.Mgonjwa mmoja agundulika
.Serikali ya Mkoa, yatoa tahadhari kwa wananchi.


DALILI ZA DENGUE ZINAVYO JITOKEZA.


 
Mtu mmoja Mkaazi wa Jijini Mwanza katika maeneo ya  kilimahewa mwenye umri wa miaka (62), amelazwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa Sekouture akisumbuliwa na ugonjwa wa Dengue mara baada ya Vipimo kuonesha.
 
Kwa miujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Baraka Konisaga katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, mgonjwa huyo alifikishwa hospitalini hapo siku moja tatu zilizopita kwa ajili ya kuchunguza afya yake, lakini mara baada ya vipimo vya kawaida hakugundulika kuwa na ugonjwa wowote ndipo ilipo mlazimu mtaalam wa maabara kumshauri mgonjwa huyo kupima vipimo vya ugonjwa wa dengue na kupatikana akiwa ameambukizwa  virusi hivyo vinavyo ambukiza ugojwa wa dengue.
 
SOMA TAARIFA NZIMA HAPA CHINI.
 
 
 
 KUWEPO KWA UGONJWA WA DENGUE   KATIKA MKOA WA MWANZA
 
TAARIFA  KWA  UMMA
 
Ndugu, Waandishi wa habari, wawakilishi wa vyombo vya habari na wananchi wote. Napenda kutoa taarifa ya kuwepo kwa ugonjwa wa Dengue katika Mkoa wa Mwanza. Hadi sasa kuna mgonjwa mmoja katika Hospittali ya Rufaa ya Sekou-toure ambaye amethibitika kuwa na ugonjwa huo.  Kufuatia taarifa hii  napenda wananchi wafahamu machache kuhusu ugonjwa wa Dengue. Ugonjwa wa Dengue husababishwa na VIRUS vinavyoitwa “Dengue Virus”  na vinaenezwa na mbu aina ya Aedes.
 
Mbu hawa hupendelea kuzaliana kwenye maji yaliyotuama karibu na makazi ya watu au kwenye vyombo vya kuhitadhia maji majumbani.
 
JINSI UGONJWA WA HOMA YA DENGUE UNAVYOENEZWA
 
Binadamu hupata ugonjwa huu baada ya kuumwa na mbu wa aina ya Aedes aliye na Virusi vya ugonjwa huu.  Mbu  hawa hupendelea kuuma wakati wa mchana.
 
Ugonjwa huu huwapata wetu wa rika zote aidha watoto wenye umri chini ya miaka mitano na mama wajawazito huathirika zaidi.
 
Ndugu wananchi
 
Dalili za Ugonjwa wa Homa ya Dengue
 
Asilimia 90 ya wagonjwa walioambukizwa ugonjwa huu uonyesha dalili awali kuanzia siku ya 3 hadi 14 baada ya kuumwa na mbu mwenye virusi vya ugonjwa huu dalili hizi ni kama zifuatazo:
·         Homa kali ya ghafla
·         Kuumwa kichwa hususani sehemu za machoni
·         Maumivu makali ya misuli pamoja na viungo vya mwili
·         Kichefuchefu au kutapika
·         Kuvimba tezi
·         Kupatwa na harara
Asilimia 10 ya wagonjwa hupatwa na dalili kali kama kutokwa na damu kwenye sehemu za uwazi za mwili mfano mdomoni, masikioni pamoja na sehemu za kutolea haja ndogo na kubwa.
 
Ndugu wananchi,
Njia za kujikinga na Homa ya Dengue
Ugonjwa wa dengue unazuiliwa kwa njia zifuatazo:-
·         Kuangamiza mazalio ya mbu
·         Kufukia madimbwi ya maji au nyunyizia dawa ya kuua viluwiluwi vya mbu kwenye madimbwi hayo
·         Kuondoa  vitu vyote vinavyoweza kuwa mazalia ya mbu kama vile vifuu vya nazi, makopo, chupa na magurudumu ya gari ambavyo vinaweza kufanya maji kutuama karibu na makazi.
·         Kufyeka nyasi na vichaka vilivyo karibu na makazi.
·         Kuhakikisha maua yanayopandwa kwenye makopo au ndoo hayaruhusu maji kutuama
·         Kufunika mashimo ya maji taka kwa mfuniko
·         Kusafisha mitaro na  gata za paa la nyumba ili kutoruhusu maji kutuama.
 
Kuzuia kuumwa na mbu kwa:-
·         Kutumia dawa za kufukuza mbu  (Repellents)
·         Kuvaa nguo ndefu
·         Kuweka wavu wa kuzuia mbu kwenye madirisha na milango
Kwa kufanya hayo, tunaamini tunaweza kuzuia maambukizi ya ugonjwa huu yasiendelee kutokea.  Naomba kila mmoja atimize wajibu wake.
 
Asanteni kwa kunisikiliza,
 
 
 
Baraka M. Konisaga
KAIMU MKUU WA MKOA
MWANZA
 

Axact

Post A Comment: