Watumishi
mkoa wa Mwanza kuwezesha kituo cha damu salama kanda ziwa kuwa na damu
yakutosha ili kuweza kukidhi mahitaji halisi yanayo fikia chupa za ujazo 78,000
kwa mwaka.
![]() |
MKUU WA MKOA WA MWANZA AKIZUNGUMZA KATIKA MOJA YA VIKAO VYAKE MKOANI HUMO. |
Hayo
yamesemwa na wakuu wa taasisi za umma waliopo Mkoani Mwanza wakati wa kikao cha
pamoja na mkuu wa mkoa wa Mwanza kama sehemu yakujitambulisha kwa mkuu huyo wa
mkoa, lakini pia kuelezea shughuli zao wanazo zifanya katika mkoa huo.
Akizungumza
kwa niaba ya wakuu wengine wa taasisi hizo mkurugenzi wa maji safi na maji taka
jiji Mwanza Mhandisi Antony Sanga, amesema wao kama Mamlaka ya maji safi na
maji taka Jijini Mwanza wapo tayari kutoa elimu kwa watumishi walioko chini yao
juu ya umuhimu wa kuchangia damu kwenye kituo cha damu salama huku akiahidi
kutoa ushirikiano wa kutosha wakati wa zoezi hilo “Katibu Tawala naomba
niwahakikishie kuwa sisi kama mamlaka tunao watumishi wengi ambao ninaimani
tukiwaeleimisha vizuri watachangia damu bila matatizo kwa kuwa suala la damu ni
suala mtambuka linalo mgusa kila mmoja wetu leo unaweza usione umuhimu wa
kuchangia lakini tatizo likikutokea kwako mwenyewe au ndugu yako ndio utaona
umhimu wake” alisema Sanga.
Kwa
Upande wake mkurugenzi wa hospitali ya Rufaa Bugando alisema ni kweli kituo cha
damu salama kimekuwa na changamoto ya uwepo wa damu salama hivyo ni vema kama
taasisi za umma wakubaliane juu ya mpango huo.
Akiwasilisha
ombi hilo kwa wakuu hao wa taasisi Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Dkt. Faisal
Issa, amesema ni jambo lisilo kubalika katika karne hii kupoteza maisha ya watu
kwa ajili ya kukosa damu salama “ karne hii hatutakiwi kupoteza watu kwa ajili
yakukosa damu alisema Issa na kuongeza tumsaidie ndugu yetu wa damu salama ili
aweze kuwa na damu yakutosha katika benki ya damu”
Awali
akijitambulisha mbele ya mkuu wa mkoa Meneja wa kituo cha damu salama kanda ya
ziwa Fedrick Venance alielezea changamoto zinazo kikumba kituo kwa sasa kuwa ni
pamoja na upungufu wa damu, alisema kwa hivi sasa kituo cha damu salama hadi
kufikia tarehe 18.12.2014 kilikuwa na damu salama chupa 300 pekee huku kikiwa na
upungufu wa chupa 77700 ambazo ndio hitaji kamili la wananchi wa kanda ya ziwa “Mhe mkuu wa mkoa zipo changamoto kadhaa ikiwapo ya
uhaba wa damu salama kwa kiwango kinachotakiwa, kwakuwa wengi tunao wategemea
katika suala la uchangiaji damu ni wanafunzi ambao kwa hivi sasa wapo likizo
hivyo kufanya kituo kupungukiwa na damu. Alisema menejaVenance.
Majibu
hayo yalifuatia swali aliloliuza mkuu wa mkoa akitaka kujua hali ya ukusanyaji
damu ilivyo kwa sasa kwa kanda ya ziwa.
Mikoa
ya kanda ya ziwa inayoundwa na Mwanza, Shinyanga, Mara, Kagera, Simiyu, na
Geita ndio kwa kiasi kikubwa hutegemea kituo hicho japo wapo wananchi wengine
ambao hufika kwa ajili yakupata damu salama kutoka maeneo mengine ya nchi.
Kukosekana
kwa damu inaelezwa kuwa ni tatizo kubwa kwa watoto walio chini ya umri wa miaka
mitano, wakina mama wajawazito wakati wa kujifungua, wazee na watu wengine
ambao hupata ajali na kutokwa na damu nyingi mwilini.
Kwa
upande mwingine Venance amesema, zipo jitihada zinazo endelea kuchukuliwa kwa
ajili kuboresha hali ya damu salama kwa mikoa ya kanda ya ziwa ikiwapo,
kuanzishwa kwa kituo cha kukusanyia damu salama kwa mkoa wa Mara kuanzia
mwezi Januari na Mkoa wa Simiyu kuanzia
mwezi Februari mwakani.
Hata
hivyo wakati wakikao hicho mkuu wa mkoa aliwaambia watendaji hao kwamba, kila
mmoja aliyewekwa katika eneo hili anatosha na ndio maana yupo hapo alipo, na
kuwaonya kuacha kutegemea kila kitu makao makuu ya taasisi husika “najua
tumefanya vizuri kwenye baadhi ya sekta lakini jambo hapa sio kufanya
vizuri suala nikwa jinsi tunaweza kuya
maintain, sasa nimekuja kuwakumbusha kwamba tunatakiwa kuyasimamia vizuri maeneo yetu ili
tusidondoke” alisema Mulongo.
Huu
ni muendelezo wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza katika kufahamiana na wadau mbali mbali
wa maendeleo katika mkoa wa Mwanza ambapo zamu hii ilikuwa kwa ajili yakukutana
na taasisi za umma zilizopo mkoani humo.
Post A Comment: