Meneja wa wakala wa Vipimo mkoa wa Mwanza,  Hemed Kipengela, wakati wa Utoaji wa Elimu juu ya Matumizi sahihi ya Mizani mkoani humo.
 
Wakala wa Vipimo (WMA) Tanzania imeendelea na zoezi la utoaji wa elimu  pamoja na uhakiki wa mizani kwenye  makampuni mbalimbali  ya wafanyabiashara Mkoani Mwanza   katika  Wilaya za  Kwimba, Magu, Misungwi  na Sengerema ikiwa ni maandalizi ya msimu wa Pamba.
 

Akizungumza na Meneja wa Wakala wa Vipimo Mkoani Mwanza  Bwana Hemed Kipengele  alisema  jumla ya mizani 448 tayari imekaguliwa kutokana na  makampuni manne ambayo  tayari yamekagulisha mizani yake na imekutwa ikiwa sahihi  ambayo ni  ICK (T) LTD  ambao walikuwa a mizani 184, SM HOLDING wenye jumla ya mizani 85 pamoja na   NYANZA COTTON  ambao walikuwa na mizani 179. Meneje aliongezea kuwa zoezi hili la utoaji elimu pamoja na uhakiki wa mizani itakayotumika kununulia Pamba linaendelea kwa Mikoa yote inayolima  Pamba ambayo ni Shinyanga, Simiyu, Geita, Kagera, Tabora pamoja na Mara.

Bwana Kipengele alisema wanatarajia kutembelea jumla ya vijiji 101 ambavyo vina jumla ya vituo vya kuuzia Pamba 150 ili waweze  kutoa elimu na kufanya kaguzi za kushutukize kwa wanunuzi wa Pamba ili kuona kama mizani waliyopima na ikaonekana ni sahihi itaendelea kununua Pamba ya wakulima kwa vipimo sahihi.
 Meneja Kipengele  aliwasihi baadhi ya wakulima wanaolalamikiwa kuweka maji, kokoto pamoja na mchanga kwenye Pamba kwa ajili ya kuongeza uzito waache tabia hiyo mara moja  sababu Sheria ya vipimo ipo na inafanyakazi kwa pande zote mbili muuzaji na mnunuzi wote kwa pamoja hawatakiwi kufanya udanganyifu wowote katika biashara.
 Kipengele alisema Sheria ya Vipimo Sura 340 inawataka Wakala wa Vipimo  kuhakiki na kupiga chapa vipimo vyote vinavyotumika katika biashara pia Wakala wa Vipimo imeongeza na uwekaji wa  sticker kwa kipimo kitakachokuwa tayari kimehakikiwa ili iwe rahisi kwa wakulima kuona na kutambua mizani iliyokaguliwa na kuruhusiwa kwa biashara kwa mwaka husika.
Alisisitiza kuwa kwa wale watakaobainika kuchezea mizani  kwa ajili ya kuwaibia wakulima adhabu ni kuanzia laki moja hadi milioni ishirini endapo mkosaji atakubali kosa, endapo kesi itafikishwa mahakamani na mlalamikiwa akakutwa kweli alikosa kulingana na ushahidi utakaokuwa umetolewa mshitakiwa atatozwa faini kuanzia laki tatu hadi milioni hamsini au kifungo cha miaka mitatu au vyote kwa pamoja. Lengo kuu  ni kumlinda mlaji ili apate faida na thamani ya kile alichozalisha  na siyo kupunjwa  na wafanyabiashara  wajanjawajanja.
Afisa wa Wakala wa Vipimo Daniel Mwakilima, akitoa elimu juu ya Matumizi sahihi na kubaini Mizani iliyo sahihi katika Wilaya ya Magu.
Tunaimani Tanzania ya viwanda itafanikiwa  endapo Mkulima, Mfanyabiashara watazingatia matumizi ya vipimo sahihi kuanzia maandalizi ya shamba, upandaji wa mazao, utumiaji wa pembejeo, uuzaji, usafarishaji, upokeaji wa mazao, ufungashaji hadi utumiaji wa mazao yenyewe , hivyo vyote vikizingatia matumizi ya vipimo sahihi viwanda vingi vitaweza kupata malighafi za kutosha sababu mkulima na mfanyabiashara  kila mtu atakuwa na imani na mwenzake kupitia matumizi ya vipimo sahihi. Msema kweli  na mleta haki katika biashara ni kipimo sahihi  kilichohakikiwa na Wakala wa Vipimo wala siyo vinginevyo.
Meneja wa wakala wa Vipimo mkoni Mwanza akiendelea kutoa Elimi kwa Wakulima katika Wilayani Magu.
Axact

Post A Comment: