Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete alipokutana na Mjumbe wa UN. Ikulu JIji Dar es Salaam

Mary Robinson Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Ukanda wa Maziwa Makuu ya Afrika amewasili nchini Tanzania, akiwa katika safari ya kiduru itakayochukua muda wa wiki moja katika nchi za eneo hilo.

Mara baada ya kuwasili mjini Dar es Salaam, Bi Robinson ameunga mkono juhudi kubwa zinazofanywa kwa ajili ya kurejesha amani  mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Aidha mwakilishi huyo wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, analipa kipaumbele kwenye safari yake hiyo suala la kufikiwa kwenye tija na mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Kinshasa na waasi wa M23 huko Kampala Uganda.

Taarifa zinasema kuwa, jana Bi Robinson alikutana na Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania, ambapo nchi hiyo hivi sasa inaongoza kikosi cha Umoja wa Mataifa kinachopambana na makundi ya waasi mashariki mwa Kongo. Imeelezwa kuwa, mwakilishi huyo wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Maziwa Mkuu ya Afrika leo ataelekea Rwanda na baada ya hapo ataelekea nchini Kongo Brazzaville.
Axact

Post A Comment: