JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


OFISI YA RAIS SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Kumb. Na EA.7/96/01/E/34 17 Februari, 2014

                                       TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1).Pamoja na kazi zingine chombo hiki kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi ya Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 517 za kazi kwa waajiri mbalimbali kama ifuatavyo:



Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Katibu Tawala Mkoa Arusha, Katibu tawala Mkoa Pwani, Katibu tawala Mkoa Simiyu, Katibu tawala Mkoa Katavi, Katibu tawala Mkoa Iringa, Katibu tawala Mkoa Tabora, Katibu tawala Mkoa Kilimanjaro, Katibu tawala Mkoa Kagera, Katibu tawala Mkoa Rukwa na Katibu tawala Mkoa Njombe.

Waajiri wengine ni Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Arumeru, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Kiteto, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Karatu, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Kisarawe, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Rufiji, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Mafia, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Mkuranga, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Kondoa, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Chamwino, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Chemba, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Mufindi, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Njombe, Mkurugenzi Halmashauri ya

wilaya ya Makambako, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Mtwara, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Kilosa, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Tandahimba, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Nanyumbu, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Magu, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Kahama, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Maswa, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Kishapu na Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Msalala.

Nafasi hizi pia ni kwa ajili ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ushetu, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Busega, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Mkalama, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Igunga, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Sikonge, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Handeni, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Karagwe, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Muleba, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Kyerwa, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Kalambo, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Mlele, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Tunduru, Mkurugenzi Halmashauri Manispaa Arusha, Mkurugenzi Halmashauri Manispaa Musoma, Mkurugenzi Halmashauri Manispaa Morogoro na Mkurugenzi Halmashauri Manispaa Tabora.
MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.

i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania.

ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.

iv. Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe katika kichwa cha habari cha barua na juu ya bahasha, kutozingatiwa kwa sharti hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.



v. Waombaji wanatakiwa kuambatisha maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.

vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwawale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka kupotea.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.

- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI

- Computer Certificate

- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)

- Picha moja "Passport size" ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.



 
vii. "Transcripts", "Testmonials", "Provisional Results", "Statement of results", hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.



viii. Waombaji wawe na umri usiozidi miaka 45.

ix. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
x. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.

xi. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

xii. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 03 Machi, 2014

xiii. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.

xiv. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).



xv. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo.
xvi. Pamoja na waombaji kuainisha waajiri, Sekretarieti ya Ajira baada ya usaili itawapangia waombaji waliofaulu, kwa mwajiri yoyote bila kujali chaguo la mwombaji.Hii ni kutokana na baadhi ya waombaji kupendelea kufanya kazi kwenye baadhi ya maeneo tu.


Katibu, AU Secretary,

Sekretariati ya Ajira katika Public Service Recruitment

Utumishi wa Umma, Secretariat,

SLP.63100, P.O.Box 63100

Dar es Salaam. Dar es Salaam.

1.0 AFISA LISHE II (NUTRITION OFFICER II) – NAFASI 21

1.1 MAJUKUMU YA KAZI

Kukusanya taarifa na takwimu za lishe kutoka kwa wadau na makundi mbalimbali na kutoa ushauri kuhusu lishe bora katika ngazi ya wilaya.



 Kuchambua takwimu za lishe na kuandaa taarifa ya watoto na makundi mengine yenye lishe duni.

 Kushiriki katika kuandaa mipango na bajeti ya lishe katika ngazi ya wilaya.

 Kutoa taarifa za mara kwa mara za hali ya lishe katika ngazi ya wilaya.

 Kusimamia kazi za lishe katika wilaya

 Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.

 

1.2 SIFA ZA MWOMBAJI

 Kuajriwa wenye Shahada ya kwanza ya Lishe, Sayansi Kimu na Lishe au Sayansi na Chakula na Teknolojia ya Chakula (BSc – Nutrition, Home Economics and Nutrition, Food Science and Technology and Food Science) au Stashahada ya juu ya Lishe (Higher Diploma in Nutrition) kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
1.3 MSHAHARA


Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS D kwa mwezi


2.0 MSAIDIZI LISHE (NUTRITION ASSISTANT) – NAFASI 16

2.1 KAZI NA MAJUKUMU

Kutambua na kuorodhesha na kuweka kumbukumbu za watoto chini ya miaka mitano na makundi mengine yanayoathiriwa na lishe duni ngazi ya kijiji na kata.



 Kufuatilia na kutoa ushauri wa lishe kwa kaya zenye watoto wenye lishe duni.

 Kuelekeza watoto na makundi mengine yanayoathiriwa na lishe duni wapelekwe kwenye kituo cha afya Kwa huduma zaidi.

 Kupokea na kukusanya takwimu zinazohusu huduma za lishe zinazotolewa kwa makundi mbalimbali kwenye kata/kijiji.

 Kukusanya taarifa na takwimu za lishe katika sehemu yake ya kazi.
2.2 SIFA ZA MWOMBAJI




Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne/sita wenye cheti cha miaka miwili cha mafunzo ya lishe kutoka chuo kinachotambuliwa na serikali.
2.3 MSHAHARA


Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS A kwa mwezi


3.0 MLEZI WA WATOTO MSAIDIZI (CHILD CARE ASSISTANT)– NAFASI 12

3.1 KAZI NA MAJUKUMU

Kulea watoto katika vituo vya malezi ya awali ya watoto wadogo mchana.



 Kutoa mafunzo kwa akina mama juu ya malezi bora ya awali ya watoto wadogo wenye umri wa miaka 0-8.

 Kusaidia shughuli za kinga za magonjwa ya watoto vijijini/sehemu au eneo la vituo.

 Kuwa kiongozi wa kituo cha malezi ya awali ya watoto wadogo.
3.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliofaulu mafunzo ya mwaka mmoja ya malezi ya awali ya watoto wadogo wenye umri kati ya miaka 0-8 kutoka katika Chuo kinachotambulika na serikali au wenye cheti cha mwaka mmoja cha mafunzo ya ustawi wa jamii.


3.3 MSHAHARA


Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS B Kwa mwezi



4.0 AFISA USTAWI WA JAMII II (SOCIAL WELFARE OFFICER II)– NAFASI 184

4.1 KAZI NA MAJUKUMU

 Kuendesha usaili kwa wahudumiwa (watu wenye ulemavu, wazee, familia zenye matatizo, pamoja na watoto na vijana wenye matatizo mbalimbali).

 Kufanya ukaguzi wa mazingira wanayoishi wahudumiwa ili kupata taarifa zao kamili.

 Kuandaa taarifa za usaili na ukaguzi wa mazingira ya wahudumiwa.

 Kupokea na kukusanya taarifa za ustawi wa jamii kutoka kwa wadau na vituo mbalimbali vya ustawi wa jamii.

 Kupokea na kukusanya takwimu zinazohusu huduma za watu wenye ulemavu, wazee malezi ya watoto na familia zenye matatizo.

 Kupokea kuchambua na kuandaa orodha ya maombi ya uandikishaji wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana, malezi ambao (foster care) na vyuo vya malezi vya watoto wadogo mchana.

 Kupokea, kuchambua na kuandaa orodha ya maombi ya msaada wa Rais kutoka kwa akina mama waliojifungua watoto watatu au zaidi kwa mara moja.

 Kupokea, kuchambua na kuandaa orodha ya maombi ya watoto yatima au wanaohitaji misaada mbalimbali.

 Kupokea, kuchambua na kuandaa orodha ya maombi mbalimbali kutoka kwenye familia na watu wenye dhiki.

 Kuhoji na kuandaa taarifa za washtakiwa.

 Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.
4.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wenye shahada ya B.A (social work or sociology) au stashada ya juu ya Ustawi wa jamii (Advanced Diploma in Sociol work) kutoka chuo cha juu kinachotambuliwa na ustawii wa jamii.


4.3 MSHAHARA


Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS D kwa mwezi.


5.0 MSAIDIZI USTAWI WA JAMII DARAJA LA II (SOCIAL WELFARE ASSISTANT II) – NAFASI 24

5.1 MAJUKUMU YA KAZI

Kutambua na kuhudumia watu walio katika makundi maalum na mazingira hatarishi.

Kukusanya takwimu zinazohusu watu walio katika makundi maalum na mazingira hatarishi.

Kuchambua na kuandaa orodha ya maombi mbalimbali kutoka kwenye familia na watu wenye dhiki.

Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.



 

5.2 SIFA ZA MWOMBAJI

 Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne au sita wenye cheti cha mafunzo ya mwaka mmoja ya Ustawi wa Jamii kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali
5.3 MSHAHARA


Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS C kwa mwezi.


6.0 MHUDUMU WA JIKONI/MESS DARAJA LA II (KITCHEN/MESS ATTENDANT) – NAFASI 4

6.1 MAJUKUMU YA KAZI

Kusafisha Vyombo vya kupikia.



 Kusafisha Vyombo vya kulia chakula.

 Kusafisha Meza itumiwayo kwa kulia chakula.

 Kuwatayarishia Wapishi/Waandazi vifaa vya Mpishi na Mezani.

 Kusafisha maeneo ya kulia chakula na kupikia.

 Kuwasaidia Waandazi na Wapishi.
6.2 SIFA ZA MWOMBAJI




Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Nne.
6.3 MSHAHARA.


Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGOS.A kwa mwezi.


7.0 AFISA MISITU DARAJA LA II (FORESTRY OFFICER GRADE II) – NAFASI 6

7.1 MAJUKUMU YA KAZI

Kusimamia upandaji na uhudumiaji wa miti na misitu.



 Kusimamia uendelezaji wa misitu ya kupandwa isiyozidi hekta 5,000 au ya asili isiyozidi hekta 10,000.

 Kufanya utafiti wa misitu.

 Kutekeleza Sera na Sheria za misitu.

 Kuendesha mafunzo ya Wasaidizi Misitu.

 Kukusanya takwimu za misitu.

 Kufanya ukaguzi wa misitu.

 Kupanga na kupima madaraja ya mbao.

 Kudhibiti leseni na uvunaji wa miti.

 Kutoa ushauri na mafunzo kwa wananchi juu ya uendelezaji na matumizi endelevu ya miti kwa wananchi.

 Kufanya ukadiriaji wa rasilimali za misitu.

 Kupima maeneo na kuchora ramani za misitu.
7.2 SIFA ZA MWOMBAJI


 

Kuajiriwa wenye Shahada ya Misitu kutoka chuo Kikuu cha kilimo cha Sokoine au Vyuo Vikuu vingine vinavyotambuliwa na Serikali.


7.3 MSHAHARA


Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.D kwa mwezi.


8.0 MSAIDIZI MISITU DARAJA LA II (FORESTRY ASSISTANT GRADE II) – NAFASI 75

8.1 MAJUKUMU YA KAZI

Kukusanya mbegu



 Kuhudumia na kutunza bustani za miti.

 Kutunza na kuhudumia miti na misitu.

 Kufanya doria.

 Kusimamia ukusanyaji mbegu na bustani za miti.

 Kukusanya takwimu za misitu.

 Kusimamia kazi za upandaji, utunzaji na uvunaji wa miti/misitu.

 Kukusanya maduhuli.

 Kupima mazao ya misitu.

 Kufanya doria.
8.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Nne au Sita wenye Astashahada (Cheti) au Stashahada (Diploma) ya Misitu kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.


8.3 MSHAHARA


Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B/C kwa mwezi.


9.0 MKUFUNZI KILIMO DARAJA LA II (AGRICULTURE GENERAL) – NAFASI 10

9.1 KAZI NA MAJUKUMU

Kusoma na kuelewa vema mihutasari ya mafunzo na kuitafsiri kwenye masomo.



 Kuandaa mtiririko na mpangilio wa masomo (lesson sequences and plans) kwa upande wa nadharia na vitendo.

 Kufundisha kozi za Stashahada na Astashahada nadharia na vitendo.

 Kuandaana kufundisha kozi za Wakulima.

 Kuandaa na kupanga somo la vitendo na kusimamia wanachuo wakati wa kujifunza.

 Kupima maendeleo ya wanachuo kwenye mitihani kwa kipindi chote kinachohusika na kutunza alama zao.

 Kupima maendeleo ya wanachuo kwa kushirikiana na Maofisa Kilimo wa Wilaya/Viwandani wakati wa mafunzo kwa vitendo (Field Practical).

 

 Kutekeleza shughuli nyingine za kikazi kadri atakavyopangiwa na Mkuu wake wa kazi.
9.2 SIFA ZA KUINGILIA MOJA KWA MOJA

Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza ya Kilimo (Bachelor of Science Agriculture General) kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali, waliohitimu kozi ya mbinu bora za kufundishia (Teaching Methodology)


9.3 MSHAHARA


Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.D kwa mwezi


10.0 MKUFUNZI KILIMO DARAJA LA II (AGRONOMY) – NAFASI 4

10.1 KAZI NA MAJUKUMU

Kusoma na kuelewa vema mihutasari ya mafunzo na kuitafsiri kwenye masomo.



 Kuandaa mtiririko na mpangilio wa masomo (lesson sequences and plans) kwa upande wa nadharia na vitendo.

 Kufundisha kozi za Stashahada na Astashahada nadharia na vitendo.

 Kuandaana kufundisha kozi za Wakulima.

 Kuandaa na kupanga somo la vitendo na kusimamia wanachuo wakati wa kujifunza.

 Kupima maendeleo ya wanachuo kwenye mitihani kwa kipindi chote kinachohusika na kutunza alama zao.

 Kupima maendeleo ya wanachuo kwa kushirikiana na Maofisa Kilimo wa Wilaya/Viwandani wakati wa mafunzo kwa vitendo (Field Practical).

 Kutekeleza shughuli nyingine za kikazi kadri atakavyopangiwa na Mkuu wake wa kazi.
10.2 SIFA ZA KUINGILIA MOJA KWA MOJA

Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza ya Kilimo (Bachelor of Science Agronomy) kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali, waliohitimu kozi ya mbinu bora za kufundishia (Teaching Methodology)


10.3 MSHAHARA


Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.D kwa mwezi.


11.0 MKUFUNZI KILIMO DARAJA LA II (HORTICULTURE) – NAFASI 1

11.1 KAZI NA MAJUKUMU

Kusoma na kuelewa vema mihutasari ya mafunzo na kuitafsiri kwenye masomo.



 Kuandaa mtiririko na mpangilio wa masomo (lesson sequences and plans) kwa upande wa nadharia na vitendo.

 

 Kufundisha kozi za Stashahada na Astashahada nadharia na vitendo.

 Kuandaana kufundisha kozi za Wakulima.

 Kuandaa na kupanga somo la vitendo na kusimamia wanachuo wakati wa kujifunza.

 Kupima maendeleo ya wanachuo kwenye mitihani kwa kipindi chote kinachohusika na kutunza alama zao.

 Kupima maendeleo ya wanachuo kwa kushirikiana na Maofisa Kilimo wa Wilaya/Viwandani wakati wa mafunzo kwa vitendo (Field Practical).

 Kutekeleza shughuli nyingine za kikazi kadri atakavyopangiwa na Mkuu wake wa kazi.
11.2 SIFA ZA KUINGILIA MOJA KWA MOJA

Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza ya Kilimo (Bachelor of Horticulture) kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali, waliohitimu kozi ya mbinu bora za kufundishia (Teaching Methodology)


11.3 MSHAHARA


Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.D kwa mwezi.


12.0 MKUFUNZI KILIMO DARAJA LA II (HUMAN NUTRITION) – NAFASI 1

12.1 KAZI NA MAJUKUMU

Kusoma na kuelewa vema mihutasari ya mafunzo na kuitafsiri kwenye masomo.



 Kuandaa mtiririko na mpangilio wa masomo (lesson sequences and plans) kwa upande wa nadharia na vitendo.

 Kufundisha kozi za Stashahada na Astashahada nadharia na vitendo.

 Kuandaana kufundisha kozi za Wakulima.

 Kuandaa na kupanga somo la vitendo na kusimamia wanachuo wakati wa kujifunza.

 Kupima maendeleo ya wanachuo kwenye mitihani kwa kipindi chote kinachohusika na kutunza alama zao.

 Kupima maendeleo ya wanachuo kwa kushirikiana na Maofisa Kilimo wa Wilaya/Viwandani wakati wa mafunzo kwa vitendo (Field Practical).

 Kutekeleza shughuli nyingine za kikazi kadri atakavyopangiwa na Mkuu wake wa kazi.
12.2 SIFA ZA KUINGILIA MOJA KWA MOJA

Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza ya Kilimo (Bachelor of Human Nutrition) kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali, waliohitimu kozi ya mbinu bora za kufundishia (Teaching Methodology)


12.3 MSHAHARA


Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.D kwa mwezi.


13.0 AFISA KILIMO DARAJA LA II (AGRO – OFFICERS) – NAFASI 71 (LINARUDIWA) KWA WALE WOTE WALIOOMBA TANGAZO LA TAREHE 27 NOVEMBA 2013 WASIRUDIE KUOMBA KWA KUWA MAOMBI YAO BADO YANACHAMBULIWA.


13.1 MAJUKUMU YA KAZI


 Kuthibiti visumbufu vya mazao na mimea,

 Kukusanya takwimu za bei za mazao kila wiki na kila mwezi,

 Kukusanya takwimu za upatikanaji wa mazao katika masoko kila wiki/kila mwezi,

 Kuendesha mafunzo ya wataalam wa kilimo,

 Kufanya ukaguzi wa ubora na matumizi ya pembejeo na zana,

 Ufuatiliaji wa mwenendo wa soko la mazao ya biashara,

 Kuendesha mafunzo juu ya hifadhi bora ya udongo na maji,

 Kutoa habari juu ya teknolojia mpya kwa wadau,

 Kuandaa/kuandika taarifa za utekelezaji kwa sekta ndogo ya mazao,

Kusimamia/kuendeleza taaluma ya uzalishaji mboga, matunda, maua na mazao mengine,



 Kusimamia/kuendeleza uzalishaji wa mbegu bora,

 Kuandaa, kutayarisha kufunga na kusambaza mbegu bora,

 Kufanya majaribio ya magonjwa kwenye mbegu,

 Kufanya ukaguzi wa mbegu mpya kwa kushirikiana na watafiti wa mbegu kabla ya kupitishwa,

 Kuendesha mafunzo ya kuzalisha mboga, matunda, maua na viungo,

 Kuhamasisha uzalishaji wa mazao ya bustani,

 Kufanya utafiti mdogo wa mazao yanayofaa kulimwa katika sehemu ya kilimo cha umwagiliaji,

 Kufanya utafiti wa udongo,

 Kuhamasisha uanzishaji wa vikundi vya wakulima/wamwagiliaji,

 Kuzalisha mbegu za msingi baada ya kuzalishwa na watafiti,

 Kuendesha/kusimamaia vishamba vya majaribio vya mbegu na uchunguzi maabara ili kuondoa utata juu ya mbegu.
13.2 SIFA ZA MWOMBAJI

 Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza (bachelor degree) ya kilimo au shahada ya sayansi waliojiimarisha katika mchepuo wa kilimo kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.


13.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS D Kwa mwezi.



 

14.0 MHANDISI KILIMO DARAJA LA II (AGRO – ENGINEERS) – NAFASI 38 (LINARUDIWA) KWA WALE WOTE WALIOOMBA TANGAZO LA TAREHE 27 NOVEMBA 2013 WASIRUDIE KUOMBA KWA KUWA MAOMBI YAO BADO YANACHAMBULIWA.

14.1 MAJUKUMU YA KAZI

 Kuandaa program za mafunzo kwa wakulima kutumia zana za kilimo,

 Kushiriki katika kufundisha wakulima na matumizi bora ya zana,

 Kushiriki kutengeneza michoro/ramani za umwagiliaji,

 Kushiriki katika ujenzi wa miradi ya umwagiliaji,

 Kushirikiana na mafundi sanifu kuwafunindisha wakulima uendeshaji wa skimu za umwagiliaji,

 Kukusanya takwimu za miradi ya umwagiliaji,

 Kushiriki kuratibu na kutoa huduma za umwagiliaji kwa vikundi vya umwagiliaji pamoja na matumizi ya maji,

 Kuandaa mafunzo/maonyesho ya matumizi ya za za kilimo,

 Kufuatilia program za mafunzo ya wanyama kazi, mafundi wa matrekta na wakulima jinsi ya matumizi ya wanyama na matrekta,

 Kuwafundisha wakulima ujenzi wa vihengo bora na

 Kushughulikia ubora wa zana na kuwashauri waagizaji na watengenezaji ipasavyo.
14.2 SIFA ZA MWOMBAJI

 Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza (Bachelor Degree) ya uhandisi yenye mwelekeo mkubwa katika fani ya Kilimo cha umwagiliaji na cha zana kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali.


14.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS E Kwa mwezi.


15.0 MUUNDA BOTI DARAJA II (BOAT BUILDER II) – NAFASI 2 (LINARUDIWA)



KWA WALE WOTE WALIOOMBA TANGAZO LA TAREHE 27 NOVEMBA 2013 WASIRUDIE KUOMBA KWA KUWA MAOMBI YAO BADO YANACHAMBULIWA.

15.1 MAJUKUMU YA KAZI

 Kusaidia kuunda boti za uvuvi

 Kuwashauri wavuvi juu ya utunzaji na matumizi ya boti

 Kufanya matengenezo ya boti.

 Kusaidia kutafsiri/kusoma michoro ya kiufundi ya boti.

 Kuandaa vifaa kwa ajili ya ujenzi wa boti.

15.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wenye stashahadaya Uundaji boti kutoka chuo cha Mbegani au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.



 

15.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS C kwa mwezi


16.0 DEREVA WA VIVUKO DARAJA LA II (FERRY / BOAT OPERATOR) – NAFASI 1 (LINARUDIWA) KWA WALE WOTE WALIOOMBA TANGAZO LA TAREHE 27 NOVEMBA 2013 WASIRUDIE KUOMBA KWA KUWA MAOMBI YAO BADO YANACHAMBULIWA.



MAJUKUMU YA KAZI

 Kufunga na kufungua kamba za kivuko.

 Kuchunga usalama wa abiria na magari yaliyomo ndani ya kivuko.

 Kupanga abiria au magari kwenye kivuko.

 Kuendesha na kuongoza kivuko.

 Kutunza daftari za safari ya kivuko.

 Kuhakikisha kwamba injini za kivuko zipo katika hali nzuri ya kufanya kazi.

 Kuangalia mafuta na vyombo vingine vya kufanyia kazi.

16.1 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa waliohitimu Mtihani wa Kidato cha IV, wenye Ujuzi wa kuendesha na kutunza Mashua/Kivuko uliothibitishwa na Chuo cha Dar es Salaam Marine Institute au Chuo kingine chochote kinachotambuliwa na Serikali kwa muda usiopungua miaka miwili; na waliofuzu mafunzo ya miezi sita ya uokoaji wa maisha majini, kuogelea na kupanga watu na magari kwenye mashua/vivuko.


16.2 MSHAHARA

Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGOS.A kwa mwezi.


17.0 AFISA MIFUGO DARAJA LA II (LIVE STOCK OFFICER II) – NAFASI 8



(LINARUDIWA). KWA WALE WOTE WALIOOMBA TANGAZO LA TAREHE 27 NOVEMBA 2013 WASIRUDIE KUOMBA KWA KUWA MAOMBI YAO BADO YANACHAMBULIWA.

17.1 MAJUKUMU YA KAZI

 Atabuni mipango ya uzalishaji mifugo wilayani.

 Ataratibu uzalishaji wa mifugo katika mashamba makubwa ya mifugo.

 Atasaidia kuratibu mipango ya ugani kuhusiana na uzalishaji wa mifugo wilayani.

Ataratibu na kuendesha mafunzo ya ufugaji bora, usindikaji wa mazao ya mifugo kwa wataam wa mifugo na wafugaji.



 

 Atafanya mapitio na marekebisho ya miundo ya masoko ya mifugo wilayani kwake na mkoani.

 Atabuni, kuanzisha na kutekeleza miradi ya maendeleo ya mifugo wilayani.

 Atafanya soroveya ya rasilimali (resource survey) kama vile mifugo, vyakula vya mifugo, malisho n.k. katika eneo lake la kazi.

 Ataendesha mafunzo kwa Mawakala, wauzaji na wataalam juu ya njia salama katika kuweka na kusambaza pembejeo za mifugo.

 Atatafiti maeneo mapya yanayofaa kwa ufugaji wa mifugo mbalimbali

 Atafanya utafiti juu ya uharibifu wa mazingira katika wilaya.

 Atashiriki katika shughuli za kudhibiti milipuko ya wanyama/viumbe waharibifu wa malisho.

 Ataandaa taarifa ya jumla juu ya maendeleo ya mifugo.

 Atafuatilia, kuweka, kuchambua na kutafsiri takwimu za uzalishaji wa mifugo.

 Atafanya kazi nyingine zinazohusiana na fani yake kama atakavyoelekezwa na mkuu wake wa kazi.
17.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza (bachelor degree) ya sayansi ya Mifugo(Animal Science) kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali au sifa inayolingana nayo.


17.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS D kwa mwezi


18.0 MHASIBU MSAIDIZI (ASSISTANT ACCOUNTANT) - NAFASI 3

18.1 MAJUKUMU YA KAZI

Kupokea na kulipa fedha.



 Kutunza daftari ya fedha.

 Kufanya usuluhisho wa hesabu za benki

 Kukagua hati za malipo.

 Kupitisha malipo kulingana na kanuni za fedha.

 Kusimamia kazi za wasaidizi wa hesabu.
18.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wenye Cheti cha kufaulu mtihani mgumu wa Uhasibu Serikalini (Higher Standard Government Accountancy Examination) unaotolewa na Tume ya Utumishi wa Umma. Au



 Kuajiriwa wenye Stashahada ya kawaida ya uhasibu kutoka Chuo/Taasisi yoyyote inayotambuliwa na serikali.

 

18.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.C kwa mwezi


19.0 AFISA USHIRIKA DARAJA LA II (COOPERATIVE OFFICER GRADE II) – NAFASI 1

19.1 MAJUKUMU YA KAZI

Kukagua vyama vya Ushirika vya Msingi vinavyoendesha miradi ya pamoja ( Jointy Venture )



 Kuhamasisha uanzishaji wa vyama vya Ushirika vya Msingi.

 Kukusanya na kuchambua takwimu zinazohusu Masoko katika Mkoa.

 Kutoa ushauri juu ya uendeshaji wa Vyama vya Ushirika vya Msingi

 Kuratibu/kushiriki katika Elimu ya Ushirika Shirikishi katika vyama vya ushirika vya Msingi.
19.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza au Stashahada ya Juu (Advanced Diploma) katika fani ya Ushirika (Cooperative management and accounting) kutoka vyuo vinavyotambulika na Serikali.


19.3 MSHAHARA


Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.


20.0 AFISA UGAVI DARAJA LA II (SUPPLIES OFFICER GRADE II) – NAFASI 1

20.1 MAJUKUMU YA KAZI

Kukusanya takwimu za kusaidia kutayarishwa makisio ya vifaa vinavyohitajika (Material Requirement Budget) na Mpango wa Ununuzi (Procurement Plan).



 Kukusanya na kutunza takwimu za utendaji za Wazabuni mbalimbali.

 Kukusanya na kutunza takwimu za upokeaji, utunzaji, na usambazaji wa vifaa.

 Kusimamia utunzaji wa maghala na hati/kumbukumbu ya vifaa vilivyomo ghalani.

 Kusimamia upokeaji, utunzaji na usambazaji wa vifaa (Physical Distribution).

 Mfumo wa uwekaji na utunzaji wa vifaa ghalani (Location Index Design).

 Kusimamia ukaguzi wa kuhesabu vifaa mara kwa mara (Perpetual Stock Checking) ghalani.

 Kutayarisha Taarifa za kazi katika vipindi maalumu.

 Kuhesabu na kutoa taarifa ya thamani ya vifaa vilivyomo ghalani kila mwisho wa mwaka (Annual Stock Taking).

 Kufanya kazi zingine ambazo atapangiwa.
20.2 SIFA ZA MWOMBAJI



 

Kuajiriwa wenye Shahada ya Biashara (B.Comm) yenye mchepuo wa ugavi au Stashahada ya Juu ya Ugavi (Advanced Diploma in Materials Management) inayotolewa na Chuo kinachotambuliwa na Bodi ya Taifa ya usimamizi wa Vifaa.


20.3 MSHAHARA


Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D mwezi.


21.0 AFISA UGAVI MSAIDIZI II (ASSISTANT SUPPLIES OFFICER) – NAFASI 1

21.1 MAJUKUMU YA KAZI

Kutunza ghala la vifaa lenye thamani ndogo.



 Kupokea vifaa vipya vitakavyoletwa na wazabuni mbalimbli na kupokea vifaa ambavyo vimetumika lakini vinahitaji kutunzwa kabla ya kufutwa.

 Kufungua na kutunza "Bin Card" kwa kila kifaa kilichopo ghalani.

 Kufungua "Ledger" ambayo itatunza kumbukumbu ya vifaa vinavyoingia, kutunzwa na kutoka kwa nyaraka mbalimbali.

 Kutoa vifaa kwa wateja na watumiaji wengine.

 Kuhakikisha kwamba ghala na vifaa vilivyomo vinatunzwa katika hali ya usafi na kwa usalama.

 Kuandaa hati za kupokelea vifaa.

 Kufanya kazi zingine atakazopangiwa.
21.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wenye cheti cha "National Store-Keeping Certificate au "Foundation Certificate" kitolewacho na Bodi ya Taifa ya Usimamizi wa Vifaa au wenye Cheti kinachotambuliwa na Bodi ya Taifa ya Usimamizi wa Vifaa.


AU

Kuajiriwa wenye Diploma ya Kawaida "Ordinary Diploma in Materials Management" kutoka Chuo kinachotambuliwa na Bodi ya Taifa ya Usimamizi wa Vifaa.


21.3 MSHAHARA


Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.A na B kwa mwezi.


22.0 AFISA UTAMADUNI II (CULTURAL OFFICER GRRADE II) – NAFASI 1

22.1 MAJUKUMU YA KAZI

Kutafiti masuala ya Lugha, Sanaa, Mila na Desturi katika ngazi ya Wilaya.



 Kufundisha fani mbalimbali za utamaduni katika Vyuo na Vituo vya Elimu na mafunzo ya utamaduni.

 Kazi nyingine atakazopangiwa na Mkuu wa kituo.
22.2 SIFA ZA MWOMBAJI



Kuajiriwa wenye shahada au stashahada ya juu katika Sanaa, Lugha au Sayansi ya Jamii na uzoefu wa kazi usiopungua miaka mitatu.
22.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.


23.0 AFISA MAENDELEO YA VIJANA DARAJA LA II (YOUTH DEVELOPMENT OFFICER GRADE II) – NAFASI 1

23.1 MAJUKUMU YA KAZI

Kuratibu na kisimamia utekelezaji wa Sera ya Vijana



 Kuratibu shughuli za mikopo/mifuko ya Vijana

 Kuhamasisha vijana ili kufufua moyo wa kujitolea nchini

 Kupanga na kuendesha mafunzo yanayohusu stadi za maisha, stadi za kazi na Afya ya Vijana

 Kuanzisha vituo vya ushauri nasaha, Ajira kwa Vijana na Elimu ya Familia kwa kushirikiana na vyama visivyo vya kiserikali (NGO)

 Kukusanya takwimu mbalimbali zinazohusu Vijana

 Kuratibu shughuli mbalimbali za NGO zinazoshughulikia masuala ya Vijana

 Kuandaa mipango ya kuboresha malezi ya Vijana

 Kuwahamasisha Waajiri na Wafadhili mbalimbali wachangie mfuko wa mikopo nafuu kwa Vijana katika maeneo mbalimbali

 Kukuza na kuendeleza vipaji mbalimbali walivyonavyo Vijana ili kuwawezesha kujiajiri

 Kuandaa mipango ya kuwahamasisha Vijana ili kuanzisha miradi midogomidogo ya kujiajiri.
23.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza (BA. in Sociology or Social Sciences) au Stashahada ya Juu ya Maendeleo ya Jamii au Ustawi wa Jamii au Maendeleo ya Vijana (Advanced Diploma in Social Works or Community Development or Youth Development) kutoka chuo kinachotambuliwa na Serkali.

23.3 MSHAHARA



Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
24.0 AFISA UFUGAJI NYUKI DARAJA LA II (BEEKEEPING OFFICER GRADE II) – NAFASI 1

24.1 MAJUKUMU YA KAZI

Kusimamia uanzishaji wa hifadhi za nyuki na manzuki.



 Kutangaza Sera na Sheria za ufugaji nyuki.

 

 Kufundisha masomo ya fani ya ufugaji nyuki.

 Kukusanya takwimu za rasilimali na ufugaji nyuki.

 Kupanga na kupima ubora wa mazao ya nyuki.
24.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wenye Shahada katika fani ya Ufugaji Nyuki au Sayansi ya Elimu ya Mimea, Elimu ya Wadudu au Elimu ya Wanyama kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.


24.3 MSHAHARA




Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.D kwa mwezi
25.0 AFISA ARDHI DARAJA LA II (LAND OFFICER GRADE II) – NAFASI 1

25.1 MAJUKUMU YA KAZI

Kusimamia uingizaji wa kumbukumbu katika kompyuta.



 Kushughulikia utayarishaji wa nyaraka za kisheria.

 Kufanya ukaguzi wa viwanja.

 Kutoa notisi na kupendekeza ubatilishaji wa miliki kwa visivyoendelezwa kwa mujibu wa sheria.

 Kuwasiliana na wateja kuhusu Hati zilizotayarishwa na kuwakabidhi.
25.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wenye Shahada/Stashahada ya juu katika fani ya Usimamizi ardhi na Uthamini au Shahada ya Sheria kutoka Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na Serikali wenye uzoefu wa kazi kwa muda usiopungua miaka mitano.


25.3 MSHAHARA


Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.E kwa mwezi


26.0 FUNDI SANIFU DARAJA LA II - KOMPYUTA (COMPUTER TECHNICIAN GRADE II) – NAFASI 1

26.1 MAJUKUMU YA KAZI

Kufanya kazi atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi


26.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Waliohitimu kidato cha VI na kufuzu mafunzo ya ufundi ya miaka miwili kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali katika fani yenye muelekeo wa kompyuta



 Waliohitimu kidato cha IV na kufuzu kozi ya ufundi ya miaka mitatu kutoka Vyuo vya Ufundi vinavyotambuliwa na Serikali katika fani ya kompyuta

 Wenye Cheti cha Majaribio ya Ufundi hatua ya I kutoka Chuo cha Ufundi kinachotambuliwa na Serikali,

 

 Wenye Stashahada ya Kawaida katika fani yenye muelekeo wa kompyuta katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
26.3 MSHAHARA




Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi
27.0 AFISA BIASHARA DARAJA LA II (TRADE OFFICER GRADE II) – NAFASI 1

27.1 MAJUKUMU YA KAZI

Kuwasiliana na Wizara nyingine ambazo zinafanya biashara, kupata takwimu ambazo zitatumika katika kutathimini mwenendo wa biashara na masuala mengine ya kibiashara.



 Kusambaza taarifa za kibiashara kwa wafanyabiashara.

 Kutathmini mwenendo wa biashara kwa kuangalia hali ya masoko katika nchi mbalimbali ambazo bidhaa zetu zinauzwa.

 Kuandaa grafu na "chart" ambazo zinaonyesha, mwenendo wa bidhaa zinazoingizwa nchini na zile ziendazo nje kwa kila nchi ambazo hufanya biashara na Tanzania.
27.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa mwenye Shahada/Stashahada ya Juu ya Biashara waliojiimarisha katika fani ya Uchumi, Masoko, Uendeshaji Biashara au inayolingana nayo kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salam au chuo kingine chochote kinachotambuliwa na Serikali.


27.3 MSHAHARA


Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.


28.0 MSAIDIZI WA HESABU (ACCOUNTS ASSISTANT) - NAFASI 1

28.1 MAJUKUMU YA KAZI

Kuandika na kutunza "register" zinazohusu shughuli za uhasibu.



 Kuandika hati za malipo na hati za mapokezi ya fedha.

 Kutunza majalada yenye kumbukumbu za hesabu

 Kupeleka barua/nyaraka za uhasibu Benki.

 Kufanya usuluhisho wa masurufu, karadha, Hesabu za Benki na Amana.
28.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wenye Cheti cha ATEC level II au "Foundation Level" kinachotolewa na NBAA


28.3 MSHAHARA


Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.B kwa mwezi


29.0 AFISA USIMAMIZI WA FEDHA DARAJA LA II (FINANCE MANAGEMENT OFFICER II) - NAFASI 1

29.1 MAJUKUMU YA KAZI

Kuandikisha na kudhibiti Amana (Securities) za Serikali.



 Kufuatilia hati za hisa.

 Kuwasiliana na watoaji mikopo/misaada kuhusu maendeleo ya utekelezaji wa miradi.

 Kuweka kumbukumbu za madeni ya nje.

 Kuweka kumbukumbu za mikopo ya ndani.

 Kufuatilia na kusimamia matayarisho ya makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali.

 Kufuatilia utayarishaji na uchambuzi wa "Flash Reports" za kila mwezi.
29.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wenye Shahada ya Sanaa yenye mwelekeo mkubwa katika fani ya Uchumi na Mipango (Major in Economics) au Biashara au Sheria (LL.B) au Stashahada ya Juu ya Uhasibu au Uchumi & Mipango au Biashara au Stashahada ya juu ya Usimamizi wa kodi kutoka Chuo/Taasisi inayotambuliwa na Serikali.



 Waombaji wenye Cheti cha Taaluma ya Uhasibu CPA (T) au sifa nyingine inayolingana na hiyo inayotambuliwa na NBAA watafikiriwa kwanza.
29.3 MSHAHARA


Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.D kwa mwezi


30.0 AFISA TARAFA – NAFASI 6

30.1 MAJUKUMU YA KAZI



(i) Kwenye Mamlaka ya Serikali Kuu.

Kumwakilisha na kumsaidia Mkuu wa Wilaya katika utekelezaji wa shughuli za Serikali Kuu katika Tarafa.



 Kuandaa na kuratibu taarifa na ripoti zinazohusu masuala ya ulinzi na usalama ya kata kwenye tarafa yake na kuiwasilisha kwa Mkuu wa Wilaya.

 Kuhamasisha na kuhimiza wananchi iliwashiriki kwenye shughuli za maendeleo kwenye Tarafa.

 Kuwa kiungo kati ya Serikali kuu na Wananchi Katika Tarafa.

 Kuwa mlinzi wa amani katika eneo lake.

 Kufuatilia na kuhimiza utekelezaji wa sera za Serikali katika eneo lake na kuhakikisha kuwa zinatekelezwa ipasavyo.

 Kuratibu shughuli zote za maafa na dharura mbalimbali katika eneo lake

 Kuandaa taarifa zote zinazohusu masuala ya Serikali Kuu kuhusu utendaji wa kazi za maafisa Watendaji wa kata wa eneo lake na kuziwasilisha kwa Mkuu wa Wilaya.

 

 Kuwa kiungo kati ya Serikali kuu na Serikali za Mitaa. katika eneo lake.

 Kufanya kazi zingine atakazopangiwa na Katibu Tawala wa Wilaya.
(ii) Kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa;

Kuwasaidia Wakurugenzi wa Serikali za Mitaa katika shughuli za Maendeleo katika eneo lake



 Kusimamia utendaji wa shughuli za Maafisa Watendaji wa Vijiji, Kata na Mitaa.

 Kushiriki na kutoa ushauri katika upangaji wa mipango ya Maendeleo katika eneo lake

 Kuhudhuria vikao vya kamati za Halmashauri na Baraza la madiwani na kutoa ushauri.

 Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake kama zitakavyopokelewa kutoka kwa Watendaji wa Kata.

 Kusimamia utekelezaji wa Sheria ndogondogo za Halmashauri ya Wilaya, Miji, Manispaa au Jiji.
30.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wenye Shahada/Stashahada ya juu katika mojawapo ya fani za Sheria,Menejimenti,Utawala,Sayansi ya Jamii, Kilimo, Mifugo,Ushirika, Mazingira, au Maji kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.


30.3 MSHAHARA


Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS D kwa mwezi.


31.0 AFISA MICHEZO DARAJA LA II (GAMES AND SPORTS OFFICER GRADE II) – NAFASI 1

31.1 MAJUKUMU YA KAZI

Kufundisha fani mbalimbali kwa Waalimu wa vyuo, shule, na vituo vya Elimu na Mafunzo



 Kufundisha fani mbalimbali za michezo kwa waalimu, Makocha, viongozi wa vyama na vilabu vya michezo

 Kufundisha fani mbalimbali za michezo kwa Timu za Michezo mbalimbali.
31.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa mwenye Shahada au Stashahada ya Juu ya Elimu ya Michezo (Physical Education) kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.


31.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS D kwa mwezi.


32.0 FUNDI SANIFU DARAJA II – RAMANI (TECHNICIAN GRADE II - (MAPPING) – NAFASI 1

32.1 MAJUKUMU YA KAZI


 

Kushughulikia madaai/malalamiko ya hati za viwanja, kuweka na kutunza kumbukumbu zake



 Kutunza kumbukumbu za "cadastrals surveys" na mahesabu yake

 Kuandaa nakala za "cadastral site plans"

 Kutunza miongozo ya ramani (maping guides) na viwanja
32.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wenye wahitimu wa kidato cha nne au sita wenye cheti cha mafunzo ya ufundi ya miaka miwili katika fani ya Ramani (Mapping)

32.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi.


33.0 FUNDI SANIFU DARAJA II- URASIMU RAMANI (CARTOGRAPHY) – NAFASI 1

33.1 MAJUKUMU YA KAZI

Kufanya maandalizi ya Uchoraji wa ramani za miji kadiri ya uwiano unaohitajika



 Kutunza kumbukumbu za ramani na plan

 Kuchora plani za hati miliki, upimaji, mashamba na vijiji

 Kutoa nakala za plani za hati za viwanja, mashamba na vijiji
33.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne au cha sita wenye cheti cha mafunzo ya ufundi ya miaka miwili au Stashahada katika fani ya Urasimu Ramani (Cartography) kutoka kwenye vyuo vinavyotambuliwa na serikali.


33.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi


34.0 FUNDI SANIFU DARAJA LA II - MAJI - (TECHNICIAN GRADE II - WATER) – NAFASI 1

34.1 MAJUKUMU YA KAZI

Ukusanyaji na ukaguaji wa takwimu za maji



 Kutunza takwimu za maji

 Kuingiza takwimu za maji kwenye fomu Na: H: 12 tayari kwa kutumiwa kwenye michoro

 Kuchora hydrograph za maji

 Utengenezaji visima vya rekoda, stendi za winchi, sinia za maji ‘cable way post" n.k.

 Kufanya matengenezo ya vifaa vyote vya kupimia maji na hali ya hewa

 Kuingiza takwimu kwenye kompyuta

 

 Kufundisha wasoma vipimo
34.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa Wahitimu wa vyuo vya ufundi vinavyotambuliwa na Serikali ambao wana cheti cha ufundi ( FTC) au Stashahada ya Rasilimali za Maji na wenye ujuzi wa kutumia kompyuta.

34.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi


35.0 AFISA WANYAMAPORI DARAJA LA II – NAFASI 1

35.1 MAJUKUMU YA KAZI

Kutekeleza Kazi za Ushirikishaji Wadau Katika Uhifadhi.



 Kudhibiti Utoaji wa Leseni za Biashara Za Nyara na Vibari vya Kukamata Wanyama Hai.

 Kushiriki Katika Kusuluhisha Migogoro ya Matumizi ya Wanyamapori

 Kudhibiti Matumizi Haramu ya Leseni za Uwindaji na Kuhahakikisha Kufuatwa Kwa Maadili Katika Kutumia Wanyamapori.

 Kuthibiti Matumizi Haramu ya Wanyamapori.

 Kufuatilia Utekelezaji wa Miongozo Mbalimbali ya Uhifadhi Wanyamapori.

 Kuhakiki Viwango vya Kukamata Wanyama Hai Kwa Ajili ya Biashara na Ufugaji.

 Kufanya Kazi za Kuzuia Ujangili.

 Kukusanya Taarifa, na Takwimu za Uhifadhi.

 Kutekeleza Kazi za Uhifadhi Katika Mapori ya Akiba.
35.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa Wenye Shahada ya Sayansi ya Wanyamapori Kutoka Chuo Kikuu Kinachotambuliwa na Serikali.

35.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi


36.0 AFISA WA SHERIA DARAJA LA II (LEGAL OFFICER GRADE II) – NAFASI 2

36.1 MAJUKUMU YA KAZI



Hili ni daraja la mafunzo katika kazi, hivyo Maafisa wa Sheria katika daraja hili watafanya kazi za kisheria kwa maelekezo ya Maafisa wa Sheria Waandamizi ikiwa ni pamoja na:

 Kutoa ushauri na kufanya utafiti wa kisheria pale anapohitajika kulingana na Wizara, Idara ya Serikali ama sehemu aliko.

 Kufanya mawasiliano na ofisi nyingine kuhusu masuala ya kisheria kwa maelekezo ya Maafisa wa Sheria walio katika ngazi za juu.

 
36.2 SIFA ZA MWOMBAJI



 Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza ya Sheria kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali na waliomaliza mafunzo ya uwakili yanayotambuliwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
36.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa mwezi


                                                                     X. M. Daudi

                         Katibu, Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
Axact

Post A Comment: