Ujerumaini imeamua kupiga marufuku simu zote za "smart" aina ya iPhone baada ya afisa mmoja wa zamani wa kijasusi wa Marekani Edward Snowden kufichua kuwa, simu aina hiyo zilitumika kufanyia ujasusi mazungumzo ya simu ya viongozi wa nchi 35 duniani.

Kabla ya hapo ilibainika kuwa, Wakala wa Usalama wa Taifa wa Marekani NSA ulikuwa unadoya na kudukua mazungumzo ya simu ya Kansela wa Ujerumaini, Angela Merkel tangu mwaka 2002, ujasusi ambao umeikasirisha mno Bundestag (bunge la Ujerumani).

Huku hayo yakiripotiwa, wabunge wa vyama viwili vikuu katika bunge la Ujerumani wamepasisha sheria inayowapiga marufuku wabunge wa nchi hiyo na viongozi wote wa ngazi za juu serikalini kutumia simu ambazo hazina kinga ya kufanyiwa ujasusi yaani simu zisizo na chujio la kudhibiti mawasiliano na barua.

Imebainika kuwa machujio hayo hayawezi kufanya kazi kwenye simu za "smart" aina iPhone zinazotengenezwa na shirika la Apple la Marekani na hivyo kuwapiga marufuku wabunge na viongozi wa ngazi za juu wa Ujerumaini kutumia simu hizo maarufu.

Wachambuzi wa mambo wanaamini kuwa, kutofanya kazi programu  hizo zinazokusudiwa na wabunge wa Ujerumaini ambazo zinachuja mazungumzo na barua katika simu ya iPhone kumetumiwa kama kisingizio tu bali ukweli wa mambo ni kuwa shirika la Apple lina makubaliano ya siri na Wakala wa Usalama wa Taifa wa Marekani NSA yanayoruhusu mawasiliano yote ya simu za iPhone yapitishwe kwenye chujio linalowasilisha taarifa zake moja kwa moja kwa wakala huo wa kijasusi wa Marekani.

 
Axact

Post A Comment: