Bibi Leah Mwainyekule, akitoa ufafanuzi kuhusu Semina hiyo juu ya utunzaji fedha katika Vituo vya Afya na Shule Jiji Mwanza |
![]() |
Kaimu Mkurugenzi wa jiji la Mwanza, Omary Kamatta akifungua Semina hiyo ya siku mbili inayo washirikisha, Waratibu Elimu kata wa Jiji na Manispaa ya Ilemela katika ukumbi wa mkuu wa Mkoa wa Mwanza. |
Akisoma
hotuba kwa niaba ya Mkurugezi wa Jiji la Mwanza, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji hilo,
Omary Kamatta, amesema ili wananchi wawe na imani na serikali yao, suala la
uwazi lazima litiliwe maanani “nielekeze matumizi ya tovuti za Mikoa na
Halmashauri katika kuweka taarifa zote za mapato na matumizi ya fedha za umma”
alisema Kamatta na kuongeza kuwa suala hilo ni maelekezo ya
Serikali, na kila mmoja analijua na anapaswa kutekeleza.
![]() |
Bwanakher Mmmoja ya Wakufunzi wakati wa Semina hiyo kwa Waratibu Elimu Kata na wasimamizi wa Vituo vya Afya. |
Kamatta
amesema, Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya
Sekta za Umma ujulikanao kwa Kiingereza kama Public Sector Systems
Strengthening, (PS3), uliowezesha mafunzo hayo ya Mfumo wa Uhasibu na
Utoaji Taarifa za Fedha kwa ngazi ya Kituo cha Kutolea Huduma [Facility
Financial Accounting and Reporting System (FFARS)], una lengo la kuongeza
ufanisi, hususan katika masuala mazima ya mapato, na ndio utakuwa mtatuzi wa
malalamiko ya wananchi.
Ameongeza
kuwa, lengo la mafunzo hayo ni
kuwajengea uwezo watoa huduma katika vituo vya kutolea huduma, na kusaidia
upatikanaji wa taarifa sahihi katika mahesabu ya mapato na matumizi katika
halmashauri kote nchini. “Mafunzo haya yanafanyika sambamba
katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu, ili kuhakikisha kwamba nyote mnakuwa
katika nafasi ya kwenda kuwafundisha watoa huduma mbalimbali katika Vituo vyote
vya kutolea Huduma Tanzania Bara, yaani (Service providers or Facilities),
ambavyo vinajumuisha Zahanati, Vituo vya Afya, Hospitali, Shule za Sekondari na
za Msingi” alisema Kamatta.
![]() |
Mkurugenzi wa Manispaa ya ilemea John Wanga, akisema maneno yakuwaasa washiriki wa Semina hiyo juu yakuzingatia yote watakayo fundishwa. |
Akitoa
maelezo ya awali, msimamizi mafunzo hayo katika Jiji la Mwanza na Manispaa ya
Ilemela, Mkuu wa Mawasiliano wa PS3, Bibi Leah Mwainyekule, amesema kuanzia
mwaka ujao wa fedha, yaani Julai 1, 2017, Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya
Tanzania itaanza kupeleka rasilimali fedha moja kwa moja kwenye vituo vya afya
kwa ngazi za vituo vya kutolea huduma ambavyo vitapokea fedha hizo vinavyojumuisha
Zahanati, Vituo vya Afya, na Hospitali za Wilaya. Aidha zoezi hilo
litakwenda sambamba na inavyotekelezwa kwenye sekta za elimu, Serikali za
Vijiji na Ofisi za Kata.
Bibi Mwainyekule amesema, Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya
Kimataifa la Marekani (USAID), wametoa mafunzo ya kina kwa wakufunzi 490
katika ngazi ya taifa na halmashauri nchini kote. Mafunzo hayo yalifanyika katika mikoa ya Dodoma,
Mbeya, Mtwara, na Shinyanga, ambao nao sasa wanajukumu kuwawezesha watumishi
katika vituo vya Sekta ya Afya na Elimu kupata ujuzi wa namna ya kutumia mfumo
mpya wa FFARS.
Mwainyekule amesema, wakufunzi hao kwa sasa
ndio wanaotoa elimu hiyo kwa watumiaji wa mwisho wa mfumo wa FFARS kwa ngazi ya
Vituo vya Afya 550, Zahanati 6800, Hospitali za Wilaya 135, na takribani Shule
za Msingi na Sekondari 20,000 katika mikoa yote 26 ya Tanzania Bara, vikiwemo
vituo vya kutolea huduma kutoka Mikoa 13 na Halmashauri 93 zinazotekeleza Mradi
wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3).
Mafunzo hayo yatahakikisha kuwa watoa huduma katika
vituo wana ujuzi unaohitajika katika usimamizi wa fedha na kutoa huduma
bora kwa wananchi wote Tanzania na kwa jamii zenye uhitaji.
Mfumo wa FFARS unatekelezwa kwa ushirikiano baina ya
Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI); Wizara ya
Fedha na Mipango; Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi; na Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, pamoja na USAID
Post A Comment: