![]() |
MHE. BERNAD MEMBE WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA TANZANIA. |
Mazungumzo rasmi yanakusudiwa kuondoa kile Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania Bernard Membe alichokiita "vita ya kimaandishi" kilichosukumwa na propaganda ya vyombo vya habari.
"Mazungumzo hayo rasmi yatakuwa ndiyo mwanzo," alisema Membe, akiongeza kwamba watarejesha imani kati ya nchi hizo mbili.Membe alikariri kwamba kwa wajibu wa Tanzania katika mgogoro huo uliopo nchini DRC ni kwa ajili ya jitihada za kuleta amani tu chini ya umoja wa mataifa. wajibu wa Tanzania katika mgogoro uliopo nchini DRC ni kwa ajili tu ya jitihada za kuleta amani tu chini ya Umoja wa Mataifa.
"Kwa mujibu wa ujumbe wetu ulioko huko Goma [mashariki mwa DRC], amani hatimaye inarejea katika eneo hilo na vijana wetu wataendelea kuwa kule kwa mwaka mmoja hadi amani itakaporejea kikamilifu," alisema Membe.
Post A Comment: