MWAKILISHI WA KATIBU TAWALA MKOA WA MWANZA, MWALIMU HAMISI MAULIDI AKIFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO, WAANDAAJI WA FILAMU NCHINI.
PICHANI NI BIBI JOYCE FISOO, KATIBU MTENDAJI WA BODI YA FILAMU NCHINI, AKIWASILISHA MADA WAKATI WA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZOWANATSNIA YA FILAMU MKOANI MWANZA.


RAIS WA SHIRIKISHO LA FILAMU TANZANIA BW. SAIMON MWAKIFWAMBA(KULIA), AKIFAFANUA JAMBO KWA MAAFISA WA  WA HIFADHI YA JAMII WA PPF KANDA YA ZIWA.
Na Lorietha Laurence-Mwanza

Mkoa wa Mwanza waweka mkakati  wa kukuza na kuendeleza sekta ya filamu kwa kuhakikisha inazalisha bidhaa bora zenye kufuata taaluma na weledi wa tasnia hiyo ili kufikia soko la kimataifa.

Hayo yameelezwa leo  na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza  Hamis Maulidi ,wakati wa ufunguzi wa warsha ya wadau wa tasnia ya filamu yenye lengo la kuwajengea uwezo wanatsnia hao.

Akizungumza katika Ufunguzi huo Maulidi  ameeleza kuwa filamu ni kielelezo muhimu cha utamaduni wa watu na jamii husika hivyo ni budi kuulinda , kuenzi pamoja na kuendeleza suala zima la filamu, huku akiahidi Mkoa wake  kusimamia ipasavyo ili kuleta mabadiliko lakini pia kuwawezesha wana tasnia hao kujiajiri.

“Ni wajibu wa jamii husika kuhakikisha kuwa tasnia ya filamu inalindwa na kuenziwa ili kuleta kuendelea kulinda na kuhifadhi  utamaduni,silka na mila zetu”

Maulidi amesema, tasnia ya filamu imeleta ajira rasmi kwa wananchi wetu ambao wamekuwa wakijihusisha na utengezaji, uaandaaji  pamoja na uigizaji wa filamu na kuziuza kwa wadau mbalimbali jambo ambalo limekuwa likiwaingizia kipato cha kujikimu kimaisha.

Awali akimkaribisa kufungua  semina hiyo ya siku tatu   Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Bibi. Joyce Fissoo, amewataka wanatasnia hao kuwa watulivu na kujifunza zaidi kupitia warsha hiyo ili kuzalisha filamu zenye kuzingatia taaluma na weledi wakati wote wa maandalizi hadi uzalishaji wa Filamu hapa nchini .

Warsha ya kuwajengea uwezo wanatsnia wa filamu Mkoani Mwanza imejikita katika kuhakikisha kuwa, tasnia ya filamu nchini inakuwa na kufikia viwango vya kimataifa ili kuwezesha ushindani katika masoko ya kimataifa.

 
Axact

Post A Comment: