Na
Lorietha Laurence-Mwanza.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella  amiomba Bodi ya Filamu Nchini, kutazama namna yakuwasaidia wasanii wa filamu nchini  kwa kuwajengea
uwezo wa 
namna ya kuwapa mbinu za uendeshaji, ujasiliamali na biashara  wadau hao ili waweze kupenya katika soko la
filamu.
 
Akifunga mafunzo ya siku tatu yaliyo washirikisha wasanii wa Filamu nchini, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.Mary Tesha ambaye ni mkuu wa Wilaya ya Nyamagana,
aliyasema alianza kwa kuipongeza Bodi ya Filamu Nchini kwa, 
“Kwanza
naipongeza Bodi ya Filamu Nchini kwa kuandaa warsha hii nzuri ambayo wadau
wangetakiwa kuilipia lakini wameipata bure hii ni kwa jinsi gani Serikali
inawajali watu wake  hivyo naomba wakati
mwingine mtakapotoa warsha mada kuhusu biashara na ujasiliamali ziwepo” alisema
Mhe.Tesha
Vilevile Mhe.Mary amempa siku saba Afisa
Utamaduni  mkoani hapo Bw. James Willium,
kuhakikisha kuwa anayafanyia kazi maadhimio yaliyoafikiwa na wasanii wa filamu
mkoa wa Mwanza.
Mkuu wa Wilaya huyo amesema Afisa
Utamaduni huyo, kwa kushirikiana na Maafisa Utamaduni wa Halmashauri zote za
mkoa wa Mwanza wanapaswa kuhakikisha wanatoa mikakati ya utekelezaji wa maadhimio
yaliyotolewa kwenye warsha hiyo ili utekelezaji huo uanze mara moja.
Naye 
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fesso, amesema  lengo la warsha hiyo ni pamoja na  kuwajengea weledi wadau wa filamu waweze  kutengeneza kazi zenye ubora ili kukuza soko
la filamu na hivyo kunufaika na kazi zao.
Warsha hiyo ya siku tatu ilihitimishwa
kwa mgeni rasmi kutoa vyeti vya ushiriki kwa wadau wa filamu zaidi ya  300 ambapo waliweza kujifunza mada mbalimbali
zilizowasilishwa  na wawezeshaji kutoka
katika vyuo Vikuu vya Dodoma na Dar es Salaam,Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
pamoja na Bodi ya Filamu nchini .
Mwisho.
 
 
Post A Comment: