Idadi ya waliofariki kufuatia shambulio la Likoni imeongezeka na kufikia 6 huku 9 waliokua wakipokea matibabu wameruhusiwa kurudi nyumbani na 6 hao walifariki kufuatia majeraha ya risasi,Polisi nchini Kenya imesema bado hawajafutilia mbali uwezekano wa kuwa lilikua shambulio la kigaidi.

Mwandishi wa habari kutoka Dw nchini  Kenya anaelezea kwa sasa kinachoendelea Mombasa>>’Hali ilivyo mjini Mombasa ni hali ya kutatanisha kukosekana kwa usalama kwa sababu kama unavyojua tukio hili  limezua hofu sana hasa kwa wakazi wa mji huu wa Mombasa’

‘Nakumbuka tukio la watu 5 waliuwawa kwenye kanisa moja hapa Likonyi ni kitendo kilichotokea siku 2 baada ya Waziri wa usalama kutoa taarifa kwa wakazi wa hapa kuwa usalama utadumishwa’

‘Hali ni tete hapa Mjini Mombasa baada ya tukio hilo ambalo watu hao waliuwawa msako wa polisi uliendelea kuimarishwa kuanzia saa 8 na msako huo uliendelea usiku kucha na taarifa tulizopokea kwa sasa ni kwamba watu 59 wametiwa nguvuni’

‘Wasiwasi upo kwa sababu hiki ni kitendo kilichotengenezwa ndani ya kanisa na unajua si mara ya kwanza kitendo hiko kutokea hapa Mombasa nakumbuka fujo zilizozuka baada ya kitendo cha ugaidi kutokea hapa Mombasa kuliokua na taharuki miongoni mwa wakazi wake hasa baina ya wakristo na waislam’

‘Hiki ni kitendo ambacho watu wanahofia kimetekelezwa kuzua hofu hasa miongoni mwa waumini wa dini hizo mbili lakini viongozi wa kidini wamekuja pamoja na kusema kwamba hiki ni kitendo kilichofanywa na magaidi tu ili kuzua mtafaruku miongoni mwa waumini baina ya wakristo na waislam hilo ni tukio linaloendelea kuchunguzwa’

‘Hadi kufikia sasa hakujawa na taarifa za kuthibitisha kitendo hiki kilitekelezwa kwa malengo gani na wakina nani hasa,hali ya wasiwasi mjini Mombasa bado ipo na kama unakumbuka kuwa tukio hili limetokea siku chache baada ya watu wawili kukamatwa wakiwa na mabomu Mabomu ambayo yaliharibiwa hivi juzi tu kwa hivyo ni tukio linalozidi kutia hofu kwa wakazi wa Mombasa’.

 
Axact

Post A Comment: