Hatma ya mgogoro wa watumishi ambao walikuwa na vyeti feki itajulikana mwishoni mwa mwezi wa sita mara baada ya zoezi la kusikilizwa kwa rufaa kukamilika.

Akizungumza Mkoani Mwanza juzi na watumishi wa Mkoa wakati wa juma la Utumishi wa Umma, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Laurian Ndumbaro    alisema, hadi kufikia Juni 30, 2017 hatma ya wale wote waliokuwa na vyeti vya bandia itajulikana mara baada ya kupitia rufaa zote ambazo ziliwasikishwa ofisini kwake.

“Baada ya uchambuzi kutokana na malalamiko yaliyowasilishwa na wahusika, mnamo kesho Juni 30 tutatoa majibu,” alisema.

Ndumbaro alifafanua kwamba wapo watakaorejeshwa lakini wapo pia ambao uwezekano wa kurejeshwa hautakuwepo kutokana na ushahidi uliopatikana.

“Lazima tuelewane katika hili, wapo ambao wao walikuwa na vyeti vya daraja sifuri, wakaenda wakatengeneza vyeti vyenye dara la pili au la kwanza au latatu, hawa tulipojaribu kuitisha vyeti vingine kama vya ndoa nk. Ilionekana kutofautina hawa itabidi watupishe” alisema Ndumbaro.

 Aidha aliongeza kamba, “wapo baadhi ambao wao walipoteza vyeti lakini kwa uvivu hawakutaka kufuatilia Polisi au barazani kwa ajili yakutapatiwa nakala zingine badala yake wakaenda kutengeneza kwa matokeo yale yale ya vyeti vyao halisi hawa tutawafikiria kwani dhamira yao ilikuwa sio kughushi bali walikwepa usumbufu,”

Ndumbaro amesema mara baada yakukamilika kutolewa kwa taarifa ndipo vibali vya ajira vitatolewa ili kuweza kuziba nafasi zitakazo kuwa zimebaki wazi, lakini pia kuongezwa kwa baadhi ya watumishi kulingana na mahitaji kwenye maeneo tofauti tofauti.

”Ni kwamba mara baada ya zoezi hilo tutakuwa tunahitimisha utumishi hao walikata rufaa na wale watakaoshindwa wataungana na wale 8000, ili watupishe tufanya taratibu zingine” alisema Ndumbaro.

Ndumbaro pia aliwaagiza watumishi wote kuwasilisha taarifa zao sahihi kwa maafisa Utumishi ili waweze kuzinakilisha kisha kuziweka kwenye mfumo wa kieletroniki.

 “Kuna watu Place of Domicile, hazieleweki ni vema sasa kila mmoja aweke mambo yake sawa nakupeleka taarifa kwa maafisa utumishi,” alisema.

Sambamba na Maagizo hayo, Katibu Mkuu huyo amesema kwasasa serikali ipo katika mchakato wa kuanzisha mfumo wa (Service Delivery point), ambayo itasaidia kutambua mtumishi mahali alipo, lakini pia kuyajua majukumu anayoyatekeleza mtumishi husika. Zoezi hili litaanza na sekta za afya na elimu.

 

Awali akisoma taarifa  ya Utumishi wa umma katika  mkoa wa Mwanza kwa niaba ya katibu Tawala wa Mkoa huo Clodwig Mtweve, Katibu Tawala Msaidizi wa uapnde wa Utawala na rasilimali watu, katika Sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza, Projestus Rubanzibwa, alisema mkoa huo umeendelea nashughuli za  uboreshaji wa shughuli za umma katika Nyanja mbali mbali ikiwapo Afya na Elimu, ambapo, katika afya Mpango wa malipo kwa ufanisi (Result Basing Financing), mpango huu ulio anza  Mkoani Mwanza Mwezi, Aprili, 2016 ulio  na lengo la kuboresha huduma za afya ya msingi, ambapo kwa upande wa watumishi mazingira ya kazi yameboreshwa kwa kuwapatia  vitendea kazi, ukarabati wa miundo mbinu ya kutolea huduma na kulipa motisha kwa watumishi wa sekta husika kwa kuzingatia matokeo ya utendaji kwa vigezo vilivyoanishwa.

 

 

Rubanzibwa amesema “Baada ya tathmini kufanyika  kupitia mpango huu  imeonekana kuwa kumekuwa na ongezeko la ubora wa takwimu kutoka asilimia 43.4 hadi asilimia 70.7 kwa kipindi cha kuanzia Aprili, 2016 hadi Aprili, 2017”. Aidha amesema “Kuongezeka kwa morale ya utendaji kazi kwa watumishi kutokana malipo yanaolipwa kupitia utendaji na ufanisi Ukarabati wa miundo mbinu ya vituo vya kutolea huduma ambapo ofisi na majengo ya vituo yamekarabatiwa” aliongeza Rubanzibwa.

Katibu Mkuu Menejimenti ya Utumishi wa Umma Laurean Ndumbaro, alipokuwa akiongea na baadhi ya watumishi wa Umma katika mkoa wa Mwanza wakati wa juma la Utumishi wa Umma.



Akizungumzia maboresho katika sekta ya elimu, Rubanzibwa amesema Mpango wa Ulipaji kwa Matokeo umeendelea kutekelezwa kama ulivyokusudiwa, kati ya mwezi Februari na Aprili, 2017 Wakuu wa Idara za  Elimu Msingi na Sekondari wa  Halmashauri walipatiwa mafunzo juu ya utekelezaji wa mpango huo. Alisema mpango huo unalenga kuinua utendaji kazi wa walimu wanaofundisha darasani pamoja na wanafunzi ili kuwezesha kusawazisha ikama (Pupil Teacher’s Ratio) kwa kulipa gharama za uhamisho kwa walimu wanaohamishwa kwenda kujaza ikama katika shule zenye upungufu.

Lakini pia kuboresha miundo mbinu kwa kufanya ukarabati wa madarasa na ujenzi wa matundu ya vyoo kutoa motisha kwa wanafunzi na walimu wanaofanya vizuri katika matokeo ya mitihani mbalimbali ya kitaifa.

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa pamoja na Halmashauri zake nane (8) kwa taarifa za Mwezi Aprili, 2017 zina jumla ya watumishi 25,734 Kati ya hao watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa ni 632 na watumishi wa Halmashauri ni 24,742.
Axact

Post A Comment: