA MKOA WA MWANZA MAGESA MULONGO AKIUPOKEA MWENGE WA UHURU WAKATI UKITOKEA KATIKA MKOA WA SIMIYU SIKU YA TAREHE 28.08.2015.
KATIBU TAWALA WA MKOA WA MWANZA DKT. FAISAL ISSA WAKATI WA MAPOKEZI YA MWENGE MKOANI MWANZA NA HAPA ALIKUWA AKIMPOKEA KIONGOZI WA MBIO HIZO BW. JUMA KHATIB CHUM


MKUU WA MKOA WA MWANZA ALIPOKUWA AKIWAHUTUBIA WANANCHI WALIOKUSANYIKA KATIKA ENEO LA KIJIJI CHA NSOLA WAKATI WA MAPOKEZI YA MWENGE.


VIJANA WA SHULE WAKIWA KATIKA MOJA YA MIKUSANYIKO YA MWENGE MWAKA 2015.


KIONGOZI MKUU WA MBIO ZA MWENGE 2015 JUMA KHATIB CHUM AKIMTWIKA MAJI MMOJA YA WAKINA MAMA KATIKA WILAYA YA MAGU.
Kama inavyo fahamika kila mwaka Mwenge wa uhuru hukimbizwa kote nchini na mkoa wa Mwanza kama iliyo kwa mikoa mingine mkoa wa Mwanza hupitiwa na mbio hizo na hapa pata kufahamu jinsi mwenge ulivyo pita na miradi iliyopitiwa na Mwenge huo.
 
Mwaka 2015, Jumla ya miradi 64 yenye thamani ya Tshs. Billioni 18,497,953,314 itaweza kufikiwa Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wa Mwanza. Katika miradi hiyo, Miradi 15 yenye thamani Tsh. Bilioni 10,167,443,654 itawekewa mawe ya msingi, miradi 21 yenye thamani ya Tsh. Bilioni 1,353,151,574   itazinduliwa, na miradi 28 yenye thamani ya Tsh. Bilioni 6,977,358,086 itafunguliwa.
Miradi yote imegharamiwa na serikali kuu Tsh. Bilioni 5,296,616,637. Halmashauri Tsh. Bilioni 2,109,308,123. Nguvu za wananchi Tsh. Bilioni 2,680,133,700 pamoja na wahisani mbalimbali ambao wamechangia Ths. Bilioni 8,411,854,854. Miradi hii ipo katika sekta za elimu, afya, barabara, maji, utawala bora, vijana, wajasiriamali, biashara, kilimo na ufugaji.
Je nini Ujumbe wa Mwaka huu.?.. Mkuu wa  mkoa wa Mwanza.
Kama mnavyofahamu ujumbe wa mwaka huu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru unasema “Tumia haki yako ya kidemokrasia: jiandikishe na kupiga kura katika uchaguzi wa 2015”.  Ujumbe huu ni muafaka kabisa kwa wakati huu na hasa ikifahamika  kuwa tarehe 25 Oktoba, 2015 kutakuwepo na upigaji wa kura ili kuchagua viongozi ambao ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge na Madiwani.  Niwapongeze wale wote waliotumia haki yao ya kikatiba na kisheria ya kujiandikisha na kupewa kitambulisho cha mpiga kura. Kujitokeza kwenu kwa wingi mumewezesha mkoa wa Mwanza kuvuka lengo la uandikishaji kwa asilimia 103 ambapo jumla ya watu 1,442,391 waliweza kuandikishwa. Ombi langu kwenu, ni kuvitunza vitambulisho mlivyopewa na siku ikifika, nendeni kwenye vituo mlivyojiandikisha  ili kupiga  kura. Mkoa umejipanga kuhakikisha amani na utulivu vinatawala kipindi chote cha uchaguzi huo.
Mkuu wa Mkoa  wa mkoa hasiti kutia msisitizo wa ujumbe wa kudumu.....
Pamoja na ujumbe mkuu wa Mbio za Mwenge wa uhuru 2015,  upo  ujumbe wa kudumu ambao unahimiza wananchi  kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI, Malaria, Rushwa na Dawa za kulevya. Takwimu za mkoa zinaonesha kuwa maambukizi ya UKIMWI yanazidi kupungua kutoka wagonjwa 979,035 mwaka 2009 hadi kufikia wagonjwa 367,545 mwaka 2014 ambapo kiwango cha maambukizi katika Mkoa ni asilimia 4.2 kwa mwaka 2014. 
 
 
Mkuu wa Mkoa wa mkoa analiona janga la dawa za kufubaza virusi vya UKIMWI.
Ombi langu kwa watanzania mnaonisikiliza na hasa wanaotumia dawa za kufubaza virusi vya UKIMWI wasiache kuzitumia.  Wakiacha kwa sababu yo yote ile wanavipa vijidudu nafasi kujiimarisha na hivyo kuhatarisha maisha yao.  Tuendelee   kuwasaidia wenzetu walioathirika na kuwahudumia badala ya kuwanyanyapaa na kuwatenga.  Na, muhimu zaidi tuwasaidie watoto yatima na wazee ambao wameachwa bila msaada wowote.
 
Vipi suala la Rushwa?
Mwaka huu, katika Mbio za Mwenge wa Uhuru naomba  nikumbushe  wajibu wa kila mmoja  kupambana na rushwa,  kwa kauli mbiu isemayo “kata mnyonyoro wa rushwa: chagua kiongozi  Mzalendo’. Ujumbe huu unakwenda sambamba na juhudi za serikali za kupambana na rushwa nchini.  Tunafahamu kuwa rushwa ni adui wa haki na kikwazo kikubwa cha maendeleo ya jamii na taifa.  Nchi ikiwa imegubikwa na vitendo vya rushwa itakosa maendeleo stahiki na watu watadhulumiwa haki zao. Kwa mfano, kwa kipindi cha miaka mitatu, yaani kati ya 2010 hadi 2013, zaidi ya shilingi bilioni 28 zimeokolewa ambazo zingeweza kunufaisha watu wachache wanaoendeleza vitendo vya rushwa. Naomba wananchi waendelee kutoa taarifa zitakazosaidia kuwatambua na kuwakamata watoaji na wapokeaji rushwa.
 
 
 
Mkuu wa mkoa analiona suala la dawa za kulenya kama kikwazo cha maendelea je! anasema nini?
Tatizo la biashara na matumzi ya dawa za kulevya limeendelea kuwa moja ya changamoto kubwa zinazolikabili taifa letu. Serikali imeendelea kufanya jitihada kubwa kupambana na changamoto hiyo.  Ugumu wa kazi hiyo unaletwa na ukweli kwamba watu wanaohusika ni wengi na wanazidi kuongezeka kila kukicha kwa tamaa ya kupata utajiri wa haraka.
Serikali haitachoka kufanya kila tuwezalo kupambana na uhalifu huu mpaka ushindi upatikane, ikiwa ni pamoja na kutumia vikundi na taasisi mbalimbali za uelimishaji wa mabadiliko ya tabia.  Wakibadili mbinu nasi tutabadili maarifa ya uchunguzi na utambuzi mpaka tuwapate. Kwa mfano, kuanzia Januari hadi Septemba, mwaka huu (2015) watu 2000 (wafanya biashara na watumiaji wa dawa za kulevya) wamekamatwa. Mashamba kadhaa ya bangi yameteketezwa, na aina mbalimbali ya dawa za kulevya ikiwa ni pamoja na kilo 681 za dawa hatari ya heroine, zimekamatwa na watuhumiwa wamefikishwa kwe Mkondo wa sheria.  Nawaomba sana ndugu zangu na wananchi wenzangu mshirikiane na vyombo vya dola katika kupambana na usafirishaji, uuzaji na usambazaji wa dawa za kulevya. 
 
Baada ya kutoa salamu hizi nachukua nafasi hii kuwaribisheni Mkoani Mwanza na najisikie mko nyumbani,
NAWATAKIA KILA LA HERI! ASANTENI KWA KUNISIKILIZA.
Axact

Post A Comment: