Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ya Tanzania imesema hadi kufikia Februari mwaka
huu watanzania 177 wamefungwa katika magereza nchini China, huku miongoni mwao
15 wakiwa wamehukumiwa kunyongwa kutokana na makosa ya dawa za kulevya.
![]() |
KITANZI TAYARI KWA KUNYONGA. |
Akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Wizara ya hiyo, John
Haule alisema watanzania hao bado hawajanyongwa kutokana na serikali ya China
kuthamini ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na China na huenda
wakabadilishiwa kifungo na kufungwa kifungo cha maisha jela badala ya
Kunyongwa.
Haule amesema
serikali ya Tanzania itahakikisha inadumisha ushirikiano na China kwa lengo la
kupatikana kwa fursa za kiuchumi na kwamba tayari serikali ya China imetoa
vifaa kwa Tanzania kwa ajili ya kugundua watu wanaosafirisha dawa za kulevya
katika viwanja vya ndege.
Post A Comment: