Asema utawafanya wakose nguvu ya pamoja.

MKUU WA MKOA WA MWANZA MHE. EVARIST NDIKILO ( Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa)
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo, amewatahadharisha Wanachama wa chama kikuu cha  Ushirika Mkoani Mwanza kinacho unganisha  Mikoa ya kanda ya ziwa ambayo ni maarufu kwa  kwa kulima pamba, Nyanza 1984 LTD, kuhusiana na fikra zakutaka kuanzishwa kwa Ushirika mwingine wa Mkoa wa Geita na kusema kufanya hivyo kutafanya Nyanza kukosa nguvu na kusababisha kuparaganyika vipande vipande.

Ndikilo  ameitoa kauli hiyo wakati akifungua Mkutano wa ishirini na nne katika ukumbi wa chuo cha Uwalimu Butimba kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, Ushirika na Chakula mkoani hapa.

Amesema wakati wanafikiria kuanzishwa kwa ushirika kwa mkoa wa Geita ni lazima wafikirie juu ya amali mbali mbali za Ushika huo, sambamba na madeni yaliyopo pamoja na matatizo mengine mengi yanayo kikabili chama hicho kikuu cha ushirika Mkoani hapa na kanda ya ziwa kwa ujumla.

“Ndugu zangu kuna usemi unaosema umoja ni nguvu Utengano ni udhaifu lakini pia waingereza wana msemo wao usemao (..divide them.., .. and role them easily), sasa wakati mnapofikiria juu yakuanzisha Ushirika mwingine lazima haya yote mwende nayo, alisema Ndikilo na kuongeza, “ Unajua mtu anaye taka kukutawala lazima ahakikishe mmekuwa vipande vipande ndipo aweze kupitisha ajenda zake kirahisi na kisha kukutawala atakavyo.

Alisema wakati huko Ulaya wanafikiria jinsi yakuongeza ukubwa kwa kuungana sisi tunafikiria namna gani tuweze kujitenga vipande pande hii haina tija wala afya kwa umoja wetu,.. narudia kusema tena ndugu zangu hii ni hatari sana kwa ushirika wetu huu.

Akaendambali zaidi na kutahadharisha kuwa kwa hivi sasa chama hicho kina madeni ambayo wadau mbali mbali wanaidai Nyanza LTD 1984 lakini pia kuna baadhi ya wadau wanadaiwa na Nyanza 1984 LTD, hivyo kuanza kugawanya gawanya vipande vipande inakuwa ngumu sana katika kushughulikia migogoro hiyo.

Awali akisoma risala ya Waziri mwenye dhamana na ushirika, Mkuu huyo wa mkoa, alisema suala la ulinzi wa mali za chama ulisha tolewa ufafanuzi na aliyekuwa waziri wa Kilimo chakula na Ushirika Steven Wasira wakati wa Mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika 2009, ambapo waziri huyo alionya wachache wajanja kutotumia mwanya wa udhaifu unaojitokeza katika chama katika kukihujumu chama hicho.

Hata hivyo kwa Mujibu wa habari ambazo mtandao huu wa www.kuninewsblogspot.com  umezipata na kuthibitishwa na Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya ushirika mkoani hapa  bwana Emmanuel Omuyanja zimesema wajumbe wote wa kamati hawakuwa tayari kukubaliana na hivyo mada ambayo ilikuwa imetayarishwa kwa ajili hiyo kuwekwa kando.
Axact

Post A Comment: