Katika kile kinacho onekana kukerwa na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya NSSF na NHIF, wadau kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Halmashauri ya Jiji na Halamashauri ya Manispaa ya  Ilemela,  wameubebesha mzigo Mamlaka ya Udhibiti ya hifadhi ya mifuko ya  Jamii (SSRA) kwa ajili yakuona kero zao zinapatiwa ufumbuzi.
 
Wakitoa malalamiko yao wadau hao ambao walikuepo katika semina ya siku moja iliyofanyika katika Ukumbi wa Halamashauri ya Jiji la Mwanza, wamesema kwa muda mrefu mifuko hiyo imekuwa haina dhamira njema na wanachama wake ikiwapo uwiano wa mafao yanayo tolewa ukilinganisha na mifuko mingine.
 
Akizungumza kwa uchungu, Afisa Utumishi mwandamizi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Bibi Farida Mushi, amesema, NSSF wamefika mahali ambapo watu wengi wamekata tamaa ya kujiunga na mfuko huo, kwani watumishi wake mara zote wamekuwa na majibu yakukatisha tamaa pamoja na kwamba wao kama wanachama ndio walio waajiri kwa maana kwamba kama pasingekuwepo na wanachama basi hata ajira zao zisinge kuwepo.
 
" Fikiria mtu kafanya kazi miaka mingi, mwisho wa siku anakwenda kuangalia mafao yake anakutana na Mil. 2,? alisema na kuhoji bibi Farida Mushi, inawezekanaje watu kama hawa wawe na vitega Uchumi ambavyo vinatokana na michango ya wanachama lakini wanachama wenyewe ukiwaona utawaonea huruma alisema kwa uchungu huku akionyakuwa itafika mahali ambapo watakimbiwa na wanachama kwakuwa wanawapa stahili zisizo faa.
 
Naye Bwana Kija Maeda ambaye ni Afisa Ushirika Mkuu, katika Sekretarieti ya Mwanza, alisema imefika mahali hata wameshindwa kuwa mawakili wema kwa NSSF kwa kuwa hawana tija kwa mafao ya Mchangiaji, " Mimi naomba ni seme tuu ukweli, "hawa NSSF walitaka wanachama wa vyama vya Ushirika wawe wanachangia lakini kutokana na mambo yao hata wanachama wetu tumewatahadharisha na mfuko huu kwani Mimi mwenyewe nimeshuhudia alivyo fanyiwa mmoja ya wanachama wake.
 
Kwa upande wake Katibu wa Afya katika Hospitali ya Rufaa Sekeutoure, Bw. Danny Temba, yeye alipeleka lawama zake moja kwa moja kwa NHIF, kwamba wamekuwa na ubaguzi kwa baadhi ya dawa ambazo hazipatikani mikoani na hasa zile za Saratani na pindi mgonjwa anapo ziitaji basi inamlazimu muuza dawa kuziagiza Dar Es Salaam, lakini gharama zote zikiwa zinabebwa na Mgonjwa jambo ambalo amesema ni unyanyasaji mkubwa kwa mgonjwa" alisema na kuongeza , "haiwezekani mtu ni mgonjwa, ... amekuwa akichangia kwa hiyari yake halafu inafika mwisho wa siku mtu huyo huyo wakati wa Ugonjwa anaambiwa eti achangie gharama za kusafirisha dawa, hakika huu ni unyanyasaji wa hali ya juu sana.
 
Awali akifungua semina hiyo, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Warioba Sanya amesema, ni vema SSRA watambue kwamba kama Wasimamizi wa mifuko hiyo basi wana kila wajibu wa kuhakikisha mifuko hiyo inakuwa kwa manufaa ya mchangiaji na sio kwa mtu ambaye si mwanachama, hivyo akatoa angalizo kwa wanasemina hao kusikiliza kwa makini na kasha kuchangia kwa kadri ya uwezo wao pindi Semina itakapo anza na akawataka wanasemina kuziangalia changamoto zote ambazo zimekuwa zikijitokeza, ikiwapo iliyo ibuliwa na Vyama vya wafanyakazi nchini.
 
Hata hivyo Mkuu wa Mawasiliano wa SSRA Bibi Sarah Kibonde Msika, amekiri kuwapo kwa malalamiko mengi katika mifuko hiyo sehemu mbali mbali nchini na akaahidi kulichukua na kulifanyia kazi katika ngazi husika.
 
SSRA wapo Mkoani Mwanza kwa ajili ya Semina kwa wadau wa Mifuko ya hifadhi ya Jamii katika  kuelimisha lakini pia kuitambulisha mamlaka kwa wadau ili wajue ni wapi wanaweza kupata suluhisho la matatizo yao pindi wanapo pata matatizo.
 
Utafiti Mdogo ulifanywa na mtandao huu umebaini kuwapo kwa mapungufu mengi katika mfuko wa NSSF na hivyo watabiri wa mambo wanasema wasipo jiangalia wanaweza kupoteza wanachama lakini uwezekano wa kusajili wanachama wapya huenda ukawa ni mgumu kwao.
 
KAIMU KATIBU TAWALA MKOA WA MWANZA, MHANDISI WARIOBA SANYA ALIPOKUWA

AKIFUNGUA SEMINA KWA WATUMISHI WA UMMA.






SSRA ilianzishwa kwa sheria namba 5 ya Mwaka 2008 ikiwa na lengo la kuhakikisha mifuko ya hifadhi ya Jamii inafanyakazi yake kwa ufanisi na kuleta tija miongoni mwa wanachama lakini nchi kwa ujumla wake. Aidha Semina hiyo itaendelea siku inayofuata kwa Mamlaka kuwaelimisha Askari Polisi katika Mkoa huo na Semina hiyo inataji kuwa na watu miamoja.
 
 

Axact

Post A Comment: