Wanafunzi wa shule wa elimu maalum Kakola wilayani Kwimba katika maadhimisho ya miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania Bara

Imeelelezwa kwamba pamoja na Tanzania kuadhimisha miaka hamsini na moja ya Uhuru bado pato la mwana Mwanza lipo chini ya kiwango cha kawaida ukilinganisha na rasilimali ziliopo mkoani humo.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evaristi Ndikilo wakatiwa maadhimisho ya miaka hasini na moja ya uhuru wa Tanzaniabara yaliofanyika kimkoa katika Wilaya ya Kwimba.


Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mkuu wa Wilaya ya Kwimba, Selemani Mzee Selemani, alisema wakati Nchi inapata uhuru wake 1961, Baba wa Taifa Mwalimu Julias K. Nyerere, aliwabainisha maadui watatu, kuwa ni ujinga, maradhi na umasikini. Hivyo kusudi Nchi iweze kupata maendeleo ni vema maadui hao watatu wakaondolewa kwanza, na ili maadui hao waweze kuondoa suala muhimu ni kutumia fursa zilizopo kwa kuwajibika,uadilifu na uzalendo ndiyo view dira katika kujiletea maendeleo.

Kuinua pato.

Alisema suala la kuanza nalo ni kuinua kipato cha mwananchi kutoka dola za sasa 500 kwa mwaka ambazo ni sawa na (Tsh 800,000/=) na kufikia kipato cha kati cha dola 5,000 ili kupunguzaumaskini wa kipato kwa Mwana mwanza akatolea mfano wa Wilaya ya Kwimba ambapo pato la Mkaazi wa Kwimba
ni chini ya Dola 300 kwa mwaka.
Alizitaja baadhi ya fursa wanazoweza kutumia katika kuondoa umasikini kuwa ni pamoja na kilimo cha Umwagiliji, kwani kwa Mkoaa wa Mwanza pekee ni Hekta 1,008 ndizo zinazolimwa kilimocha umwagiliaji kwa hivi sasa, wakati ya eneo linalofaa kwa kilimo cha Umwagiliaji ni Km za Mraba 32,000,

Aliwaagiza maafisa Ugani kutokaa Maofisini na badala yake waende mashambani kwaajili yakuwaongezea stadi za kilimo cha kisasa wakulima, ili waweze kulima kilimo chenye tija, alisema na kuongeza kuwa, wakulima watumie mvua zinazo endelea kunyesha na kulima mazao yatakayo waletea mavuno bora huku
akitolea mfano wa mbegu zinazo zalishwa na kituo cha Utafiti cha Ukiliguru akatolea mfano mbegu za kisasa za mihogo ya Mkombozi, Meremeta na Kyaka.

Vyumba vya Maabara.

Kwa upande mwingine Mkuu huyo wa Mkoa aliwahimiza wanamwanza kwa ujumla kuhakikisha kila shule inajenga vyumba vitatu vya maabara yaani ya fizikia,bailojia na kemia ili kukabilia na changamoto ya Elimu, alisema kama vile wnamwanza walivyo kubali kujenga vyumba vya madarasa niwakati sasa wakukabilina
na adui ujinga kwakujenga maabara za sayansi ili kuwawezesha watoto wa kitanzania kujipatia elimu bora na sio bora elimu akahimiza watoto waliofika umri wakwenda shule kuandikishwa.

Alisema uhuru na maendeleo unategemea sana suala la afya na ustawi wa jamii, hivyo kwa sasa serikali imeagiza kila kijiji kujenga zahanati, na kila kata kujenga kituo cha afya, lengo likiwa nikupunguza vifo vya mama na mototo.

Mkuu huyo wa Mkoa alionya juu ya tabia iliyoanza kujitokeza hivi sasa ya baadhi ya watu wasio itakia mema nchi hii kwa kuanzisha fujona kisha kuporamali za watu wengine, kuingiza udini na ukanda katika suala la maendeleo jambo ambalo alisema ni hatari kwa Taifa kama Tanzania, kwani Uhuru na maendeleo ni sawa na yai na kuku kila mmoja ana mtegemea kingine alsema mkuu huyo wa Mkoa.

Awali akitoa salam za Wakuu wa wa wilaya, Mkuu wa wilaya ya Magu, Bi. Jaquline Lyana alisema, watanzania wametiza miaka hamsini na moja bila machafuko kutokana na umoja wao waliokuwa nao, hivyo Mtu yeyote asiwadanganye juu ya kutuvurugia umoja huu, Wenzetu Congo hawana amani, Misri, Somalia na kwingineko sasa tukifarakana watanzania tutakimbilia wapi? Alihoji nakuongeza, hatuna pakukimbilia. Tutunze amani yetu Watanzania tulio achiwa na waasisi wa Taifa hili, hayati baba wa Taifa Mwalimu Julias Nyerere na Mwenzie Amani Abed Karume wa Zanzibar waliotangulia mbele ya haki, alisema Mkuu
huyo wa Wilaya ya Magu.

Mbali na salam na hotuba za vingozi mbalimbali wa Serikali sherehe hizo pia zilihudhuriwa na Vingozi wa Dini, Vyamavya siasa, na wanachi wakawaida ambao walionesha shughuli mbalimbali za kimaendeleo katika wanzozifanya.

Sherehe za Uhuru wa Tanzania bara husheherekewa kila ifikapo Dec. 09 ya kila mwaka, na kwa Mwaka 2012, Mkoa wa Mwanza uliadhimisha sherehe hizo Kimkoa katika Wilaya ya Kwimba.

PICHA MBALI MBALI ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 51 YA UHURU WA TANZANIA BARA-TANGANYIKA MKOA WA MWANZA-WILAYANI KWIMBA
Mzee Salum Bakari Askari wa Vita vya Pili vya Dunia akimuonesha Mkuu wa Wilaya Tuzo aliyopewa Mwaka jana na Raisa Kikwete wakatia miaka 50 ya Uhuru wa tanzaniabara ( Picha zote na Atley Kuni)

Nayo vilevile ni Elimu maalum Kwimba Katika Serehe za Miaka hamsini na moja ya Uhuru wa Tanzania Bara.

Huyu ni Mama aliye kutwa na Kamera hii Eneo la Station jijini Mwanza, mara baada yakusika Treni inakuja Mwanza, Hapa alikuwa anajiandaa Kwaajili yakuanza Biashara ya Samaki Eneo la Railways, Miaka ya nyuma wanawake wengi walikuwa wakijishughulisha na biashara hiyo. Hii nikatika miaka 51 ya Uhuru wa Tz.

Wajasiriamali mbalimbali katika Wilaya ya Kwimba wakionesha bidhaa zao kwenye Viwanja vya KWIDECO Siku ya Uhuru.
Axact

Post A Comment: