Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Bw. Ndaro Kulwijira.
Wathaminishaji kutoka kanda ya Ziwa wamepigwa msasa wa siku nne ili kuwaongezea uwezo katika utendaji wao wa kila siku, akifungua semina hiyo kaimu Katibu tawala wa mkoa wa Mwanza, ndugu Ndaro Kulwijira, amesema sekta ya ardhi imekuwa ikilalamikiwa kutokana na utendaji kwa muda mrefu ima kutokakana na watendaji kufanya kazi kwa mazoea au kwa makusudi.

Alisema taaluma ya uthamini, ni oja ya taaluma muhimu katika kukuza sekta ya Uchumi wa nchi  kwa kuwa na kiwango kikubwa inatoa huduma zinazogusa moja kwa moja jamii yetu ambayo ni masikini.

Ameongeza kuwa kwa muda mrefu ofisi ya uthamini wa fidia imekuwa ikilalamikiwa na wananchi kuwa fidia wanayoitoa kutokidhi mahitaji stahiki ya wananchi. vilevile amewaagiza  wathamini wa kanda hii kuhakikisha kuwa wanahuisha viwango ili viendane na na hali ya soko ya sasa.

Katika hatua nyingine wathamini hao wameaswa kuyazingatia mafunzo hayo ya siku tano.
Axact

Post A Comment: