.

Jumla ya Waendesha Pikipiki 1167 wamepatiwa mafunzo ya kuendesha Pikipiki na kupatiwa Leseni daraja “A” katika kipindi cha Januari – Agosti, 2013.

 

Boda boda hii kama ilivyonaswa ikiwa imekiuka sharia usalama barabarani.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo mtandao huu umezipata ni kwamba mpango huo unatekelezwa baina ya Polisi Mkoa wa Mwanza, VETA na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) unao lengo la kupunguza tatizo la ajira kwa Vijana pamoja na kuepusha ajali za barabarani zinazo weza kusababishwa na makosa ya kizembe kutokana na kutijua sharia.

 

“Ni kweli tuna mpango wa kuwafanya Vijana waweze kujiajiri wenyewe ili kuweza kujiongezea kipato lakini pia mpango huu unasaidia kupunguza ajali za barabarani” aliniambia Sajini Kitia wa jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza kitengo cha usalama barabarani tuliyezungumza naye kwa njia ya simu.

 

Imeelezwa pia katika mpango huo Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza kwa kushirikiana na Chuo cha Ufundi VETA, huwapatia mafunzo na badaye jeshi la polisi kwa ushirikiano na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), huwakatia Leseni za daraja “A” na kuwasajili kwenye maeneo wanayofanyia kazi pamoja na kufatilia mwenendo wao wa kazi za kila siku.

 

Ni kwamba kiwango cha ajali kimepungua kwa asilimia 17.8% ikilinganishwa na kipindi kama hicho cha Januari – Augusti, 2012, ambapo kulitokea ajali 118, ikilinganishwa na ajali 97 kwa kipindi hicho hicho cha Januari hadi Agost 2013.

 

Mpango huo unafuatia agizo lililotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kuwaelekeza  Viongozi wa Polisi Mkoani hapa kubaini mbinu zitakazosaidia kupunguza ajali za barabarani kwa asilimia ikilinganishwa na mwaka uliopita 50%.

Hivi sasa Mkoani humo hali imekuwa tofauti ilinganishwa na siku za nyuma wakati biashara hiyo yakundesha pikipiki ikonekana kama biashara haramu na iliyokuwa ikipoteza nguvu kazi ya taifa kutokana na ajali zilizokuwa zikitokea.

Hata hivyo uchunguzi uliofanywa na Blog hii ya kuninews.blogspot, umeonsha kwa bado kuna baaadhi ya waendesha boda boda wasiotii sheria  kwa kupakiza abiria zaidi ya mmoja huku wakiwa hawana kofia ngumu za kujikinga na ajali.

 
Axact

Post A Comment: