Al Bashir na Kiir wajadili kadhia ya Abyei na mipaka



Rais Omar Hassan al Bashir wa Sudan na mwenzake wa Sudan Kusini Salva Kiir wamekutana leo na kufanya mazungumzo mjini Juba katika safari yake ya pili huko Sudan Kusini baada ya nchi hiyo kujitenga.
Pande hizo mbili zimeafikiana juu ya kufunguliwa tena mipaka ya nchi mbili. Vilevile viongozi hao wamejadili suala la kuanzishwa idara ya pamoja ya eneo la Abyei linalogombaniwa ambao limesababisha mapigano ya hapa na pale kati ya majeshi ya Sudan na Sudan Kusini.
Mgogoro wa eneo la Abyei unatishia makubaliano ya amani yaliyotiwa saini mwaka 2005 na kukomesha vita vya ndani vya Sudan vilivyoendelea kwa kipindi cha zaidi ya miongo miwili.
Al Bashir na Kiir pia wamejadili na kuchunguza maamuzi ya Umoja wa Afrika kuhusu mgogoro wa pande hizo mbili na vilevile suala la kuimarisha uhusiano wa kibiashara na kiuchumi.
Axact

Post A Comment: