Katibu Tawala Msaidiz Mipango na Uratibu Mkoa wa Mwanza Bibi Issabela Marick.

KIKAO cha kamati ya ushauri cha Mkoa wa Mwanza (RCC ) kinatarajia kufanya mkutano wake tarehe 14/12/2012, katika Ukumbi wa Chuo cha Benki jijini Mwanza.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mratibu wa kikao hicho, Katibu Tawala msaidizi wa Seksheni ya mipango na uratibu Bibi Issabela Marick, amesema katika kikao hicho mambo kadhaa ya Maendeleo yatajadiliwa na kutolea tathmini ya mambo ambao yalikuwa yamejadiliwa katika vikao vilivyopita.

Ameyataja baadhi ya mambo ambayo yatajadiliwa kuwa ni pamoja na kujadili na kutoa tathimini ya hali ya chakula katika Mkoa wa Mwanza, suala la Elimu na maendeleo ya elimu Mkoani humo,hali Miundombinu na mambo mengine ya kiutawala.

Sambamba na mabo hayo vilevile wadau wengine nao watapata fursa yakuwasilisha Mada katika kikao hicho.

Amewataja wadau hao kuwa ni Kanisa katoliki Jimbo Kuu la Mwanza, ambao watawasilisha mada kuhusiana na uwanzishaji wa Chuo kikuu kwaajili ya Watoto wa kike pekee, wengine ni Mamlaka ya usuluhishi na utatuzi wa migogoro ya kazi sehemu za kazi, na namna yakushughulikia migogoro hiyo nao watapata fursa kuwasilisha mada katika kikao hicho.

Kwa upade mwingine bibi Marick Amesema, Itatolewa tathmini juu ya Uwanzishaji wa Chuo kikuu cha umma kwa Mikoa ya Kanda ya Ziwa.

RCC ndicho kikao kikubwa kabisa cha maamuzi katika ngazi ya mkoa na kipo kwamujibu wa sheria namba 19 ya mwaka 1997 juu ya uanzishaji wa Sekretarieti za Mikoa na kuhuishwa na tangazo la Novemba 2011 lililo sainiwa na Mhe. Rais.


Na : Afisa habari RS- Mwanza.
Axact

Post A Comment: