Alex Ferguson amponda David Beckham.


Aliyekuwa meneja wa klabu ya Manchester United ya Uingereza Sir Alex Ferguson amesema David Beckham alilazimika kuondoka katika klabu hiyo kutokana na tabia yake ya kujiona ni mkubwa kuliko meneja wake.
Katika kitabu kipya kuhusu historia ya maisha yake Ferguson amesema enzi za uongozi wake walitofautiana na Beckham kutokana na kumkosoa kuhusiana na kiwango chake katika matokeo ya ligi ya FA 2003.
Mchezaji huyo alionekana kuwa na msimamo unaoonyesha kujiona mkubwa na kutokubali maelekezo .
Furguson amesema kuwa tabia ya Beckham ilionekana kubadilika tangia alipomuoa mwanamuziki maarufu wa miondoko ya pop Victoria kutoka kundi la Spice Girls
"David ni mchezaji pekee ambaye nilimuwezesha kumuweka katika mazingira ya umaarufu wa soka kidunia, lakini sikufurahishwa na maisha ya umaarufu wake na hasa kujiona yeye ni bora zaidi' alisema Ferguson.
Ferguson amesema haijalishi ni Alex Furguson ama Pete the plumber, lakini mamlaka ni mamlaka tu, hangeweza kuwa na mchezaji ambaye haheshimu mamlaka,nadhan kama ni kuondoka ni bora alivyoondoka tu.
Beckham aliyeshinda mara sita katika ligi ya Premier ya uingereza,vikombe viwili vya FA na moja katika Champions League akiwa na klabu hiyo baadaye aliuzwa kwa Real Madrid kwa dola million 25 katika msimu wa joto 2003, kabla ya kwenda nchini Marekani kuchezea klabu ya LA Galaxy.
Sir Alex Ferguson yeye amestaafu mwezi May mwaka huu umeneja katika klabu hiyo ya Manchester huku akiwa ni miongoni mwa mameneja walifikia mafanikio makubwa katika historia ya kuiongoza timu hiyo.
Axact

Post A Comment: